wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) jijini Dar wakikutana leo ili kujadili mstakabali wao baada ya kile kinachohadithiwa kuwa ni kutaka kugoma kuingia madarasani kutokana na kupanda kwa ada ghafla bin vuuuup kwa asilimia kati ya 50 na 70. habari zaidi zitakuja kadri zitavyopatikana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. BONGO SIO KABISA MI SIRUDI TENA KWA MAMBO WALIYONIFANYIA UDSM KUNIFELISHA NIKIWA MWAKA WA 3 NAINGIA WA 4 KISHA NADAI HAKI YANGU SITAKI TENA HABARI TZ DAILY MATATZO

    ReplyDelete
  2. Mtoa maoni wa kwanza acha fksi bwana. UDSM watu huwa hawafelishwi kwa sababu nyingine yeyote ila kama wewe ni dhaifu. Watu kibao walisingiziwa ma ishu ya ajabu sana lakini wakayamaliza. kama wewe ni dhaifu ki-taaluma pale hakuna mchezo. That is a fact bwana mkubwa ambaye nina dhani ulikuwa unakula nondoz za fani ya sayansi. Pamoja na Mizengwe kibao ila bado pale UDSM kuna discipline ya kitaaluma. Nina nondoz zangu mbili za hapo acha mchezo.

    La pili hao wala nondoz wa IFM wanahaki ya kuquestion upandaji wa ada hovyo kama hauna sababu ya msingi. Hiyo ni sehemu ya maisha yao ili wakimaliza shule wajue pia kutetea haki za wanyonge. Sisi tulipambana pia enzi zetu na wote walipitia vyuo hasa vya umma huo ni utaratibu wa kawaida. Ndiyo tofauti ya kusoma ONLINE au DISTANCE Learning na kuwa Kampasi. Kuwa kampasi unapata taaluma pia unapata elimu ya maisha na namna ya kutatua matatizo...
    Ankali nawapa support hao jamaa wa IFM ila wasifanye uharibifu wa mali wala fujo za kitoto.

    ReplyDelete
  3. KWANI ADA IKIPANDISHWA INAKUWAJE? SI ITAWA-AFFECT WANAOKUJA SI NYINYI AMBAO TAYARI MKOA HAPO! NA HIVYO NDIVYO ILIVYO DUNIANI KOTE ADA IKIPANDA INAPANDA KWA WALE WAJAO SI WALE AMBAO TAYARI WALISHAANZA, KWA HUO NI MKATABA UKIKUBALI OFFER YA KUSOMA ULIYOPEWA UMEKUBALI KILA KILICHOANDIKWA KWENYE OFFER NA MABADILIKO YOYOTE YA ADA HUWA NI KWA WALE WAPYA WAJAO. mimi nimesoma huku ulaya miaka minne nimelipa ile ile niliyokubalia offer, na zimepanda lakini ni kwa watu wanaokuja si sis ambao tayari tulikuwa pale

    ReplyDelete
  4. Ada haikupanda leo. ilipanda toka 2008. Kila mtu alitaarifiwa. Ila hawa wenzetu wanatabu kidogo. Wamekula hela ya mkopo. Katika hao wanaogoma, wengi hawajalipa hata ada ya semester moja. Kama Ada ilikwua ni 1M, mtu hajalipa hata laki moja, ana haki gani ya kugoma ikiwa imepanda hadi 1.5? Angekuwa amelipa angalau hiyo ya zamani, au kiasi ingeeleweka. Mi naona wanatuchafulia tu hali ya kula nondo zetu.

    ReplyDelete
  5. Kachuo kenyewe ni advanced nursery school...mnagomea nini?

    ReplyDelete
  6. Mimi swali langu ni moja na dogo tu kuwa hiyo ada imepandishwa kwa wanaume tu? mbona sketi na magauni siyaoni hapo kwenye picha? au ndiyo mfumo dume huo ambao siku zote huwaweka Beijing nyuma ya wanaume?

    ReplyDelete
  7. Mimi swali langu ni moja na dogo tu kuwa hiyo ada imepandishwa kwa wanaume tu? mbona sketi na magauni siyaoni kwenye picha hapo? au ndiyo athari za mfumo dume ambao siku zote huwaweka Beijing nyuma ya wanaume?
    naomba kuwasilisha hoja.

    ReplyDelete
  8. Mimi maswali yangu ni 2 na madogo tu kuwa hiyo ada imepandishwa kwa wanaume tu? mbona sketi na magauni siyaoni kwenye picha hapo? Au ndiyo athari za mfumo dume ambao siku zote huwaweka Beijing nyuma ya wanaume? Pili huyo Nimrod Mkono wao si amwage miela hapo gogoro liishe?
    naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  9. Mimi maswali yangu ni 2 na madogo tu kuwa hiyo ada imepandishwa kwa wanaume tu? mbona sketi na magauni siyaoni kwenye picha hapo? Au ndiyo athari za mfumo dume ambao siku zote huwaweka Beijing nyuma ya wanaume? Pili huyo Nimrod Mkono wao si amwage miela hapo gogoro liishe?
    naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  10. Wanafunzi wanatakiwa kugoma kwa sababu za msingi na sio kugoma kwa kuwa wanashinikizana tu. Mimi sipo Tanzania lakini kuna kipindi nilikuwa nafatilia kujua ada ya IFM kwa ajili ya mdogo wangu na nikaona kwenye prospectus ya chuo chao kuwa ada inapanda kutoka 1m to 1.5 mil. Hiyo ilikuwa zaidi ya mwaka sasa umepita, haki iko wapi sasa ya hawa wanafunzi kugoma ilhali kila kitu kilikuwa kinajulikana!

    ReplyDelete
  11. Eti, sh 1.5 m? Sio ndio ada ya sekondari za seminary hapo Bongo.

    Shule ya FEZA sekondari ada yake ni 3.5m na kuna nussary kibao zinalipisha Sh 2m/ na hizi shule za primary zote zinazojiita 'international au academy' Je hizi ni za tabaka gani.. watoto wa mafisadi?

    Mimi nadhani karo halisi ni kama million 4 na hizi zilipwe na serikali kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi na wakulima kutokana na kodi.

    Watoto wa Mafisi wapo Ulaya. Achana na Bodi ya Mikopo na sera ya kuchangia asili mia 100

    Turudi kwenye ujamaa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...