Ndugu, jamaa na marafiki waliungana na watoto wa marehemu Balozi Daudi Mwakawago kumwombea dua mzee wetu mjini Boston Jumamosi. Inshaalah tunamwomba Mwenyezi Mungu atupokelee dua zetu, ampunguzie adhabu za kabri, na amjaalie kuwa na amali njema siku ya hukumu...Amin!!!
baadhi ya waliuohudhuria kwenye hitma hiyo
Maalim Isaack Kibodya akitoa nasaha wakati wa hitma
dua ikipigwa wakati wa hitma
baadhi ya kinama waliohudhuria kwenye hitma hiyo







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Michuzi, Hao ni watoto wa Marehemu kuanzia kulia mwenye kanga nyekundu ni Lugudo Lulu, Imani na Mtage, poleni sana

    ReplyDelete
  2. Pøleni sana wafiwa.Utanzania ndio huu.Kwa kweli kuna imani kubwa ya ushirikiano,upendo.umoja ambao hakuna mataifa mengine yanaweza kutufikia.Watanzania tudumu kupendana na kufarijiana kwenye majonzi,shida na raha.baba wa Taifa(RIP)umetuachia urithi mkubwa wa kutobaguana ki dini.kabila nk.Mola amlaze peponi Ameen.Inshallah mola atawapa subra wafiwa.

    ReplyDelete
  3. Poleni Kiye,Imani,Lulu na Tage kwa msiba wa baba yetu, Inshallah mwenyezi mungu atawapa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Tumepoteza mzazi ambaye hatutaweza kumsahahu kwa busara zake and ukarimu wake i always felt like home wakati wowote ule nilipopata muda wa kusimama nyumbani kwenu pale New York nikiwa hapo kwa matembezi. Tunamwombea mungu amlaze mahala pema peponi, Amina. Inshallah tutawaona tena Jumamosi kwa balozi Mahiga kwenye shughuli ya kumkumbuka balozi wetu, baba yetu mpendwa tuliyekaa naye na kushirikiana kwenye kila jambo la raha na shida. Poleni sana ndugu zangu na mama yetu tunamwombea mungu ampe nguvu aweze kuendelea kutunza familia.

    ReplyDelete
  4. Kazi ya Mungu haina makosa ila ni kushukuru kwa kila jambo atuletealo kila siku,nawapa pole watoto wote (Gudo,Kiye Imma na Tage)na mke wa marehemu,kwa msiba lakini kubwa tunawaweka katika sala zetu za kila siku na Mungu awape nguvu na upendo na hasa katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  5. R.I.P Mzee Mwakawago. Your kindness will always be remembered.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...