Matawi ya Nje ya CCM si Ubaguzi
Wapo wengine wanaosema matawi ya nje yanaleta ubaguzi miongoni mwa watanzania waishio ughaibuni. Ni ubaguzi gani huo? CCM ni chama cha kitaifa wala si chama cha kidini, kimkoa au kikabila. Ni chama chenye historia ya kusimama kidete kupinga ubaguzi wa aina yeyote. Iweje leo kuanzishwa kwa matawi yake ya nje kutafsiriwe kuwa ni kuleta ubaguzi kwa watanzania waishio nje?
Wapo wengine wanaosema matawi ya nje yanaleta ubaguzi miongoni mwa watanzania waishio ughaibuni. Ni ubaguzi gani huo? CCM ni chama cha kitaifa wala si chama cha kidini, kimkoa au kikabila. Ni chama chenye historia ya kusimama kidete kupinga ubaguzi wa aina yeyote. Iweje leo kuanzishwa kwa matawi yake ya nje kutafsiriwe kuwa ni kuleta ubaguzi kwa watanzania waishio nje?
Tukumbuke kwamba matawi haya yanafunguliwa na wana-CCM kwa hiari yao kama ambavyo wafanyavyo wana-CCM wa Chunya, Kondoa au Bunda. Lakini kuwa mwanachama wa CCM na kufungua tawi la CCM hakuwazuii wana-CCM kushirikiana wasio wana-CCM katika shughuli za kimaendeleo za uzalishaji mali, kijamii na kisiasa. Kufunguliwa kwa matawi hakuui udugu, urafiki na upendo kati wana-CCM na wasiokuwa wana-CCM.
Sasa hii hoja ya ubaguzi inatoka wapi? Bila shaka anayesema hivi ndiye mbaguzi wa kwanza. Kwanini anawabagua wana-CCM kwa sababu tu wamefunga tawi London? Watu wa namna hii ni wa kuogopwa kama ukoma. Wanapanda mbegu chafu ya ubaguzi na inshallah dhambi hii itawatafuna wenyewe wasipoacha kuiendeleza.
Ndio, tuko ughaibuni, na wote ni watanzania lakini kama ilivyo nyumbani – Tanzania kuwa wote watanzania hakuwazuii watu kuwa na itikadi tofauti za kisiasa na kufanya za chama chake bila kutishwa au kubughudhiwa ili mradi tu hawavunji sheria za nchi.
Pale yanapotokea masuala yanayohusu watanzania wote, mfano harusi, msiba, sherehe za kitaifa au kukutana na viongozi wetu wa serikali kitaifa, kama ilivyo nyumbani, wote tunajumuika kwa pamoja kama watanzania. Sisi sote ni ndugu. Ni marafiki. Ni majirani.
Na pale watanzania wana-CCM wanapokuwa na jambo linalohusu chama chao basi nao wako huru kujumuika pamoja kichama. Ni haki yao ya kidemokrasia. Sasa kwa nini yawepo maswali kuhusu muda wana-CCM kukutana wanaupata wapi. Hili la kukutana au kufanya kazi za chama ni lao wana-CCM wanajua wataupataje muda kuhudhuria vikao vyao vya chama.
Shutuma Dhidi ya Mabalozi
Ni bora pia nikalizungumzia hili la shutuma dhidi ya mabalozi wa Tanzania ughaibuni kuwa wanawapendelea wana-CCM tu. Kwamba inapotokea akaja kiongozi wa kitaifa wana-CCM tu ndio wanaalikwa, na kwamba wanafungua matawi ya CCM tuuuuu. Hizi shutuma si za kiungwana hata kidogo.
Ni bora pia nikalizungumzia hili la shutuma dhidi ya mabalozi wa Tanzania ughaibuni kuwa wanawapendelea wana-CCM tu. Kwamba inapotokea akaja kiongozi wa kitaifa wana-CCM tu ndio wanaalikwa, na kwamba wanafungua matawi ya CCM tuuuuu. Hizi shutuma si za kiungwana hata kidogo.
Nitoe mfano wa balozi wetu nchini Uingereza Mheshimiwa Mwanaidi Maajar ambaye ameshutumiwa kwa kuwapendelea wana-CCM.
Kwanza kabisa inabidi ieleweke wazi kabisa kuwa balozi Maajar haiwakilishi CCM ingawa ni mwanachama wa CCM. Yeye ni mwakilishi wa nchi na si vinginevyo na wala hachanganyi shughuli za CCM na zile za serikali. Pili balozi Maajar si mbaguzi wa kisiasa au kichama.
Huwaalika watanzania wote kukutana viongozi wa juu wa serikali wanaokuwa Uingereza kikazi; na mara zote hutoa tangazo la mwaliko huo kwenye tovuti ya ubalozi wetu.
Tatu balozi Maajar amejiwekea utaratibu wa kukutana na watanzania wote wenye shida ya kumuona kila mwezi. Na anapokutana nao sijasikia hata mtu mmoja akisema balozi alimuuliza kama ni mwana-CCM. Balozi hujishughulisha na suala linaloletwa mezani kwake. Haangalii chama atokacho mtu, dini yake au kabila lake.
Juu ya hayo kama balozi Maajar angekuwa mbaguzi wa kisiasa basi asingefanya kila jitihada kuianzisha jumuiya ya watanzania waishio Uingereza ili kuwaunganisha watanzania waishio Uingereza kuwa kitu kimoja. Kama angekuwa mbaguzi wa kisiasa kwa nini asaidie kuanzisha jumuiya ya watanzania ili hali kuna tayari kuna tawi la CCM?
Jumuiya hii ya watanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika nchi nyingine. Hongera sana balozi Maajar na viongozi wa jumuiya kwa kazi nzuri. Na jitihada zake za Diaspora haziegemei kwa wanaCCM. Ni za watanzania wote.
Ni kweli kwamba miongoni mwa waanzilishi wa tawi la CCM la Uingereza ni ndugu Sharif Maajar ambaye ni mume wake balozi Maajar lakini hili la mume wake balozi kuwa mwanzilishi wa tawi halina uhusiano wowote na utendaji kazi wa balozi kama mwakilishi wa nchi. Haya ni mambo mawili tofauti kabisa. Kwa nini yanaowanishwa?
Hitimisho
Nitumie fursa hii kuwaomba wale wanao tafsiri kuanzishwa kwa matawi ya nje kama ni ubaguzi waache kuendelea kupanda mbegu hii ya uovu miongoni mwa watanzania kwani haijengi umoja, udugu, urafiki, upendo na mshikamano bali inabomoa. Matoke yake ni kujenge uhasama, chuki na uadui miongoni mwa watanzania waishio nje mambo ambayo si mazuri kwetu, kizazi chetu na nchi yetu.
Kwa wana-CCM walio nje na hata nyumbani wautumie muda wao wa ziada kuisoma zaidi na kuielewa, kuitekeleza na kuitetea siasa ya chama. Pia tutumie vipawa, elimu na ujuzi tulionao kubuni mbinu na sera mpya za kuijenga nchi yetu ili kuboresha zaidi na zaidi elimu, huduma ya afya na kila sekta ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Kwa kufanya hivi tutakiwezesha Chama
Cha Mapinduzi kuendelea kuwa madarakani.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Kamaradi Amani Millanga
Kamaradi Amani Millanga


Poleni mafisadi-in-waiting, kazi mnayo. Mtanzania yeyote mwenye akili timamu hawezi kwa namna yoyote kushiriki katika huu upuuzi. Kama si ubaguzi, ni nini hasa kinachowasukuma, je ni tamaa, rushwa, wizi, uonevu, utawala usiofuata sheria, ufisadi nk. zinazoshamiri nchini kwa baraka na kwa kivuli cha CCM. CCM imekuwa kama chuo wanakojiunga vijana na kuhitimu wakiwa mafisadi wa kutupwa. Acheni huu ujinga, mnawaaibisha vijana wa Tanzania.
ReplyDeletePOLE SANA NDUGU YANGU...
ReplyDeleteYAONEANA HUNA DATA NA HATA KUJISHUGHURISHA KUZITAFUTA HUTAKI.
YOTE HAYA HUYASEMAYO NI NADHARIA YU ILI MUENDELEA KUTUMIA VIBAYA PESA ZA WATANZANIA WALIO MASIKINI NA KUTAFUTA KWENU UFALME DUNIANI
NAOMBA IELEWEKE KUWA MAISHA YA HUKU UGHAIBUNI NI TOFAUTI SANA NA HUKO NYUMBANI. HUKU NI UGENINI NA KWA KWELI TUNAHITAJI SANA KUWA KARIBU KULIKO ITIKADI ZETU. SASA TUKILETA MAMBO YA CHAMA INAKUWA TAABU SANA. JE INAPOTOKEA WEWE NI WA CHAMA FLANI NA UKO PEKE YAKO INAKUWAJE? MAMBO YA VYAMA HUKU HAINA MAANA, SANA SANA NI KULETA UBAGUZI KWA UCHACHE WETU. TUYAACHE HUKO BONGO TU JAMANI. HUKU SISI NI WATANZANIA NA TUACHWE TUWE WATANZANIA, TUKIRUDI BONGO BASI TUTAENDELEZA VYAMA VYETU.
ReplyDeleteKwa matawi ya ccm uk ni tabu tupu kwani mwenyekiti ni alikuwa mume wa balozi na kila ufunguzi balozi yupo unataraji sisi wa vyama pinzani haki itakuwepo??na kila ukisikia rais anakuja wale wa ccm ndio wenye kupewa kipaumbele kuliko wengine kama sio ubaguzi ni nini?kaa mdau alivyosema hapo juu huku ni ugenini na maswal aya dini kabila wala rangi hayaitajiki wote ni watanzania sasa tukianza mambo ya vyama na dini na kababila wengine tutakuwa tumepotea na wala hamtatuona huko ubalozini kwenu
ReplyDeleteNAONA NI YALE YALE. WEWE UMETUMWA ILI UJE HUKU KUMSAFISHIA NJIA HUYU MAMA BAADA YA KUSIKKIA ANAHAMIA DC. SASA MPE UJUMBE YEYE NA MUMEWE TENA MWAMBIE HUKU SIYO UK NA HATUTAKUBAOI HUO UBAGUZI WAO NA HAYO MATAWI YA CCM. AJE AWAKILISHE WATZ WOTE NA TUTAMPA SUPPORT ILA AKIANZA YA CCM NA VIKAO KILA SIKU ATAJUA KWANINI DC IMESHINDIKANA. AU NI BORA ANYAMAZE KIMYA KAMA SEFUWE AFANYE KAZI ZAKE. HAPA SIYO LONDON NA NCHI HII INA MITAZAMO TOFAUTI NA WATZ WALIOKO HAPA WANA FIKRA TOFAUTI. ACHA KUMSAFISHIA HUYU MAMA. TUNAMSUBIRI KWA HAMU TUONE SERA ZAKE. KAMA ANAKUJA KULETA UMOJA TUNAMKARIBISHA ILA KAMA AMETUMWA KUJA KUFUNGUA MATAWI HUKU KAMA YUKO PIA TUPO TAYARI KUMPOKEA.
ReplyDeleteKama sio UNAFIKI ni nini?
ReplyDeleteWana-CUF wamekuwa na Tawi London miaka yote, tangu mwana 1995.
CCM wamefungua Tawi juzi juzi, mwaka 2007 (12 Years Later baada ya CUF).
Lengo la kufungua Tawi ni kuunganisa Wana-CCM, nyie msio Wana-CCM mnalalamika! Eti mnataka Wana-CCM wasijishughulishe na chama chao kwa sababu wako Ulaya!!
Wana CCM (kama Tawi) tayari ni UMOJA wa Watanzania kama ilivyo Wana-CUF. Kwa pamoja wakishirikiana na wana jumuiya/ kundi jingine ambalo sio la Wana-CCM au CUF matokeo yake ni kupanua umoja zaidi badala ya utengano; sasa hii dhana ya kubaguliwa au utengano inatoka wapi?
NE,
Reading, UK
Anonymous said... Tue Mar 16, 10:30:00 PM.
ReplyDeleteIna maana ukiwa Tanzania, wewe ni Mwana-CCM, CUF, Chadema na sio Mtanzania?!!
KWA NINI TUSIJIULIZE...
ReplyDeleteKUNGEKUWA NA UPINZANI MAKINI TANZANIA, CCM INGEKUWA NA MUDA WA KUFIKIRIA MATAWI YA NJE??
Woote wanaopinga matawi ya ccm ni wanachama hasa wa Chadema, tena wao wana Tawi lao kuubwa kwenye mtandao, wanajiunga humo, wanatoa michango humo, na wana forum yao ya kujadiliana mambo yao kupitia mtandaoni.
ReplyDeleteKinachonishangaza wao wanafanya, wakifanya wenzao inakuwa mwao, wasi wasi wao ni nini? Wanaona nafasi ya kuchukua utawala wa nchi inawaponyoka? Nafasi za wengine kupata vyeo inawaondoka? Unapojiunga na chama cha siasa kisiri au kidhahiri unakuwa na malengo, sasa malengo hayo na wenzenu wanayo vile vile.
Hebu acheni kupiga kelele za kitoto, matawi matawi wakati nyie yenu mumefungua kwenye mtandao.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Mwanachama hai wa CCM ninayeishi popote pale duniani ili mradi sivunji katiba za watu.
Hivi kijana uliyeenda shule na kubahatika kuelewa jinsi nchi yetu inavyoendeshwa una haja ya kuisupport CCM? simaanishi uwe upinzani lakini tunahitaji kutafuta namna ya kuwabana wala nchi yetu na si kuwaunga mkono. Nchi imekuwa katika wakati mgumu sana hasa katika kipindi cha uongozi uliopo madarakani kwa sasa, bora hata enzi za Ben.
ReplyDeleteenyi wagalitia nani aliyewaloga.....kati ya mambo aliyoharibu nyerere ni kulifanya taifa linaendeshwa kwa fear..the communist-uchwara party still holding firmly something on the hand we gonna smash s*&$ until they open up. mwache aje alete masharti ya kijani america.
ReplyDeleteJamani mie ni CCM damu yaani piga ua lakini sikubaliani na CCM-London, nk.
ReplyDeleteMwenye katiba ya sasa ya CCM, atuambie ni ukurasa wa ngapi unaonyesha nafasi ya matawi ya CCM nje ya Tanzania.
Biblia inasema, si wote wanaosema Bwana, Bwana watauona ufalme wa mbinguni.
Ujumbe: Wana CCM-London, mwenzenu huyo anaelekea Washington.
jamani naomba nijieleze kidogo,mimi niko hapa uk kwa miaka kama mitano hivi lakini kabla ya hapo nimeishi nchi zifuatazo,ugiriki,italy,ufaransa,
ReplyDeleteuholanzi na ubeligiji,baada ya hapo nikaja uk,ukweli hapa nimekuta mambo wanayofanya watanzania huwezi kuyakuta DUNIA yoyote ile!,hasa kwa mara ya kwanza nafika nchi hii naambiwa kuna matawi sijui ya ccm,sijui chama gani nilishangaa sana!maana huko kote nilikotoka tulikuwa na umoja wa watanzani tu,hakuna vyama wala nini,leo nafika huku kuna mambo ya kisiasa,ninachojua mimi kwa uelewa wangu mdogo,mnaweza kuanzisha matawi ya chama kama nchi yenu haijawa huru,kama kilivyokuwa chama cha ANC kilikuwa na tawi kila kona ya afrika hata hapo nyumbani walikuwa na tawi lao,baada ya mambo kuwa shwari je ANC ipo hapo!??na niulize hapo nyumbani waingereza wapo wengi je ulishawahi sikia TAWI LA LABOUR nchini TANZANIA?tawi la CONSERVATIVE nchini tanzania? natumai jibu hapana,ila kuna umoja wa waingereza,umoja wa wajerumani na mataifa mengine,huko ulaya nyingine ukienda hasa italy na greece ukaleta mambo ya siasa ndugu zangu msithubutu utaondoka bila kuaga na wala huta rudi tena,kwa ufupi wabango huko wanaumoja hasa ndiyo maana mbongo akifariki ktk nchi hizo nilizokutajia lazima mwili utaenda kuzikwa nyumbani kwa ghalama yoyote ile,je uk vipi hilo lipo au tutaangalia huyu wa chama gani???,wanaopenda kuona wabongo wanafanya nini nchini ugiriki(umangani) unaweza kuwapata kwa
www.tanzaniansingeece.com, naishi Bradford huku tunaumoja wa watanzania tu mambo ya vyama au matawi hakuna kabisaaaaaa,anayetaka matawi ayafuate Reading na london,tunakutana kila baada ya miezi miwili
tunawakaribisha watanzania ambao wako tayari kuitwa watanzania siyo katoka chama gani
TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WANGU WOTE,NA WATANZANIA WOTE NAWAPENDA!
ASANTENI
Mkuu, sawa lakini kwa watu makini kujiingiza katika kuanzisha matawi ya vyma ughaibuni ni kujisumbua kwa kitu ambacho hakina manufaa ya kitaifa bali binafsi, najua hapa UK tuna mambo mengi nyuma ya uanzishaji wa matawi hayo, lakini kwa wale wasio na mambo hayo katika nchi nyingine hawawezi kujisumbua kufanya haya, pengine UK bado inaruhusu mambo haya chini ya sera yake ya multi-culture lakini kwa nchi makini kufanya hivi ni kuruhusu uhaini, fikiria kama watu wataamua kuanzisha chama ughaibuni unafikiri wataeleweka? ndiyo maana mie naona hakuna sababu ya kujisumbua na mambo ya siasa ughaibuni isipokuwa pale kunapokuwa na agenda kibao za siri. Habarindiyo hiyo mkuu.
ReplyDeleteanony wa tue mar 16, 11:34:00 umeongea point.
ReplyDeleteanyway hapa sio kuhusu matawi wala ccm, is all about Zanzibar na Tanganyika, nani anabisha? Wazanzibar hawataki kujichanganya na wa Tanganyika bila ya kificho, sasa na leo wa Tanganyika wameamua kujitenga kelelee nyiiingi, nini? kote wanataka wao. sasa muone raha ya kujitenga ilivyo, wenzenu walishawajua ila walikuwa wanajipanga na wao kwa mgongo wa ccm.
thanks GOD sina chama, ninachojua mimi ni Mtanzania.
hapa nilipo siko vacation au nimetumwa na nchi kutembea. i am economic refugee living abroad....kwa sababu nchi yangu inaendeshwa na few alogance clown hapo juu kwa matakwa yao sio ya nchi, kwa hiyo nikijiunga na ccm sure ni ujinga wangu...nasitakubali kuwa mjinga. i have no nerve to see this sh**
ReplyDeleteAlishasema Sumaye ukitaka ufanikiwe basi lazima uwe mwana CCM, wapo waliopingana na hili (hasa wafanyabiashara) madhara yake waliyapata,sina haja ya kuongea mengi lakini kama hii hali ikiachwa iendelee basi hata balozi zetu soon zitakuwa ni sawa na matawi ya CCm, binafsi naamini kwamba u CHADEMA, uCCM, u CUF u CCJ ni u sisi, na usisi ni ubaguzi
ReplyDeletena ubaguzi ni tofauti ya itikadi.
Kama kawaida, hoja ikitolewa na mwanaCCM basi atasema kila mwenye mawazo tofauti mwendawazimu, hana akili nk. Vitu viwili vinavyoongoza kwa kutenganisha watu ni dini na siasa. Kwa nini watu mnaanza kuvileta ughaibuni? Badala ya kutaka kusimama kama Watz mnataka kusimama kama wana CCM na wana vyama vinginevyo. Kesho na keshokutwa mtataka kusimama kama wana CCM Waislamu na wana CCM Wakristo nk. Ikitoka hapo mtakuwa wana CCM Wadigo na Wamatumbi.
ReplyDeleteMtz uliye ughaibuni unatakiwa kufikiria kutetea nchi yako kwanza, sio chama fulani. Ukizingatia kwamba wana vyama vya ughaibuni hamna hata nafasi ya kutoa input kwenye sera za vyama vyenu, mnaishia 'kusimama kidete' kutetea wanayoamua wengine bila kuwahusisha.
Nasema Tanzania kwanza!!!
Kwa nini kwana mmewajibu? Kwani kuna chama kilichokatazwa kufungua matawi? Demokrasi ipo wapi? Wana CCM tupo kibao hapa USA, hatujaamua tu kuanzisha matawi au mmesahau wana CUF walivyoandamana kwenye ubalozi wetu miaka iliyopita? Kila mtu ana uhuru wa kushiriki na kujiunga chama chochote kile kitakachoweza kufungua matawi yake ughaibuni na sioni kwa nini CCM inakuwa ni issue. Mkumbuke wote sisi tumelelewa na CCM. Wengi waliozaliowa miaka ya 60's na 70's na kurudi nyuma tunajifanya kusahau wema wa CCM. Tumesoma bure, matibabu bure, vyuo tumekwenda bure, jeshini tumekwenda na kulipwa posho uliza waafrika wengine maisha walioishi. Babu na bibi zetu wana maji safi vituo vya afya mpaka madongo poromoka. Kila mkoa una ka-mji kakubwa ambako unapata huduma muhimi. Posta kila mahali enzi hizo tunatumiwa telegram za maneno na pesa. Acheni hizo tumetoka mbali. Wote sisi tumetokea CCM na ndiyo tukasambaratika. CCM imeijenga nchi yetu na hatuwezi kukataa. TUIPENDE NCHI YETU NA TUPENDANE BILA KUJALI WEWE NI MWANACHAMA WA CHAMA GANI TOFAUTI NI ITIKADI ZETU HIVYO CCM IKIFUNGUA TAWI YANINI KUPANDISHA JAZBA? NA WEWE ITISHA WANITIKADI WAKO NA MFUNGUE LAKWENU KWANI BILA UPINZANI HAKUTAKUWA NA MAENDELEO. CCM JUU, JUU, JUU, JUU ZAIDI. KIDUIMU CHAMA CHA MAPINDUZI. MTOTO WA CCM BY BLOOD! KARIBU MAMA BALOZI TUSHIRIKIANE KUJENGA NCHI YETU.
ReplyDeleteMiranga wamekusikia ndugu yangu, ukirudi utapewa udiwani au ukuu wa wilaya! kwani mwenye njaa ana aibu basi?
ReplyDeletehawa wanajikomba tu kwa huyu mama Maajar Mwanaidi.njaa inawasumbua.
ReplyDeleteKwa kweli huyu aliyeandika hii post hana tofauti na Sheick Yahaya, wote wametumwa. CCM inapoona inalemewa inawatumia watu wenye IQ ya chini kama huyu na Sheick Yahaya ndio wanakuja na hoja kama ukimpinga Kikwete utakufa ghafla nk. Jamani huu ni upuuzi. Hata ukiwauliza waliopo ughaibuni urtagundua kwamba kujiunga na CCM ni ishu ya kutafuta ulaji tu.
ReplyDeleteJamani kuweni na huruma na pesa za waTZ. Mtu yeyote makini hawezi kujiunga na matawi ya vyama huko nje, maana huko siasa ni ya nini zaidi ya kuweka vikao vya kimbea na kutafuta kula pesa??
kaka Gee.
Jamani mimi siyo mwanasiasa wala shabiki wa chama chochote cha siasa. Ila nina observation kidogo na naomba nitumie haki yangu kuongelea.
ReplyDelete(1) Kwa kweli sidhani kama ni jambo la maana sana kushabikia siasa ya chama chochote nje ya nchi. kama watafuta maisha halisi wanatakiwa wajihusishe zaidi na masuala ya maendeleo ya familia zao na nchi yao kwa kutumia utaratibu wowote wanaouona unafaa. mimi sijawahi ona Wakenya, Waganda, Waafrika Kusini, Waingereza, nk.nk katika nchi ya kigeni wakiwa bize wanafungua matawi ya vyama na blabla...sidhani kama yana faida sana zaidi ya propaganda. hivyo nawashauri Watanzania walio nje watumie muda mwingi kwa masuala ya maendeleo na siyo siasa.
(2) Nimeguswa na mtoa maoni mmoja hapo juu akitahadharisha Mheshimiwa Balozi mpya aliyehamishiwa DC kukaa chonjo na utamaduni uliozoeleka kule Uingereza wa kushabikia siasa za chama fulani nadhani ndo maana inaonekana kama ubaguzi- kwa kweli ninavyoifahamu Marekani kila mtu yuko bize na masuala ya maendeleo na siyo siasa kama tunavyozipa uzito. hata vyama vinapingana kwa hoja kuliko propaganda. Na sijawahi kumsikia Balozi yeyote wa nchi akiwa kwenye mkutano wa kushabikia chama cha siasa hata makada wakongwe kama Mjomba Jaka Mwambi kule Moscow sijamsikia kwenye mitandao akiwa bize na mambo haya. nadhani yuko bize na ushirikiano wa Tanzania na Urusi na anajua ni kwa nini anatakiwa awe neutral kwa kuwa anawakilisha watanzania wa itikadi zote.
Maoni yangu hayana maana kuwa nawanyima mashabiki wa siasa kuendelea na propaganda zao.
mtoa maoni wa nne nadhani ana hoja ambayo ni nzito sana. Mimi ninavyofahamu watumishi wa umma kama huyu balozi Maajar hawaruhusiwi kabisa na sheria kujihusisha na siasa za chama chochote kwa sababu ya kazi zao. sasa kama wanaonekana hadharani mstari wa mbele kwenye siasa inakuwa taabu hata kwa wananchi wa kawaida na nadhani ndiyo sababu inaonekana kama wanabaguliwa.
ReplyDeleteKwa kweli hili ni tatizo. nakumbuka mhadhiri mmoja alipoteza kazi hapa UDSM kwa sababu ya kuonekana anaitikadi za siasa. Na waziri wa utumishi akaja juu kwenye vyombo vya habari kulelezea kwa nini amenyimwa ajira. Sasa hiyo fomula inatumika pia kwa watumishi wa umma kama huyu mheshimiwa Maajar ambaye anazifahamu sheria vizuri?
ali ya nyumbani atakama wewe ni mremavu wa macho na masikio au upofu uwezi kusema ujuwi nini kinacho endelea tz kwa watu wa chache kuwanyonyo wengine yani kama wewe ni kijana a leo huwezi kusema nchi yetu inako erekea ni kuzuli kwa faida ya watoto wetu kina mama watoto wazee wanakufa kutokana na kukosa uduma muhimu kwa kukosa utawala wenye masirai ya watu wote. au nyinyi mmetoka sehemu zisizo na magari alafu mmeona magari yalivyo jazana dar na miundo mbinu mi bovu ndio mahana mnafikilia ndio maendeleo waliyo tufanyia . du mna tukatisha tamaa . du nyinyi kiboko au kjp kawai soo
ReplyDeleteHivi sheria za nchi mlipo zinawaruhusu kuunda vyama vya siasa kwa ajili ya harakati za kisiasa za nchi mlizotokea? Ni sawa na Wanyarwanda walio Tanzania wakianza kuendekeza siasa za kwao ndani ya nchi yetu.
ReplyDeleteWewe Anony unaedai kuwa inchi imekuwa mbovu, bora hata enzi za Ben sikubaliani na wewe kabisa. Maovu yote yanayosikika sasa na ufisadi uliokithiri nchini kwetu, mizizi yake imetokea kwenye utawala wa Ben. Na mpaka sasa hivi simuelewi yule mzee Mkapa, kwani anajifanya kama kiziwi na Bubu pale anapodharau tuhuma dhidi yake.
ReplyDeleteKama kweli tuna uchungu na nchi yetu na tunataka watu kama "Ben" wajibu tuhuma zao na kutueleza ukweli wa ufisadi huu, basi hatuna budi kuendelea kuikosoa CCM. Hivyo basi, tabia ya kuendelea kujipendekeza kwa CCM kwa kufungua matawi zaidi huku nje ya nchi haitotusaidia. Mimi nakubaliana kabisa na baadhi ya maoni kuwa wanaofungua matawi haya, hawana uchungu kabisa na nchi yetu, ni walafi na mafisadi chipukizi, ambao wakipata nafasi za kuongoza nchi yetu ufisadi ndio utazidi kushamiri.Ndugu zangu CCM inahitaji kukosolewa kwa nguvu zote, na sio kuweka matumbo mbele na kushangilia viongozi wake kwa mgongo wa shati la kijani na kofia ya njano. Namalizia kwa kusema kuwa, Matawi ya CCM huku nje, hayafai,kwani yanazidi kutugawa na kudhoofisha nchi yetu.
CCM wanatumia kodi na rasilimali za nchi vibaya,kwa kugharamia haya matawi, ambayo lengo kuu ni kurubuni wadau walio nje kama wanavyoendelea kuwarubuni wa kule nyumbani. Nina imani kuwa wadau wengi wa nje tumesoma au tunaendelea kujielemisha kutokana na fursa inayopatikana huku nje. Hivyo basi, ni matumaini yangu kuwa mtauona mtego huu(kama baadhi yetu)na kukataa Matawi haya feki.Mama Maajar karibu DC,Ila ujue wazi kuwa huku hatutaki matawi ya CCM (wala chama chochote). Balozi anatakiwa awe balozi wa waTanzania wote na si wale wa CCM tu.Ningependekeza kuwepo na umoja wa waTanzania popote walipo, ambao utakuwa unaangalia mustakabali wa siasa Tanzania na utendaji wa serikali katika nyanja mbalimbali. Umoja huu hauna haja ya kufungamana na upande wowote wa chama, bali ni umoja tu wa watanzania ambao wana uchungu na nchi yao. Mpaka sasa bado hatuna chama cha upinzani cha kweli dhidi ya CCM. Kwahiyo, sio CCM tu anayehitaji kukosolewa, bali hata vyama vya upinzani, ambavyo mpaka sasa hizi malengo yake hayaelewi kivitendo.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE!
KWANI WEWE MHESHIMIWA NI MSEMAJI WA HUYO BALOZI????INAKUWAJE UELEZEE KWA UNAGA UBAGA NAMNA BALOZI ANAVYOFANYA KAZI ZAKE?WEWE NI MTUNGA STORI NA MZUSHI TU KWANI HUWEZI KUELEZEA UTENDAJI KAZI WA OFISA WA SERIKALI ILIHALI WEWE SIO MSEMAJE WAKE HUKO NI KUJIPENDEKEZA AND THAT SHOWS HOW IRRESPONSIBLE WITH POOR DECISIONS YOU ARE.BALOZI ANGEJIBU TUHUMA MWENYEWE SASA WW KUMJIBIA HAISAIDII KWANI WATANZANIA WATAENDELEA KUAMINI THE SAME KUHUSU BALOZI HADI TU PALE WATAKAPOSIKIA KAULI YAKE MWENYEWE.ACHA KUJIPENDEKEZA KIJANA
ReplyDeleteHello wandugu wa ULAYA, hivi kila chama kikifungua tawi itakuwa Vipi? Tanzania tuna vyama 16, kila city kama kuna mwanachama wa chama fulani, afungue Tawi itakuwaje? au wasomi wenzengu hamuwazi hivyo? Najua suala lililopo hapo ni kujitambulisha kwa wakubwa kuwa mpo ili mpewe hata nafasi katika serikali ya JK, ok sawa mtaonwa, lakini dhamira yenu ni kuwasaidia watanzania kweli kweli au kuna kitu kingine hapo?
ReplyDelete1. Kuna Watz wengi sana wanaoishi na pia kutembelea Kenya kuliko UK. Mbona hamuazishi matawi hapo Kenya ambapo hata tunaelekea kungana katika mambo mengi ya kimaisha?
ReplyDelete2. Hata ANC walikwahi kuwepo Mazimbu - Morogoro, walipopata uhuru wao sijaona bendera tena za ANC.
3. Hivi ni kipi kipaumbele zaidi, kufungua matawi ya CCM UK au kuwawezesha Watz waishio UK kote kuweza kupiga kura ambayo ni haki yao ya uraia?
4. Hivi huko hayo matawi yana legality ipi. Yanaandikiswa kama NGOs? Maana hayapaswi kuwa chini Ubalozi (ambaye ni mwakilishi wa Serikali na vyama vyote vya siasa ni Tz ni vyake). Legality ya CCM Tanzania haiwezi kuwa transferable kwenda UK.
Hivyo inawezekana watu hawajalifikilia hili mara mbili maana Matawi haya yanaweza kuwa ni ya kichina tu, yaani hakika kisheria ni feki maana yana hang tu na Mwenyekiti anaweza kutoweka na michango yote na namna ya kumshitaki katika sherika za uingereza itakuwa kichekesho kikubwa sana.
5.Hivi wilaya na mikoa ya haya matawi ni wapi? Na tukumbuke kuwa kila wilaya na kila mkoa inatakiwa kuwa na wawakilishi katika Mkutano Mkuu wa Taifa. Swali je sasa zile nchi ambazo hatuna matawi wao hawana haki ya kuwakilishwa???
Mimi na Ukoo wangu wote ni WanaCCM damu lakini SIKUBALIANI KAMWE NA MATAWI HAYA. Yafungwe mara moja na ughaibuni ziundwe tu Jumuiya za zinazowaunganisha Watanzania wote na zinaweza kuandikishwa kama NGOs n.k. CCM si NGO wala CBO wala Kampuni!.
Mdau uliyotoa hii mada ni Pumbavu sana wewe!
ReplyDeletemimi nashangaa sana na watanzania waliopo nje,especially uk..cha ajabu nchi yetu inakataa kupitisha sheria ya uraia wa nchi mbli duo nationality,b[kutoa vitambulisho vya kitaifa]ids,tanznia ndio nchi pekee duniani wananchi wake hawana ids..same like old stone age. ndio maana hata wakongo,warundi,wasomali,wote ni watanzania hii inatokana kukuosa card za vitambulisho vya nchi,sasa nyinyi mnaonadi matawi ya ccm au chadema au cuf.hamlioni hili jambo na kulijadili kama watanzania na sio kama wana ccm au cuf au chadema?eti mnajidai mmesoma na kukaaa ulaya na kumbe akili zenu finyu kama funza na ndio maana mnashabikia mambo ya vyama vya siasa ughaibuni mimi nafikiri ajenda zenu zipo kwenye ufisadi,sisi tunateseka hapa bongo kwa uovu wa wanasiasa uchwara waliopo kwenye uongozi kupitia ccm.na nyinyi bado mnafikiria mbinu hizo hizo za kuwa back up kwa kuanziasha matawi ya kipuuzi,tafuteni elimu na fanyeni kazi kwa bidii na mlijenge taifa letu kama watanzanzania ,sio mambo ya vyama vya siasa ughaibuni.alafu ukifuatilia kwa makini uatagundua nyinyi wabeba box sio raia wa tanzania mmeukana utanzania sasa inakuaje mshabikie mamabo ya siasa ya tanzania mkiwa nje?kama kweli mnataka kuindeleza tanzania tumieni elimu yenu na mrudi huku nyumbani muonyeshe wa vitendo .sio kushabikia unazi wa simba na yanga huko uk.na kwingineko..ole wenu kama mna dili za kifisadi na ajenda zenu za siri tuambiane..alafu nyinyi sio watanzania mnatumia uraia wa somali,ruanda ,burundi n.k hapo uk sasa je kwa nini leo mnashabikia siasa chafu ya kibongo huko ughaibuni?kwa taarifa yenu tutawapa taarişfa home offices za hapo uk..juu ya status zenu kwamba nyinyi sio wasomali waruanda.warundi kwamba nia waongo mmewadanganya waingereza na hapo hapo manaleta dirty politics kwa kujihusisha na mafisadi wa tanzania kama vibaraka wao. ole wenu tutawaripti acheni kushabikia mambo ya siasa nje ya nchi mkitaka njooni huku huku bongo alafu tutawachambua kama kweli nyinyi mpo kwa masalahi ya umaa au matumbo yenu?njaa aina aibu ndio maana mnasahabikia siasa chafu
ReplyDeleteupuuzi mtupu na kutaka misifa ya kijinga ovyo sana wala haina mvuto nauliza kuna chama cha watani wa jadi huko?? au ni nyinyi tu kiherehere kimewanana
ReplyDeleteHaya matawi ya vyama vya siasa ughaibuni hayatakiwi. Nivi na sisi tukishutukia hapo Dar ufunguzi wa vyama vya siasa vya ma-Talibani na Hezborah,Likudi n.k tutaweza kumudu vishindo vyao?
ReplyDeleteBottom line.
Wanaofungua matawi ni watu wanaotaka vya kunyonga na na wahakikishia kuwa mkirudi kugombea huku ni kuwabwaga chini puu!!
Kama mna ubavu rudini mjichangaye huku muone. Hakatizi mtu hapa na longolomgo la matawo ya chama Uingereza. Hilo ndilo liliwapeleka huko?
Joto ya jiwe imeshaanza muulizeni kiongozi wetu mmoja (jina kapuni) wa Tawi huko alivyomwagwa huko Shirati kipindi kilichopita. Na wembe ni huo huo.
Badala ya kutumia mbongo zetu na upeo wenu kuimarisha diplomasia ya uchumi kwa ajili ya Tz na pia kudai haki zenu za kupiga kura ninyi mnaibuka na upuuzi huu.
CCM tunakataa na ninapanga kupeleka agenda hii katika mH/ Kuu tuone.
michuzi pongezi nyingi kwa kazi iliyotukuka mungu akutangulie kwa kweli aya matawi ya ccm uk ni kero kubwa sana akuna umuhimu wake kabisa uwezi kupiga kura ufisadi ndio umejaa ccm na watu wanatengeneza ulaji tu sasa najiuliza naishi uk sitegemei kwenda kuishi nyumbani hivi karibuni siwezi kupiga kura sasa hiyo kadi ya ccm ni yanini ??????? ni ujinga mtupu mnapiga domo vigogo wanaendelea kula epa richmond vijicent rada akuna aliekwenda jela sasa ccm inafanya nini nyumba ya gavana inajengwa kwa bilion 1.4 sisi ni wadanganyika we need revolution tuamke wabongo jamani acheni ujinga wa kuzidi kufungua matawi ya ccm nje ya nchi michuzi umesema ubagui naomba usibanie maoni yangu inanikera sana
ReplyDeleteKama sijakosea Balozi ni mfanyakazi wa Serekali ya Tanzania na si mwakilishi wa Chama. Pamoja na kwamba ameteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM. Kwahiyo anapokuwa Ubalozini kazi yake ni kuiwakilisha Serekali na siyo kwa namna yoyote ile kusaidia (direct or indirect) kufungua matawi ya CCM.
ReplyDeleteKama Anons wengine walivyosema hakuna katiba zozote za vyama zinazotaka matawi kufungulia nje ya Nchi unless ni kwa nia ya kuiondoa serekali iliyopo madarakani. Sana sana inaweza kuishia kwenye matumizi mabaya ya pesa za serekali katika kusupport Ujinga kama huu au njia za mafisadi kuwa na connections na nje katika kuiibia nchi.
Kwa USA kuna vyama vya Watanzania kila states, States nyingine mpaka viwili hivyo kama Balozi anataka kushirikiana na Watanzania njia ipo wazi.
BALOZI WA NCHI HUWAKILISHA TAIFA HUSIKA NA SI CHAMA FULANI CHA SIASA.
ReplyDeleteMAMBO YA VYAMA VYA SIASA YANAISHIA HUKO HUKO TANZANIA, NJE YA TANZANIA TUNAENZI UTANZANIA KAMA TAIFA MOJA NA ITIKADI MOJA YENYE KUJENGA UTAMADUNI WA TAIFA LA TANZANIA.
KAMA MMEZOEA MAMBO YA KWA BIBI UK UJE HAPA MAREKANI HAYO HAYAPO NA KUNA SHERIA HAPA MAREKANI AMBAYO HAIRUHUSU ITIKADI ZA KISIASA YA NCHI NYINGINE NDANI YA MAREKANI. JARIBU ANZISHA TAWI LA CCM HAPA UPAMBANE NA FBI.
HATA HAPA MAREKANI KWA UZOEFU WANGU SIJAONA MATAWI YA VYAMA VYA REPUBLICAN AU DEMOCRATIC YAKIPEPERUSHA BENDERA ZA VYAMA MITAANI KAMA WAFANYAVYO BONGO AU SIJUI HUKO UK.
HAPA TAIFA HURU NA LINALINDA HAKI NA USAWA KWA RAIA WOTE BILA KUJENGA ITIKADI ZA KISIASA KWA MISINGI YA VYAMA VYA KISIASA.
TUWE WATU TULIOPEVUKA KIMATAIFA TUSIFIKIRI TUNACHOFANYA BONGO NDO TUFANYE KATIKA NCHI ZA WENYEWE TUNAJIONYESHA JINSI TULIVYO NYUMA KATIKA MENGI YATUPASAYO.
WENZETU WANACHOONA KATIKA MAMBO HAYO NI ITIKADI NDANI YA CHAMA HICHO SI UTITIRI NA BENDERA ZA VYAMA MITAANI, USHAMBA HUO.
Watanganyika kupinga uwepo wa matawi ya CCM UK ni upumbavu ama kutokujua chanzo na asili yake. CUF imekuwa na matawi hapa UK miaka mingi na Maalim Seif amekuwa akisafiri mara kwa mara kuja kuimarisha matawi yake, na kufanya mikakati yao na mapicha mmeyaona kwenye mitandao. Sasa CCM wamejibu mapigo kwa kufungua matawi na wao hapa UK hao hao CUF wanapiga kelele na nyie Wadanganyika mnawaunga mkono bila hata ya kujua asili na chanzo ni nini.
ReplyDeleteHakuna watu wasiri duniani kama Wapemba, nyie subirini warudishe utawala wa Sultani sio Zanzibar, bali hata Tanganyika pia, nikimaanisha Tanzania nzima ndio mtajua kwa nini wenzenu walikuwa na mikakati ya kukutana kama Watanganyika na si Watanzania huko UK.
Hivi mmmeshasikia Wazanzibar walikuwa wanapiga kelele kuhusu kuwepo kwa matawi ya CUF nje ya nchi? Hivi mnajua thamani ya kuwa na kadi ya CUF? Unajua hiyo kadi inafungua nini?
Kalaghabaho na Ubozi wenu.
Aliyedata