Mambo vipi mzee wa Libeneke pole na majukumu ya kuhabarisha jamii na kwa kukuza jina la nchi yetu ya Tanzania kwa wale wasioijua na pia wanaojua wajue kwa undani zaidi,tunashukuru kwa kazi yako na pia tuko pamoja katika majukumu yako.

Ningependa uwarushie wanajamii hii video yetu ya jiji la A-Town inayoonyesha mambo ambayo wengi hawajui kama yanapatikana nchini kwetu,nimejitolea kutengeneza hii video baada ya kusoma habari iliyoandikwa na The Lonely Planet kwamba mji wa Arusha umeshika namba nane(80) kati ya miji mibayta ulimwenguni kitu ambacho si kweli hizo ni chuki ambayo imekaa kibiashara zaidi na kutaka kutudidimiza kiutalii.

Pia nimetengeneza page kwa facebook kwa nia hiyo hiyo kwa wenye facebook account wanaweza kujiunga kwa kupitia;

http://www.facebook.com/pages/ARUSHA-A-TOWNGENEVA-OF-AFRICA/226440818964

kazi hii naifanya kiuzalendo zaidi ningependa watanzania tujifunze kuwa wazalendo na nchi yetu kitu ambacho hatunaga lakini tunaweza kujifuza hapo kwa majirani zetu.


Habari ndio hiyo.
Mzalendo wa kujitegemea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Great job

    Kwa kuadd kama unagood camera ungeadd yale majumba yaliyo Arusha ya zamani pia inasaidia kwa watalii wanaopenda kwenda nchi kuoa historia za zamani....

    1. Picha za national milling
    2. Picha za shule za zamani kama ilboru secondary
    3. Picha za makarisha ya zamani au misikiti ya zamani
    4. Kuna jumba moja pale sijui lilikua la serikali au nini wanasema zamani walikua wananyonga watu..Lilikua jeupe hivi kama unaenda AICC ukitokea Goliondoi road baada ya round about upande wa kulia....
    5. AICC sijaona picha za lile jumba zinazoeleweka online
    6. open markets au lile soko la mjini.

    Nimeondoka Arusha siku nyingi sana but still is one of my lovely town....Little quite town

    ReplyDelete
  2. HIVI UNAJUA HICHO KITU WANATUFANYIA FITINA HAWA MAJIRANI ZETU WANAFIKI WAKUBWA, MIMI BINAFSI HUWAZI KUAMINI KATIKA FAMILIA YANGU NIMEPIGA MARUFUKU KUTUMIA BIDHAA ZA HAWA WANAFIKI, BIDHAA YOYOYE ILIYOANDIKWA MADE IN KEENYA HAIKATIZI NDANI KWANGU, NI KWAMBA HAWA JAMAA NI WANAFIKI HUKU WANAKOMAA TUUNGANE HUKU WANATUCHAFUA, WANAPIGA MARUFUKU BIDHAA ZETU KICHINICHINI, HEBU FIKIRIA SWALA LA KWANINI DUNIANI WATU WANACHANGANYIKIWA KUHUSU MLIMA KILIMANJARO UPO WAPI? HATE KEENYA

    ReplyDelete
  3. Naomba nijue nani kaimba wimbo unaoambatana na video hii, na pia jina la wimbo please

    ReplyDelete
  4. WANAWAONEA NINI? ARUSHA NI KWELI NI MJI MCHAFU,NASHANGAA WATANZANIA WANAPOSIFIA KUWA NI SWISS OF AFRICA UCHAFU MTU,UJAMBAZI NDIYO NYUMBANI,NA HAUPO KIMPANGILIO KABISA MIUNDO MBINU MIBOVU,BARABARA HAKUNA UNASHANGAA KUWA NA FOLENI KWA MJI MDOGO KAMA ARUSHA SABABU BARABARA ZA KUAMINIKA KUU NI MBILI TU,

    ReplyDelete
  5. JAMANI KWANZA KABISA NAPENDA KUKU PONGEZA ULIYE TENGE NEZA HII MOVE YANI UMENIKUNA SANA MWENZIO NINA KUJA ARUSHA MWEZI UJAO.KAZI MZRURI SANA LAKINI UMESAAU THE AFRICAN TULP HILE HOTE USIPINME BABAKE,

    WACHE WACHONGE KWANI WEWE UJUI KWAMBA ARUSHA NIKUZURI KULIKO MIKOA MINGINE YOTE?

    ReplyDelete
  6. Wooow i love Arusha somuch

    iam from kilimanjaro growng up in arusha that is my home!

    I LOVE YOU ARUSHA

    ReplyDelete
  7. Kazi nzuri mzalendo,
    na karibu sana ktk libeneke la kuwahabarisha wazalendo wengine kuhusu vivutio vya nchi yetu ili wao ndio wapate kuwa ma-balozi wa hivi vivutio.

    safari ndefu huanza na hatua ya kwanza, tusonge mbele...

    tembeatz.blogspot.com

    ReplyDelete
  8. Lazima tukubali ukweli. Kwa sisi tuliozaliwa hapa, Arusha umekuwa mji ovyo kabisa. (1) City centre ya Arusha imetawaliwa na machokoraa, vibaka na matapeli. Imekuwa jahanamu kwa watalii. Makampuni mengi ya watalii ya nje inawashauri watalii waiepuke Arusha kutokana na kero wanaoipata kutoka kwa machokoraa na vibaka. Mimi mwenyewe nimeshuhudia mwenyewe mara nyingi watalii wakibughudhiwa na kuibiwa na kuripoti manispaa , lakini jibu lao hiyo ni kazi ya polisi na polisi nao wanasema hilo ni tatizo la manispaa. (2)Pamoja na kuwa Arusha ina mapato makubwa sana, mji huu ni mchafu sana na - ukiondoa barabara za city centre - barabara zake ni ovyo kabisa. Hebu nendeni soko kuu na masoko mengine hapa msikie harufu ya uchafu. Tokeni nje ya maeneo ya AICC, mahoteli na Uhuru road muone barabara zilivyo chafu. (3) Mbinu ya manispaa ya hapa ni ile ya DANGANYA TOTO! Kwa kuwa wanajua wakubwa na watu kutoka nje wanakuja AICC, basi maeneo ya mjini na mahoteli peke yake ndiyo yanashughulikiwa. (4) Manispaa ya Arusha inanukia ufisadi. Master Plan ja mji huu haiheshimiwa. Open areas na green areas karibu zote zimeuzwa na kuna tetesi kuwa sasa wanataka kuwauzia wafanyabiashara makaburi yageuzwe stendi ya basi na maduka ya watu binafsi. (5) Bdala ya kulalamikia Lonely Planet, tujirekibishe na kuifanya Arusha irudie hali yake ya 1970's ilpokuwa "the cleanest and best organised town in East Africa". Morani Halisi.

    ReplyDelete
  9. Kwa alieuliza jina la huo wimbo,huo wimbo unaitwa haturudi nyuma. Na muimbaji ni kidumu ft juliana ni wimbo mzuri.

    ReplyDelete
  10. morani halisi ni kweli uliyoyasema arusha kupo ovyo sana mji umejaa machokoraa na matapeli vumbiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii lazima uumwe macho hali y ahewa baridi ni nzuri ila no mvutoo sio kihivyo barabara ziiiiiiiiiiiiiiii ukimwi uko juuuuuu sana mererani ndio wasambazaji wakuu!!

    ReplyDelete
  11. hakuna kitu sikipendi kama unavyosema arusha geneva of africa.mwaka 2006 nilikuja na waingereza hapo,walishangaa sana kuona manispaa imeandikwa arusha geneva of africa.huo ni utumwa mambo leo,just image useme mwanza l.A of africa.haimake any sense.arusha ibaki arusha ya tz.nakushaurei ubadilishe lile group lako kwenye facebook hilo neno geneva of africa.maana wageni wanatuona malimbukeni.

    ReplyDelete
  12. NI KWELI KABISA ARUSHA SIO MJI TENA UMESHAHARIBIKA SANA NA NI MCHAFU NA HAKUNA AMANI KABISA. UJAMBAZI NDIO MAKAO MAKUU PALE NA BARABARA ZA LAMI NI MBILI TATU TUU.. WEZI ,VIBAKA WAMEONGEZEKA SANA WATU WANAISHI KWA WASIWASI. SISI TATTIZO LETU TUNATAKA KUSIFIWA TUU WAKATI HATUFANYI JUHUDI YEYOTE YA KUBORESHA MAMBO!! PIA NAUNGA MKONO KABISA KUWA KUSEMA ARUSHA NI 'GENEVA OF AFRICA' NI ULIMBUKENI MTUPU, SIJUI NI NANI ALILETA HILI JINA!!. INA MAANA HAKUNA MATUMAINI KABISA KUWA ARUSHA INAWEZA KUWA NZURI ZAIDI YA GENEVA? AU ARUSHA SIO MJI WA KIPEKEE? WATALII WANAKUJA ARUSHA KWA SABABU YA ARUSHA NA VITU VYAKE VYA ASILI SIO KWA SABABU KUNA MAJENGO YA MIKUTANO KAMA GENEVA. TUACHE ULIMBUKENI WA KUWALALAMIKIA WANAOTUKOSOA HAOHAO NDIO WATATUFANYA TUREKEBISHIKE TUWE BORA ZAIDI.. TUSIPENDE SIFA ZISIZOKUWA ZETU LAZIMA JUHUDI IFANYIKE KUFANYA MABORESHO.. ETI TUNAWALAUMU WAKENYA.. HILO SI SURUHISHO, DAWA NI KUFANYA JUHUDI YA KUWAZIDI SIO KUKAA KULALAMIKA TUU WAKATI WENZETU WAKO NA MIPANGILIO ZAIDI YETU. NI KWELI KABISA KENYA WAKO JUU KWA MAMBO MENGI ZAIDI YETU KWA HIYO NI CHANGAMOTO KWETU KUJIBORESHA NA KUACHA LONGOLOGO.

    Mzozaji

    ReplyDelete
  13. Nakubaliana 100 % na morani halisi. Mji wetu umekuwa mchafu na barabara zilizojificha zimesahauliwa kabisa. Watoto wa mitaani wavuta gundi na machokora wanafanya wanavyotaka. Pia nakubaliana na jamaa hapo juu aliyesema tuachane na huo ujinga wa geneva of africa kwa kuwa ni kasumba ya kijinga na pia hizi slums ya a-taun naona sasa zimekuwa nyingi mno kwa kuwa hamna surveys yoyote ya kupanga mji. Jamani eeh tujitahidi sasa kufanya mambo vizuri na kuufanya mji mkuu wa EAC upendeze kabla ya kufika mahali ambapo hatutaweza kurekebisha problems zote hizi. Ol-Vayan. (e unoto 1990).

    ReplyDelete
  14. Uzalendo gani lakini kuita Arusha "Geneva of Africa"? Arusha haiwezi kuwa na heshima yake kwa kuwa Arusha tu mpaka ichukue jina la mji wa Ulaya? Tuache unyonge. Usitegemee hata siku moja New York ikawa Dar es Salaam of US.

    ReplyDelete
  15. Ninasikitika kila siku nikiambiwa kuwa Arusha ya sasa hivi sio ile ya zamani. Ni kwanini tumeiacha ikaharibika? Mimi ni mchagga lakini nimekulia Arusha na 1990 ndio mara ya mwisho kutia mguu huo mji. Sasa nasikia siku hizi kunabanana tu kama Dar. Kumekua na vumbi sana na baridi sio kama ile ya zamani. Watu sio wasafi tena kama zamani. Enzi zetu wanafunzi tulikua wasafi kweli na wazazi masaa yote wako soap soap. Nasikia metropole ya siku hizi sio ile ya zamani. majumba hayapigwi rangi nje mara kwa mara kwa vile zamani.

    na kweli Arusha ya geneva sijui nini hiyo ni kujidhalilisha. Hatujiamini kusema Arusha ni Arusha? Who came up with that name?

    ReplyDelete
  16. Video nzuri ya kuelezea kanda ya kaskazini hususan Arusha.

    Ila tuombe Juliana na Kidumu wasiweke ngumu wimbo 'Haturudi Nyuma' ukanyofolewa na youtube tukabakia na video clip bubu.

    Nimeona ile clip ya Kidum ft Jualiana iliyowekwa ktk globu ya jamii kwa jina 'Hatutrudi Nyuma' imeshanyofolewa na youtube.

    Inaonekana kila mwa globu ya jamii alikuwa anafyonza 'Hatutrudi kwa kasi ya ajabu', tuache hizo tuombe wasanii ruhusa yao, au tununue CD?Video halali.
    Mdau
    Arusha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...