Msongamano wa magari katika barabara ya Chalinze - Segera,maeneo ya kijiji cha Manga mara baada ya kontena kuanguka katikati ya barabara na kufanya gari zingine zisiweze kupita.utaratubu wa kuliondoa kontena hilo barabarani hapo ulichukua muda mrefu sana kutokana na kuwepo mbali kwa break down ya kunyanyulia magari makubwa. baadhi ya watumiaji wa njia hiyo wakibadilishana mawazo huku wakifikiria jinsi watakavyoondoka hapo.
foleni ilikuwa ni ndefu sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. DU, HII HIGHWAY YETU HATA KICHOCHIORO KIPANA. NDIYO MANA TUNAKUFA KAMA MBWA VILE, HALAFU TUNALAUMU MADEREVA. NAONA TUZIITE "DEATH HIGHWAYS". 40+ YRS BAADA YA UHURU BADO TUNA HIGHWAYS ZILIZODISIGNIWA NA WAKOLONI, HALAFU TUNAJIITA WASOMI. HATA KUKOPY ANA KUPASTE MAENDELEO TUNASHINDWA. KWELI BONGO TAMBARARE. BONGO HOYEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  2. Polen. sasa we mpiga picha mbona hujatuonesha picha za hilo contena lililoanguka na wakati likinyanyuliwa? au we uliondoka kwa miguu kabla hawajanyanyua.

    ReplyDelete
  3. we mdau wa 21:00 pm
    tunakusubiri wewe utulete maendeleo toka uhuru watu wa miaka 40 so fanya chap chap wacha kulaumu tuonyeshe umefanya nini kama mtanzania mzalendo katika nchi yako.

    ReplyDelete
  4. bado kidogo tu tataanza foleni hadi kwenye ndege angani, hii nchi usafiri karaha kweli kweli!

    ReplyDelete
  5. Du! yaani barabara nyembamba kweeli kweli, halafu magari mawili yapishane yakiwa spidi 150km/saa lazima watu wafe.

    Mdau
    Dayaspora

    ReplyDelete
  6. sasa hapa tukisema watanzania tubadilike hii barabara ni muhimu sana. kwanini tusipanue na kuzifanya nne. Mbili kwenda na kurudi. Na ndiyo maana kulikuwa na treni za abiria na mizigo kutoka DAR/Arusha lakini wajanja wakaona hazifai haya malori yangekuwa machache kwenye hizi barabara hata ajali zingepungua kutokana na ushindani wa kibiashara. Mbona nchi za watu wengine treni ni usafari wa kutegemewa sana?

    ReplyDelete
  7. BONGO HAMNA WASOMI WALA NINI WOTE MAFISADI TU NDO WAMEJAA,

    SISI NI WADANGANYIKA FULL STOP

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...