Mgodi wa Bulyanhulu umetoa taarifa ya ajali iliyotokea kati ya saa 8 na saa 9 leo alfajiri, ambapo mwamba uliporomoka katika eneo la kazi lililopo wastan wa mita 900 chini ya ardhi. Mwamba huo uliangukia mashine aina ya Jumbo na kuwabana wafanyakazi watatu.
Kikosi cha uokoaji kilianza kazi mara baada ya tukio, shughuli za uokoaji zimekua zikiendelea kwa mfululizo mpaka sasa.
Shughuli za uchimbaji zimesimamishwa ili kupisha jitihada za uokoaji, mpaka hapo zitakapokamilika.
Mgodi tayari umeshafikisha taarifa kwa wanafamilia wa wafanyakazi husika, vile vile taarrifa zimefikishwa kwa vyombo mbali mbali ikiwa ni pamoja na Polisi, na uongozi wa mkoa na wilaya.
Mgodi unatumia uwezo wake wote katika jitihada za kuokoa wafanyakazi wake na kuwarudisha salama.
Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kadri zinavyopatikana.
Kwa taarifa zaidi;
Teweli Kyara Teweli
Meneja Mahusiano & Mawasiliano
+255 767 308 600
tteweli@barrick.com

chances of getting those out ni ndogo.maisha ya mgodi ni magumu.i remember one day when i lost one of my close friend geologist in 2005,kila siku nilikua naongea nae kabla hajashuka chini.good help them and the family
ReplyDelete