JK akijiandikisha kupiga kura kwenye kituo kipya cha kupigia kura kijijini kwake Msoga,wilayani Bagamoyo. Pembeni akiangalia ni msimamizi wa kituo cha kuandikisha wapiga kura cha Msoga Bi.Diana Fredrick. Kituo cha zamani cha JK kilikuwa Bwilingu, Kata ya Chalinze, wilayani Bagamoyo. Mama Salma Kikwete pia alijiandikisha kupiga kura kwenye daftari hilo la kudumu la wapiga kura kijijini hapo.
JK na Mama Salma Kikwete wakikagua kwa makini vitambulisho vyao vipya vya kupiga kura walipojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kupatiwa vitambulisho vipya huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo.Kushoto ni msimamizi wa kituo hicho cha wapiga kura Msoga Bi.Diana Fredrick

historia ya JK Msoga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na Mama Salma Kikwete, jana, Jumatano, Machi 3, 2010, wamejiandikisha kama wapiga kura katika kijiji cha kwao cha Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete waliwasili kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura cha Shule ya Msingi Msoga, kijiji cha Msoga, kiasi cha saa nne asubuhi, na kupokelewa na msimamizi wa kituo hicho, Ndugu Diana Frederick.

Kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2005, Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete walipiga kura kwenye mji mdogo wa Chalinze wilaya hiyo hiyo ya Bagamoyo lakini zamu hii wameamua kujiandisha, ili waweze kupiga kura kijijini kwao.

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wamejiandikisha katika kituo kipya kufuatia kuanza kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kwa Kanda ya Mashariki.

Uboreshaji wa Daftari la Wapigaji Kura kwa Kanda ya Mashariki ulianza Jumatatu ya wiki hii, Machi Mosi, 2010, na umepangwa kumalizika keshokutwa, Machi 6, 2010.

Chini ya uboreshaji huo, wanaandikishwa wapigaji kura wapya, walioamua kubadilisha vituo vyao vya kupiga kura, ama waliopoteza shahada zao za kupigia kura.

Kufuatia hatua yake hiyo, Rais Kikwete amerudia tena wito wake kwa wananchi wenye sifa za kupiga kura kutumia nafasi ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa kujiandikisha kwa mara ya kwanza kama wapigaji kura, na kwa wale waliopoteza shahada zao kujiandikisha upya, ili wapate sifa za kutumia haki yao ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. haaaa!!
    mimi nakumbuka niliandikishwa,sikujiandikia!mbona mwenye nchi ana andika mwenyewe?!na huu utaratibu wa mwenye ofisi kusimama na mteja kukaa unakuaje!?

    ReplyDelete
  2. hahahaaaaaaaaa anoy wa hapo juu 12:05:00pm comment yako imeniacha hoi sanaaa!!!
    mdau-Ukerewe

    ReplyDelete
  3. hivi mtu unajiandikisha mahali popote au pale unapoishi? maana huyu tawi lake na kila kitu huwa anaenda ile kata ya mchafukoge na ndo kituo chake cha kupigia kula, 2005 nilikuwa nakaa tabata sasa nimehamia sinza nitajiandikisha na sinza afu nipige kula sehemu zote

    ReplyDelete
  4. Mhmm!12:05, protocal izo jamani,ila hapo chichemi kitu nchije nkapigwa nchale.

    ReplyDelete
  5. Huyu mKuu wa kijiji si anaishi Magogoni na 2005 akikuwa Mikocheni.....sasa hii inakuwaje?

    ReplyDelete
  6. Bradha naweza kupata kontakts za huyo Msimamizi hapo?

    ReplyDelete
  7. Mpeni kura Msoga

    ReplyDelete
  8. Candid ScopeMarch 04, 2010

    Ni uelewa mdogo kwa wengi wetu. Nikifika Ikulu ofisi ni yake lakini akija kwangu mie ndo mwenyekiti, sasa dada kamwachia kiti wakati ndo haki yake. Mapokeo ya ujamaa na ukiritimba vigumu kufutika mpaka kitabu kiwapitie wote wajue haki yao

    ReplyDelete
  9. Huyo Mwandikishaji ni lazima kapitia mchujo mzito na kuambiwa cha kufanya pindi muheshimiwa akifika. Unatakiwa kusimama umpishe akae then ajiandikishe mwenyewe wewe kazi yako ni kuangalia tu.

    ReplyDelete
  10. EBU TULETEENI HIZO CLIPS ZA VIDEO NI NZURI SANA JAMANI EBU ENDELEENI KUTUNDIKA

    ReplyDelete
  11. Jamani kama hapo ndio kijijini kwa mheshimiwa na amekuwa akienda kujiandikisha kwenye uchaguzi mara kadhaa mnategemea kweli sehemu nyingine za nchi yetu zitabadilike? Kama hata huwezi kupatengeneza kwako utawezaje kutengeneza kwa mwenzio!!?
    Hapa tumeliwa kwa kweli hata kashule ka maana? barabara, zahanati, maji safi?? au ndio usawa, kwamba hata na kijijini kwake hapapendelei? Jamani hamna hata comment moja imeongelea hilo swala ina maana tumeridhika au ndio tusehe wengine hiyo clip hamjaiona??

    Mdau Ukonga

    ReplyDelete
  12. Kwa Mdau Ukonga (Fri Mar 05, 09:56:00 AM).

    Viongozi wetu wangekuwa na mtazamo kama wako, hali ingekuwa mbaya. Unataka shule iwe na vigae wakati kuna maeneo ambayo hayana hata shule. Maamuzi ya rasilimali gani iende wapi yanatakiwa yafanyike kwa kuzingatia uhitaji siyo NINATOKA WAPI.

    ReplyDelete
  13. Hivi watu kwa nini wanalilia hivi vyeo RAISI,WAZIRI MKUU,ni shida tupu JK kabla ya Urais au hata ile miaka miwili ya kwanza alikuwa anawakawaka handsome but now mnajionea wenyewe sasa akimaliza je?si bora ule kuku kwa mrija kama mimi hapa?

    ReplyDelete
  14. hii si heshima yaani mbele ya raisi mwanamama anavaa kinyume na maadili,nilipokua cameraman bongo wakati nikirikodi raisi au mawaziri tu bsi hufatwa na maafisa wa usalama kuniambia vua cap au badilisha t-shir za kimarekani vaa nguo za heshima sasa mambo yamebadilika,Pili ingekua JK ni Raisi wa Zanzibar angejiandikisha mahala gani?maana kila siku yupo nje ya nchi na Zenji ukaazi ni miaka 5,naomba jibu wazee,michuzi niachie hii tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...