Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo(katikati) akisikiliza maelezo jana kutoka kwa Mkulima wa Mpunga Mohamed Shaban(kulia) juu ya scheme ya umwagiliaji ya kilimo cha mpunga ya heka 900 katika Kijiji cha Mawemailo wilayani Babati. Wengine wanaosikiliza ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mercy Sila(kushoto). Waziri Mkullo alikuwa na ziara ya kutembelea mashamba hao na kujionea shughuli za uzalishaji wa mpunga na pia kupata maoni kutoka kwa wakulima hao kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa zao hilo kupitia uwezeshaji wa Serikali.
Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo(katikati) akiwahutubia wakulima wa zao la mpunga wa Kijiji cha Mawemailo wilayani Babati mara baada ya kutembelea scheme yao ya umwagiliaji yenye heka 900 mashamba ya mpunga. Waziri huyo aliwasisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano wao waliouonyesha ili kuzalisha zao hilo kwa manufaa yao na Taifa. Wengine kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Dkt Ian Langibori na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Emmanuel Kamba.

Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Emmanuel Kamba akisisitiza mshikamano kwa wakulima wa zao la mpunga wa katika Kijiji cha Mawemailo wilayani Babati mara baada ya kujionea juhudi za wananchi hao za kilimo cha zao hilo katika mashamba yao yanayofika heka 900. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo ambaye alikuwa na ziara ya kutembelea mashamba hao na ushirika wa wakulima wa mpunga wa Mshikamano SACCOS kwa ajili ya kusilikiliza maoni yao. Picha na Tiganya Vicent wa MAELEZO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni vizuri kwa viongozi kufanya ziara kwa wananchi ila sioni sababu ya kupamba kwa vitambaa wakati ukuta unaonekana kabisa ni wa tofali za kuchoma ambazo zinakaribia kuanguka. Wakati mwingine ni vizuri tofunika ili viongozi wetu wazione vizuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...