JK akipita kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Bi. Clara Mahundi, Mke wa aliyekuwa Mkuu wa Jesji la Polisi nchini Inspekta jenerali mstaafu Harun Mahundi nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar leo mchana. Mama Mahundi alifariki juzi huko India alikokuwa akipata matibabu.

akiweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Bi.Clara Mahundi mke wa aliyekuwa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta Jenerali Harun Mahundi,nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo mchana.

JK akimfariji Inspekta Jenerali mstaafu wa Jeshi la Polisi Harun Mahundi kufuatia kifo cha Mke wake Bi.Clara Mahundi,wakati Rais alipokwenda nyumbani kwa Kamanda Mahundi kuifariji familia. Mazishi yamefanyika leo jioni katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. RIP Mwalimu wangu mpendwa Clara Mahundi! Huyu mama nakumbuka alikuwa ndio mwalimu wetu mkuu pale Upanga Primary School(LY 94) na alichangia sana katika kunirekebisha tabia. Kwani nilikuwa ni mtoto mtukutu sana, na kama si juhudi zake na walimu wengine pale shuleni, basi huenda ningekuwa Segerea leo hii. Poleni sana wana familia.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana kwa msiba wa mama. Namkumbuka mama huyu alikuwa mstaarabu sana. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Poleni sana Fadhili na wengineo. ni mimi mdau wa oysterbay hospital

    ReplyDelete
  3. Poleni sana kina John Mahundi, mama alikuwa mtu mkarimu sana. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Ameen.

    ReplyDelete
  4. Jamani hata siamini kusikia aliyekuwa Mwalimu wangu mkuu Upanga Primary School. It's being a longtime, sijapata kumsikia wala kuonana nae tangu nilipomaliza 1993. Leo hii naona picha yake na kusikia amefariki. Mungu ailaze roho yake mama, mwalimu mpendwa wetu mahali pema peponi, Amin. Alikuwa mwalimu mkuu mpole na sijapata kuona lakini alitumia busara kurekebisha nidhamu na wala si kwa kutumia fimbo au ukali, jamani.

    ReplyDelete
  5. Pole sana John mapenzi ya Mungu.

    ReplyDelete
  6. poleni sana kina john na grace. nimesikitika sana mwalimu wangu wa Upanga primary kututoka. alikuwa na upendo sana, alinipenda na kunipa zawadi sana ingawa nilikuwa mtundu sana.mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

    maulid

    ReplyDelete
  7. pole sana john na familia nzima. Aminatha.

    ReplyDelete
  8. POLE SANA JK KWA MISIBA

    ReplyDelete
  9. Poleni sana wanafamilia wote. Alikuwa mama yetu mpenzi, ametulea katika maadili mema sana Tutakukumbuka daima!
    POLE sana Fadhili,grace,John,Mzee Mahundi.

    Mgaza Kossey

    ReplyDelete
  10. Poleni familia ya Mahundi ni wakati mgumu sana mbele yenu lakini tunaomba Mungu azidi kuwatia nguvu. RIP Mama.
    Toka kwa familia rafiki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...