Home
Unlabelled
JK aongoza kikao cha halmashauri kuu ya CCM leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ukosefu wa mfumo mzuri wa elimu nchini umefanya kukosekana kwa marubani wa helkopta za binafsi na hivyo kuwalazimu kwenda kutafuta wataalamu hao nchini Kenya.
ReplyDeleteHayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, wakati akihutubia mkutano wa operesheni sangara katika uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari Kibakwe, Wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma juzi.
“Huyu rubani wetu tumemtoa nchini Kenya baada ya kutafuta nchini na kukosa rubani wa kuendesha helkopta binafsi…hapa wanapatikana jeshini,”alisema na kuongeza kuwa hilo linatokana na serikali ya CCM kushindwa kujenga mfumo mzuri wa elimu.
Alisema maeneo mengi ya mkoa huo aliyoyatembelea, amegundua shule nyingi zenye wanafunzi 600 zina walimu wawili, jambo ambalo linasababisha kukosekana kwa wataalamu mbalimbali wakiwemo marubani.
“Hapa kinachofanyika ni kuwapaka ujinga badala ya kuwapa elimu,”alisema Mbowe.
Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema, alisema helkopta inayotumika katika mikutano imesaidia chama kufanya mikutano mingi ya hadhara.
Alifafanua kuwa chama kimeweza kufanya mikutano 14 kwa siku kwa kutumia helkopta lakini kwa kutumia usafiri wa magari ni mikutano minne tu ingeweza kufanyika kwa siku.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo , alihoji je, Chadema inawezaje kufahamu matatizo ya wananchi hasa ya miundo mbinu wakati wanapita angani katika operesheni zao.
Akijibu swali hilo, Mrema alisema mbali na kupita angani lakini wanachadema zaidi ya watu 44 ambao wanapita katika mikutano tofauti kwenye kata zote za jimbo la Kibakwe.
Naye Mkurugenzi wa Oganizesheni na Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaila, aliwataka wananchi hao kuchagua viongozi wenye akili za kuleta maendeleo katika jimbo hilo badala ya kuangalia umbile ama sura.
Kigaila ameonyesha nia ya kuwania jimbo hilo ambalo linashikiliwa na Mbunge wa CCM, George Simbachawene.
sahihisho kidogo:
ReplyDeletekikao hiki ni cha kamati kuu na si halmashauri kuu
Kwanini wajumbe wa vikao vya Halmashauri kuu ya CCM kutoka Zanzibar siku zote wakikutana na wale wenzao wa bara kwenye vikao rasmi vya kichama huwa hawavai mavazi ya Kijani ya chama?? Hili nimeliona siku nyingi kidogo.
ReplyDeleteMshika Dau.
Wachungaji wamjia juu Sheikh Yahya
ReplyDeleteNa Restuta James
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini wamemjia juu Mnajimu maarufu, Sheikh Yahaya Hussein, kutokana na utabiri wake alioeleza kuwa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautafanyika na kueleza kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangwa.
Viongozi hao ambao walikuwa kwenye kikao jijini Dar es Salaam kwa wiki tatu sasa, wameeleza kusikitishwa kwao na utabiri wa Sheikh Yahya na kuwataka Watanzania kumpuuza na kuendelea na maandalizi ya uchaguzi kama kawaida.
Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste, William Mwamalanga, aliliambia gazeti hili Dar es Salaam jana kuwa ni aibu kwa taifa na Watanzania kutabiriwa mambo yao na kueleza viongozi wa dini wataliombea taifa ili liondokane na dhana hiyo. Alisema Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa amani na utulivu na kwamba watu wanaoitabiria nchi mabaya Mungu hatowavumilia.
“Uchaguzi Mkuu ni jambo kubwa sana ambalo limefanyiwa maandalizi makubwa ikiwemo kuwaandaa wananchi kwa ajili ya kuchagua viongozi wao, hauwezi kupingwa na mtu anayeangalia nyota na mwezi,” alisema.
Mchungaji Mwamalanga aliwaonya wanasiasa na watu wote wanaotegemea nguvu za giza na utabiri wa Sheikh Yahya wataanguka kwenye nyadhifa zao na kuwataka wamrudie Mungu kwa kutubu ili waweze kufanikiwa katika shughuli zao.
Alisema utafiti walioufanya hivi karibuni umebaini kuwa wabunge 43 na Mawaziri 11 wanategemea nguvu za giza na utabiri wa Sheikh Yahya.
Hata hivyo, viongozi wa dini wamewaonya viongozi hao kuachana mara moja na imani hizo na kumrudia Mungu kwa kuwa katika uchaguzi mkuu ujao hawatashinda.
Mchungaji huyo amemwonya Sheikh Yahya kuacha mara moja utabiri kwa kuwa nia yake ni kuvuruga amani ya nchi na kuwajengea hofu Watanzania.
Mapema wiki hii, Sheikh Yahya aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine alitabiri kuwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautafanyika kwa madai kuwa nchi itakumbwa na machafuko.
IKULU NI SEHEMU MUHIMU SANA KATIKA KUTATUA MATATIZO YA MTANZANIA NA SIO KUHUSU ISSUE ZA CCM.
ReplyDeleteVYAMA VYA UPINZANI MKO WAPI? WANANCHI MPO WAPI? WANASIASA MPO WAPI? CCM ILITAKIWA KUFANYA SHUGHULI ZAKE ZA KICHAMA NJE KABISA YA IKULU NA KTK MUDA WA PEKEE WA RAIS NA SIO VINGINEVYO!
HII NI AIBU KWA RAIS, WASHAURI WAKE NA KWA TAIFA, KUTUMIKIA MALI ZA UMMA KTK MANUFAA YA KIPEE NDIO HAYA.
KAKA MICHUZI TUPO KTK WAKATI WA UHURU WA DEMOKRASIA NA UHURU WA SAUTI NINAKUOMBA UIWEKE HII COMMENT HEWANI.
Nilidhani Ikulu ni makao makuu ya serekali na wala si ya chama !
ReplyDeleteAma tumerudi enzi za chama kushika hatamu ?
Mdau Kaima
Yale yaleeeee!!
ReplyDeleteKumbe Chenge bado anashika nafasi CCM?
Jamani kwani vyama vingine vimeenda kuomba kufanyia kikao ikulu vikakataliwa?
ReplyDeleteNi IKULU NDOGO au Ofisi ndogo ya CCM Lumumba? Maana italeta maneno!! Kuhusu nguo za kijani si baadhi ya wazanzibari tuu hata Mstaafu MKAPA huwa pia havai mashati ya kijani nina wasiwasi asije akaingia mitini!!
ReplyDeleteNAWAUNGA MKONO KABISA KUHUSU MAONI YA KUTOKUWEPO USAHII WA KUFANYIA SHUNGULI ZA CCM IKULU. HIVI KWELI CCM HAWANA OFISI YENYE SEHEMU YA KUFANYIA MIKUTANO HAPO DAR? IKULU NI JUMBA LA WATANZANIA WOTE NA SI SAWA KUTUMIWA KWA SHUGHULI ZA KICHAMA. TULIDHANI MAMBO YA CHAMA KUSHIKA HATAMU YALISHAKWISHA, KUMBE...
ReplyDeleteMara nyingi vikao vya Kamati Kuu ya CCM vikikutana hukutania Ikulu. Nadhani si sahihi. hapa ni kutumia rasilimali za Serikali kwa manufaa ya CCM. Sehemu sahihi ya kukutania inatakiwa iwe Ofisi ndogo ya CCm Lumumba au Dodoma yaliko Makao Makuu ya CCM. mbona sehemu hizi hazitumiki? au hazina hadhi? zifanyiwe marakebisho.
ReplyDeleteanyway
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=mT2DwfJUD5M
ReplyDeletejust watch
Vipi wajumbe CCM ZNZ hawana mavazi ya Chama????
ReplyDeleteWakereketwa wa zanzibar tuna sare nyingi sana za ccm ila kuvaa ni kujionesha tu kwani nani hajui km Rais Karume ni CCM na kuvaa nguo si ishara ya kua mkereketwa na hyu hakuanza leo hii inaitwa individual lazima ujitofautishe na wengi jamani duniani binaadam hatuppo sawa kabisa. Km hio haitoshi hakuna kipengele cha katiba cha CCM kinachosema ni lazima tuwe tunavaa sare kwenye vikao vyetu.
ReplyDeleteTuwe makini tunapochangia tunaweza kusababisha mmsuguano.
Nkereketwa Zenji.
MCHANGIAJI 08:14 NIMEKUELEWA, HIVI KUNA CHAMA KILISHAOMBA KIKANYIMWA!!! HEBU TUCHANGIE MAMBO YA MSINGI
ReplyDelete