
Balozi wa China Nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete mipira soka na vifaa vingine ikiwemo baiskeli,pikipiki, chupa za maji na mshine za kushonea nguo kama mchango wake kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko Kilosa mkoani Morogoro
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia viatu vilivyotolewa msaada na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini dar es Salaam leo asubuhi.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko wilayani kilosa,Mkoani Morogoro. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepanda katika pikpiki aliyokabidhiwa na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xingshen kama seshemu ya msaada wa China kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Hafla hiyo ilifanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Misaada mingine iliyokabidhiwa katika hafkla hiyo ni pamoja na baiskeli, chupa za maji na mashine za kushonea nguo.
Rais Jakaya Kikwete akikagua pikipiki ikiwa ni sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na nchi ya China kupitia kwa Balozi wa nchi hiyo Liu Xinsheng (mwenye suti kushoto) kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo nchini. Makabidhiano hayo ya vitu mbalimbali vikiweo vifaa vya usafiri, vifaa vya nyumbani na vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 51 yamefanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam.




(Picha na Fredy Maro Ikulu /Aron Msigwa)
Watanzania tunakilema cha misaada sana jamani, tupende kujitegema wenyewe siyo misaada lika siku!
ReplyDeleteTunawashukuru, lakini robo tatu ni feki
ReplyDeleteWAAFRIKA BWANA...WEWE WAPATIE MIPIRA YA FUTBOLI, VIATU, NA PIKIPIKI, WENYEWE WATAKUPATIA ARDHI YA KUCHIMBA MADINI NA MAFUTA MPAKA YAISHE....AFRIKA TAMBARARE !!!
ReplyDeleteI can't believe our prez is being used for publicity for only Ths 51 million! Ama kwlei umaskini utatupeleka pabaya. Huo msaada ulitakiwa upokelewe na mjumbe wa kama ya kijiji, labda mwenyekiti wa kijiji kama huna shughuli za zingine.
ReplyDeleteaah jamani!! yaani ikulu anaenda KUMUONA RAIS kwa kupeleka chupa za maji na yeboyebo!!! Jamani mnamshusha hadhi JK! jamani wasaidizi ikulu ni mahali patakatifu. Milioni 51!!! Jamani hii fujo sasa! Ukamuone Obama kwa ndala na maji ya Uhai, kwani katibu kata, mkuu wa mkoa na naibu waziri wako wapi!! AIBU
ReplyDeletePlz hivyo vitu vipelekwe TBS kabla ya kutumia.
ReplyDeletesasa apokee mipira ya tanzania wakati hamna muachen apokee tu za pikipiki za mchina mchina oooooyeeeeeee
ReplyDeleteMUUNGWANA Ujeshi keshasahau siku hizi.
ReplyDeleteAmeionea pikipiki kwa sababu iko chini chini na ina matairi mapana kidogo.
Baikeli ameogopa kuipanda kwa sababu iko juu juu na matairi membamba.
Tehe teh tee te!
HAWA JAMAA WANAFAHAMU WANACHOKIFANYA, WANATUPATIA VIATU, MIPIRA, PIKIPIKI ETC HALAFU TUNAWAPA MADINI, ARDHI NA WANAKATA MITI/MAGOGO KWA WINGI "TANZANIA NA CONGO"
ReplyDeleteMisaada na rais Dr Kikwete. What a bleeping shame. Go back to work man.
ReplyDeleteKikwete Mbona hajakamatwa hapo kapanda bila Kofia la kichwa au sababu hajaendesha? hahahaha. Ila mdau hapo juu kasema kweli wa Africa tumepewa hivyo vitu tu basi tunawapo Ardhi ya kuchimba.
ReplyDeleteWow! nilizania Million $51 kumbe ni Tshs million 51 ...Mungu wangu....
ReplyDeleteDisapora mko wapi? Tukijipiga piga tu kikweli kweli hiyo hela ya kumdhalilisha president wetu tunayo wenyewe...
Baada ya snap hao wachina wanaweza kufanya advertising stint in their countries! Huyu jamaa sijui anasomaga hizi comments? Mkulu hatutaki mambo ya misaada ikulu! Tunaomba utusitiri na aibu Mkulu!
ReplyDeleteI luv My Prezidaa.... Very humble and simple. kwani nnini bwana!! hata kama ni yeboyebo mbona wewe hujatoa kitu.... wacheni hizzoooo
ReplyDeletemmmmmh jk hivyo viatu viangalie vizuri maana vinaweza kupewa jamaa zetu na jua la bongo vikayeyukia miguuni
ReplyDeleteI am truly disgusted by the way they have managed to manipulate and use our president extremely well to market their products. I mean, they pay nothing for the nation to know what they are after in this beautiful country of ours. I hate to say that these people, not matter how good they seem to be, what they give is a total humiliation to us all, 51m is nothing worth of a president to waste his people's precious time to receive.
ReplyDeleteWale wadau wanaoona dharau hapa, tafadhali nenda darasani usome nguvu ya uchumi wa nchi: masikini hachagui. Tukifika mbali kiuchumi ndio tutaweza kuringa, tusijitie sisi Afrika Kusini wakati hata madawati na viatu vya shule vya watoto tunashindwa kuwanunulia.
ReplyDeleteRAISI JK HIVI WASHAURI WAKO WANAKWAMBIA KABLA MADHUMUNI AU UNASTUKIA WAMESHAKARIBISHWA NDANI? KUNA KAMATI YA MAAFA AMBAYO IKO CHINI YA WAZIRI MKUU KUNA WASAIDIZI WAKO, KUNA MAKAMU WA RAISI HIVI KWELI WANAINGIZA PIKIPIKI HADI NDANI SITTING ROOM? BASI ANGALAU WANGEZIACHA HAPO UWANJANI KAMA ZILE PIKIPIKI ULIZOLETEWA JUZIJUZI?HII NI AIBU KUBWA SANA, LAKINI MAKOSA NI YA WATU WAKO NA NDIO MAANA HATA SIKU HIZI UNAKONDA KWA MAWAZO POLE MZEE MZIMA. NAOMBA UYAREKEBISHE HAYA WATAKUPANDA HADI KICHWANI NIDHAMU IKULU IMEPUNGUWA
ReplyDeleteSijui nicheke, sijui nikae chini nilie..............
ReplyDelete