Ankal,
Hii ni harakati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhifadhi mazingira kwa kuwakamata na kuwaangamiza ndege aina ya kunguru ambao imekuwa ni kero kwa jamii na hata kutishia kupoteza aina nyingine ya ndege (species).

Inasemekana ndege hawa (Kunguru) ambao wanaishi muda mrefu kuliko ndege wa aina yeyote hadi kufika miaka mia (100yrs) walioletwa visiwani humu mwaka 1890 kwa lengo la kutumika kama scavenger , lakini sasa wamekuwa wanaleta bugudha kwa kuharibu mazalia ya ndege wengine, kuharibu mazao na pia huchangia katika kuleta maradhi ya mlipuko kutokana na tabia zao.

Kwa kuliona hilo SMZ chni ya mradi wa MANCEP wameanzisha vita dhidi ya ndege hawa ikiwa ni muendelezo wa mradi kama huu iliowahi kufadhiliwa na Serikali ya Finland katika miaka ya nyuma ambao ulileta mafanikio makubwa kwa kiasi fulani.

Mtego uliopo pichani unaonesha "wadau" wakiwa tayari wamenashwa katika mtego uliopo AMAAN INDUSTRIAL PARK (Viwanda vidogo vidogo), mtego ambao kwa mujibu wa wataalam wa Kunguru umeshanasa karibu kunguru 250 tokea tarehe 16/12/2009 mpaka sasa. (takwimu hizi haziusishi walioko kwenye mtego sasa)

note:tarehe inayoonekana kwenye picha
ni kutokana na settings za camera
Mdau Ibra wa Zenji
Kunguru tunduni
hatoki mtu hapa
mtego






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. hawa ndege ni wasumbufu sana,na kadiri wanavyoishi mahali wanajifunza mazingira na kuwa na akili sana,wanatumia akili kuliko unavyoweza kudhania uwezo wao.
    kunguru wanavituko pia,kuna mmoja aliwahi kuninyea maeneo ya hapo kinondoni vijana wakati nasubiri daladala.hahaha
    kunguru mwoga huficha lake bawa,ndege mjanja hunaswa na tundu bovu. JE WEWE PIA NI NDEGE MJANJA ktk maisha hasa ya NGONO?oohhh:-)))
    bora uwe kunguru mwoga!vinginevyo kama kila ukiona laptop unataka kuanza ku google,na ikikosea ikafungua page tu basi unachomeka flash yako na kuanza kuinstal xp!!unazidi kujaza GB tu hukumbuki kuwa unaweza lamba trojan horse! bora uwe mjinga,ukishindwa basi instal kwa CD na uhakikishe kuwa antivirus sio outdated:-))))
    kinyogoli.

    ReplyDelete
  2. Mkuu!
    hiyo picha moja maelezo yake inasema "hatoki mtu hapa" nilidhani ingetakiwa kuwa hatoki KUNGURU hapa.Au ni aje?
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  3. Anon Wed Mar 03, 10:03:00 PM,

    Hatoki mtu hapa maana yake hao jamaa wanaowafuga ni kwa interest zao tu, sio kwa ajili ya kutoka(kupata pesa kihivyoo).

    Umenipata

    ReplyDelete
  4. "wadau" wakiwa wamenaswa, ha ha ha

    ReplyDelete
  5. Hawa kweli ni waharibifu wakubwa sana. Lakini kuna mbinu nyingi za kuwafukuza wasikusumbu wakiingia kwenye banda la kuku wanakula vifaranga vyote washenzi hawa. LAKINI UKIWA NA KIOO UKIELEKEZA UPANDE WAO ILI KUSHARABU AMA KUHAKISI MWANGA (Yaani jua lipige hapo kwenye kioo na mwanga kurudi upande wao) wanakimbia vibaya sana hawatakaa warudi hapo hata kidogo. Ingawa suluhisho ni kuwaua lakini na hii inasaidia kwa muda kwani ni wasumbufu sana washenzi hawa

    ReplyDelete
  6. Kunguru Hafugiki!!!

    ReplyDelete
  7. Katika zoezi hili tukumbuke haki za ndege/wanyama kwa kutafuta namna bora ya kuwaangamiza ili tusije shitakiwa kwa kosa la ukatili dhidi ya ndege. Hivyo basi, nashauri utafiti ufanyike au tunaweza kuomba uzoefu wa Wachina (wazee wa kula kila kiumbe) ili ikiwezekana na kama wanafaa wawe wanagawiwa kama kitoweo. Ni suala la ubunifu na kuthubutu tu. Hii kuwaua tu tutapoteza muda wa kuwafukia na hata kuongeza nzi bure kama hatutakuwa waangalifu katika kufukia mizoga yao. Simaanishi iundwe tume.

    ReplyDelete
  8. wadau hapo juu mmechemsha "hatoki mtu hapa " ni hao kunguru humo ndani walimofungiwa hawatoki ng'ooo ndo maana hayo maneno yako chini ya picha kudhibitisha hatoki mtu hapo na wala sio ati hao jamaa hawapati kitu sijui nini na hii ni misemo ya humu bloguni sawa eeeh hajakosea mtu hapo!!! hii ni mbinuya kukufanya wewe mdau ucheke unenepe

    ReplyDelete
  9. asa mbona kuna sahani ndani ya mtego? ina maana wanawalisha?

    ReplyDelete
  10. wewe Anonymous wa Thu Mar 04, 10:42:00 AM, tumia akili, sahani nayo ni sehemu ya mtego

    ReplyDelete
  11. ok hii picha imenikumbusha nyimbo ya zamani kwetu zanzibar:

    kungure ndege laghai
    ana tabu kumnasa
    hata ukifanya rai
    weka mbele kumkosa.

    ReplyDelete
  12. enzi za ujinga pale zenji ndege huyu alikua akiwindwa kwa bunduki afanaaleik.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...