Bw. Allan Sugar

Stay tuned, I'll be back in June
KIPINDI cha TV cha The Apprentice UK kawaida huonyeshwa kila mwezi wa tatu (Machi) kila mwaka katika kanati (channel) ya TV ya BBC London.

Kipindi ambacho huchagua mfanyakazi bora baada ya kupitia wiki takriban 12 katika washindani 12 au 13 ambao wanagombea nafasi moja ya kuwa The Apprentice wa kufanya kazi katika kampuni mojawapo ya makampuni ya bosi wa kipindi hicho Sir Alan Sugar kwa mshahara usiopungua £100,000 kwa mwaka.

Kipindi hicho mwaka huu kimehairishwa badala ya kurushwa hewani mwezi Machi 2010, kitarushwa hewani mwezi Juni 2010 kwenye kanati ya BBC kwa kinachosemekana kuwa kipindi hicho kifanyike baada ya uchaguzi mkuu wa kitaifa wa UK wa mwaka 2010 ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Mei 2010.

Bwana Alan Sugar alipoulizwa na waandishi wa habari wa gazeti la "The Mirror" maoni yake kuhusu kuhairishwa kwa kipindi hichi mpaka Juni 2010 badala ya kuwa Machi 2010 alisema, “They’ve delayed it for some political reason which is a bit of a joke in my opinion."

Sir Alan Sugar hivi karibuni (2009) amechaguliwa na serikali kuwa mmoja wa mabwana "Lords" katika kuchangia fikra za kiuchumi nchini UK.
Mwaka jana mmoja wa aliyeshiriki katika mashindano ya kufanya kazi na Sir Alan Sugar alikuwa ni Mtanzania MONA LEWIS.

Zenjydar Community Association
www.zenjydar.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hapa nimejifunza msamiati "kanati" ikiwa na maana ya channel. Vizuri sana. Najishangaa ni mtoto wa kitanzania lakini nilikuwa sijui channel kwa kiswahili inaitwaje.
    Big-up Anko Michuzi kwa kutuhabarisha.

    ReplyDelete
  2. no news is good news. Sasa hii post inasaidia nini globu ya jamii?

    Afadhali ungeandika kipindi cha akina Zecomedi, kimeahirishwa na unatoa taarifa

    Ze apprentice ? zey don't help us.

    Mzee wa Tanangozi iringa

    ReplyDelete
  3. Samahani labda sifahamu vizuri hii habari inatusaidiaje sisi wananchi wa Tz?Ghrrrrrrrrrr watu wengine bana siyo kila habari ukiona huko unaleta hapa kaa tafakari na siyo kukurupuka tu!ah

    ReplyDelete
  4. Hii habari inahusiana nini na Tanzania? Camon now! Acheni kumtumia Michu kila kitu.

    ReplyDelete
  5. watu waache lawama kwani habari zinzotolewa humu ni za tanzania peke yake?mbona kuna habari za dubai mafuriko hamlalamiki?wacheni zenu wabongo huu mtandao huria ukiwa nalako popote unakaribisha kulileta hewani.wacheni choyo

    ReplyDelete
  6. Hivi mmesahau kuna tawi la CCM hapa London. Naona CCm inajiandaa kuanza kuboresha miundo mbinu ya hapa London. Tanzania Taifa kubwa ati?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...