Charles Hilary wa BBC

Na Freddy Macha, London

Wapo baadhi ya wasomaji wa blogu hili la jamii waliolalamika kwamba kongamano la Watanzania Uingereza (London Diaspora Conference) wikiendi iliyopita halikuwa na maana yeyote. Labda upo kweli; labda hamna.
Maelfu ya wataalamu wanaishia nchi za nje huku ujuzi wao ukihitajika sana nyumbani. Akili zao zinaishia chini; lakini si kwamba hawaijali Bongo yetu. Madhumuni ya kongamano la London yalikuwa kuangalia mustakabal wa wananchi hawa. Jamii yetu changa inahitaji utaalamu wao.
Tuyaache hayo, kwanza.
Moja ya mada iliyowasha sana sigara, ilikuwa suala la Mtanzania na pasi mbili (“dual passport” au “dual citizenship”). Wakati mkutano huu mahsusi ukiendelea baadhi ya wazungumzaji waishio huku Uzunguni walisikika wakisema : “Uraia Mbili” ama “ Uraia Miwili” (du!!!), “Citizenship mara mbili”, na “Uraia mara mbili”..... lakini.... URAIA PACHA ilikuwa kiboko.

Aliyestawisha nahau au msemo huu si mwingine bali mtangazaji wa Kiswahili, Idhaa ya BBC, Charles Hillary, ambaye aliteuliwa kuwa mchangamshaji (MC) wa makutano. Na katika wadhifa huo mboreshaji huyo wa Kiswahili Mama (Kiswahili Babu) akasaidia kutangaza neno jipya la Kiswahili fasaha yaani :
URAIA PACHA.
Kiswahili ni lugha inayokua; isiyolala; lugha askari; yenye mabawa : mbayuwayu, yange yange; duma mwenda mbio; jogoo asiyechoka kuwika; vigelegele; lugha moto ya Waafrika.
Hongera kaka Charles Hillary.

Barua pepe: kilimanjaro1967@hotmail.com
Blogu: http://www.kitoto.wordpress.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hayo masuala ya ujuzi ni porojo na hoja ya kisiasa ambayo haina maana yeyote mbona hapa ndani ya Tanzania kuna watanzania wengi wenye ujuzi na uzoefu wa kazi lakini serikali haiwatumii, wamesoma nchini na wengine wamesoma nje na kurudi nchini. Tatizo la Tanzania sio ujuzi ni siasa kwani siasa ndiyo inakula bajeti kubwa, mawazo ya watanzania wengi yako kwenye siasa na maauzi ya nchi hii yanafanywa na wanasiasa kwa manufaa ya kisiasa zaidi

    ReplyDelete
  2. Ankal, tunaomba tuwekee hizo presentation au hotuba ili nasi tuzione na kudiscuss, pia ukiweka na ka-clip ka presenation yako kwenye Diaspora 2 siyo mbaya

    ReplyDelete
  3. kabla sijaongea sana niwaulize diaspora:

    kwanini mlikua mnaongea KIINGLISHI?ata hotuba ya nani yule nimesahau ilikua nje ya lugha yetu tukufu kiswahili
    1.ina maana kuna diaspora hawajui kabisa kiswahili?
    2.kudharau lugha ya nyumbani-kiswahili?
    3.hamjawai ingiliana na wabongo wezenu mjifuze lugha/kujikumbusha ili isisahaulike kwenu?
    4.hakuna mahali pa kujifunza kiswahili ili muendeleze utamaduni?

    me nimekaa nje sijawai sahau kiswahili labda maneno yaliyokua ss,napo nilijitaidi sana kutafuta news thr net..MMEBOA SANA

    ***nikirejezea wenzetu waisrael-mfano,wakorea,wachina,waarabu nk ambao wameishi karne na karne nje ya nchi mama na HAWAJAWAI SAHAU LUGHA YA KWAO vizazi toka enzi

    ReplyDelete
  4. Nimemuota Baba wa Taifa mwl J.K. Nyerere, na tuliongea yafuatayo (ndotoni)

    Mi naona bana ze double-dual-pacha mbili raia cizitensheep mambo ya kizamani. Ze peeplo need to be more patriotic and commitmented to theyr country.

    Huwezi kutumikia two masters at the same time. Je nchi yako Tanzania ikiwa kwene vita na huko unakobebea maboksi utapigania upande gani?....

    Nyie bana kaeni uko Ulaya...tuachieni Tanganyika yetu. Msiludi kuja kututesa huko na vitu vya ulaya....hii siyo vacation spot folks, If you wanna come visit we will treat your backsides as a visitor....you wanna go to Ngorongoro, you will be charged as a tourist. And don't you dare to overstay....Mgambo is going to get you out! No more free rides. By the way, when you get old and you can't do all that hard work anymore....stay where you are at (Nursing homes). Tanzania is not a senior assisted living facility. We need young energetic productive citizens now. Sio vibabu na vibibi vilivyotusaliti.

    Kha! tupigwe na jua kujenga nchi yetu afu mje kula kiulaini tu! I say Hell No!

    LOL ay that was a joke.

    ReplyDelete
  5. I have a simple question to all those who were involved in this meeting: What was either achieved or agreed on this meeting?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...