Katika kuashiria kuwa bodi na wanafunzi wa Kitanzania nchini Algeria ni damu damu kwa sasa, mhasibu mkuu wa bodi (wapili kushoto)na ujumbe wake alipata lanchi ya usiku viongozi wa ATSA. Mhasibu mkuu wa bodi ya Mikopo Bw. Adbullah KHATIB(katikati mwenye suti nyeusi) na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi baada ya kikao na wanafunzi hao
Mhasibu mkuu wa bodi ya mikopo (wa tatu kutoka shoto)akipokea dosia za ki-benk kutoka kwa mwanafunzi Said LUE ambaye mpaka leo hii hajapata pesa zake za kujikimu huku makamu wa rais wa ATSA Habibu RUHOMBO(wa nne toka shoto)akishuhudia mhasibu mkuu ameahidi kulishughulikia tatizo hilo mara tu atakapo rudi tz kwa sababu lipo ndani ya uwezo wake.
Kwaherini!!!mhasibu mkuu wa bodi akikaguliwa na afisa wa airport tayari kurejea nyumbani.ujumbe huo umeondoka Algeria j’mosi na kufika tz juma3 ucku.
Makamu wa rais ATSA Bw. Habibu Ruhombo akimsikiliza kwa makini mkaguzi wa serikali Bi. Mwajuma Sepetu pindi waliposindikizwa airport .

ASSOCIATION OF TANZANIAN STUDENTS IN ALGERIA (ATSA) wikiendi hii ilibahatika kutembelewa na ujumbe mzito kutoka bodi ya mikopo ukiongozwa na mh.ABDALLAH SALUM KHATIB -mhasibu mkuu wa bodi hiyo akiambatana na Bi.Mwajuma Seleman Sepetu na Bw Deogratius Patric Mtenga -wakaguzi wa pesa za serikali(NAO).

Ujumbe huo umetembelea ALGERIA ukiwa na lengo la kuhakiki kuwa pesa za umma zina wafikia walengwa, mbali na lengo hilo ujumbe huo ulipata fursa la kuongea na wanafunzi hao kwa kuwaeleza juhudi zinazo fanywa na bodi katika kuhakikisha pesa zinawafikia walengwa kwa wakati mbali na matatizo yanayo jitokeza ya hapa na pale.

ATSA kwa upande wake ikiongozwa na Seif PEPO akisaidiwa na Habibu H.RUHOMBO viongozi wengine imeridhika na kuyasifia majibu na maelezo yaliyo tolewa na mhasibu huyo mkuu wa bodi mh.Khatib.

Wanafunzi hao walibahatika kumuuliza Mhasibu huyo matatizo mbali mbali yanayowakabili wanafunzi hao yakiwemo ucheleweshaji wa pesa hizo na mengineyo,wanafunzi wote walitoka kwenye kikao hicho wakiwa na furaha tele na imani kubwa kwa bodi pale waliposikia kuwa wakubwa wa bodi wapo kwenye mchakato wa kuongeza boom kwa wanafunzi.

Ugeni huu umesaidia kurejesha imani kubwa iliyokuwa imetoweka kati ya wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Algeria na bodi hiyo muhimu.
Aidha, Kigogo huyo wa bodi na ujumbe wake wamefurahishwa kuona kuwa ALGERIA hakuna wanfunzi hewa kama vile ilivyokuwa ikifikiliwa. Pia amekishukuru chama cha wanafunzi(ATSA), kwa ushirikiano mkubwa walio uonesha katika kukamilisha lengo la safari yao.
Imetolewa na idara ya mawasiliano –ATSA
SIMU: Rais wa ATSA (Seif PEPO) - 00213 554 333 727
Makamu rais wa ATSA (Habibu H.RUHOMBO) -00213 551 71 3920


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Duuh lanchi ya usiku hii kali.
    Mdau
    Kisiju pwani

    ReplyDelete
  2. Kwani hawa jamaa wa bodi ni lazima waende huko Algeria? Hakuna ubalozi wa TZ hoko mimi naona hayo ni matumzi mabaya ya fedha za serikali,hiyo kazi ingeweza kufanywa na ubalozi wa TZ huko.

    ReplyDelete
  3. mpenzi mbona sikuoni hapo????pliz unajua iyo nchi ilivo kaa na wenzio

    vipi ilikua siku ya pepa nini jamani?

    ReplyDelete
  4. HERI YENU WATU WA ALGERIA.HUO UGENI UJE NA HUKU URUSI JAMANI TUNAOMBA BODI WATUKUMBUKE NA SISI WAJE WASIKIE VILIO VYETU,WANAFUNZI TUNAOSOMA URUSI TUNA MATATIZO MENGI YAHUSUYO BUM,KWANZA HUWA PESA ZINACHELEWA KUPITA KIASI,PIA PESA HAZITUTOSHELEZI KWA MAISHA YA HUKU MORE THAN EXPENSIVE,KAMA IJULIKANAVYO JIJI LA MOSCOW LINAONGOZA DUNIANI KWA KUUZA BIDHAA EXPENSIVE,NA KILA MWAKA VITU VINAPANDA BEI.HUU UONGOZI TULIONAO MADARAKANI UKIONGOZWA NA BWANA ISAAK HAWAFATILII KWA UKARIBU MATATIZO YETU,PRESIDENT WETU HAJIAMIN NA KILA KITU ANAAMUA YEYE.LICHA YA UHUSIANO MZURI TULIONAO SASA NA UBALOZI LAKINI WANASHINDWA KUTUSAIDIA TUONGEZEWE BUM ILHALI WANAJUA HALI YA MAISHA YETU.OMBI NI KWAMBA WATU WA BODI TUNAWAOMBA SIKU MJE MTUTEMBELEE NA SISI TUNAWAHITAJI NA TUNA SHIDA NYINGI SANA.
    MPENDA AMANI NAWAKILISHA.
    BIG UP BLOG YA JAMII.

    ReplyDelete
  5. Hamna kitu....mbona hela zetu hamjatupa nyie watu wa Bodi? Kwa taarifa yenu tunajua kinachoendelea na siku si nyingi mtajibu kwa JK, oohoo shauri yenu.

    Mdau, China

    ReplyDelete
  6. Watu kwa kupenda kulalamika bwana.
    Kuna wanafunzi wako malysia, India na kwingineko, hawalipiwi fedha za kusoma na hawajalalamika kiivyo.
    Nyinyi mlio Urusi kuweni na akili, mnalalamika sana kila siku. Watu mko Moscow lakini mtafikiri mko manzese. Kwani hizo degree mnazosoma hazipo Algeria, ili muhamishiwe huko mkamalizie hizo degree zenu.

    ReplyDelete
  7. Hi Mary Ligunda,
    I can see you. Hongera sana. I guess I am seeing you correctly, right? Wanawajali sana serikali yenu, kwakweli.
    Best wishes with in your studies,
    M.M.

    ReplyDelete
  8. heee kale katoto kako algeria au machoyangu....kuweni makini huko algeria lol!!masomo mema!!

    ReplyDelete
  9. kuna mijitu mingine lazima iongee tu hata kama ni pumba, we mdau wa pili nani kakuambia kule ALGERIA kuna ubalozi wa Tanzania?wacha mara moja kuifundisha serikali kufanya kazi zake tena chunga sana mdomo wako kabla hatua za kinidhamu hazijachukuliwa juu yako." ooooh matumizi mabaya ya pesa za serikali "we unataka serikali ikununulie nguo za ndani ndio uone inatumia pesa kihalali?wanfunzi wa ALGERIA wametuwakilishia mtatizo yetu sote yanayotukabili wanafunzi wote wa tz tunaosoma nje ya nchi wee viipii!!!!.one, two three ,viva l'Algérie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...