Simba SC Ughaibuni
YANGA FC Ughaibuni

Mpambano wa Yanga na Simba mgeni rasmi kutoka ubalozini,homa yazidi kupamba mashabiki wazidi kutambiana,Rashidi Mkakile(Bamchawi) mpaka sasa hivi hajatamka lolote kuhusiana na huu mpambano ambapo Simba watauchukulia kama mpambano wa kulipiza kisasi,katika pambano la mwisho September 6 2009 Simba ilibanjuliwa 6-2 dhidi ya mahasimu hao wa jangwani.

kwa sasa timu zote zipo kwenye mazoezi makali tayari kwa mpambano huo,Simba inaonekana kubadilisha kocha na kuita wachezaji wake wa mikoani kuja kusaidia kuokoa jahazi,kocha Kenyata(Patrick Phiri) ambaye anadai amekuja na mbinu mpya kuitungua Yanga,alisikika akisema Yanga safari hii wasitegemee mteremuko,kipigo watakachopata hawata kisahau,aliendelea kusema anawasiliana na kocha wa Simba takribani kila siku akimpa mikoba ya kuifunga Yanga,

Mpambano huo wa kukata na shoka utachezwa jumapili April 4 itakua ni zawadi nzuri ya pasaka,kwa mshindi na washabiki wake,mechi itachezewa wanja jipya la 1417 Kalmia St,Nw,Washington Dc,

kocha wa Yanga Yasini Randi amesema anasikia Simba wanaleta wachezaji kutoka mikoani,Simba hata walete wachezaji toka mbinguni hii ndio Yanga kiboko ya Simba safari hii watalia,watakiona cha mtema kuni,mwaka jana huyo Bamchawi alikimbia uwanjani baada ya bao la 4 mpira ulipokwisha hakuonekana uwanjani,safari hii namuonya asifike uwanjani anaweza akazimia au akija aje na maji akianguka ajimwagie.

Jumamosi April 3 kutakua na mechi nyingine ya Stars na Maryland untd lakini mechi hii haizungumuziwi kabisa na habari zisizokuwa rasmi viongozi wa Yanga na Simba wanataka kuwazuia wachezaji wao waliomo Stars waikache mechi hiyo kwa madai mechi hiyo sio muhimu na itawafanya washindwe kucheza vizuri kwenye mechi ya Yanga na Simba.

Kiongozi wa TFF ya ughaiubuni ambae hakutaka kutajwa jina lake ameonya kama habari hizo ni za kweli basi kiongozi atakaye husika na mchezaji atakaekataa kuripoti kambi ya Stars atakua amejifungia mwenyewe,hataruhusiwa hata kufika uwanjani siku ya mpambano na kiongozi atakae husika kupigwa faini $500 na mchezaji $300

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...