Profesa J, The Heavy-Weight MC of Tanzania


Ukisikiliza wimbo huu wa Prof.Jay (the heavy Weight- Mc) utakutana na yote ambayo yanatokea sasa si tu katika serikali yetu bali pia katika sehemu ya maisha yetu ya kila siku.
Sasa kijana kama Mnyika anapotaka kuchukua hatua, waosha vinywa na wasiofikiria wanaibuka na kuleta hoja za ajabu halafu huyo ndo anayetegemewa kwa ushauri nyumbani kwao (Kuku hauzwi mpaka aseme yeye). Shame upon you!
Big up Prof.Jay, na wasanii wengine wafuate mfano wako sio kila siku nyimbo za mapenzi tu, mapenzi na njaa tumboni wapi na wapi?
Kwa wimbo huo ambao hamjausikia, tembelea.
http://www.bongocelebrity.com/2010/03/06/msilie-prof-jay-ft-chid-benz/
Mfuatiliaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. patachimbika tz mafisadi jiandaeni madogo hawataki longolongo

    ReplyDelete
  2. Hivi Michuzi hao vijana wenu wa kibongo flava wanapovaa majaketi na nguo za baridi hapo bongo wanajisikiaje kichwani mwao?

    ReplyDelete
  3. Mdadu namba 2, hivi wewe umewahi kufika Mufindi na sehemu nyengine za nyanda za juu?

    Nenda ukajionee mwenyewe kibaridi cha kiwinter usidhani winter iko Ulaya tu.

    Fika Mufindi mwezi huu wa Machi halafu usiku jaribu kutembea na ka T shirt kama utaweza!

    ReplyDelete
  4. Go Prof.Jay Go!

    Nime-replay single hii mara 15 at a time. Unaweza lia hayo yaliyomo katika wimbo huo.
    Nimeipenda sana kazi yako, yaliyomo humo ni mazito. Pro.Jay huwa hauchuji siku zote. Ni kama vile chemsha Bongo kabla hujapagawa au Bongo-Dar es Salaam.
    Hii ni kweli changamoto kwa wasanii ya kibongo. Natabiri huu wimbo utatumika sana wakati wa kampeni ukifika. Ankal tunapenda maada za kujenga kama hizi, ila inasikitisha pia kuona watu wanaibuka na yao kuhusu makoti, ni kweli mtu kama huyo ndo anayetegemewa kwa ushauri kwao (Kuku hauzwi mpk atoe yy ushauri) akifika hapa anafanya utoto, namaanisha nje ya mada!

    Mdau Germany

    ReplyDelete
  5. mleta mada acha longolongo,sasa kila anayojitokeza kugombea aungwe mkono kisa kijana,kwani kina masha na ngeleja si vijana,acha kubadilisha mada,tatizo la mnyika always anadandia vitu kwa juu,umoja wa mataifa umepata report kuhusu mgogoro congo yeye kaindandia juĂș juu tu,baadae umoja wa mataifa umesema sio wao wanausika na taarifa ile bali kikundi kidogo kinachofanya kazi na un,tatizo la dogo anataka kuiga watu,hayuko yeye mwenyewe,mbona zito tunamkubali sana tu,kwa sababu anaongea anachoonya yeye,yuko radhi hata kuwa tofauti na chama chake,mnyika zero,hakuna kitu analongolongo mingi tu hakuna kitu,zito ndo kijana wa kujivunia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...