MPENDWA WETU HAMIDU
AHMED BISANGA(Hambis)

Ni siku, miezi na sasa mwaka tangu ututoke ghafla kwa ajali ya gari mnamo tarehe 29 march. Ni vigumu kukusahau tunakukumbuka daima kwa upendo, busara na hekima zako. Hakika hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu yeye ndo muweza ya yote.

Unakumbukwa sana ma mkeo mpenzi bi Tunu,watoto,mjukuu wako Alma,ndugu,jamaa na marafiki. Kila siku tunakuombea kwa Allah akusamehe dhambi.

Tunakupenda sana baba.
Inns lillah waina ilayhi rajiuum.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Duu, Hamidu Bisanga; namkumbuka sana miaka ile bado vijana; yeye na kipikipiki chake na miye na changu. Yuko Daily News, miye Uhuru na Mzalendo miaka ileeee ya Sabini; mcheshi mcheshi, siku zote anatabasamu.
    Hana makuu.
    Watu wa ina hiyo ndiyo huwa rahisi kupata, kuandika na kufahamisha habari.

    ReplyDelete
  2. Raha ya milele umpe ee bwana. kaka yetu mpendwa apumzike kwa amani AMEN

    ReplyDelete
  3. Rest in Peace dear friend, you will always be missed and remembered.

    ReplyDelete
  4. Tunamuomba Muumba amlaze Hamidu mahali pema peponi. Nawawapa pole wanafamilia wake. Tuliobahatika kumjua tutamkumbuka kwa ucheshi wake na upendo wake kwa watu.

    ReplyDelete
  5. Tunamuomba Muumba amuweke Hamidu mahali pema peponi. Pia nawapa wanafamilia yake pole tena. Tuliobahatika kumfahamu Hamidu tunamkumbuka kwa ucheshi wake na upendo wake kwa watu wote.

    ReplyDelete
  6. Is as if msiba umetokea leo kwangu,namkumbuka sana, alikuwa ni mshauri mzuri, nilipofikia leo hii ni pamoja na ushauri wake, alinishauri mengi bila shaka M/Mungu anajua zaidi, rest in peace my dear brother!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...