Habari ya kazi ankal,
Ninaomba uniwekee hii katika blog yako ili wahusika waweze kusikia kilio chetu.Mimi ni mkazi Tegeta Salasala karibu na IPTL, kero yangu mimi pamoja na wakazi wa maeneo haya ni hili generator la kufua umeme wa gas mali ya TANESCO, kusema kweli tunapata kero kubwa sana kutokana na makelele yasiyokuwa na kikomo ya hili generator.
Kuanzia mwaka jana mwezi wa kumi na mbili walipoanza kuliwasha imekuwa taabu sana kwa sisi wakazi wa maeneo haya kwani mchana kutwa, usiku kucha ni muunguromo/makelele/mtikisiko ambayo imepelekea nyumba nyingi kupata nyufa kutokana na mtikisiko huu mkubwa.
Tunawaomba wahusika, Tanesco, na wizara husika waliangalie hili kwani hata watoto wetu wadogo wengi tumewahamishia kwa ndugu kwani makelele haya yanaweza kuwaletea madhara hapo baadae, pia usiku tunashindwa kulala kutokana na makelele.
Hivyo ombi letu tunaomba kama kuna uwezekano wa kurekebisha hii mitambo ili isipige makelele pamoja na kuondoa huu mtikisiko kwani na sisi tuna haki ya kuishi kwa amani na utulivu.Tafadhali usiibanie hii kwani ni muhimu. ( email yangu usiiweke) asante

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ni bora hameni kwenye eneo hilo kwani afya zenu ni muhimu sana kwenu na sehemu za kukaa ni nyingi. Ni budi mjue kuwa nasi kamwe hatuweziishi bila umeme.

    ReplyDelete
  2. Hapa nashangaa wabongo.sijui mnasubiri nini kuchukua hatua once and for all kukomesha tabia hizi za kufanya mambo bila kuangalia athari kwa wengine...kesi rahisi sana hii,hakikisheni kila kitu mna document kuanzia uharibifu wa mali zenu mpaka mazingira yenu na mtafute lawyer mzuri,na msiishie kudai waondoe kelele zao lazima mshtaki na kudai fidia kwa jinsi walivyoharibu maisha yenu,siasa basi na makelele yasiyo na mpango ni NO...action sasa!

    ReplyDelete
  3. Badala ya kulalamika anzeni mapema kuhama au mnangojea mlipukiwe nini?!Au mpaka mbomolewe nyumba?!
    Wenzenu Mbagala na Ukonga hawakuhama cha moto wakakiona na kule kipawa nako sasa ni mbio hukohukona huko wakati ilishajulikana siku nyingi kwamba wako kwenye hifadhi ya kiwanja!Wabongo bwana kazi kwelikweli!

    ReplyDelete
  4. TANZANIA ni nchi kuubwa sana, acheni kelele hameni hapo kaanzeni upya maisha sehemu nyingine, sie tunaytaka maendeleo kama hivyo kupata umeme, na maendeleo hayaji bila matatizo, ONDOKENI HAPO na hakuna kudai fidia, serika;li haina hela za mchezo.

    ReplyDelete
  5. Acheni kudeka ninyi! Mbona sisi huku Sinza,Kinondoni,Ubungo nk kelele kibao hatujaadhirika??Maeneo yapo mengi fanyeni hima kabla jirani zetu wa isti africa hawajakuja kuyatwaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...