Juu na chini ni washiriki katika mafunzo elekezi kuhusu usajili wa vizazi,vifo na ndoa yanayofanyika kwa siku 2 kuanzia leo katika hoteli ya New Dodoma Hotel mjini Dodoma.
Mafunzo haya yamefungulkiwa asubuhi hii na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mh.Oliver Mhaiki na kushirikisha makatibu tawala wa wilaya za Tabora, Dodoma, Morogoro na Singida pamoja na wasajili wasaidizi wa shughuli za vizazi,vifo na ndoa. Kaimu Mtendaji Mkuu wa RITA Bw.Phillip Saliboko, Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa haki za kisheria-RITA Bi. Emmy Hudson pia wapo kusimamia na kuratibu mafunzoi haya muhimu.



Mgeni rasmi (suti ya kijivu, kati) akiwa na uongozi wa
RITA pamoja na washiriki katika mafunzo hayo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ni faraja kuona RITA mmajitahidi kuelimisha umma na vyombo mbalimbali kwani Shughuli zenu zitafanikiwa kwa kiwango kikubwa kama hilo litafanyika. Aisee msisahau kupiga ule mziki wa RITA alioimba Bw. King Kikii katika siku ya kufunga mafunzo. Alafu nadhani ule mziki unaweza kuelimisha sana watu kama utakuwa unapigwa na vyombo vyetu vya habari kwani hata ladha ya utamu ipo.

    By Mdau.

    ReplyDelete
  2. Hawa watu wanaonyesha wako na mawazo mengine na confidence zao ziko chini. Sijui kama walifuatilia vizuri hii warsha.
    Mambo ya perdiem. Bongo kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  3. Hawa RITA hawana tatizo kama baadhi ya Taasisi za Serikali. Wala sijawahi kuwasikia wakikimbizana na maworkshop lukuki wakati kazi yao ni serious sana. Mimi nawapa RIOTA big five na waendelee na utaratibui wao wa kusimamia na kutekeleza sheria za nchi katika eneo lao. tafadhalini msikaribishe ufisadi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...