Mafuriko jijini Dar baada ya mvua kubwa kunyesha
Na Benjamin Sawe -Maelezo
Mamlaka ya hali ya hewa nchini imezishauri taasisi mbalimbali kuwa makini na athari zinazoweza kuletwa na mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Haya yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Agnes Kijazi alipokuwa akiongea na wanahabari kuhusu mwelekeo wa hali ya mvua za masika katika kipindi cha mwezi Machi na Mei 2010.

Bi Kijazi alisema kutokana na mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa vina vya maji kweye mabwawa na mito.

Hata hivyo Bi Kijazi alisema rasilimali iliyokuwepo katika maeneo yenye uhaba wa mvua yatumike kwa uangalifu mkubwa.

Pia alizishauri kamati za maafa kuchukua hatua muafaka zitakazokabiliana na athari zitokanazo na na mafuriko,mmomonyoko wa ardhi na uharibifu wa miundombinu katika sehemu zinazotarajiwa kupata mvua za juu ya wastani.

Akizungumzia Sekta ya Afya Bi Kijazi alisema kuna uwezekano mkubwa wa milipuko ya magonjwa ya kipindupindu na malaria kwenye maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani hususani maeneo ya kanda ya Ziwa na mikoa ya magharibi mwa nchi.

Alitoa angalizo kwa jamii kuwa mwaka huu ni mwaka wa El Nino na kusema kuwa haitarajii kuambatana na mvua kubwa kama za mwaka 1997/98 kwa sababu viashiria havionyeshi mwelekeo wa ongezeko la joto la maji ya bahari magharibi mwa bahari ya Hindi.

Pia kupungua kwa joto la maji ya bahari katika maeneo ya Indonesia huchangia kuleta mfumo wa ongezeko kubwa la mvua katika miaka ya El Nino.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hali ndiyo hii huku matawi ya chama yanafunguliwa ulaya sasa!!!!!eti wapinzani hamna hoja!!!

    ReplyDelete
  2. kwa nini tusitengeneze vifaa vya kuyavuna hayo maji ili ukame ukitokea tunayatumia kuendesha mitambo ya ugavi wa umeme! Mungu katupa neema sisi tunalalamika eti mafuriko!!!

    ReplyDelete
  3. Asante nambari wani.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  4. Hii noma!

    ReplyDelete
  5. tumeona wapi mtu kujenga nyumba asiwe na choo kwenye nyumba...ndio haya ndio tunayoyaona...kujenga barabara kushindwa kuweka njia za mitaro....wanajadili mambo ya yajuu yanashindwa madogo....KWA MWENYE AKILI MALARIA HATOISHA KATU KWANMNA HII TZ.

    ReplyDelete
  6. Bongo tambarareee! tutaendelea kukanyaga vinyesi mjini hadi lini?

    ReplyDelete
  7. HAYA SI MAFURIKO BALI NI MAJI YALIYOTUWAMA BAADA YA KUKOSEKANA MIFEREJI YA KUONDOA MAJI YA MVUA. MSITUJENGEE HOJA YA KUOMBA MISAADA NJE ILI MNEEMEKE.

    ReplyDelete
  8. Bora utabiri wa shehe yahaya unatoka miezi sita kabla, lakini huu unatoka baada ya mvua kubwa kunyesha, hii sikubaliani nayo.

    ReplyDelete
  9. Mamlaka ya hali ya hewa hamko serious,kila siku mnatupa warning after tukio[mvua kunyesha].Serikali iwezesheni hii mamlaka ili ifanye kazi yake vizuri sio mpk mvua inyeshe ndo tuwasikie hatutaki mambo ya kubahatisha.

    ReplyDelete
  10. Kuna wale waliokuwa wanasema kama SNOW ingekuwa inaanguka bongo basi hata sisi tungeihimili, Mvua ya masaa 3 inatushinda Snow ya siku nzima tungeiweza?

    ReplyDelete
  11. Bwana Michizi!! nilitoa maoni kuhusu wale viongozo wa tawi la CCM london, mbona umebaniaa hukuyatoa, na yalikuwa ya muhimu kwa vijana walioko nje ya nchi, na maendeleo ya nchi!!
    blog yako ni ya jamii nzima ya watanzania,
    na ushauri mwingine ni kwamba blog yako ni ya mambo ya CCM tuu, ama pia vyama vyote vya siasa TZ, jaribu kubalance ili kuleta changamoto kwa wote bila kubagua kama itawezekana
    Thanks

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...