Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkullo (kuume) akizindua kampuni ya BUMACO Insurance Company usiku huu katika kituo cha mikutano cha Dar es salaam International Conference centre jijini Dar. Wengine ni Alilya Kwayu ni mkurugenzi wa masoko Bumaco Insurance Company Ltd. Tanzania, na anayefuata ni Mwenyekiti na Mkurugenzi mtendaji Mr. Clement Zablon Kwayu, akifuatiwa na kamishna wa Bima Tanzania Bw. Israel Kamuzora.
Mh. Mustafa Mkullo akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo. Wengine toka shoto waliokaa ni Principal Officer wa Bumaco Mr. Ramadhan Mongi, akifuatiwa na Mkurugenzi Mr. Arthur Shoo, akifuatiwa na Commisioner wa Insurance Tanzania Mr. Israel Kamuzora, akifuatiwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji Mr. Clement Z. Kwayu.
Mh. Mustafa Mkullo akifungua hati ya bima ya moto ya kwanza kutolewa na BUMACO kabla ya kumkabidhi mwakilishi wa Luther House
mwakilishi wa Luther House akitoa risala fupi
Mwenyekiti wa bodi na Mkurugenzi Mtendaji wa
Bumaco Insurance Company Mr. Clement Z. Kwayu akitoa shukurani Mkurugenzi Mr. Ramadhani Mongi, Mkurugenzi Mr. Arthur Shoo, Mhe. Waziri wa Fedha, Mr Mustafa Mkullo, na Mr. Israel Kamuzora wakishangilia.
MC alikuwa Godwin Gondwe a.k.a Double G
wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo
kwa maelezo zaidi ya kampuni hii mpya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mbona hata tovuti hawana......jamani watanzania hii ni dunia ya Teknolojia !!!hawa watakuwa ni wafanya biashara au?maana naona wanashindwa kwenda sawa na mazingira ya sasa ya kibiashara.

    ReplyDelete
  2. Jamaa tovuti wanayo ila tatizo naloliona ni kuwa hiyo tovuti imetengenezwa India......jamani watanzania hatuna hata vijana wanaojua HTML na Php,ASP na VB.net..hii aibu yaaani hata web site zinatengezwa nje,sasa vijana wetu tunawasomesha ili iweje?

    ReplyDelete
  3. Nyumba zikiunguwa mtalipa? Maana hamchelewagi kutafuta chanzo kibaya na kutolipa wa2 fidia zao.Maana wabongo wakiona m2 anaedai anakuja ofisini, mnakuwa mnakimbia mukiwaona kwa mbali.
    Mmachinga from Kigogo mbuyuni

    ReplyDelete
  4. Hawa Bumaco mi nawajua sana ni kampuni ya muda mrefu na ina repetition nzuri esp mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na Huyu Bosi wao namjua anaishi Machame ila mbona jina lake ni Clement Kwayu?michuzi hebu fafanua...

    ReplyDelete
  5. Kwenye picha ya kwanza huyo dada mwenye top nyeupe ni Alilyah Kwayu?
    Kama ni yeye anazidi kuwa kupendeza.

    mdau,
    London

    ReplyDelete
  6. Nipo ktk kampuni moja kubwa sana hapa TZ, tuliamua kuwawezesha vijana wa hapa kutu designia tovuti, ktk mwaka mzima tulibadili vijana kama watatu wa designing lakini waaapi...mwishowe tukaamua kudesigniwa na Muhindi tena kaletwa from Idia, kila mtu anaisifia now, before tulikuwa tunaambiwa kampuni kubwa tovuti zero...so u see, vijana wetu bado sana ktk designing kusemakweli..acha hawa waende tu huko Idia kama wanataka quality

    ReplyDelete
  7. Wee mpiga picha na mwaandishi mbona watuchanganya na jina la boss kuwa Bw.Arthur Shoo wakati picha yamwonyesha Bw.Clemence Kwayu tunayemjua kuwa ndiye boss wa BUMAKO!? na mwanae ndiye huyo mwenye t-shirt nyeupe, Alilya Kwayu...
    Kuwa makini mnaporusha news, coz u never know who knows who...

    ReplyDelete
  8. naona mdau ameshabadili majina kwenda sawa..tovuti company inao lakini hiyo inaongelea zaidi upande wa consultancy kuliko insurance, hiyo kampuni inapande ya insurance na pia management consultancy na research..hii kampuni ya Bumaco inaheshima sana shauri Bwana Clement Kwayu ni mtu genuine sana sana, na ni ya muda mrefu na ya tanzania haina wadau wa nje...so wewe unayesema tovuti hamna uko wapi urudi nyumbani kuja kusaidia maendeleo ya nchi..dont hate congratulate... si bora hao walioamua kufungua kitu nyumbani? Hongera sana BUMACO

    ReplyDelete
  9. Mkome mnaosema tovuti ni watu wa ngapi Tanzania wanaangalia tovuti .Kwa ujumla ni 1% moja tu inayo weza kuona tovuti. Kampuni hii ni ya uhakika hamna fisadi wala mabepari. Ni watanzania halisi waliounda hii kampuni. Ni kampuni ya Uhakika na ina mogopa Mungu. Ukifanya haki katika Maisha utaona Baraka zake siku zinazokuja. Wewe unaosema tovuti je ya kwako iko wapi? Na unalalamika kwa nini wameenda india… India ndio mambo yote katika mambo ya teknologia na sayansi. Kabla ujaanza kufakamia kampuni binafisi kaulize tovuti ya nchi yako iko wapi? Ata Rwanda wametuacha mbali

    ReplyDelete
  10. Hongera sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...