miti katika barabara ya kuelekea ngurdoto, A-Taun
Hodi....Ankal na Wadau wa Blogu ya Jamii, naombeni kuelimishwa. Ningependa kujua mambo machache kuhusu hii miti kwenye hizi picha Tafadhali:
1. Majina yake (kwa Kiswahili ikiwezekana)
2. Iwapo Itastawi Dar es salaam
3. Naweza kupata wapi miche au mbegu zake jijini Dar es salaam?
4. Vingezo vyovyote muhimu kuhusu ustawi wake na matunzo.

Natanguliza shukhrani.
Shukhrani za pekee kwa mdau wa

kwa hizi picha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. mi naona kama ungewasiliana na ngurdoto wenyewe watakupa all the details, kuanzia mbegu, maintanace na kama kwenye hili jangwa letu la Dsm inaweza kuota. Kuhusu jina lake inaonekana unajua kwa kingereza tafuta kamusi ya English to Swahili utapata jina lake

    ReplyDelete
  2. Safi sana mdau kwa kuuliza hii, hata mimi ningependa kujua. Hii miti imependeza, Jamani hakuna mtaalamu wa miti humu?

    ReplyDelete
  3. Mimi si mtaalam wa miti ila napenda miti sana. Kuna mawakala wa miti wapo Morogoro Tanzania Tree seed Agent (TTSA)
    Box 373 Morogoro Tanzania
    email:ttsa@mogoro.net
    Mtafute huyu Technical Unit Manager anaitwa
    Ludovick O.N.Uronu
    Email:Luronu@yahoo.co.uk
    cellphone 0787 838345 atakusaidia

    website www.ttsa.co.tz
    phone 023 260 3192/ 023 260 3903Fax 023 260 3275 wana mbegu zote na wanahamasisha sana, mbegu zao wanauza kwa kg na bei zao kuanzia elf 3000/- inategemea unataka mbegu za mti gani. Nakutakia kila la kheri

    ReplyDelete
  4. Hiyo ni graville robusta (migravilea au mierezi) huku dar inaota ingawa kwa tabu kidogo, wasiliana nami kwa kutumia blog yangu mitiki.blogspot.com nikushauri zaidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...