miti katika barabara ya kuelekea ngurdoto, A-Taun
Hodi....Ankal na Wadau wa Blogu ya Jamii, naombeni kuelimishwa. Ningependa kujua mambo machache kuhusu hii miti kwenye hizi picha Tafadhali:1. Majina yake (kwa Kiswahili ikiwezekana)
2. Iwapo Itastawi Dar es salaam
3. Naweza kupata wapi miche au mbegu zake jijini Dar es salaam?
4. Vingezo vyovyote muhimu kuhusu ustawi wake na matunzo.
Natanguliza shukhrani.
Shukhrani za pekee kwa mdau wa
kwa hizi picha.


mi naona kama ungewasiliana na ngurdoto wenyewe watakupa all the details, kuanzia mbegu, maintanace na kama kwenye hili jangwa letu la Dsm inaweza kuota. Kuhusu jina lake inaonekana unajua kwa kingereza tafuta kamusi ya English to Swahili utapata jina lake
ReplyDeleteSafi sana mdau kwa kuuliza hii, hata mimi ningependa kujua. Hii miti imependeza, Jamani hakuna mtaalamu wa miti humu?
ReplyDeleteMimi si mtaalam wa miti ila napenda miti sana. Kuna mawakala wa miti wapo Morogoro Tanzania Tree seed Agent (TTSA)
ReplyDeleteBox 373 Morogoro Tanzania
email:ttsa@mogoro.net
Mtafute huyu Technical Unit Manager anaitwa
Ludovick O.N.Uronu
Email:Luronu@yahoo.co.uk
cellphone 0787 838345 atakusaidia
website www.ttsa.co.tz
phone 023 260 3192/ 023 260 3903Fax 023 260 3275 wana mbegu zote na wanahamasisha sana, mbegu zao wanauza kwa kg na bei zao kuanzia elf 3000/- inategemea unataka mbegu za mti gani. Nakutakia kila la kheri
Hiyo ni graville robusta (migravilea au mierezi) huku dar inaota ingawa kwa tabu kidogo, wasiliana nami kwa kutumia blog yangu mitiki.blogspot.com nikushauri zaidi
ReplyDelete