Shirika la Umeme nchini a.k.a TANESCO
limetangaza rasmi mgawo wa umeme kwa saa 5 kila siku kuanzia leo.

TANESCO imetangaza mgao huo kufuatia katikakatika ya mara kwa mara ya umeme kwa siku kadhaa kwa nyakati tofauti na kuzua kero kwa watumiaji miongoni mwao wakiunguliwa vitu vyao.

Taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugezni Mkuu Tanesco, Bw. Stephen Mabada, imesema tatizo hilo limetokana na kuharibika kwa mitambo kadhaa katika vituo vya kuzalisha umeme vya Kidatu, Kihansi, Pangani na kile kipya cha Gesi Ubungo.

Ratiba ya katizo hilo la umeme inataraji
kuanza saa 12 jioni hadi saa nne usiku.
Habari ndiyo hiyo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 54 mpaka sasa

  1. Tanesco Tanesco!
    Nakupenda kwa moyo wote!
    Kila niamkapo nchi ipo gizani!

    ReplyDelete
  2. TZ inasikitisha sana,
    vitu kama umeme vinatusumbua kichwa tangu nchi imepata uhuru 1961 na bado tu hatuwezi patia ufumbuzi.
    something is wrong somewhere....

    ReplyDelete
  3. huku duniani mambo kama hayo wamesahau longtime wanafikiria vitu vingine vya kuzidi kusonga mbele

    halafu tukiangalia huko shimoni kwetu ndio tunajitangaza eti nchi inapata maendeleo kaazi kweli kweli

    maendeleo gani ikiwa umeme tu bado kizaazaa haya twendeni tu

    poleni sana ndugu jamaa na marafiki wote mliopo nyumbani.

    ReplyDelete
  4. TANGANYIKAMarch 17, 2010

    NASHINWA HATA CHA KUANDIKA KWA KWELI,NIMELIA SANA BAADA YA KUONA HABARI HII,HIVI TATIZO HILI MPAKA LINI KWA KWELI,NIMEFIKIRIA SANA NA NIMEKUMBUKA HATA NDUGU ZANGU WALIOKO HUKO TANZANIA MAANA NAJUA ADHA YA KUKOSA UMEME,MIMI KAMA MTANZANIA MWENYE UCHUNGU NA NCHI KWA KWELI INAUMA SANA,NAJUA WENGINE WATAONA KITU CHA AJABU KWANINI KINANIUMA ILA KAMA WEWE NI MTANZANIA MWENYE MAPENZI NA NCHI YAKO ITAKUUMA SANA.KWELI JAMANI SERIKALI IMESHINDWA KABISA KUTATUA TATIZO HILI MIAKA NENDA MIAKA RUDI?INATIA UCHUNGU SANA SIJUI TUNAELEKEA WAPI.MUNGU TUSAIDIE,WASAIDIE HATA HAWA VIONGOZI WETU WAONE MWANGA KWA KWELI MAANA MACHONI PAO PANA KIZA KINENE.

    ReplyDelete
  5. Tubinafsishwe nji nzima..
    Najua mtachonga...
    Lakini ni fact.. sisi ni hopeless
    Hali ya kuridhika na hali ni kidhibiti tosha

    ReplyDelete
  6. If you fail to plan you plan to fail!

    ReplyDelete
  7. Hii ni habari ya kusikitisha sana.Hivi ni kweli kuwa serikali yetu imeshindwa kabisa kupata ufumbuzi wa tatizo hili la umeme?Inakuwaje mitambo yote ya umeme inaharibika kwa wakati mmoja?
    Serikali yetu ETI inahitaji wawekezaji kuja kuwekeza,watawekezaje katika mazingira mabovu kama hayo?Miundo mbinu shida,maji shida,umeme shida.Nadhani umefika wakati wa kulivalia njuga hili swala la umeme kwani ni hasara kwa wale wote wenye biashara zitegemeazo umeme(ambao nadhani ni wengi).TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA JE BILA GIZA HAIWEZEKANI?

    ReplyDelete
  8. Mitambo minne mikuu yote itaharibikaje mara moja???

    ReplyDelete
  9. Dawa mojawapo iliyoko ni serikali inunue mitambo mtambo mitano ya Dowans (megawati 100) (mitambo minne ni brand new) kama ilivyopendekezwa na kamati ya mheshimiwa Dk. Slaa ili kuinusuru nchi regardless ya matakwa ya Prof. Mwakyembe. Kama kuna mafisadi waliohusika na kashfa ya richmond basi wachukuliwe hatua za kisheria badala ya wakubwa kuidhalilisha nchi kwa kukomoana kisisasa.

    ReplyDelete
  10. WADAU MLIOPO NCHI NYINGINE ZA KIAFRIKA TUFAHAMISHENI HALI YA UMEME YA HUKO;,
    KWANI KUNA MTU ALIKUWA BOKINAFASO KWA MWAKA MMOJA ;ALISEMA HAKUWAI KUWASHA KOLOBOI; ANGALI KWA WENZETU MAJI NI HABA:

    ReplyDelete
  11. Mimi kama msomi najiuliza; hivi kikwete anafanya kitu gani au hao marais waliopita walifanya nini katika hili suala zima la tanesco? Yaani toka 1961 mpaka leo hii bado tuna tatizo la umeme kweli? Kikwete kama hao wakurugenzi wa tanesco wanashindwa kupata ufumbuzi kwa nini usiwatimue lete hata waafrika kusini washikirie mabango hapo tanesco, kwa kweli rais wetu uzalendo unakushinda. Hii ni haibu na inaonyesha kabisa kuwa wananchi wako hawawezi kushika nchi, badala ya kukaa na kufikiri namna ya kuleta maendeleo wao wananfikiria kuiba mapema na kutia nchi hasara, je tutafika kweli hapa?

    ReplyDelete
  12. Tatizo ni kwa wapiga kura wa tanzania ni kichwa cha mwendawazimu inangalikuwa nchi ingine CCM isiangalipata kura hili ni tatizo kubwa sana karne hii umeme tatizo !!na tuna Gesi ya kumwaga kule Songosongo mungu atupe nini tena????Unakumbuka ??
    Ili tuendelee tunahitaji ELIMU,SIASA SAFI NA UONGOZI BORA kwa tanzania bado hatuna siasa safi na uongozi bora

    ReplyDelete
  13. GELESHA TU HIYO YA 5 ILA NGOMA HIYO KILA SAA CHWAAAAAAAAAAAA ITABIDI UMEME WATU BILL ZAO WASAMEHEWE ZA MWAKA NDIO AZABU AU MIEZI SITA.

    ReplyDelete
  14. i said it before and i will say it again, SOLAR POWER, SOLAR POWER, SOLAR POWER!
    wewe mtu kama umejenga nyumba yako, achan na Tanesco, ingia garama tena umalizane na hilo tatizo sugu once and for all! haizidi milioni 2, au nenda Malawi mkawaulize wenzenu, tena wao ni less than milion wanafunga solar, ushauri wa bure.

    ReplyDelete
  15. Viongozi wetu wamelala tu kwenye tatizo kama hili. Hawajui kuwa suala la umeme na mawasiliano ni suala la usalama wa taifa? They need to fix this shit once and forever.

    ReplyDelete
  16. Mimi ni Mtanzania ninaye ishi Marekani na ninatafuta jinsi ya kutatua hili tatizo la Umeme huko Tanzania.

    Ninataka kuunda group la watu wenye nia ya kutatua hili tatizo,angalau kuanza project ndogo ndogo,kama solar farm,steam generators na technologia zilizopo za kupatia umeme.

    Kama uko kwenye field kama za Engineering, Environmental na zingine ziko related na maswala ya Umeme na Maji.Basi tunaweza kuanza hapa.

    Nitakuja kusoma tena hii topic.

    ReplyDelete
  17. Bai Bai Bongoland. Siku miss hata siku moja.

    Mdau wa majuu.

    ReplyDelete
  18. Tatizo la umeme ni kweli linakera sana! lkn nakerwa zaidi na mijitu inayofananisha au kulinganisha Tz na USA, UK au nchi yoyote iliyoendelea! huo ni upuuzi! Tusidharau tulikotoka, turudi kwetu basi tukajenge nchi! Nani atajenga nchi km si mm na wewe tulioikimbia nchi! eti nchi za duniani zimesahau tatizo la umeme!upuuzi mtupu!

    ReplyDelete
  19. HUYO WAZIRI ANAYESIMAMIA HIYO NISHATI AFUKUZWE KAZI, MAANA ANATUAIBISHA TU, NA MBONA KUNA UMEME MBADALA KIBAO TU NA PESA ZETU ZIMETUMIKA KULIPIA UMEME WA IPTL SASA IMEKUWAJE TENA, HAWA WATU HAWANA AKILI HATA KIDOGO, KUNA UMEME WA UPEPO, UMEME WA JUA NA HATA UMEME WA NYUKLIA SASA HUYU WAZIRI AMBAYE SIYE MBUNIFU NI WANINI HAWA VIMEO HATUWATAKI, KWENYE NCHI YETU. WANASUBIRI MWISHO WA MWEZI TU HAKUNA WANACHOKIFANYA

    ReplyDelete
  20. YAANI UMEME UTAZANI TUNAPATA BURE... SERIKALI UIMTUPE JELA WAZIRI HUSIKA NA WATUMISHI WANAOHUSIKA. SASA NA MIMI NITAGOMBEA URAISI ILI NIYAMALIZE HAYO MATATIZO

    ReplyDelete
  21. "tatizo hilo limetokana na kuharibika kwa mitambo kadhaa katika vituo vya kuzalisha umeme vya Kidatu, Kihansi, Pangani na kile kipya cha Gesi Ubungo." Hii haingii akilini vyote kwa pamoja viwe na matatizo? Hapo bado kile cha kufua umeme wa gesi Mtwara

    ReplyDelete
  22. Mgao...munapiga kelele.Je mungekuwa zenji??!! si mungekufa....kwa kweli!!!

    ReplyDelete
  23. Sasa walikuwa wanatudanganya nini. mara "oh, hakuna mgao"; mara "oh, katika katika ni kwa ajili ya line mpya ya Hi Voltage"

    Siyo tu mmeshindwa kazi, lakini hii kudanganya wananchi inadhirihisha kuwa hamfai.

    Hili shirika libinafsishwe kama Breweries. Mnauza bidhaa yenye demand kama umeme na bado mnashindwa biashara!

    ReplyDelete
  24. TANESCO MWOGOPENI MUNGU.Haya ni maneno ya Askofu Kakobe.TANESCO mlijifanya wababe kupitisha zile nyaya kwa nguvu sasa mnajionea wenyewe.Watanzania tutubu kwa hiyo dhambi pamoja na nyingine zilizofanywa na viongozi wetu ili Mungu atuondolee hii laana na tuweze kupokea baraka.

    ReplyDelete
  25. NAOMBA KUULIZA

    HIVI WHAT IS THE PRIORITES OF THIS COUNTRY??

    Hivi kweli serikali inataka kujadili hili jamani, kama nchi imewashinda si waiache tuu,
    asanteni

    ReplyDelete
  26. Shame on you Taa nesko. Tukwishayajua haya kuwa nayakuja kwani mlikwisha sema pale mlipogomewa kununua mitambo ya dowainzi kuwa yatakapotokea matatizo mbeleni tusilalamike. Iweje mitambo minne yote iharibike kwa wakati mmoja kama sio hujuma na hila zenu mbaya?. Mbona mlianza kutukatia umeme kila siku saa moja usiku mpaka saa nne bila kutupatia taarifa, mlikuwa bado hamjapata uongo wa kusema? Mlaaniwe Taanesko na viongozi wenu wote mafisiadi kwa umaskini mnaotusababishia kwa makusudi yenu.

    Mdau wa mbezi mwisho

    ReplyDelete
  27. Kakobe tuonee huruma

    ReplyDelete
  28. Mimi cku hizi ni furaha tu, hata wakate masaa 24...maana luku ya 40,000 kwa mwezi inakaa miezi mitatu...hureeeeeeee tanesco ongezeni mgao tu, hata mkizima kabisa hiyo mitambo yenu, tumeshachoka

    ReplyDelete
  29. Nchi hii inahitaji maombi mazito.Mungu ashukuriwe sana.

    ReplyDelete
  30. Chanzo cha tatizo la tanesco SI kakobe. Matatizo ya tanesco yalianza 1983. Miaka mibaya kuliko yote ilikuwa 1997 na 2005. CHANZO CHA MATATIZO YA TANESCO NA MASHIRIKA YA UMMA YA TANZANIA (idara ya maji, ttcl, air tanzania, et.) ni Uzembe, ufisadi na kutojali kwa watanzania ambao tunaona mashirika hayo ni miradi ya kujinufaisha na hivyo kutayaonea uchungu wala kutokua na matakwa ya kuyaendeleza. Watanzania tubadili outlook yetu ya kujua mali ya umma ndiyo "shamba la familia" yetu (tz) na siyo yatima fulani.

    ReplyDelete
  31. haha ha ha ha ha ha TANESCO mnafanya JOB ORDER usiku mpate OVERTIME ha ha ha aha ha ha


    JK !!!! upo hapo

    ReplyDelete
  32. Kelele tutapiga sana, umeme utakatika katika mpaka tukome. Ila June mambo yatakuwa sawa mpaka uchaguzi uishe, umeme hata kucheza hautacheza.

    Mi nimechoka siku nyingi sana na Tanesco, tena ukiwapigia EMERGENCY pale mikocheni 0784768584 wanapokea kwa adabu na maneno matamu. Sitamani vita nikiwawaza dada na mama zetu ila this is TOO MUCH.
    Hata usipopigia kura CCM mfano, bado upinzani wenyewe wanasuasua, wako kibao mpaka wananiboa!!
    Dawa hapa ni kusali makanisani na misikitini. Itatusaidia hata tukiwa gizani, lakini Peponi kuna UMEME MILELE!

    ReplyDelete
  33. BIBI UMEMEMarch 18, 2010

    mdau umelia nini sasa mdau uliyejitambulisha kama 'mtanganyika'
    yeyote anayetaka maelezo ya kina please go through www.tanesco.co.tz log in kwenye info au complaints , register it na utajibiwa majibu muafaka...hata kama umeme hautarudi but utajua kwanini haupo...hope itapunguza makali :)

    ReplyDelete
  34. Yaani hili swala la mgao wameamua kutangaza tu ila walikuwa wameshaanza maana karibia kila siku umeme unakatika na ukikatika jioni ni mpaka saa tano usiku. Jamani hivi kweli kuna maendeleo yeyote hapa nchini????????????? inauma sana kuona nchi kam Tz inakosa umeme mara kwa mara. Tatizo ni Tanesco? Serikali au nani???? Tusaidieni jamani hiiiii hiii hiiii na machozi yanatoka

    ReplyDelete
  35. Tanesco, Taanesco kwa kweli mnatumalisa na alafu mkisema mgao basi bora uwe wa halali unakuta maeneo flani inakuwa mgao ++, jamani tunaseteka pia watoto wanateseka kwa joto, kuweni na huruma na ikiamulika kuwa ni mgao basi uwe sawa kwa wote...Especially kinondoni tunaonewa mno hakuna siku iendayo kwa rabana tusikatiwe umeme....SIO HAKI JAMANI KUWENI FAIR

    ReplyDelete
  36. NATAMANI IENDELEE HIVYO HIVYO NA NCHI NZIMA IWE GIZA WAKATI WA KUPIGA KURA TEHE TEHE...!!!!1

    TANESCO HOYEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!

    - MDAU ALIYEZOEA GIZA

    ReplyDelete
  37. Maneno yote haya yanazidi kulaani Tanesco...Hamjui mameno yanaumba.. umeme mgao ni kwamba tulikua hatujajiandaa kwa umeme utakaotumika Zanzibar sasa hautoshi au kama mnabisha wakati Zanzibar hawana umeme mgao ulikuwa hatufahamu maana yake nini.. na si vizuri kuacha ndugu zetu umeme hawana.. sasa tunazidi kuitakia mafanikio mengi Tanesco na Baraka tele.. ili waweze kutatua haya matatizo na vizazi vijavyo visahau kabisa hili swala... Tanesco we count on u

    ReplyDelete
  38. Umeme janga la kitaifa na kiingereza pia janga la kitaifa. Ebu muangalie huyo bwana mdogo alichoandika hapo juu:

    "WHAT IS THE PRIORITES OF THIS COUNTRY??"

    Kama english yako ni ya kuunga unga unatuchanyia ya nini. Utakuwa wa maana sana ukituandikia kiswahili.

    Jivunie lugha yako.

    ReplyDelete
  39. Hivi kweli haya ni maisha gani wajamenii? tunaelekea wapi?? JK upo? na unalikubali hili.Je viongozi wote mnawezaje kulala wakati tuna balaa kama hili hapa nchini? Ulituahidi kwamba suala la umeme litakwisha rasmi Novemba 2009. sasa inakuwaje tena??? tutaabika sana ningekuwa na uwezo ningehama Tanzania.

    ReplyDelete
  40. Thats where i see we need dual citizenship.watu tuchanganyike na watu walioishi sehemu tofauti zilizoendelea na tupatE inputs mpya.watu mmeng'ang'ania tu na ubinafsi.
    haya ndo hapo tuwachoke viongozi walewaleeeee waliozeeeka hawana mpya sera zao za mwaka 47.hawa accept changes.we need new direction,new leadership ya watu waliosoma.watu wanaOpenda maendeleo ya nchi na wapo tayari kutulea maendeleo.tunahitaji highways,tunahitaji mahospitali ya nguvu na madactari mabigwa hasa,vyombo vya kisasa na technolojia ya kisasa huko tanesco na different sectors.
    WE NEED A CHENGE IN THIS COUNTRY. CHANGE IS POSSIBLE.IT HAS TO START WITH US BY ELECTING RESPONSIBLE PEOPLE.
    YES WE CAN!YES WE CAN!YES WE CAN!
    GOD BLESS TANZANIA.

    ReplyDelete
  41. TANESICO MITAMBO YOTE IHARIBIKE KWA WAKATI MMOJA?????? HIYO NI JANJA YENU KWA VILE MITAMBO YA DOWANS HAIKUNUNULIWA NA WATU WALIKWISHA JIWEKEA 10% ZAO BASI CHA MOTO TUTAKIONA SISI WATU WA CHINI MAANA WENYE HAZO WATANUNUA MAJENERETA. AIBU!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  42. kichefuchefu bin fezeha bin ccm bin michuzi bin libeneke bin wana jamii bin ankal bin bongo nyoso

    bongoland sikumiss, sikuhitaji, sikupendi, sina mpango na wewe, na hata nikiwa milionea siwezi kukusaidia, unatia aibu duniani, unaabisha jamii, passport yako hata bure watu hawaitaki.

    unajuwa kwanini nasema hayo wana jamii?????

    ni kwa sababu nchi imeoza na viongozi wake wanaongoza kwa kuzipenda nafsi zao hawajali wengine

    manyangau, mapapa watu, masubiani, mafisadi, huko burundi na rwanda kulikuwa na vita kinoma na hakuna matatizo ya umeme

    eti oooh bongo ipo juu kimaendeleo wananchi wamezama kwenye deep dark

    wana wa nchi amkeni msilale msikubali kuteseka hali yakuwa nchi yenu ina mali kibao migodi na kila aina ya vitu vya thamani

    yote hayo ikiwa hayasaidii kwa taifa mnategemea kusaidiwa mpaka lini??? mali zenu zinatosha kabisa kuinua taifa lenu

    nasema kwa mara ya 2 kuwa siimiss bongo na wala hakuna kitu kitakachonifanya nirudi huko ikiwa maji na umeme havipatikani kwenye majumba.

    ReplyDelete
  43. Kila mtu ategemee kuvuna anachopanda.Haya ndiyo matokeo watanzania kuwekeza zaidi kwenye siasa na kusahau huduma za jamii.Huko Tanesco yaonekana mamabo ni magumu sana nahuenda siku moja nchi ikajikuta gizani kwa saa 24 kwa siku 366.Uchakavu wa miundo mbinu isiyo na mwenye uchungu nayo katika shamba la bibi ndiyo sasa tumefikia hapa.Ni vema sasa wanasiasa wetu wakubali kulitumikia taifa letu kwa kujitolea badala ya kuzoa mafao ambayo yangetumika kwa ajili ya kuimarisha huduma za jamii.

    ReplyDelete
  44. halafu kutwa kukaa kumsifia nyerere wenu kila siku baba wa taifa wakati taifa lenyewe linashinda gizani kila kicha ni ujinga wa hali ya juu ati alileta maendeleo ! angeimarisha hii kitu umeme maji nchi ingekuwa murua viwanda vingezalisha kwa sana tuu uchumi ungepanda kwa kasi na sio mambo ya ujamaa ushuzz hapa kweli inauma sana hii hali itaisha lini??????

    ReplyDelete
  45. mdau hapo juu nakuunga mguu hata mimi sipamiss bongo ng,ooo kwa kipi haswa?? barabara maji safi umeme hospitali au??? hizo huduma sio ombi ni za lazima lakini bongo hayo mavitu ni dhahabu! kweli sitaaaaarudiiii ... sitaaarudiiii

    ReplyDelete
  46. hiyo serikali yaao wameichagua wenyewe, sasa waona giiza wapiga kelele.. mtajijuuuuuu

    ReplyDelete
  47. Mbona Maoni yangu mmeyatupa kapuni? Nilikuwa nawauliza wana CCM kufungua matawi UK na US, huku umeme hakuna nchini Maana yake nini? Haya mama njoo huku DC uendeleze libeneke la matawi ya CCM. Miaka Zaidi ya 40 Hakuna nishati ya kueleweka. Maendeleo yatapitia wapi yaje Tanzania?

    ReplyDelete
  48. Kwa kweli Tanzania ni ngumu,kutokana na mgao huu wa umeme si nimeenda kununua genereta ndogo ya aina ya Tiger,nikawaambia guarantii wakanikatalia wakaniambia wao sio maagent kwa hiyo hawatoi lakin wakaniambia ni nzuri manake katika watu walionunua hamna hata mmoja aliyerudi kulalamika wakaniwashia pale wakanifungashia nilipofika nyumban nikawasha kitu haiwaki tena naulizia watu wanasema hizo genereta ni feki sana,yaani tanzania kwa sasa hivi kila kitu ni mchosho tu

    ReplyDelete
  49. TANZANITE+DHAHABU+ALMASI+SONGOSONGO+MAFUTA+MT KILIMANJARO+MBUGA ZA WANYAMA+ARDHI KUBWA YENYE RUTUBA+SIASA CHAFU+MAFISA+PAYE(INCOME TAX)+WANANCHI TULIOLALA .

    WATANZANIA TUAMKE KUDAI HAKI ZETU NADHANI TUANZE NA MAANDAMANO YA NCHI NZIMA KUWANG'OA VIONGOZI WABOVU WASIOWAJIBIKA,IKISHINDIKANA TUWE TAYARI KUGAWA NCHI TANZANIA KASKAZINI NA TANZANIA KUSINITUMECHOAKA KWANI UKUBWA WA NCHI UMEKUA MZIGO KWA VIONGIZI WETU

    ReplyDelete
  50. NYIE WATANGANYIKA UMEME UMEKATIKA SIKU MBILI TU TENA NI WA MGAO KELELE NYIINGI SISI WAZANZIBARI UMEME UMEKATIKA MIEZI SITA TENA FULL NA TUKO KIMYA.ACHENI HIZOO.

    ReplyDelete
  51. These people are not serious! You know why? Do we need a Ph holder in order to be able to run TANESCO? Why cant you appoint Mr. Mabada as a CEO and I am sure TANESCO will be again on the right track! This company must have an engineer as CEO not bla bla Ph holder in economics. We are fed up with Mr Idrissa theories which have proved failure!

    Mtiifu

    ReplyDelete
  52. Huku nikitambua kuwa mimi ni sehemu ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania (JMT),
    Na nikikiri kuwa mimi ni mmoja wa Watanzania wenye elimu na ujuzi
    Na nikijiona kuona nina uwezo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi, natamka kuwa:

    Wanzanchi, TANESCO na serikali ya JMT poleni sana kwa changamoto zinazotukabili.

    Ninawaombea na kuwatia moyo wataalamu wote na wadau wote wa umeme wanaojitahidi kutafuta suluhisho juu ya adha hii.


    Ninasikitika na kuomba msamaha kwa jinsi ambavyo mimi Mtanzania sijafanya bidii ya kutosha katika kuchangia maendeleo ya nchi yangu kutokana na akili, vipaji na uwezo mbalimbali alionipa Mola na wanadunia.

    Niko tayari kubadilika na kuchangia zaidi na naomba wengine pia waniunge mkono maana kwa kufanya hivyo siku za usoni tutakuwa tunatuma 'responses' za kupongeza nchi yetu na kufurahia matunda ya mendeleo yetu wenyewe.

    Ni mimi mwananchi niliyeokolewa kijamii,

    umkhonto2@hotmail.com

    ReplyDelete
  53. Diaspora IndiaMarch 18, 2010

    Hii nchi hakuna la kujivunia.Tuna mabilioni ya kujenga nyumba 2 za magavana lkn hatuwezi kumaintain mitambo ya umeme inayotupa huduma sisi wenyewe.Hatuna pesa za kuwasaidia raia wetu kwenye majanga ya mafuriko kama ya kilosa mpaka wageni wanatuumbua kwa kutujengea nyumba nyingi kwa gharama nafuu.Ufisadi unamaliza nchi yetu.Maendeleo tuyasahau kwa hali hii maana dunia ya sasa kila kitu kinahitaji umeme.

    ReplyDelete
  54. nakumbuka mada ya mdau mmoja hapa,alisema kuhusu kukatika umeme na mimi nilichangia ata mwanza ni balaa yani kila dk/masaa umeme unakatika unawaka,,,nikasema ivi si watangaze tu kuna mgao wa umeme kwanini kila siku umeme unakatika??na TAREHE 9sept 2010 umeme ulikatika nchi nzima almost maana tuliwasiliana na watu mikoa zaidi ta 8 ivi na hawakuwa na umeme kuanzia saa 12 jioni hadi 4 usiku SIKUAMINI!!

    nilisema kitu kimoja tu "ee Mwenyezi kwanini tuna watu/viongozi washenzy ivi na wanakula nchi,wanalindana adi sasa hatujui kesi za RICHMONG,GAS,IPTL nk walipe wote wanaotuweka nchi katika umaskini huu"

    nchi ina maji,gas,madini,maliasili nk

    so tanesco ndo mmetangaza rasmi baada ya muda wote huu???????????

    wataalamu??????????

    maneno yetu yatarudi tu kwenu,ngojeni!!mwanadamu hateseki bure kumbukeni....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...