
Shirika la Umeme nchini a.k.a TANESCO
limetangaza rasmi mgawo wa umeme kwa saa 5 kila siku kuanzia leo.
TANESCO imetangaza mgao huo kufuatia katikakatika ya mara kwa mara ya umeme kwa siku kadhaa kwa nyakati tofauti na kuzua kero kwa watumiaji miongoni mwao wakiunguliwa vitu vyao.
Taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugezni Mkuu Tanesco, Bw. Stephen Mabada, imesema tatizo hilo limetokana na kuharibika kwa mitambo kadhaa katika vituo vya kuzalisha umeme vya Kidatu, Kihansi, Pangani na kile kipya cha Gesi Ubungo.
Ratiba ya katizo hilo la umeme inataraji
kuanza saa 12 jioni hadi saa nne usiku.
Habari ndiyo hiyo...


Tanesco Tanesco!
ReplyDeleteNakupenda kwa moyo wote!
Kila niamkapo nchi ipo gizani!
TZ inasikitisha sana,
ReplyDeletevitu kama umeme vinatusumbua kichwa tangu nchi imepata uhuru 1961 na bado tu hatuwezi patia ufumbuzi.
something is wrong somewhere....
huku duniani mambo kama hayo wamesahau longtime wanafikiria vitu vingine vya kuzidi kusonga mbele
ReplyDeletehalafu tukiangalia huko shimoni kwetu ndio tunajitangaza eti nchi inapata maendeleo kaazi kweli kweli
maendeleo gani ikiwa umeme tu bado kizaazaa haya twendeni tu
poleni sana ndugu jamaa na marafiki wote mliopo nyumbani.
NASHINWA HATA CHA KUANDIKA KWA KWELI,NIMELIA SANA BAADA YA KUONA HABARI HII,HIVI TATIZO HILI MPAKA LINI KWA KWELI,NIMEFIKIRIA SANA NA NIMEKUMBUKA HATA NDUGU ZANGU WALIOKO HUKO TANZANIA MAANA NAJUA ADHA YA KUKOSA UMEME,MIMI KAMA MTANZANIA MWENYE UCHUNGU NA NCHI KWA KWELI INAUMA SANA,NAJUA WENGINE WATAONA KITU CHA AJABU KWANINI KINANIUMA ILA KAMA WEWE NI MTANZANIA MWENYE MAPENZI NA NCHI YAKO ITAKUUMA SANA.KWELI JAMANI SERIKALI IMESHINDWA KABISA KUTATUA TATIZO HILI MIAKA NENDA MIAKA RUDI?INATIA UCHUNGU SANA SIJUI TUNAELEKEA WAPI.MUNGU TUSAIDIE,WASAIDIE HATA HAWA VIONGOZI WETU WAONE MWANGA KWA KWELI MAANA MACHONI PAO PANA KIZA KINENE.
ReplyDeleteTubinafsishwe nji nzima..
ReplyDeleteNajua mtachonga...
Lakini ni fact.. sisi ni hopeless
Hali ya kuridhika na hali ni kidhibiti tosha
If you fail to plan you plan to fail!
ReplyDeleteHii ni habari ya kusikitisha sana.Hivi ni kweli kuwa serikali yetu imeshindwa kabisa kupata ufumbuzi wa tatizo hili la umeme?Inakuwaje mitambo yote ya umeme inaharibika kwa wakati mmoja?
ReplyDeleteSerikali yetu ETI inahitaji wawekezaji kuja kuwekeza,watawekezaje katika mazingira mabovu kama hayo?Miundo mbinu shida,maji shida,umeme shida.Nadhani umefika wakati wa kulivalia njuga hili swala la umeme kwani ni hasara kwa wale wote wenye biashara zitegemeazo umeme(ambao nadhani ni wengi).TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA JE BILA GIZA HAIWEZEKANI?
Mitambo minne mikuu yote itaharibikaje mara moja???
ReplyDeleteDawa mojawapo iliyoko ni serikali inunue mitambo mtambo mitano ya Dowans (megawati 100) (mitambo minne ni brand new) kama ilivyopendekezwa na kamati ya mheshimiwa Dk. Slaa ili kuinusuru nchi regardless ya matakwa ya Prof. Mwakyembe. Kama kuna mafisadi waliohusika na kashfa ya richmond basi wachukuliwe hatua za kisheria badala ya wakubwa kuidhalilisha nchi kwa kukomoana kisisasa.
ReplyDeleteWADAU MLIOPO NCHI NYINGINE ZA KIAFRIKA TUFAHAMISHENI HALI YA UMEME YA HUKO;,
ReplyDeleteKWANI KUNA MTU ALIKUWA BOKINAFASO KWA MWAKA MMOJA ;ALISEMA HAKUWAI KUWASHA KOLOBOI; ANGALI KWA WENZETU MAJI NI HABA:
Mimi kama msomi najiuliza; hivi kikwete anafanya kitu gani au hao marais waliopita walifanya nini katika hili suala zima la tanesco? Yaani toka 1961 mpaka leo hii bado tuna tatizo la umeme kweli? Kikwete kama hao wakurugenzi wa tanesco wanashindwa kupata ufumbuzi kwa nini usiwatimue lete hata waafrika kusini washikirie mabango hapo tanesco, kwa kweli rais wetu uzalendo unakushinda. Hii ni haibu na inaonyesha kabisa kuwa wananchi wako hawawezi kushika nchi, badala ya kukaa na kufikiri namna ya kuleta maendeleo wao wananfikiria kuiba mapema na kutia nchi hasara, je tutafika kweli hapa?
ReplyDeleteTatizo ni kwa wapiga kura wa tanzania ni kichwa cha mwendawazimu inangalikuwa nchi ingine CCM isiangalipata kura hili ni tatizo kubwa sana karne hii umeme tatizo !!na tuna Gesi ya kumwaga kule Songosongo mungu atupe nini tena????Unakumbuka ??
ReplyDeleteIli tuendelee tunahitaji ELIMU,SIASA SAFI NA UONGOZI BORA kwa tanzania bado hatuna siasa safi na uongozi bora
GELESHA TU HIYO YA 5 ILA NGOMA HIYO KILA SAA CHWAAAAAAAAAAAA ITABIDI UMEME WATU BILL ZAO WASAMEHEWE ZA MWAKA NDIO AZABU AU MIEZI SITA.
ReplyDeletei said it before and i will say it again, SOLAR POWER, SOLAR POWER, SOLAR POWER!
ReplyDeletewewe mtu kama umejenga nyumba yako, achan na Tanesco, ingia garama tena umalizane na hilo tatizo sugu once and for all! haizidi milioni 2, au nenda Malawi mkawaulize wenzenu, tena wao ni less than milion wanafunga solar, ushauri wa bure.
Viongozi wetu wamelala tu kwenye tatizo kama hili. Hawajui kuwa suala la umeme na mawasiliano ni suala la usalama wa taifa? They need to fix this shit once and forever.
ReplyDeleteMimi ni Mtanzania ninaye ishi Marekani na ninatafuta jinsi ya kutatua hili tatizo la Umeme huko Tanzania.
ReplyDeleteNinataka kuunda group la watu wenye nia ya kutatua hili tatizo,angalau kuanza project ndogo ndogo,kama solar farm,steam generators na technologia zilizopo za kupatia umeme.
Kama uko kwenye field kama za Engineering, Environmental na zingine ziko related na maswala ya Umeme na Maji.Basi tunaweza kuanza hapa.
Nitakuja kusoma tena hii topic.
Bai Bai Bongoland. Siku miss hata siku moja.
ReplyDeleteMdau wa majuu.
Tatizo la umeme ni kweli linakera sana! lkn nakerwa zaidi na mijitu inayofananisha au kulinganisha Tz na USA, UK au nchi yoyote iliyoendelea! huo ni upuuzi! Tusidharau tulikotoka, turudi kwetu basi tukajenge nchi! Nani atajenga nchi km si mm na wewe tulioikimbia nchi! eti nchi za duniani zimesahau tatizo la umeme!upuuzi mtupu!
ReplyDeleteHUYO WAZIRI ANAYESIMAMIA HIYO NISHATI AFUKUZWE KAZI, MAANA ANATUAIBISHA TU, NA MBONA KUNA UMEME MBADALA KIBAO TU NA PESA ZETU ZIMETUMIKA KULIPIA UMEME WA IPTL SASA IMEKUWAJE TENA, HAWA WATU HAWANA AKILI HATA KIDOGO, KUNA UMEME WA UPEPO, UMEME WA JUA NA HATA UMEME WA NYUKLIA SASA HUYU WAZIRI AMBAYE SIYE MBUNIFU NI WANINI HAWA VIMEO HATUWATAKI, KWENYE NCHI YETU. WANASUBIRI MWISHO WA MWEZI TU HAKUNA WANACHOKIFANYA
ReplyDeleteYAANI UMEME UTAZANI TUNAPATA BURE... SERIKALI UIMTUPE JELA WAZIRI HUSIKA NA WATUMISHI WANAOHUSIKA. SASA NA MIMI NITAGOMBEA URAISI ILI NIYAMALIZE HAYO MATATIZO
ReplyDelete"tatizo hilo limetokana na kuharibika kwa mitambo kadhaa katika vituo vya kuzalisha umeme vya Kidatu, Kihansi, Pangani na kile kipya cha Gesi Ubungo." Hii haingii akilini vyote kwa pamoja viwe na matatizo? Hapo bado kile cha kufua umeme wa gesi Mtwara
ReplyDeleteMgao...munapiga kelele.Je mungekuwa zenji??!! si mungekufa....kwa kweli!!!
ReplyDeleteSasa walikuwa wanatudanganya nini. mara "oh, hakuna mgao"; mara "oh, katika katika ni kwa ajili ya line mpya ya Hi Voltage"
ReplyDeleteSiyo tu mmeshindwa kazi, lakini hii kudanganya wananchi inadhirihisha kuwa hamfai.
Hili shirika libinafsishwe kama Breweries. Mnauza bidhaa yenye demand kama umeme na bado mnashindwa biashara!
TANESCO MWOGOPENI MUNGU.Haya ni maneno ya Askofu Kakobe.TANESCO mlijifanya wababe kupitisha zile nyaya kwa nguvu sasa mnajionea wenyewe.Watanzania tutubu kwa hiyo dhambi pamoja na nyingine zilizofanywa na viongozi wetu ili Mungu atuondolee hii laana na tuweze kupokea baraka.
ReplyDeleteNAOMBA KUULIZA
ReplyDeleteHIVI WHAT IS THE PRIORITES OF THIS COUNTRY??
Hivi kweli serikali inataka kujadili hili jamani, kama nchi imewashinda si waiache tuu,
asanteni
Shame on you Taa nesko. Tukwishayajua haya kuwa nayakuja kwani mlikwisha sema pale mlipogomewa kununua mitambo ya dowainzi kuwa yatakapotokea matatizo mbeleni tusilalamike. Iweje mitambo minne yote iharibike kwa wakati mmoja kama sio hujuma na hila zenu mbaya?. Mbona mlianza kutukatia umeme kila siku saa moja usiku mpaka saa nne bila kutupatia taarifa, mlikuwa bado hamjapata uongo wa kusema? Mlaaniwe Taanesko na viongozi wenu wote mafisiadi kwa umaskini mnaotusababishia kwa makusudi yenu.
ReplyDeleteMdau wa mbezi mwisho
Kakobe tuonee huruma
ReplyDeleteMimi cku hizi ni furaha tu, hata wakate masaa 24...maana luku ya 40,000 kwa mwezi inakaa miezi mitatu...hureeeeeeee tanesco ongezeni mgao tu, hata mkizima kabisa hiyo mitambo yenu, tumeshachoka
ReplyDeleteNchi hii inahitaji maombi mazito.Mungu ashukuriwe sana.
ReplyDeleteChanzo cha tatizo la tanesco SI kakobe. Matatizo ya tanesco yalianza 1983. Miaka mibaya kuliko yote ilikuwa 1997 na 2005. CHANZO CHA MATATIZO YA TANESCO NA MASHIRIKA YA UMMA YA TANZANIA (idara ya maji, ttcl, air tanzania, et.) ni Uzembe, ufisadi na kutojali kwa watanzania ambao tunaona mashirika hayo ni miradi ya kujinufaisha na hivyo kutayaonea uchungu wala kutokua na matakwa ya kuyaendeleza. Watanzania tubadili outlook yetu ya kujua mali ya umma ndiyo "shamba la familia" yetu (tz) na siyo yatima fulani.
ReplyDeletehaha ha ha ha ha ha TANESCO mnafanya JOB ORDER usiku mpate OVERTIME ha ha ha aha ha ha
ReplyDeleteJK !!!! upo hapo
Kelele tutapiga sana, umeme utakatika katika mpaka tukome. Ila June mambo yatakuwa sawa mpaka uchaguzi uishe, umeme hata kucheza hautacheza.
ReplyDeleteMi nimechoka siku nyingi sana na Tanesco, tena ukiwapigia EMERGENCY pale mikocheni 0784768584 wanapokea kwa adabu na maneno matamu. Sitamani vita nikiwawaza dada na mama zetu ila this is TOO MUCH.
Hata usipopigia kura CCM mfano, bado upinzani wenyewe wanasuasua, wako kibao mpaka wananiboa!!
Dawa hapa ni kusali makanisani na misikitini. Itatusaidia hata tukiwa gizani, lakini Peponi kuna UMEME MILELE!
mdau umelia nini sasa mdau uliyejitambulisha kama 'mtanganyika'
ReplyDeleteyeyote anayetaka maelezo ya kina please go through www.tanesco.co.tz log in kwenye info au complaints , register it na utajibiwa majibu muafaka...hata kama umeme hautarudi but utajua kwanini haupo...hope itapunguza makali :)
Yaani hili swala la mgao wameamua kutangaza tu ila walikuwa wameshaanza maana karibia kila siku umeme unakatika na ukikatika jioni ni mpaka saa tano usiku. Jamani hivi kweli kuna maendeleo yeyote hapa nchini????????????? inauma sana kuona nchi kam Tz inakosa umeme mara kwa mara. Tatizo ni Tanesco? Serikali au nani???? Tusaidieni jamani hiiiii hiii hiiii na machozi yanatoka
ReplyDeleteTanesco, Taanesco kwa kweli mnatumalisa na alafu mkisema mgao basi bora uwe wa halali unakuta maeneo flani inakuwa mgao ++, jamani tunaseteka pia watoto wanateseka kwa joto, kuweni na huruma na ikiamulika kuwa ni mgao basi uwe sawa kwa wote...Especially kinondoni tunaonewa mno hakuna siku iendayo kwa rabana tusikatiwe umeme....SIO HAKI JAMANI KUWENI FAIR
ReplyDeleteNATAMANI IENDELEE HIVYO HIVYO NA NCHI NZIMA IWE GIZA WAKATI WA KUPIGA KURA TEHE TEHE...!!!!1
ReplyDeleteTANESCO HOYEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!
- MDAU ALIYEZOEA GIZA
Maneno yote haya yanazidi kulaani Tanesco...Hamjui mameno yanaumba.. umeme mgao ni kwamba tulikua hatujajiandaa kwa umeme utakaotumika Zanzibar sasa hautoshi au kama mnabisha wakati Zanzibar hawana umeme mgao ulikuwa hatufahamu maana yake nini.. na si vizuri kuacha ndugu zetu umeme hawana.. sasa tunazidi kuitakia mafanikio mengi Tanesco na Baraka tele.. ili waweze kutatua haya matatizo na vizazi vijavyo visahau kabisa hili swala... Tanesco we count on u
ReplyDeleteUmeme janga la kitaifa na kiingereza pia janga la kitaifa. Ebu muangalie huyo bwana mdogo alichoandika hapo juu:
ReplyDelete"WHAT IS THE PRIORITES OF THIS COUNTRY??"
Kama english yako ni ya kuunga unga unatuchanyia ya nini. Utakuwa wa maana sana ukituandikia kiswahili.
Jivunie lugha yako.
Hivi kweli haya ni maisha gani wajamenii? tunaelekea wapi?? JK upo? na unalikubali hili.Je viongozi wote mnawezaje kulala wakati tuna balaa kama hili hapa nchini? Ulituahidi kwamba suala la umeme litakwisha rasmi Novemba 2009. sasa inakuwaje tena??? tutaabika sana ningekuwa na uwezo ningehama Tanzania.
ReplyDeleteThats where i see we need dual citizenship.watu tuchanganyike na watu walioishi sehemu tofauti zilizoendelea na tupatE inputs mpya.watu mmeng'ang'ania tu na ubinafsi.
ReplyDeletehaya ndo hapo tuwachoke viongozi walewaleeeee waliozeeeka hawana mpya sera zao za mwaka 47.hawa accept changes.we need new direction,new leadership ya watu waliosoma.watu wanaOpenda maendeleo ya nchi na wapo tayari kutulea maendeleo.tunahitaji highways,tunahitaji mahospitali ya nguvu na madactari mabigwa hasa,vyombo vya kisasa na technolojia ya kisasa huko tanesco na different sectors.
WE NEED A CHENGE IN THIS COUNTRY. CHANGE IS POSSIBLE.IT HAS TO START WITH US BY ELECTING RESPONSIBLE PEOPLE.
YES WE CAN!YES WE CAN!YES WE CAN!
GOD BLESS TANZANIA.
TANESICO MITAMBO YOTE IHARIBIKE KWA WAKATI MMOJA?????? HIYO NI JANJA YENU KWA VILE MITAMBO YA DOWANS HAIKUNUNULIWA NA WATU WALIKWISHA JIWEKEA 10% ZAO BASI CHA MOTO TUTAKIONA SISI WATU WA CHINI MAANA WENYE HAZO WATANUNUA MAJENERETA. AIBU!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeletekichefuchefu bin fezeha bin ccm bin michuzi bin libeneke bin wana jamii bin ankal bin bongo nyoso
ReplyDeletebongoland sikumiss, sikuhitaji, sikupendi, sina mpango na wewe, na hata nikiwa milionea siwezi kukusaidia, unatia aibu duniani, unaabisha jamii, passport yako hata bure watu hawaitaki.
unajuwa kwanini nasema hayo wana jamii?????
ni kwa sababu nchi imeoza na viongozi wake wanaongoza kwa kuzipenda nafsi zao hawajali wengine
manyangau, mapapa watu, masubiani, mafisadi, huko burundi na rwanda kulikuwa na vita kinoma na hakuna matatizo ya umeme
eti oooh bongo ipo juu kimaendeleo wananchi wamezama kwenye deep dark
wana wa nchi amkeni msilale msikubali kuteseka hali yakuwa nchi yenu ina mali kibao migodi na kila aina ya vitu vya thamani
yote hayo ikiwa hayasaidii kwa taifa mnategemea kusaidiwa mpaka lini??? mali zenu zinatosha kabisa kuinua taifa lenu
nasema kwa mara ya 2 kuwa siimiss bongo na wala hakuna kitu kitakachonifanya nirudi huko ikiwa maji na umeme havipatikani kwenye majumba.
Kila mtu ategemee kuvuna anachopanda.Haya ndiyo matokeo watanzania kuwekeza zaidi kwenye siasa na kusahau huduma za jamii.Huko Tanesco yaonekana mamabo ni magumu sana nahuenda siku moja nchi ikajikuta gizani kwa saa 24 kwa siku 366.Uchakavu wa miundo mbinu isiyo na mwenye uchungu nayo katika shamba la bibi ndiyo sasa tumefikia hapa.Ni vema sasa wanasiasa wetu wakubali kulitumikia taifa letu kwa kujitolea badala ya kuzoa mafao ambayo yangetumika kwa ajili ya kuimarisha huduma za jamii.
ReplyDeletehalafu kutwa kukaa kumsifia nyerere wenu kila siku baba wa taifa wakati taifa lenyewe linashinda gizani kila kicha ni ujinga wa hali ya juu ati alileta maendeleo ! angeimarisha hii kitu umeme maji nchi ingekuwa murua viwanda vingezalisha kwa sana tuu uchumi ungepanda kwa kasi na sio mambo ya ujamaa ushuzz hapa kweli inauma sana hii hali itaisha lini??????
ReplyDeletemdau hapo juu nakuunga mguu hata mimi sipamiss bongo ng,ooo kwa kipi haswa?? barabara maji safi umeme hospitali au??? hizo huduma sio ombi ni za lazima lakini bongo hayo mavitu ni dhahabu! kweli sitaaaaarudiiii ... sitaaarudiiii
ReplyDeletehiyo serikali yaao wameichagua wenyewe, sasa waona giiza wapiga kelele.. mtajijuuuuuu
ReplyDeleteMbona Maoni yangu mmeyatupa kapuni? Nilikuwa nawauliza wana CCM kufungua matawi UK na US, huku umeme hakuna nchini Maana yake nini? Haya mama njoo huku DC uendeleze libeneke la matawi ya CCM. Miaka Zaidi ya 40 Hakuna nishati ya kueleweka. Maendeleo yatapitia wapi yaje Tanzania?
ReplyDeleteKwa kweli Tanzania ni ngumu,kutokana na mgao huu wa umeme si nimeenda kununua genereta ndogo ya aina ya Tiger,nikawaambia guarantii wakanikatalia wakaniambia wao sio maagent kwa hiyo hawatoi lakin wakaniambia ni nzuri manake katika watu walionunua hamna hata mmoja aliyerudi kulalamika wakaniwashia pale wakanifungashia nilipofika nyumban nikawasha kitu haiwaki tena naulizia watu wanasema hizo genereta ni feki sana,yaani tanzania kwa sasa hivi kila kitu ni mchosho tu
ReplyDeleteTANZANITE+DHAHABU+ALMASI+SONGOSONGO+MAFUTA+MT KILIMANJARO+MBUGA ZA WANYAMA+ARDHI KUBWA YENYE RUTUBA+SIASA CHAFU+MAFISA+PAYE(INCOME TAX)+WANANCHI TULIOLALA .
ReplyDeleteWATANZANIA TUAMKE KUDAI HAKI ZETU NADHANI TUANZE NA MAANDAMANO YA NCHI NZIMA KUWANG'OA VIONGOZI WABOVU WASIOWAJIBIKA,IKISHINDIKANA TUWE TAYARI KUGAWA NCHI TANZANIA KASKAZINI NA TANZANIA KUSINITUMECHOAKA KWANI UKUBWA WA NCHI UMEKUA MZIGO KWA VIONGIZI WETU
NYIE WATANGANYIKA UMEME UMEKATIKA SIKU MBILI TU TENA NI WA MGAO KELELE NYIINGI SISI WAZANZIBARI UMEME UMEKATIKA MIEZI SITA TENA FULL NA TUKO KIMYA.ACHENI HIZOO.
ReplyDeleteThese people are not serious! You know why? Do we need a Ph holder in order to be able to run TANESCO? Why cant you appoint Mr. Mabada as a CEO and I am sure TANESCO will be again on the right track! This company must have an engineer as CEO not bla bla Ph holder in economics. We are fed up with Mr Idrissa theories which have proved failure!
ReplyDeleteMtiifu
Huku nikitambua kuwa mimi ni sehemu ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania (JMT),
ReplyDeleteNa nikikiri kuwa mimi ni mmoja wa Watanzania wenye elimu na ujuzi
Na nikijiona kuona nina uwezo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi, natamka kuwa:
Wanzanchi, TANESCO na serikali ya JMT poleni sana kwa changamoto zinazotukabili.
Ninawaombea na kuwatia moyo wataalamu wote na wadau wote wa umeme wanaojitahidi kutafuta suluhisho juu ya adha hii.
Ninasikitika na kuomba msamaha kwa jinsi ambavyo mimi Mtanzania sijafanya bidii ya kutosha katika kuchangia maendeleo ya nchi yangu kutokana na akili, vipaji na uwezo mbalimbali alionipa Mola na wanadunia.
Niko tayari kubadilika na kuchangia zaidi na naomba wengine pia waniunge mkono maana kwa kufanya hivyo siku za usoni tutakuwa tunatuma 'responses' za kupongeza nchi yetu na kufurahia matunda ya mendeleo yetu wenyewe.
Ni mimi mwananchi niliyeokolewa kijamii,
umkhonto2@hotmail.com
Hii nchi hakuna la kujivunia.Tuna mabilioni ya kujenga nyumba 2 za magavana lkn hatuwezi kumaintain mitambo ya umeme inayotupa huduma sisi wenyewe.Hatuna pesa za kuwasaidia raia wetu kwenye majanga ya mafuriko kama ya kilosa mpaka wageni wanatuumbua kwa kutujengea nyumba nyingi kwa gharama nafuu.Ufisadi unamaliza nchi yetu.Maendeleo tuyasahau kwa hali hii maana dunia ya sasa kila kitu kinahitaji umeme.
ReplyDeletenakumbuka mada ya mdau mmoja hapa,alisema kuhusu kukatika umeme na mimi nilichangia ata mwanza ni balaa yani kila dk/masaa umeme unakatika unawaka,,,nikasema ivi si watangaze tu kuna mgao wa umeme kwanini kila siku umeme unakatika??na TAREHE 9sept 2010 umeme ulikatika nchi nzima almost maana tuliwasiliana na watu mikoa zaidi ta 8 ivi na hawakuwa na umeme kuanzia saa 12 jioni hadi 4 usiku SIKUAMINI!!
ReplyDeletenilisema kitu kimoja tu "ee Mwenyezi kwanini tuna watu/viongozi washenzy ivi na wanakula nchi,wanalindana adi sasa hatujui kesi za RICHMONG,GAS,IPTL nk walipe wote wanaotuweka nchi katika umaskini huu"
nchi ina maji,gas,madini,maliasili nk
so tanesco ndo mmetangaza rasmi baada ya muda wote huu???????????
wataalamu??????????
maneno yetu yatarudi tu kwenu,ngojeni!!mwanadamu hateseki bure kumbukeni....