Bw. Nehemia Mchechu
Kwa mujibu wa kifungu Na. 18 (1) cha Sheria Na. 2 ya 1990, iliyounda Shirika la Nyumba la Taifa (The National Housing Corporation Act No. 2 of 1990) Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amemteua Ndugu Nehemia Mchechu (37) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Uteuzi huu unaanzia tarehe 1/3/2010.

Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nehemia Mchechu alikuwa Mkurugenzi
Mkuu (Chief Executive Officer) wa Benki ya “Commercial Bank of Africa”.
Chini ya Uongozi wake benki hiyo imepata mafanikio makubwa sana hapa nchini, na ni moja kati ya benki tano zilizoanza utaratibu wa kutoa mikopo ya nyumba kwa Watanzania.
Ndugu Nehemia Mchechu akishirikiana na Bodi mpya ya Shirika hili na timu ya Menejimenti ya Shirika hili, amepewa jukumu la kulifanyia mageuzi makubwa Shirika hili ili liingie katika biashara kubwa ya kujenga nyumba katika Mikoa yote na kuziuza kwa mikopo kwa watanzania wa kipato cha chini na kati, ambalo ndilo lengo kuu la Shirika hili tangu lilipoanzishwa mara tu baada ya Tanganyika kupata Uhuru Desemba 9, 1961.
Wakati huo huo, na kwa mujibu wa Sheria Na. 2 ya 1990 iliyounda Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Bwana K. Masudi Issa Msita kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo. Bwana K. Masudi Issa Msita ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ujenzi (National Construction Council).

Wakati huo huo, na kwa mujibu wa Sheria hiyo hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo.
1. Msajili wa Hazina - (Wizara ya Fedha).
2. Mkurugenzi wa Nyumba - (Wizara ya Ardhi).
3. Prof. W.J. Kombe - (Chuo Kikuu cha Ardhi).
4. Bwana Enock Maganga - (Benki Kuu).
5. Bi Subira Mchumo - (Sekta Binafsi).
6. Bwana Elius Mwakalinga - (Wizara ya Miundombinu).
7. Bi. Shally Raymond - (Mbunge)
Uteuzi huu unaanza tarehe 28/02/2010 na ni wa miaka mitatu.
Imetolewa na:-
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 52 mpaka sasa

  1. Congrats,

    But you are now going to public sector which is very different compared with private sector. Public sector has too much politics so you have to spend a lot of your vital time to deal with politics instead of business issues.

    Anyway all the best, let us hope for the better.

    ReplyDelete
  2. Kaka michuzi waziri wa Ardhi kachemka,hiyo bodi aliyoiteua ni batili,sheria mpya wa bunge hairuhusu Mbunge yoyote kuwa kwenye bodi.Vema waziri akamtoa Mbunge huyo haraka,otherwise maamuzi yoyote yatakayofanyika yatakuwa batili.

    ReplyDelete
  3. Ashomire Rugaimukamu, Ishozi BKMarch 04, 2010

    Nina hamu ya kujua huyu jamaa alivyopiga shule, si mnajua tena tunapenda kujilinganisha na nondozzz za hawa wateule?

    ReplyDelete
  4. Hongera Bw Nehemia,lakini watanzania CEOs hamjaweka historia nzuri...

    Nasikitika umekuwa wewe ndio mtanzania wa mwisho kutoka katika benki za nje.

    KCB - Heri Bomani (tz) Kaondoka kaingia Mkenya

    Barclays - Bade Rashid (tz) - Kaondolewa kupelekwa Makao makuu ku-push papers - kaletwa Mkenya

    Standard Chartered Bank - Mkenya

    CBA - Nahemia kaondoka atakuja Mkenya

    NHC ni challenge kubwa siasa na usifikiri utaleta mabadiliko huko, sasa wewe sijui ndio umeamua - lets join them?

    Good luck

    ReplyDelete
  5. Congrats Mr. Nehemia.

    Ila ankal ningependa kujua jinsi jamaa alivyokula hizo nondoz. maana naona umri wake ni mdogo sana ukilinganisha na achievement yake

    mdau,
    Kennedy

    ReplyDelete
  6. All the Best Nehemiah, i know you can. Of course you have gone to school and in anycase, school is meaningless without commitment to delivery.What matters in Nehemiah's case is the fact that this young boy has demonstrated his capacity to deliver and has shown results. This is what we need!

    ReplyDelete
  7. HONGERA NEHEMIA , NATUMAINI KUWA ULIYOFANYA CBA UTAENDELEZA HUKO NHC,INGAWAJE CBA WATAKUWA WAMEPATA PENGO.VIJANA KAMA WEWE NDIO WANAOHITAJIKA. WAJUMBE WA BODI ULIOPEWA NI WAZURI INGAWAJE NI WAKUBWA KWAKO KIUMRI, LAKINI NAAMINI HILO GURUDUMU LA MAENDELEA LITAKWENDA.

    ReplyDelete
  8. wadau tujulisheni Nondoz za jamaa toka sekondari hadi Vyuo vikuu vya University.

    ReplyDelete
  9. quite impressive, young and energetic, go do the job bro,,,..!!! wishing you all the best,...kaka.

    Magpie..!!

    ReplyDelete
  10. shule yake ni ya kawaida sana.....kwenye utendaji shule na madegree hayamati saaaaaaaaaana. jamaa kapiga BCOM udsm,amekuwa standarchartered bank kwa muda mwingi kidogo,baadaye akawa consultant kwa muda mfupi na baadaye ndo akaula CBA na sasa NHC.
    the guy is inteligent though hakuwa na matokeo ya kutisha ya degree yake...binafsi namfagilia sana na i guess he is still under 40yrs. kuna kipindi alikuwa anahojiwa kwenye tv,watu wakasema huogopi kuwa top leader at your age?wakimaanisha ukimess up huwezi kuwa na pa kushika. aliwahakikishia kuwa hatamess up na kwa kweli amefanya vema sana....
    Bravo brother

    ReplyDelete
  11. Mdau namba moja hapo juu....mambo yote yako PUBLIC SECTOR....(Mifweza kiulaiiiin....nazungumzia ukiwa kwenye post lenye akili kama alilolikwaa jamaa).....tofauti ni kwamba mifweza ya private sector inaliwa kwa STRESS!......Hongera mzee mzima......wewe ni lazima utakuwa unanyemelea SIASA.....CONGRANT!!

    ReplyDelete
  12. NYIE WENYE KUTAKA NONDOZ ZAKE NI WIVU UNAWASUMBUA, JARIBUNI NA NYIE MFIKIE HUKO ACHENI LONGOLONGO.
    JAMAA NIMESOMA NAYE MLIMANI KATI YA MWAKA 1996-1999 NA ALIKUWA KIONGOZI WETU WA DARASA KWA KAMA MIAKA MIWILI HIVI, ALIKUWA NI MWEREVU SANA DARASANI, ALIONGEA NA KILA MTU NA PIA ALIKUWA MCHANGIAJI MZURI KWENYE MIJADALA YA KIMASOMO NA KIMAISHA, BAADA YA HAPO ALIFANYA MASTERS HAPA HAPA BONGO NA SIO MTONI KAMA NYIE MALOFA WENGINE MFIKIRIAVYO.
    KIKAZI ALIBAHATIKA KUPATA KAZI MARA TU BAADA YA KUMALIZA CHUO NA KUANZIA HAPO KUTOKANA NA UFANISI WAKE MZURI AMEWEZA KUBADILISHA MAKAMPUNI KADIRI ATAKAVYO, HIVYO SIO KWAMBA ANATUMIA REFAS BALI NI MTAALAM WA KWELI.
    NATUMAI ITAWAPUNGUZIA VIROHO KOROSHO VYENU.

    ReplyDelete
  13. Angechaguliwa mzee, mngesema vijana wanakoseshwa ajira. Kachaguliwa kijana, pia mnalalamika. Hivi mie huwa nashindwa kuwaelewa wa-TZ wanataka nini hasa.

    ReplyDelete
  14. Hongera Dogo...ila huko uendako ni public sector punguza majivuno na uache kujiita nehemiah..jiite nehemia kama tulivyokuzoea ulivyokuwa mdogo lasivyo watakuendea bagamoyo..by the way one task jaribu kubadilisha utaratibu wa kupata nyumba NHC kuna rushwa mbaya ndio maana wahindi wamejaa nyumba zote...ni hayo tu ushauri wa bure sio hater

    ReplyDelete
  15. ADILI NA NDUGUZEMarch 04, 2010

    Hongera Ndugu Mhechu. Ninaamini utaweza. Kafanye kazi. Wasaidieni Watanzania wa kawaida nao wajenge mnyumba kwa mikopo nafuu. I hope NHC itajihusisha na mortgage refinancing? All the best.

    ReplyDelete
  16. Nehemia, what else to say - job well done.

    Does this mean Heri is on the way to Tanesco??

    ReplyDelete
  17. Mdau Enock

    Hebu kuwa acha utoto, shutuma zako hazina msingi. Watu kutaka kufahamu wasifu (CV) ya Nehemia haimaanishi wanawivu kwani nafasi ni moja ni lazima ishikwe na mtu mmoja ata a time. Watanzania ni best thinkers ila utamaduni wa kuzibwa midomo ndiyo utatufanya kuwa waoga wa maamuzi kwa kuhofia bwana mkubwa atakufukuza usipomfurahisha. Private sector is different from Public sector kwani sasa hivi anapoingia ni kwenye kutumia ufundi wa kuongea zaidi (LONGOLONGO) kuliko utaalam wake. ndiyo maana watu wanataka jua CV yake waone kama wamepoteza kichwa muhimu kwenye private sector.

    Believe me akikaa miaka mitatu tu huko asippokuwa makini analemaa akili kabisa. Maana anaowatumikia sasa hawana uwezo wa kuanalysize mambo kitaalam kama yeye hivyo itabidi ajishushe kulinda UNGA.

    By the way hongera sana kwa kuteuliwa ila kazi ndiyo kwanza inaanza, utaombwa Pesa ambazo hazipo na hujui pa kuzitoa, ukitumia professional basi utaanziwa majungu. Cha muhimu ni kwamba jua kula na Kipofu that's all.

    ReplyDelete
  18. I am delighted with Nehemiah's appointment. He is a DOER, DREAMER & ACHIEVER. He will certainly make a HUGE impact, politics and all. Go make us proud Mr Mchechu!

    ReplyDelete
  19. Congrats my brother duh! am proud of you!

    Jamani politics is everywhere bwana you can't avoid it Mr. Mchechu songa mbele achana na waoga najua unajiamini sana keep it up!

    ReplyDelete
  20. Am proud of you Mr. Nehemiah Kyando-Mchechu all the best

    ReplyDelete
  21. hata kama amepewa bodi members wazee kama ni mtu anayejiamini ataweza tu

    ReplyDelete
  22. Nilitamani zaidi ungekuwa bosi wa bandari nadhani pale ungefaa zaidi maana your a doer haswaaa

    ReplyDelete
  23. UNaetaka kusoma historia yake omba vodacom wakupe newsletter yao ya mwisho ametolewa yeye toka akisoma makete hadi UD. Pia tambua kwamba kujifananisha na mtu kwa ajili ya masters au phd unachemsha kuna watu wanaitwa " born leaders" hawahitaji longolongo za shule hizo ni nyongeza tu

    ReplyDelete
  24. Kwanza Hongera....hiyo nafasi ni kubwa na inaushawishi hadi wizarani....basi Tanzania tuwe na ujenzi wa kisasa na miji iliyopagwa na si mambo yale ya Buguruni na Tandale.....tupate hata mitaa kama ya ARea D and C pale dodoma.......na mkuu wale wahindi kwenye nyumba zetu wa nini...mungu akutie ujasiri FUKUZA WOTE WALE.kwani vijana wetu huko India hata hiyo residential permitt kupata ni shughuli.

    ReplyDelete
  25. Hongera Bwana Nehemia Msechu. Walaa usishangae hao wa"dual citizenship(DC)" wanavyouliza CV yako, maana kulilia kote huko hilo dudu la DC walikuwa wanategemea wao watoke huko nje waje wapewe post kama yako. Lakini sasa Mzee mzima umepewa wewe, ndio maana maneno yanakuwa mreefu! Kwa akili yao wao wanafikiri TZ iko static, watu hawasomi, wala hawajiendelezi wanawasubiri wao watoke huko ughaibuni waje washike nafasi kama hiyo yako, kwa uzoefu wao wa kubeba mabox!

    Eti jamaa CV yake? Eti tujue CV yake! Mnajiona nyie ndio mna akili kuliko hao waliompa hiyo kazi sio? Au kwa sababu hamumjui kama kina fulani kutwa kwenye mitandao na miforamu sijui hata wanafanya kazi saa ngapi.

    Waaapi, mmeula wa chuya, ngoja nilikamue hili jipu nililolipasua sasa hivi pwaaa!

    ReplyDelete
  26. tuuziwe nyumba za nhc zote sasa.

    ReplyDelete
  27. Kila la kheri kijana mwenzetu. Kikubwa jilinde na kirusi kilichopo kwenye mfumo utendaji serekalini. Tunategemea tuliyoyaona CBA tuyaone NHC, mambo ya shauri kuchukua miaka si pahala pake!

    ReplyDelete
  28. wabeba mabox mliokimbia nchi na kwenda kusoma kadegree kamoja miaka nenda rudi mnaona mambo ya vijana wadogo ndio bongo siku hizi kila kona kuna vijana wanakava nafasi

    ReplyDelete
  29. Kwa mdau aliyeuliza; ninavyojua Nehemia ana B.Com (Finance) kutoka UDSM.

    What a big step kutoka kuwa CEO wa 1 Branch Bank to NHC..

    Hengera kaka, hayo ni majukumu makubwa sana.

    Tunakutakia kila la kheri.

    ReplyDelete
  30. http://www.africarecruit.com/Tanzania_Event/speakers_profile.php


    Nehemiah Kyando Mchechu - Chief Executive Officer & Managing Director, Commercial Bank of Africa Tanzania Limited.

    Nehemiah is an inspirational and transformational leader with high level of liveliness in business management. He was born and grew in Tanzanian where he emerged as the youngest CEO in East Africa region within 7 years, particularly in the highly regulated financial sector. He is a B.com (Finance) of the University of Dar es salaam. He started his career (1999) as a junior banker at Citibank and thereafter briefly joined Barclays Bank Tanzania before joining Standard Chartered Bank Tanzania Limited as a Head of Trading – responsible for Bank’s balance sheet management, (assets and liabilities)(2001 – 2002).

    In 2002 – 2004 he took further responsibility as a Head of Global market, before his promotion to the alternate director position – Head of Global Markets and Co – Head of Wholesale Banking where he served from 2004 – 2006.

    His legacy has always been remarkable and his hand has always turned stones into gold, while at Standard Chartered Bank – he grew the business and at a later stage the business become a major contributor of revenue to the bank from 45% to 87% in 2005, whilst the number of products increased from 3 to 12.

    In June 2006, he joined United Bank of Africa Tanzania which he managed to turn around from a loss making to profit making bank in less than a year.

    Despite the aforementioned inspirational changes, Nehemiah has been a catalyst in various Financial and Economic reform activities; this includes working in various involvements in different capacities, as President of ACI- Financial Market Association – Tanzania Chapter and Chairperson of the Tanzania Financial Market Leadership Forum. He spent time to introduce global financial products while at Standard Chartered Bank this involved both BOT and Tanzania Bankers Association. Nehemiah, worked as a team Manager of the first successful Subordinated debt issue from a Commercial Banks in Tanzania and first one to be listed in the Dar Es Salaam Stock Exchange. This is the longest maturity corporate bond in East Africa to date.

    He is currently the chairperson of the University Of Dar Es Salaam Faculty Of Commerce Alumnae (UDS-FCM Alumnae), A Board Chairman of the Rightways Schools, a board member of National Investment Company Limited (NICOL) and he is also a member of several country task forces.

    ReplyDelete
  31. wadau mnaozungumzia sana nondoz naomba nikupeni mfano hao ni kwamba kule zanzibar alikuwepo raisi kwa jina anaitwa karume huyo raisi alifanya mambo makubwa sana ya kuwafurahisha wananchi na ukiangalia hana nondoz wala nini,sometimes nondozz sio big dil.mdau nchi za magharibi.

    ReplyDelete
  32. Nondo zake ni kama ifuatavyo:
    1. O-level = Mbeya (Day) Secondary.
    2. A- level = Shinyanga secondary (kama sikosei)
    3. Bachelor - UDSM
    4. Master's - UDSM
    5. PhD - 'mbado'

    Semeni jingine, msifikiri amesoma shule za st.kata secondary school huyo

    ReplyDelete
  33. Hongera sana brother Nehemia,wewe ni mtendaji mzuri kazi yako inaonekana. Tunategemea kazi yako itaonekana huko NHC pia. Mungu akutangulie katika majukumu yako mapya.

    ReplyDelete
  34. Kwa nini Mtu akipata nafasi za juu tunsema AMEULA???? Kwani huko anakwenda kula ama kuchapa kazi na kuleta ufanisi na maendeleo yaliyokusudiwa?? Hizi ni dalili za kuzoea kuiba tu sehemu za kazi !! tubadilike !!

    ReplyDelete
  35. Wabongo bwana, ushamba na ujinga umetujaa ndio maana hatuendelei. Hivi nani kwaambia midigrii kibao ndo inamfanya mtu aweze kufanya kazi? Ndo maana vijana wamebakia kuhangaika kusoma midigrii kibao lakini haiwasaidii kwenye utendaji. Hivi nani hajuai kuwa Bill Gates hana digrii? Sasa kuna Kampuni gani kubwa kuliko Microsoft? Acheni ushamba na roho korosho. Au mlitaka baba zenu wenye miaka 65 ndo wapewe hiyo post? Pambaff !!!!

    Eee Bwana mkubwa uliyeteuliwa...waonyeshe hao washamba kuwa vijana pia tunaweza...na kuwa kwenye kazi hizi si lazima jina la baba yako liwe...flani....watu na digrii za boksi...tunazijua, za ubabaishaji...kingereza kingi...kazi hamna kitu....wameniboa sana...kwaheri. Mnaruhusiwa kujibu.

    ReplyDelete
  36. Hongera saaaaaanaaaaaaaa!!!!

    Nimefurahi kuona kijana ameshika nafasi kama yako. Sasa ni wakati wako wa kutoa mchango wako kwa taifa. MABADILIKO YA KWELI. Ufanisi wa walio chini yako unategemeana na UFANISI WAKO. Wafanyakazi wa NHC watafuata mfano wako. Tupe changamoto vijana wenzako kwa ufanisi wako.

    KUMBUKA - Ukijiingiza kwenye rushwa si rahisi kutoka!

    TUPE CHANGAMOTO, MFANO, VIWANGO, MABORESHO, MAENDELEO....nimeishiwa maneno.

    Kila la kheri katika kuitumikia jamii

    ReplyDelete
  37. Napenda kumuweka sawa mtoa maoni ya Tarehe Thu Mar 04, 11:12:00 PM


    Hivi nani hajuai kuwa Bill Gates hana digrii? Sasa kuna Kampuni gani kubwa kuliko Microsoft?

    Kampuni kubwa katika sekta gani? kama ni katika software kampuni kubwa ni IBM. Msiwe mnatoa mifano msiokuwa na uhakika nayo.
    kasome hapa http://en.wikipedia.org/wiki/World%27s_largest_software_companies

    ReplyDelete
  38. Sidhani kama wadau wanaoulizia nondo za jamaa wana nia mbaya. Kwa tulio kwenye sekta binafsi tena kwa wawekezaji tunaelewa kwamba huwezi kukamata nafasi nzito kama aliyokuwa nayo jamaa bila kuonyesha uwezo. Hongera sana.

    ReplyDelete
  39. Hongera Nehemia.

    Naombeni mnielimishe...hili Shirika lina faida gani kwa Watanzania??

    Kwa nini tusiwauzie hizo nyumba Wananchi kwa bei ya Sokoni kisha hizo fedha tuzitumie kuanzisha Benki ya Mikopo ya Nyumba (Building Society). Naamini, tukiweka mfumo mzuri wenye UWAZI na sheria madhubuti za Mikopo ya kujenga nyumba hatuhitaji kuwa na Shirima la Umma linalojenga nyumba Tanzania.

    Kinachosababisha Wananchi wengi kukosa nyumba kwa sasa sio kipato (sababu hata hawa wa Ulaya hawana kipato cha ajabu, na ndio sababu wanakopa kwa miaka 15 hadi 35). Tunahitaji kuwa mfumo mzuri wa mikopo unaoanzia kwa kila Mtanzania mwenye kibapo kuweza kukopa kwa kutumia kazi yake.

    Network Engineer (NE),
    Reading, UK.

    ReplyDelete
  40. Anaoneka kidole hakina pete.Jamani mimi nauliza ameoa.Natafuta mchumba.Mseleleko wa maisha hapo.

    ReplyDelete
  41. Anon Friday March 05 JIBU NI KWAMBA AMEOA
    TENA CLASSMATE WAKE WA UDSM NA HUYO BINTI NAE YUKO JUU ILE MBAYA

    ReplyDelete
  42. Jamani Wapendwa Watanzania wenzangu mbona tu waoga sana? Kumbe ndio maana hawa jirani zetu wanakuwa Ma- CEO wa benki zetu kwa vile tunadhani kuwa CEO ni hadi huwa na Madigrii na Mamaster na MaPHD poleni sana. Uongozi ni 'KUTHUBUTU" nilisoma makala ya Huyu Nehemia na nilifurahi sana kwani alisema alipokuwa STD Bank alikuwa na nafasi nzuri lakini alifikiria kwa nini Wa-TZ hatudhubutu kuwa Ma-CEO kwenye bank za kigeni? Basi akaamua kuchukua hatua na kujiunga na UBA kama CEO na ameweza ....na ndio maana amepata hiyo post mpya acheni wivu jamani loh!

    Hata kama umekaa nje miaka kumi JIAMINI, THUBUTU, TENDA kila kitu kinawezekana. Bado BANDARI, TANESCO, TTCL, TANZANIA POSTAL, TANZANIA RAILWAY, ATCL NK TUNAHITAJI VIJANA .... PLEASE JIPENI MOYO TUNAWEZA...

    ReplyDelete
  43. anauliza kuwa ameoa...?eti hajaona pete! mkono wa pete hajauonesha hapo,tunavaa pete mkono wa kushoto...wewe kweli hujaoa/olewa hata hujui mkono wa pete!!
    the guy is married to the Luhangas family....he is 37 now. if someone is not married at this age,then there is a probblem somewhere....

    ReplyDelete
  44. Hongera sana Bro!!,
    Mdau (Tarehe Fri Mar 05, 11:43:00 AM,) acha mambo ya kizamani eti "if someone is not married at this age,then there is a probblem somewhere...." hii mbaya sana inalazimisha watu kuingia katika ndoa kwa nia ya kuondoa maneno lakini mwishowe ndoa zavunjika. kama ujapata anayefaa tulia usisikilize ya watu

    ReplyDelete
  45. Kwani umeambiwa akioa ndio hataki kuongeza mke mwingine. Acheni kuzibiana nyie.

    ReplyDelete
  46. mnaotaka kujua degree zake leteni kwanza za kwenu mkiambatanisha na picha zenu badala mumpe hongera zake mnaleta ushuzz wenu hapa hao waliosoma havard wamesaidia nini nchi? au ni kujidai tuu nina phd sijui degree kina billy g hajabukuwa wala nini lakini mifweza uspime na hao wasomi woote wanatumia mimacrosoft ya jamaa degree moja inatosha saana tu hata kuongoza nchi tizameni mapredent wa dunia hii wenye phd wachache sana achilia mbali madoctor! penye riziki hapakosi fitina!!

    ReplyDelete
  47. NYIE VIPI MMESIKIA KILA MTU ANAVAA PETE<, PETE MAMBO YA WAGIRIKI HAYO YESU HAKUWEKA MAMBO YA KUVAA PETE HAYO MAMBO YA KIENGEREZA NA UGIRIKI MAPADRI WENU WANAHITAJI KUSOMA TENA KUELEWA PETE NI NINI?.

    ReplyDelete
  48. heeee kumbe wee wa kusini??ale vakuboma,,tena mkeo "sina uhakika umeoa?"ni luhanga???wawooooo

    hongera saaaaana,ila rushwa ukiingia tu basi kwaheri kabisa na umo wavojaa manunda mazee NHC lol Mungu akutie nguvu akuwezeshe ufanikiwe lile lililo lengo lako kuu nalo ni KUNUFAISHA WABONGO na sivinevo...

    ila nyie mnaosema tena eti kwa herufi kubwa ndo nini???mwanaume wa kibongo MKE SI MMOJA tutabanana

    ata me niko safi na ni mwanamke so we make a perfect machi my kijana

    mwaaaaaaa (ivi ankal uyu jamaa anasoma izi comments?)

    ReplyDelete
  49. quote anon:FR mar 05,11:43:00AM
    "the guy is married to the Luhanga's family...he is 37 now,if someone is not married at this age,then there is a problem somewhere...."
    who told you that marriage time is stipulated somewhere and specificaly set that if you cross it then you are categorized as having a problem? that is your grand pa's idea right? marriage time is a decision and not a dogma! only the country law set the legal minimum age to enter into matrimonial bond but not the maximum! i guess you get this!!!
    nyie ndio walewale mtu akiamua ku adopt mtoto na kutozaa mnaanza ooh huyu ni hanithi hazai au ni sterile hana mbegu.vitu vingine maamuzi tu.sio kila siku ni ijumaa siku zingine j'3 zingine j,4 n.k
    mnoko

    ReplyDelete
  50. Mungu Akutangulie naamini unaweza kwa sababu umeonesha uwezo katika sehemu ulizokwishafanya kazi. Bravo my lovely bro

    ReplyDelete
  51. The Network Engineer (NE) is got a point, Msechu and bloggers plz revisit.

    ReplyDelete
  52. bravooo Nehemia Kyando Mchechu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...