Mpiga Picha Mkuu wa Globu ya Jamii mdau Francis Dande akimpa mkono wa pole Maalim Seif Shariff Hamad kitandani pake katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar alikolazwa kwa matibu
Maalim Seif Shariff Hamad akipokea mkono wa pole toka kwa Dk. Swedi ambaye ni mmoja wa watu kadhaa waliokwenda kumjulia hali leo hospitali ya Hindu Mandal Jijini Dar
Maalim Seif akiongea na TBC leo

Wanahabari wa TBC-1 wakimhoji Maalim Seif leo

Hali ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad, imeimarika kiafya baada ya kupata matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar leo.

Kuimarika kwa afya ya mwanasiasa huyo mwandamizi wa kambi ya upinzani na Katibu wa CUF imeondoa hofu na minong’ono iliyoenea jijini kwamba Maalim Seif, amefariki dunia.

Maalim Seif amesema tatizo linalomsumbua ni kupanda kwa shinikizo la damu na kwamba juzi lilimsababishia kushindwa kusafiri.

Amesema shinikizo la damu lilipanda ijumaa saa 11 jioni alipokuwa akisubiri kupanda ndege kwenda Oman kwa ajili ya shughuli zake binafsi.

“Kweli nilipata matatizo ya kiafya kidogo ijumaa iliyopita kama kwenye saa 11 jioni wakati nasubiri kwenda Oman kwa shughuli binafsi, ndiyo hali ilipobadilika ghafla... lakini sasa naendelea vizuri tatizo kubwa ni high blood pressure (kupanda kwa shinikizo la damu) ila tangu nilipolazwa haijapanda tena.

“... Ugonjwa huu unanisumbua tangu mwaka 1989 lakini kwa kipindi kirefu ulikuwa under control (chini ya uangalizi) ila kwa sasa naona limekuwa kubwa mno, nadhani ni kwa ajili ya kazi nyingi.

“Madaktari wamenipima moyo wameona upo safi, damu safi na mapigo ya moyo yapo safi sasa wamenipumzisha na Mungu akipenda leo jioni au kesho Inshaalah nitaruhusiwa,” alisema Maalim.

"Kwa sasa hali yangu imeimarika na nipo chini ya uangalizi wa madaktari kwa ajili ya kupumzika wakati wakiendelea kudhibiti shinikizo hilo la damu alisema mkongwe huyo wa siasa visiwani Zanzibar."

Aidha, Maalim Seif liwashukuru Watanzania walioguswa baada ya kupata taarifa za ugonjwa wake na wengi wao kmtumia salamu za pole hali iliyomfariji na kuona jinsi wananchi wanavyoshirikiana.
-----------------
Unaweza kumuona na kumsikia
Maalim Seif alipohutubia London majuzi
kwenye video hii iliyoletwa na Da' Subi na
kuandaliwa na mdau wa London (maelezo chini)

DVD zinapatikana kwa kuwasiliana na wahusika kwa namba zifuatazo (+44) {07957632385} au (+44) {07595485727} au kwa email ebrahim628@hotmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mmh jamani hakuna privacy? hivi mgonjwa anawezaje kupumzika? kila mtu on his face? Ndiyo mwanzo wa kumpelekea magonjwa mengine kama mafua, na jinsi ambavyo watu hawana mazoea ya kunawa. Waacheni nduguze ndiyo wakamuone

    ReplyDelete
  2. mmh publicity hadi kitandani? ebu mpeni nafasi mgonjwa na wagonjwa wengine.

    ReplyDelete
  3. Pole sana mtu mzima, kama shughuli za chama tu zimekuwa nyingi sana mpaka zinafanya hali iwe hivyo. Je ukiwa Raisi, tena wa Zanzibar?

    pole sana mkuu

    ReplyDelete
  4. watanzania wengi hasa wa kanda ya pwani na mijini tuna high blood pressure kwa ajili ya kula mafuta mengi na mapishi ya nazi ni muhimu sana kuangalia mafuta tunayotumia yale ya chipsi za mitaa ni hatari zaidi kwa sababu hayabadilishwi nazi ni hatari kwa sababu mwilini inaganda na inasababisha high cholestrol inaenda kublock mishipa ya damu.mafuta mazuri ni alizeti na sio kujipasua michapati mimaandazi mapilau na machipsi kuleni michemsho na kuwa active.

    ReplyDelete
  5. GET WELL SOON MAALIM!!!!HOPE ALLAH WILL BE WITH YOU.INSHAALAH.
    Mdau wa UK

    ReplyDelete
  6. Pole sana Maalim Seif.
    Tungekushauri bora ujipumzishe,ubishi haufai bw.mkuu.
    Sasa kama utachaguliwa kuwa Rais si Ikulu itahamia mahospitalini?
    Mkuu jimpuzishe ubishi haufai

    ReplyDelete
  7. wimbo wa hii video huko london upo poa sana.anyway pole sana maalim seif uzushi wa watu ni kheri kwako utaishi miaka mingi endeleza libeneka baba.

    ReplyDelete
  8. Michuzi au mdau yeyote ambaye anaweza kunielekeza jinsi yakupata kanda za mashaili kama haya anielekeze nitashukulu sana.Mimi ni mkristu sio muislam lakini naipenda dini la kiislam.Aslaam walekum.Ni mdau wa Amsterdam.

    ReplyDelete
  9. Hakuna anayewapata waingereza kwa misamiati...kwenye hali kama ya Maalim wangekuambia....SERIOUS BUT STABLE!

    ReplyDelete
  10. mie mkristo lakini huo utenzi umenisimamisha nywele za shingo. very good

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...