KIKOSI CHA ZIMA MOTO KUWACHUKULIA HATUA WATU WOTE WATAKAO KAIDI AMRI YA KUNUNUA VIFAA VYA KUDHIBITI MOTO.
(Na Veronica Kazimoto – MAELEZO)
(Na Veronica Kazimoto – MAELEZO)
Naibu Kamishina wa Usimamizi na Uangalizi wa vikosi vya Zima moto na uokoaji Bwana Rogatius Kipali amesema ifikapo tarehe 30, Aprili mwaka huu watu wote ambao hawatakuwa wamenunua na kufungiwa vifaa vya kudhibiti moto – fire extinguisher, watalipa faini ya shilingi laki moja na kuendelea kulingana na ukubwa wa maeneo yao pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza ofisini kwake jijini Dar leo, Bwana Kipali amesema zoezi hili litafanyika nchi nzima na faini hizo zitahusisha majengo yote, ofisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali pamoja na maeneo ya biashara.
“Ni wajibu wetu kusimamia uwekaji wa vifaa vya kudhibiti moto kwenye majengo ya watu, ofisi, magari na maeneo yote ya biashara na kama watu hawatatekeleza agizo hili basi watatakiwa kutoa faini ya pesa tathilimu na wengine chukuliwa hatua za kisheria.” Amesema Bwana Kipali.
Kuhusu suala la uelimishwaji juu ya matumizi ya vifaa vya kudhibiti moto Bwana Kipali amebainisha kuwa mawakala wote waliopewa kibali cha kuuza na kufunga vifaa hivyo wana watalaamu ambao huwaelimisha wananchi namna ya kuvitumia na kuvitunza pindi wanapovinunua kutoka kwenye ofisi zao.
“Mawakala wote tuliowapa kibali cha kuuza na kufunga vifaa vya kudhibiti moto wana wataalamu wa kuwaelimisha wananchi namna ya kutumia vidhibiti moto na ndio wanaohusika kufunga vifaa hivyo kwenye maeneo ya wananchi na kuvifanyia ukarabati pindi huduma hiyo inapohitajika.” Ameongeza Bwana Kipali.
Amewataja baabhi ya mawakala waliopewa kibali kuuza na kufunga vidhibiti moto kuwa ni Adjef Intergrated LTD walioko Sinza A, Modern fire & General services walioko mtaa wa Miteja Temeke, Wino works LTD walioko mtaa wa Mafia Kariakoo na Sagom General Enterprises walioko mtaa wa Muhonda namba 9 Jangwani.
Wengine ni Unifarm Industrial Services walioko Mwanza mjini, Zanzibar Fire Protection Engineering walioko Amani Magogoni Zanzibar, Tradegate Investments walioko barabara ya Bagamoyo na taarifa za mawakala wengine hupatikana katika ofisi za zima moto zilizoko mikoa yote Tanzania.
Hata hivyo Bwana Kipali amekili kuwa mwitikio wa wananchi kununua vifaa vya kudhibiti moto ni mdogo sana hivyo anawaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kununua vifaa hivyo kwa mawakala walioko maeneo mbalimbali nchini kabla ya tarehe iliyotajwa hapo juu.
Agizo hilo la kununua na kufunga vifaa hivyo vya kuzima moto limefuatia kukithiri kwa matukio mengi ya moto nchini zikiwemo shule. Hivyo Serikali kupitia Jeshi lake la Zima Moto imejipanga kukabiliana na kutokomeza matukio hayo.

Hivi taxes tunazolipa pesa zinakwenda wapi? Kwahiyo tulipe taxes halafu mtupige mikwara tena kuwa mtatupiga faini kwa nyinyi kushindwa kutekeleza majukumu yenu? Masalaaallleeee BONGO NI TAMBARARRRRREEEEEE
ReplyDeleteNchi nyingine duniani tax payers' funds zinatumika kugharamia zimamoto. Tanzania tax payers funds zinatumika kwenye kampeni za kisiasa. Ndio maana tuko masikini miaka 50 baada ya uhuru.
Sijawahi kuona sehemu yoyote duniani iwapo mtu analazimishwa kunua kifaa cha kuzimia moto nyumabni kwake.
ReplyDeleteKwa kawaida serikali inatakiwa kuingilia kati katika masuala ambayo likitokea litamuathiri mtu mwingine bila ya yeye kuwa na makosa mfano ajali inayosababishwa na gari inaweza kummuumiza mtu mwingine ndiyo maana "third party insurance" ni lazima lakini "comprehensive insurance" siyo lazima.
Kinachotakiwa ni elimu na watu kuwa na bima za moto badala ya kutumia nguvu. Swali la msingi ni kuwa ni vipi gharama hizi zitaonyesha unafuu katika gharama za bima ya moto?
Kwa maoni yangu mimi hii ni njia nyingine ya serikali kukusanya fedha kwa ajili ya kikosi cha zima moto. Nadhani wangetafuta njia nyingine ya kutafuta fedha.
nchi yetu hii mambo ya kupigiana cross kwa kulazimisha watu kununua kitu wasichohitaji yataisha lini, walileta dili la vidhibiti mwendo wakalazimisha wenye mabasi wafunge,
ReplyDeletewalileta mgao wa umeme usio na mpango ili watu wauze majenereta, sasa wanaleta habari ya fire extinguishers, wakati fire brigades za dar zina sifa ya kufika eneo la tukio bila kuwa na maji ya kuzimia moto!
huyu anaetoa hii amri na yeye achukuliwe hatua za kisheria!
Hii nchi ni nchi ya ajabu nafikiri duniani hakuna. Nyie viongozi wa serikali mko wapi? mtu anaishi kwa siku kwa matumizi ya chini ya dola moja ya kimarekani leo ukamwambie afikirie kununua fire extinguisher? Muda wa Kampeni umefika sasa mmeanza kufikiria wapi mpate pesa. tutaandamana nchi nzima. Hatununui Extinguisher zenu. mmelazimisha watu wenye magari wa nunue mmeona pesa haitoshi sasa nyumba kwa nyumba. Ngojeni basi muone kama tutanunua.
ReplyDeleteWadanyanyika tunavunwa kimtindo. Ukiona hivi ujue wapuuzi walishaleta mzigo wa kutosha na commissions zimeshatembea.
ReplyDeleteJAMANI HII IKO VIPI SI AFADHARI WATU WANGEANZA NA KOZI YA KUZIMA MOTO KWANZA PAMOJA NA KUJIOKOA MOTO UNAPOTOKEA. HAPA NAONA MZEE MZIMA HAJA WEKA KINGA BADO ILA KAONGEZA MTAJI TUU.
ReplyDeleteSERIKALI ITAJENGA LINI MABOMBA YA KUZIMIA MOTO MITAANI HAPO VIPI?. TOA KWANZA KIJITI KWENYE JICHO LAKO
ReplyDeleteHivi zimamoto na uokoaji wana hedikopta hata moja? ndege ya kuzimia moto je? je meli ya kusaidia kuzima moto baharini?? na je, mji mkuu Dodoma umeshapata zimamoto baada ya ile zimamoto moja iliyokuwepo mkoa mzima kupata ajali? hivi moto ukiwaka gorofa ya 35 ya jengo jipya la TPA mtaweza kuzima? kuokoa watu je?
ReplyDeleteHuyo anayetoa orders aache upuuzi...huwezi ghafla waambia watu wanunue vifaa,watu wanaishi kwa mpangilio kutokana na vipato vyao...hiyo faini ni kutaka kuwanyanyasa wananchi,huo ni upumbavu...vitu vinaenda taratibu wape watu muda...toeni elimu ya watu kujiepusha na majanga ya moto kwanza.
ReplyDeleteINA MAANA HATA NYUMBA ZETU ZA MTAANI TUNATAKIWA KUNUNUA FIRE EXTINGUISHER? TUSIPONUNUA NDO FAINI, EBU NAOMBA JIBU KWA HILO. HATA HIVYO SIKUBALIANI NA HUYO OFISA WA SERIKALI WA ZIMA MOTO, KWANZA HANA UWEZO WA KUTUNGA SHERIA, SHERIA ZINATUNGWA NA BUNGE TU NA HATA SHERIA NDOGO NDOGO HUTUNGWA NA MADIWANI SI YEYE, PIA HANA UWEZO WA KUPANDA FAINI YEYE NI NANI, KIKWETE EBU FUKUZA KAZI HUYU MTU ASIYEJUWA MIPAKA YA KAZI YAKE, ATAFANYA TUCHUKIE SERIKALI YAKO BURE NA HUU NI MWAKA WA UCHAGUZI TUTAMPA NNJI HII MREMA, TUNATAKA UFAFANUZI WA HILI, TUTAFIKISHANA MAHAKAMANI. wananchi tusimamie haki zetu miaka ya kuburuzana imepita
ReplyDeleteNdugu Mheshimiwa:
ReplyDeleteLENGO HASA HASA HASA HASA LA MRADI NI NINI??????
NA HATIMAYE KWA AKILI YENU MMELENGA KUFANIKISHA KITU GANI?????
Waelezeni wananchi malengo mahsusi ya 'mradi wenu wa fire extinguishers' na jinsi wananchi watakavyonufaika. Hii sio nchi ya kijeshi ya kukurupuka asubuhi na kutoa amri kwa wananchi wafuate unachotaka!!
Wiiiizi Mtupu! Ukiona hivi ujue wanafanya fundraising ya kisirisiri kuwakamua walipa kodi!
ReplyDeleteWalikuwa wapi siku zooote why now? Mwaka wa uchaguzi?? Mnadhani wa TZ mandondocha hawana uwezo wa kufikiri? Acheni sanaa na wizi wa asubuhi kweupeee!!
HATUNUNUI, NYIE NDO MTUNUNULIE UNLESS KITENGO CHA ZIMAMOTO KIFUTWE TUWE TUNAJITEGEMEA KATIKA KUJIOKOA NA MAJANGA
ReplyDeleteHii ni nchi ya kulala na kuamka kufikiria la kufanya bila mipango maalum.
ReplyDeleteHuyu jamaa wa zimamoto kaona hana kazi ya kufanya, hivyo na huu ni mradi wa kujiingizia ela kama wengine wote wanavyofanya. Hawana uchungu na wananchi, wao kwao ela tu. Alafu matakwa yao yanakuja kwa vitisho. Ufisadi bongo hadi lini?
Wabongo kaeni IMARA.
tenda ya nani hiyo...inaelekea kuna kiboba mmoja ameingiza hizo fire extingisher nyingi sasa kaona hazitoki akaenda kubeep ili iwekwe sheria watu wakazinunue ....bongo tambaraaaaaare
ReplyDeletesinunui kamwe!!ya gari tu inantosha basi
ReplyDeletetuone sasa
NDUGU ZANGU WADANGANYIKA ! KWA KWELI HII SERIKALI SASA IMETUCHOKA, WANATUFANYA WANANCHI KAMA WAGAGAGIGIKOKO , KWA DUANIA YA SASA LAZIMA KILA KITU KIWE NA MPANGILIAO , KINA KERO NGAPI ZIKO JUU YA MEZA ZAO HAZIJASHUGHULIKIWA ? HILA INAPOFIKA WAKATI WA KUMKABA KOO MWANANCHI WANANJIFANYA WAO WAJANJA ...NADHANI HUYU JAMAA HAYUKO SAWA SABABU HIZO AMRI ZIPO KWENYE SERIKALI ZA KIJESHI WAKITAKA KUSAIDIA WANANCHI KWANZA WAANZE NA KILIMO KWANZA , WAKITAKA MSAADA WAPUNGUZE MATUMIZI YA SEMINA ZISIZO NA TIJA, MAGARI YA KIFAHARI ,NA SAFARI ZISIZO NA UMUHIMU , TUNAMPONGEZA JK KWA KUANZA KUDELEGATE SAFARI ZAKE ..LAKINI TUNAMWOMBA AMSHUGHULIKIE HUYU KAMISHAN KWANZA... ALAFU WAONYESHE MFANO KUANZIA KWENYE OFISI ZA SERIKARI, MAGARI YA SERIKARI , ALAFU WAWEKE MABOMBA YA KUZIMIA MOTO KWENYE MITAA YENYE MAGHOROFA MAREFU ..WAO WENYEWE HATA MFANO HAWANA ALAFU WANALETA AMRI SIZIZO NA KICHWA WALA MIGUU..HATUPINGI ILA ELIMU NA BUSARA ZITUMIKE SIO KWA KUWAENEMESHA WATU WENGINE [HETI TUKANUNUE HIVYO VIFAA KWENYE MADUKA YALIYOTAJWA NA KAMISHNA KWA SABABU YEYE ANA % YAKE ] TAKUKURU INGILIENI KATI SIO MNALALA LALA TU ASUBUHI WAKATI HUU
ReplyDeleteee bwana weeee? fire extinguisher kwenye gari? sio basi au lori gari ya kawaida mtu anatakiwa awe na fire extinguisher? heko tanzania!!!
ReplyDeletesuali ni moja tu ni nani muingizaji mkuu na distributor mkuu wa vifaa hivi nchini tanzania?