Mshambuliaji Peter Crouch (shoto) akishangilai moja ya mabao yake mawili yaliyoiwezesha England kuitoa Misri kwa bao 3-1 uwanja wa Wembley huko London usiku huu.
Huko Mwanza, Taifa Stars iliyomenyan na Uganda imepigwa bao 3-2 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwa mujibu wa kalenda ya FIFA. Yafuatayo ni matokeo ya michezo mingine kwa mujibu wa BBC SPORT

Albania1-0Northern Ireland
Algeria0-3Serbia
Angola1-1Latvia
Armenia1-3Belarus
Austria2-1Denmark
Belgium0-1Croatia
Bosnia-H2-1Ghana
Cyprus0-0Iceland
England3-1Egypt
France0-2Spain
FYR Macedonia2-1Montenegro
Georgia2-1Estonia
Germany0-1Argentina
Greece0-2Senegal
Hungary1-1Russia
Italy0-0CameroonFT
Ivory Coast0-2South Korea
Luxembourg1-2Azerbaijan
Malta1-2Finland
Moldova1-0Kazakhstan
Netherlands2-1USA
Nigeria5-2Congo DR
Poland2-0Bulgaria
Portugal2-0China PR
Romania0-2Israel
Scotland1-0Czech Republic
Slovakia0-1Norway
Slovenia4-1Qatar
South Africa1-1Namibia
Switzerland1-3Uruguay
Turkey2-0Honduras
Wales0-1 Sweden
Tanzania 2-3 Uganda
For Source

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Nilivyockia ile nyimbo ya wagosi wakaya FATI na SOKA nikajuwa 2mefungwa maana hii nyimbo mara nyingi inapigwa 2kifungwaga 2 why????

    ReplyDelete
  2. Tanzania bado tuna safari ndefu.. mechi ya nyumbani hatujui wafungaji wala hamna picha, mechi ya ugenini, wafungaji wanajulikana na picha ziko hewani.
    Na hapo ni Michuzi, vyombo vya habari vingine.. hadi kesho au keshokutwa.. Tabu sana.
    Shukrani kwa habari hizi.

    ReplyDelete
  3. Hivi kuna mechi ambayo sisi tutashinda kweli..well, ngoja tujipe matumaini lakini safari ni ndefu..

    ReplyDelete
  4. nauliza hivi ni kweli afande sele alimpiga MABUSU madee mbele ya screen wakati wa final ya maisha plus?

    ReplyDelete
  5. watu hawakawii kuibua mjadala wa maximo hapa

    ReplyDelete
  6. Waandishi wa habari wameshamwondoa Maximo nchini ndio sababu unaona kimya. Waliona anawadharau kwa sababu alikuwa hapangi listi wanayotaka wao. Matokeo yake wameanza kuua na hamasa ya wazalendo. Tusubiri kina Mmatumbi wakikabidhiwa labda watatufikisha.

    ReplyDelete
  7. Hata kama tukiletewa kocha aliyefundisha mabingwa wa kombe la dunia (Italia) hatutafanya vizuri tuu.

    Jamani, mipira yenyewe ya kujifunza ukubwani, tutafika wapi? Mtu tayari amekwishaanza kulea ndiyo anakwenda kujifunza mpira, wapi bwana!! Ataweza wapi kunyumbuka kupiga chenga, krosi za haraha haraha, mashuti ya papo kwa papo!! Hata wacheza sarakasi tu hawaanzii ukubwani, wanaanza udogoni ili iwe rahisi kujikunjakunja.

    Tatizo letu tunataka mafanikio ya haraka haraka. tuanzeni mbali basi. Kila mkoa uwe na timu za kujenga vipaji kuanzia shule za msingi, hata ikiwezekana kuanzia Awali. Hapo tutafanikiwa. Vinginevyo, tutaishia kupeana majina ya vichwa vya wendawazimu.
    Kama hatuwezi, basi tuamue kuacha kabisa kuliko kung'ang'aniza kitu tusichokiweza. tulikuwa tunaweza kukimbia, sasa nako tabu tupu. WAPI TUTAMUDU NA KURUDISHA HESHIMA?
    Tutamaliza makocha tu wala hatutafanikiwa. Mipango ya katika makaratasi na ahadi za ushindi wa mdomoni, ooh, sisi ni mabingwa. Unfortunately, we are best impractical.

    KAZI TUNAYO MICHUZI!!

    KWAHERI.

    ReplyDelete
  8. Mjadala wa Maximo ni muhimu. Ukichukulia kipigo ilichokipata stazs kwa Uganda. Binafsi sioni tija ya kua ma maximo.Stazs bila Maximo inawezekana.

    ReplyDelete
  9. Mkuu wa wilaya ya nanii BBC wameweka mechi za jana Tanzania na Uganda walicheza juzi, ila umejitahidi kutuweka na Tanzania kwenye ramani ya dunia japo kupitia blog ya jamii. Ila BBC wameisia na Wales 0 - Sweden 1

    ReplyDelete
  10. Michu umejitahidi kuichomeka TZ na Uganda ila umechesha kitu kimoja. Hukugundua kuwa Jamaa walipanga nchi ki Alphabet Tanzania V Uganda ilitakiwa uipachike kati ya (Switzerland V Uruguay) and (Turkey V Honduras)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...