Pichani ni waigizaji mahiri wa Filamu hapa Bongo, Irene Uwoya na Dr Cheni wakiigiza moja ya Filamu itakayokuwa ya aina yake iitwayo MR DREAMS,ambayo inashutiwa na kampuni mahiri ya Rj Productions ikiongozwa na Ray a.k.a The Greatest.
Ukitaka kujua kuhusiana na mambo lukuki juu ya Filamu hiyo na mambo mengi mengineyo ya wasanii wa Filamu na uandaaji wake basi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. bongo bwana!yaani kikianza kitu basi kila mmoja akili hukohuko,sasa kaibuka kanumna anajiita the great,huyu aye sijui ray ameamua ajiite the greatest,sasa the greater than ajitokeze maana hakawii. hii yote ni dalili ya ubongo kutokuwa active kufikiria mbali.

    ReplyDelete
  2. Hiyo Movie ikiuzika, huyo Camera man alipwe pesa nzuri ili naye atakate kidogo na kutoa shavu.

    Msimbanie mshiko wakati kazi yote yeye ndo kahangaika na hali yake ndo hiyo kama tumuonavyo.

    ReplyDelete
  3. Which is which - 'The Dream(s)' au 'MR. Dream'?

    ReplyDelete
  4. Jamani acheni Irene is Beautiful!!!

    ReplyDelete
  5. Hivi we Michuzi. Kwani huyu Airin Uwoya kaachika au amekuja likizo?

    Si mlisemaga kuwa aliolewaga na mcheza mpira mmoja na sasa anaishi Saiprus?

    ReplyDelete
  6. mi hapo wabongo ndo wanaponiachaga hoi..waangalia hizo ''muvi'' zao kwa kiasi kikubwa kabisa ni waswahili..lakini angalia hayo majina..sijui mr.dreams, mara sijui the blind side of marriage mara sijui upuzi gani..kwani masela lazima muvi zenu zitamkwe ''kidhungu''?hao waangaliaji wenyewe utakuta anasimulia muvi flani lakini ukimwambia nitajie jina anapata tabu kuumba maneno kutaja jina..asa mazee huu si utumwa wa kiakili?tuwekeeni majina ya kiswahili kama muvi nzuri itanunulika tu..afu pia mnaboa sana kwenye zile tafsiri za lugha (subtitles) mnazoweka mkipeleka muvi Dstv..kuna moja (jina kapuni) dada alikuwa anashuka ghorofani mwenzie anamsubiri sebuleni basi akamwambia nisubiri nashuka lakini subtitle ikasomeka: wait i am coming from top up to down!!!kama mmeamua kwenda international kwa nini msitafute watu wanaojua lugha wawatafsirie?ni mtizamo wangu tu wadau msijenge chuki..

    ReplyDelete
  7. aaaah yani nimecheka!!

    irene analipa saaana,wenye majina aya kiboko

    ReplyDelete
  8. Dah bongo bwana....kwa hiyo The great ni Kanumba ,the greater(labda cheni ) ,the greatest(Ray)--
    Halafu hivi ni lazima kuwa na titles za kizungu kwenye filamu zetu za kiswahili??au ndio sheria za filamu???
    Yeah Irene iko makini ila amejiachia...amenenepa --taratibu shosti

    ReplyDelete
  9. NINAAMINI LUGHA INAYOTUMIKA KWENYE PICHA HIYO NI ILE INAYOENDANA NA TITTLE YAKE VINGINEVYO ITAKUWA MALI YA MCHINA.

    ReplyDelete
  10. Yaani huyu jamaa anamwacha mywife wake anakumbatiwa hivi. Mimi sikubali hata kidogo, mambo mengine huanza taratibuuuuuu....

    ReplyDelete
  11. We namba mbili acha utoto. Jamaa namfahamu vizuri anashinda gym anafanya mazoezi. Makaratasi yenye picha ya baba wa taifa na wanyama mbali mbali hayampigi chenga hata kidogo. Usifikiri kafulia anazo huyo bali ana adabu katika KULA. Nami nina mpago wa kumwiga siyo kila siku Mbuzi katoliki, mtu ananenepeana mpaka anatisha

    ReplyDelete
  12. JAMANI MBONA GLOBAL PUBLISHER VIP? NAWATAFUTA ONLINE LAKINI SCREEN BLANK, ANAEJUA TATIZO PLEASE LET ME KNOW HUWA WANA NYUUZI NZURI NA UDAKU KWA SANA

    ReplyDelete
  13. Ndoto ya mchanaMarch 03, 2010

    Hivi hizi wanazohita movies au sinema ni sinema kweli au michezo ya kuigiza wanayoita movies au sinema?Sidhani kama zina viwango vya kuitwa sinema.Kuna udhaifu mkubwa sana toka kwa wapiga picha,uchanganyaji wa picha,waigizaji wenyewe,waandishi wa hadithi wa hizo sinema,vitu vingi vya kiufundi vinakosekana.Ila kuna nafasi nyingi ya kurekebisha hayo.

    ReplyDelete
  14. kwlei kabisa anon hapo juu utakuta actor huyo huyo ndo director, ndo editor , ndo producer, ndo location manager, ndo cast manager and kila kitu . Hebu niambie huyo ray na kaumba wamesomea wapi movie making kama sio kutulisha kanyaboya halafu sasa wanvyojisifia no utakoma . Hebu tujaribu kujali professionalism na sio kujifanya tunajua kila kitu. I dont envy them but this is the truth and they have to live with it

    ReplyDelete
  15. we mdau hapo juu irene hajaachika ng'oooo amekuja kushoot hiyo movie then anarudi visiwa vya syprus kwa husband wake umeelewa eehh ina maana mamako akienda likizo kwao naye kaachika?? acheni hizoooooooooooooooooooo!!!

    ReplyDelete
  16. kaa we mkware jitahidi hata kuandika basi eti Airin mara syprusi.

    ReplyDelete
  17. hebu jamani niulize swali!hivi mtu anajisikiaje pale anapo jibandika title ambayo hana,ama kuridhia kuendelea kuitiwa title hiyo wakati huna tutle hiyo.
    tunafahamu waigizaji wengi sehemu tofauti duniani huigiza katika role tofauti za maisha halisi,wengine kama wakurugenzi,raisi,maafisa wa kijeshi au viongozi wa kisiasa na kidini,lakini mara baada ya movie,comedy,drammer zao huwa hawaendelei ku-retain majina ya title hizo pamoja na majina waliyoyatumia katika sanaa zao hizo.
    sasa inakuwaje hawa kina cheni waendelee kujiita/kuridhia kuitwa Dr.cheni kisa eti aliwahi kuigiza kama daktari,wengine wajiite maprofessor n.k jamani title zingine msidhani zinapatikana kimzaha chondechonde!!!mbona wanaoigiza kama wagonjwa,marehemu,mwasaidizi wa ndani,n.k hawaendelei kujiitia role hizo katika maisha ya kawaida?
    nadhani hapa kuna mushkeli kidogo.

    ReplyDelete
  18. Hizo ni Drama, kuna tofauti kati ya Move na Drama, they call them Soaps not Movies, Like ISIDINGO, TAUSI, EAST ENDERS, EMMERDALE these are not moves they are DRAMA, SOAPS.

    ReplyDelete
  19. Hata mimi nasema huu upuuzi wa kuandika majina ya kizungu wala haulipi. Mimi napenda foreign movies na kuna mahali ninarent kila weekend movies zinatoka italy, france na spain. Zote zina majina ya kikwao na wanaongea kikwao nazina market kishenzi hapa nilipo. Na zingine zimeshaalikwa kwenye Sundance film festival....

    Sasa kama na nyie mnataka kufikia huko na ikipendwa zaidi ndio hivyo tena...jitahidini na kukeep culture na language yetu UP.....

    Halafu movie moja pia niliona kuna msichana mmoja hivi ..sijui yeye ndio najua kidhungu mwenyewe...yeye anaongea kingereza wengine wanamjibu kiswahili. Kama ni kiswahili kwanini msiongee wote kiswahili au kama ni kidhungu kwa nini msiongee wote kidhungu?

    Halafu mambo ya kuweka miziki ya watu kwenye movie zenu siku zikiwafikia wenyewe mtafilisika mpaka mkome. Sijui mnalipia hizo nyimbo au hamjui mambo ya copyright...Movie nimeona wameweka wimbo wa Celine Dion yeye alikua napepea kwenye ship wao wanaenda kule masaki sijui oyestebay kwenye ile mwamba wanapepea na kupiga wimbo wa celine ..."my hearth will go on...." Kwani hao wanamziki wote hapo bongo hamuwezi kuwaambia wakuandikie wimbo kuendana na movie yako na kurekordiwa kwa kiswahili?

    Chukueni hizi movie za france, italy na spain muoangalie mtaelewa what I am talking about.

    Halafu kingine kama mnataka zije kwenye masoko ya kimataifa mpunguze muda au mtafute editor mzuri. Movie ina twist and turns kibao ...movie inaanza na idea hii inaishia na ile... movie ina party one, two na hata three agrrrr. Nani anahuo muda wakuangalia movie moja kwa party tatu...si muwele siquel then kieleweke......nenda na wakati......

    Jersey Girl

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...