Miss TZ 2006 Richa Adhia akipungia baada ya kutawazwa Samsung Miss TZ India 2010 na kuwa mwakilishi wetu katika fainali za Miss India Worldwide zitazofanyika mwisho wa mwezi huu huko johanesburg sauzi.
richa adhia akipokea LCD ya samsung kama moja ya zawadi zake
bango la samsung miss tanzania india likizinduliwa
balozi wa india nchini Mh. K.V. Bhagirath akitoa hotuba yake

balozi wa India nchini Mh. Bhagirath akimpa kadi mama yake richa wakati wa hafla hii
mdau Josh wa EATV na kikosi kazi chake wakijiandaa kufanya intavyuu na richa
ankal alikuwepo kupiga konozzz
Richa na wadogo zake
ankal hashim lundenga na miss tz 2009 miriam wakimpongeza richa
simba theatre troupe walitoa burudani
THT waliburudisha na miondoko ya kihindi
mwandaaji na mbunifu wa mitindo mustafa hassanali na mamodo wake
balozi wa India nchini Mh. Bhagirath (wa pili kulia) na wageni waalikwa
SAMSUNG Miss Tanzania India yazinduliwa rasmi.
*Richa Adhia kuwakilisha TANZANIA
*Uwakilishaji wa TANZANIA kwa mara ya
kwanza kwenye 19th MISS INDIA WORLDWIDE

Samsung Miss Tanzania India imezinduliwa jana usiku kwa tafrija iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar-es-Salaam.

Miss Tanzania India ni jukwaa linalotoa fursa kwa wanawake wa Kitanzania wenye asili ya Kihindi kuweza kushindana kuonyesha urembo na vipaji vyao ambapo mshindi ataiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kidunia ya Miss India worldwide.

Ikiwa ni mara ya kwanza, Miss Tanzania India imedhaminiwa na Samsung Electronics, kampuni inayoongoza kwenye nyanja ya mawasiliano duniani na hivyo kufanya ipewe kipaumbele kwa kuliitwa kwa jina la Samsung Miss Tanzania India.

“Mshindi wa Samsung Miss Tanzania India mbali na kuitangaza Tanzania kimataifa pia atajihusisha na shughuli za kijamii ikiwa na pamoja na kuchangisha fedha zitazotumika kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ya Kitanzania” alisema Bi. Sati Gadhvi msemaji mkuu wa Miss Tanzania India.

“Mwaka huu ikiwa ni mara ya 19 kwa mashindano ya Miss India Worldwide yatakayofanyika tarehe 27 Machi 2010 kwenye ukumbi wa International Convention Centre mjini Durban, Afrika Kusini. Mrembo Richa Adhia ataipeperusha bendera ya Tanzania kwenye mashindano hayo” aliongezea Bi. Gadhvi.
Uzinduzi wa Samsung Miss Tanzania India umeenda sambamba na kusheherekea siku ya Wanawake duniani kwa tafrija ya “Bollywood Party” pamoja na DJ maarufu kutoka jijini Mumbai nchini India DJ JULZ.

“Sisi kama Samsung tumeona kuna umuhimu wa kuunga mkono shughuli za maendeleo ya wanawake. Miss Tanzania India imeandaa jukwaa maridhawa kwa kuweza kujadili mambo mbalimbali ya kijamii na kutatua matatizo yatakayoelekea kuboresha maisha ya jamii husika na kuhamasisha vijana kukabiliana na matatizo mbalimbali .
Hii si kwa ajili ya urembo tu bali pia kuboresha mwonekano maridhawa inayoelekea kwa Samsung kuwa na bidhaa zinazoongoza kwenye nyanja za mawasiliano” amesema Simon Kiriithi, Meneja wa Samsung Tanzania.
“Uzinduzi wa Samsung Miss Tanzania India Inaenda sambamba na kusherehekea siku ya wanawake duniani” Alihitimisha Bi. Gadhvi

Kuhusu SAMSUNG Miss Tanzania India
Miss Tanzania India ni jukwa linalotoa fursa kwa wanawake wa Kitanzania wenye asili ya kihindi kuweza kushindana kuonyesha Urembo na Vipaji vyao ambapo mshindi atavikwa taji na kuiwakilisha Tanzania kwenye fainali za Kidunia za Miss India Worldwide
Shughuli hiyo yameandaliwa kusherehekea urembo na sanaa Kutoka bara la Hindi na kulipatia Mrembo Mtanzania mwenye asilia ya Kihindi kuitangaza Tanzania kimataifa na kujihusisha na shughuli za kijamii ikiwa pamoja na kuchangisha fedha zitazotumika kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ya Kitanzania.
Samsung Miss Tanzania India ni wakala rasmi was mashindano ya kimataifa ya Miss India Worldwide nchini Tanzania
Kuhusu Samsung Electronics Co., Ltd.
Samsung Electronics Co., Ltd. ni kampuni inayoongoza duniani katika Nyanja ya technologia na mawasiliano ikiwa na rekodi ya mauzo ya dola za kimarekani 96 billioni ikiwa sawa na 12.96 trillioni kwa pesa za Kitanzania mwaka wa 2008. Inajumla ya waajiriwa 164,600 kwenye ofisi 176 katika nchi 61 duniani.
Kampuni ya Samsung ina biashara saba tofauti zinazojitegemea ikiwa pamoja na Visual Display, Mobile Communications, Telecommunication Systems, Digital Appliances, IT Solutions, Semiconductor na LCD.
Imetambulika kama ni kampuni inayokua haraka duniani , Samsung electronics inaongoza kwa kutengeneza digital TVs, memory chips, mobile phones na TFT-LCDs.
Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea tovuti
www.samsung.com

Kuhusu Richa Adhia
Richa Adhia alizaliwa jijini Mwanza, na amekua akijihusisha na shughuli za uanamitindo tangu mwaka 2003 alipogunduliwa na Mustafa Hassanali. Aliiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya fainali za “Miss Earth”nchini Ufilipino mwaka 2006 na baadae kuwa Vodacom Miss Tanzania mwaka 2007 ambapo alipata fursa ya kuiwakilisha Tanzania kwenye fainali za kumtafuta mrembo wa dunia “Miss World” mjini Sanya nchini China.

Richa sasa ni mjasiriamali anayemiliki saluni ya urembo iitwayo Radiance, iliyopo Upanga jijini Dar-es-Salaam na ataiwakilisha Tanzania tarehe 27 Machi 2010 kwenye fainali za Miss India Worldwide nchini Afrika Kusini.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. nimeipenda kazi ya mustafa.

    ReplyDelete
  2. Beautiful, extremely beautiful.

    ReplyDelete
  3. haswaaa hilo ndio taji lake na sio miss tanzania.

    ReplyDelete
  4. PETER NALITOLELAMarch 07, 2010

    I AM SO COMBERSOME ASTONISHED HOWEVER THEREFORE THERE WERE MANY INDIANS BUT BY THE WAYS MISS RICHA ADHIA WAS ELECTED WITHOUT NONE JUST HERSELF, THERE IS MANY MANY INDIANS IN TANZANIA BUT I CAN NOT CONCLUDE WHY THEY JUST PICK ADHIA WITHOUT ANYTHING COMPETITION NOT SO EVER. I CAN NOT SAY SHE IS NOT CUTE BUT AM SURE SHE WILL WIN EVERY THING HELP ME GOD. I WERE HER FAN SINCE THE DAY I WERE IN MUZUMBE CHUO KIKUU MULOGOLO AND MANY PEOPLE LIKE ME KNOW ADHIA IS GOING TO WIN MISS INDIA AND TANZANIA RESPECTIVELY. MICHUZI THANKS NO THANKS FOR BEING OVER THERE BRING US MORE CUMBERSOME PICTURES,ASANTENE WOTE.

    ReplyDelete
  5. Walisema ni Msukuma wa Nzega...........haya sasa......yetu macho.....kweli Bongo Tambarare.

    ReplyDelete
  6. sasa hii ndio nini - miss tanzania india?

    je kuna miss india tanzania?
    miss kenya tanzania au miss uganda tanzania?

    mbona mimi sijaielewa? jamani nifungueni macho, kuuliza si ujinga!

    mdau Tanangozi Iringa

    ReplyDelete
  7. Richa Adhia alipovikwa taji la Miss Tanzania,kuna wengi waliona astahili kwa madai ya kuwa ni Mhindi.Mimi sikua mmoja wao.

    Richa Adhia alinukuliwa akisema yeye ni msukuma.
    Leo Richa huyo huyo ni MISS TANZANIA INDIA.
    Ina mana walodai hastahili kuwa miss TZ kwa kuwa ni mhindi walikua sahihi?
    Can one be both msukuma and Indian?
    THE SON OF AFRICA a.k.a KIJANA WA KIJIJINI

    ReplyDelete
  8. hapa!wala atulalamiki maana amefiti na taji lake la kutuwakilisha,na wala
    wa-Indi hawawezi kumkana kwa kuwa wanajua ni raia wao aliyezaliwa nje ya india,pia nina uhakika BOLLYWOOD watampa kazi ya kucheza filamu,
    Richa Hongera sana!Miss India uleyezaliwa Tanzania

    ReplyDelete
  9. IS SHE A INDIAN DIASPORA LIVING IN TANZANIA????? if so walemnaopinga dual citizenship,whats ur opinion..?

    ReplyDelete
  10. Kwa kweli nilivyoelewa hapa ni kwamba huyu dada anawakilisha miss Tanzania India. Yaani kunamashindano ya mamiss kule India halafu yeye anatuwakilisha kutoka Tanzania. Kitu kimoja sijaelewa ni kwamba kulikuwa na mchakato wowote wa kuwapambanisha mamiss wote wa Tanzania na yeye akaibuka mshindi? Pia sijaelewa "Kuwakilisha Tanzania India?" Ni mashindano ya Mamiss ya kidunia yanafanyika huko India? Kama ni hivyo si tuna Miss Tanzania ambaye anatakiwa kuwakilisha? Kama sio ni aina gani ya mashindano hayo basi?

    Mwenye Ufafanuzi anieleweshe jamani

    ReplyDelete
  11. Yeye ni Tanzanian India kama kina Obama.African American wanavyoitwa.

    ReplyDelete
  12. it's not hard to realize: miss Tanzania India==Indian miss in Tanzania. nothing else.

    ReplyDelete
  13. Jamani Msukuma wa hivyo hakuna, kuwahi kuishi kwa wasukuma na kujua lugha kidogo hakumfanyi awe msukama.

    ReplyDelete
  14. UNAWEZA KUWA MSUKUMA LAKINI MWINGEREZA, THE SAME TO HER NI MHINDI LAKINI NI MTANZANIA. NA ANAKWENDA KWENYE MASHINDANO YA INDIANS WORLWIDE, JAMANI INDIANS WORLDWIDE NA YEYE NI MHINDI WA DUNIA HII LAKINI NI MTANZANIA SO SHE HAD ALL RIGHTS TO BE MISS TANZANIA. UNATAKA KUNIAMBIA IKOTOKEA MASHINDANO YA MISS AFRICANS WORLDWIDE WA-AMERIKA WEUSI WASIGOMBEE KWA VILE HAWAKUZALIWA AFRICA? HUYU BINTI HAWEZU KUGOMBEA MISS INDIA KWA VILI SI RAIA WA INDIA.

    ReplyDelete
  15. Hii ni dual citizenship au????

    ReplyDelete
  16. Ankal! Mbona hii sii elewi, Miss India Tanzania? Ina maana hili shindano linashirikisha Wahindi walio nje ya India? au Ni shindano linalofanyika India but kushirikisha Warembo toka nje ya Nchi? If so,Why Richa Adhia, mbona hamna warembo wengine wawe Weusi ama Wahindi, na audience kubwa mbona ni kina kanjubai, thats why tunapojifanya kuwa sisi tunapenda saana watu nachukia, coz we are not treated as we treat them. Sasa Richa ni Msukuma ama Muhindin kama mdau alivyouliza hapo juu? Sometimes nyinyi wenyewe mnatupa ya kusema then mnatuita wabaguzi wa rangi while hamna wabaguzi kama hawa wakina kanjubai ambao zikifika ishu fulani wanajidai Watanzania then zikija nyingine wanadai sisi ni Wahindi. Umeshaona Kijana wa Kitanzania akao Muhindi na kukubalika kwao, most of the times huwajaza mimba dada zetu na kuwakataa, afadhali jama zetu matasha inter-recial za kumwaga. Mhindi gani aliye zaliwa Ocean Road hajui kutamka wewe na kusema veve, alafu mnataka tukubali ni ndugu zetu. Ona sasa Miss Tanzania India sijui Miss India Tanzania, anyways mtajua wenyewe Bwana, maana Bongo usanii kibao na ukarimu usiokuwa na mpango! Pleas Michuzi wakilisha usiibane!

    ReplyDelete
  17. picha ya pili toka chini,namuona huyo mama wa kihindi kavaa nguo kama za wamama wa kihindi huku nilipo Appolo Hosptal India.
    Ni mimi
    Mgonjwa Mtanzania India.

    ReplyDelete
  18. Leo nimeamua kujipachika cheo cha Uwalimu wa Upee 1. Hili ni shindano la kumtafuta miss mwenye Asili ya India ulimwengu mzima kwahio sio miss India Kama nchi ni miss Indian world wide sio kwa Raia wa India ni kwa mtu mwenye Asili ya India popote alipo duniani mpoo hapo na inafanyika Africa huko suncity jhb Nafikir Wadosi wa Durban Ndo wameandaa manake Durban kama Bombay vile kama hamjaelewa nakuja na KIBOKO na ubao mwenusi na chaki kwaleo inatosha mie Mgosi kutoka MARAMBA TANGA

    ReplyDelete
  19. TOFAUTI KUBWA KATI YA NCHI ZILIZOENDELEA NA NCHI ZETU MASKINI NI UWEZO WA KUJITUMA. WANANCHI WA NCHI ZILIZOENDELEA HUJITUMA ZAIDI KULIKONI SISI.
    HII TAARIFA YA MISS INDIA WORLDWIDE ALIYOWEKA MICHUZI AMETOA NA LINK AMBAYO INAJIELEZA YENYEWE NA WALA HUHITAJI MTU KATI (MIDDLEMAN) AKUELEZEE. MAELEZO YA MASHINDANO HAYO YAPO WAZI KABISA NA VIGEZO VYOTE VYA USHIRIKI WA RICHA KATIKA MASHINDANO HAYO VIMEONESHWA.
    TATIZO LETU KUBWA HATUJITUMI KUTAFUTA HABARI NA KUJIELEMISHA MATOKO YAKE TUNAANZA KULIZA KICHWA CHA NG'OMBE KIKO WAPI WAKATI PEMBE TUNAZIONA.


    ALL ABOUT THE

    MISS INDIA WORLDWIDE PAGEANT

    Miss India Worldwide Pageant is produced by the IFC, based in New York City.

    The IFCis a pioneer organization in conducting Indian pageants and fashion shows in the USA and worldwide. The committee has also been conducting the Miss India New York and the Miss India USA Pageants annually since 1980.

    In 1990, Mr. Dharmatma Saran, Chairman and Founder of the IFC, decided to take the pageant one step further to an international level and started The First Miss India Worldwide Pageant. For the first time ever, Asian-Indian communities from all over the world came together in New York for this event. The pageant was an instant success and was acclaimed as ‘the most glamorous Indian function in the world.” To the best of our knowledge, no other ethnic organi­zation has ever conducted a pageant of this magnitude on an international level.

    In line with other prestigious international pageants, we have also started staging Miss India Worldwide in various parts of the world. In 1997, the pageant was organized in Bombay to salute India on its 50th anniversary of independence. In the year 1998, the pageant was organized, in associa­tion with UTV International, in the exotic and beautiful city of Singapore.

    The IFC selects distinguished local organizations in various parts of the world and authorize them to conduct national pageants in their respective countries. At this time we have affiliates in over twenty five countries.

    The contestants in all the pageants are of Indian origin, between the ages of 17 and 27, never married, and are citizens, residents, or born in the country which they represent. The pageant consists of four segments - Evening Gown, Indian Dress, Talent and Question-Answer. The winners of all the various national pageants from all over the world vie for the glamorous and prestigious title of the Miss India Worldwide.

    The IFCmotivates and guides its winners and contestants to take up charitable causes. Many of our past winners have raised substantial amount of money for various charities, especially for handicapped children.

    The name Miss India Worldwide was registered under the trademark act of USA and has been granted Trade Mark by the Commissioner of Patents and Trademarks of the United States Government.

    IFC

    ReplyDelete
  20. Ni kwamba kuna mashindano ya kutafuta Mamiss ya Wa Kihindi wanaoishi duniani kote hivyo kutoka Tanzania amechaguliwa yeye kama mhindi kwenda kuwakilisha warembo wa kihindi waishio Tanzania. Tatizo ni kwamba yeye alishakiri kuwa yeye ni M-TZ swali ni kwamba je! Ushiriki wa hayo mashindano hayajali wewe ni Citizen wa wapi?

    ReplyDelete
  21. Mimi yangu mawili:
    #1: Hawa wadada watatu wanafana baba yao hakuibiwa hata kidogo#

    #2: Michuzi kwanini waweza mambo makubwa unashindwa vitu vidogo???!!. Kila siku waambiwa jinsi na mahala pa kuweka konoz wewe bado washindwa tu!!

    ReplyDelete
  22. Swali langu nikuwa kwani hamna warembo wengine wakihindi nao wakajaribu bahati yao? yeye si alishaeenda miss sijui world au universe? Wangechagua mwingine I am sure wahindi wako wengi tu wazuri na very talented.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...