Asslam Alekum "Ankal"
Pole sana Ankal kwa kazi nzito unayoifanya mimi ni mpenzi mkubwa sana wa blog ya jamii, mimi ni Mtanzania n,naishi Finland naitwa Mwasiti,tafadhali Ankal naomba uweke hii taarifa kwani ni faida ya Watanzania wote!
Kama kuna mtu ama watu wanataka kuja kusoma ama kufanya kazi kwenye hizi nchi za Scandinavia kuna deal imetoka kwa nchi za Africa tu sasa naona huku wenzetu wa Africa magharibi,Nigeria,Ghana,Cameroun nk wanazichangamkia.
sasa sina jinsi jingine ya kuwajulikisha Watanzania wenzangu ndio maana nimeamua kukuandikia wewe mkuu wa blog ya jamii,maana ikifika hapo nafikiri kila mtu ataweza kuisoma na ntakuwa tumesherikiana ili Watanzania pia wafaidike.
Sasa kwa wale watakaotaka wanaweza kuwasiliana na agent ambaye ni mama wa Kifinland anaitwa Gloria Thomson Boiko kwa kupitia e-mail yake
hapo watapata information zote kwa ujumla.
Mwisho kabisa nakutakia afya njema Ankal na kila la kheri na Mungu akujalie neema,subira na upendo Waasslam
Mdau Mwasiti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Shukrani sana kwa Mwasiti na Michuzi kuwezesha habari hii kutufikia, lakini binafsi sijaridhishwa na namna ilivyofika. Japo nitaonekana kuwa ni wale wale wazee wa diss lakini ningependa habari hii ingekamilika yaani ioneshe link za website ambapo anayetamani na kuvutiwa nayo akiwa na vigezo aweze kujaribu kuomba. Hii itampa fursa na uwanja mpana wa kufanya utafiti wa kutosha. Nasema hivyo binafsi niliomba kusoma Finland nikapata chuo ambacho nilipewa full scholarship lakini nijilipie accomodation, health insurance, na air ticket pamoja na nauli za kwenda na kurudi shule kila siku. Nilimudu kwa miezi 7 tu nikachemsha maana kwa mwaka accomodation pekee ilihitaji niwe na euro 12000.Sababu nadhani hata Mwsiti atakua shaidi yangu Finland pagumu na bahati mbaya nilienda mwaka 2008 hali ilikua ngumu, kazi za part time chache mno. Samahani kama nitakua nimewkwaza ila ningependa kujaribu lakini namna habari ilivyokuja labda iwekwe vizuri zaidi ili kutusaidia sie Watanzania maana naamini dada huyu anania ya kutusaidia hadi kuamua kutuma ujumbe huu kwetu

    ReplyDelete
  2. naungana na mdau George.kweli ni vizuri akatupatia links

    ReplyDelete
  3. Napenda niungane na mchangiaji mwenzangu aliyetangulia hapo juu.Maelezo ya kiana yatatusaidia japo pia nadhani ukimuandikia huyo agent mwenye e-mail address aliyo toa dada amwasiti unaweza kupata taarifa zaidi.
    Najua naweza kueleweka tofauti ila huu ni mtazamo wangu binafsi.Kama itawezekana na nitakuwa sijakukwaza,naomba mawasiliano yako dada ili kwakuwa wewe upo huko una weza kunisaidia kujibu baadhi ya maswali kadhaa hata kabla sija ongea na huyo agent.
    NATANGULIZA SHUKRANI.

    ReplyDelete
  4. mimi ni mtanzania ninayeishi huku africa magharibi ambaye naijua vizuri michezo ya watu wa huku hasa wanigeria ambao huwa wanalink hadi na baadhi ya wazungu feki ila jina limenistua la huyo mama jina bioko ni jina la watu wa huku ili hupata uhakika hoyo dada msamaria angeweza kiurefu kama ni tangazo au nini ili watu wajue vigezo vinavyotakikana

    ReplyDelete
  5. Hmmm,hii mbona imekaaa vibaya vibaya,Nipo huko na hizo kazi wenyeji tu hawana sasa huyo mama ni kazi gani anazo? hawa jamaa wana mikakati kabambe ya kupunguza wahamiaji sasa hivi na hii huenda ikatokea baada ya uchaguzi mkuu mwakani,hadi wanatishia kuua viongozi wao wanaotetea malticaltural,sasa ni vema ukaweka source ya information zako,hii yako imekaa kidaku zaidi labda uwarushie global publisherz

    ReplyDelete
  6. Ni kweli kabisa Ankal!,ninaungana na wadau wote hapo juu hususani mdau George aliyewahi kuishi Finland,kuhusiana na issue hii ya dada yetu kutaka kutusaidia watanzania kimasomo na hali kadhalika kujipatia chochote cha kula na kuishi, binafsi nimeipenda mnoo,maana ni ukweli ulio dhahiri ya kuwa wenzetu wa Africa Magharibi wako haraka sana kwa kuhangaikia maisha yao na hata kujitafutia namna ya kusoma na kutoa njia kwa wenzao waliobakia nyumbani,lakini tatizo kwa waTz na Africa mashariki sijuwi ni nni!!,anyway tusijilaumu sana sababu ya umasikini labda tuwalaumu wanaokula pesa za nchi kwa kutowasaidia wananchi wetu,japo wenzetu wanakula na kusaidia wenzao. Infact nchi zote za ukanda wa Scandinavia na Magharibi mwa Ulaya zinashabihiana kwa ugumu wa maisha, ukweli mtu akiandika na kuwaambia ya kuwa hata Ulaya kuna ugumu wa maisha inaonekana ya kuwa hutaki wengine wafike au waendelee,lahasha! ila ugumu unakuja endapo umepata nafasi ya kusomeshwa huko bila pesa za kuongezea ongezea mfuko,maana ni kweli elimu hailipiwi huko,ila pesa za malipo ya nyumba,health insurance, na chakula huleta utata mno kama kweli hiyo scholarship haihusianishi mambo hayo, so badala ya kuitafuta elimu wengi mno hushindwa inabidi waingie kazini tuu,sasa ni vyema kupata link ya website ya huyo mama ili mtu ajisomee na kuangalia kama anahitaji kupiga Box tuu bila shule au kusoma na Box, ili kuweza kujipanga, isije kuwakuta wenzetu yaliyomkuta kaka George aliyekuwa hapo Finland, naandika hili sababu nami nimeona wanavyohangaika wale wanaosoma na kuishi huko kwa kujitegemea wao wenyewe bila kuongezewa pesa za kujikimu,japo wanafanya kazi lakini maisha wanayatolea jasho mnoooooo,so tuone link ili tujuwe kama ni kubeba Box pekee au Box na shule,ili mtu asiaibike ugenini kwa kukosa hata nauli hahaha.
    Tushirikiane wadau tuikomboe TZ
    JipyaGshenko far East!

    ReplyDelete
  7. Kuweni makini na watu feki. Mimi ninaishi hapa Finland na ninajua jinsi ilivyo vigumu kwa foreigners kupata kazi hapa. Sasa hilo dili sijui imetoka wapi?

    ReplyDelete
  8. KUSEMA UKWELI JAMANI ANGALIE SANA HAPA KWA SABABU WATU TUNASETIA

    HAMNA UKWELI KABISA HALAFU KWA NINI HUHOY MWANAMKE AWENA EMAIL KAMA YMAIL ...

    MTALIZWA WATU HAPO INAWEZEKANA KUNA GROUP LA 419 YA KINAGERIA HAPO

    ReplyDelete
  9. Mimi nimejaribu kutuma na amejibu,ila kama inavyojulikana kuwa wajanja nwapo wengi siku hizi,hivyo basi ni vizuri wenzetu mliopo huko mkatusaidia kuangakia huyu mtu kama ana nia ya kweli au anataka kutupiga changa la macho.
    ANGALIZO.Tuwe makini hasa Tanzania kwani watu wa ukweli wapo na weziwa[po na ndiyo wengi.Mimi nimesha wahi kuibiwa fedha nyingi tu hapo Dar kwa mtindo unaofanana sana na huu.

    ReplyDelete
  10. ANGALIZO: HILI JINA SIO LA KIFINN, KWA HIYO KUWA MACHO NA NDUGU ZETU WA MAGHARIBI. PILI, BW, GEORGE, ACCOMODATION SIO EURO 12000 KWA MWAKA, NI EURO 300X12 NI EURO 3600(HOAS). KAMA ULILIPA ZAIDI YA HAPO UMELIWA

    ReplyDelete
  11. WAJEMENI MIMI NAISHI HELSINKI FINLAND. HUU NI UONGO MKUBWA KUPINDUKIA. KWANZA HAKUNA JINA LA MTANZANIA ANAYEITWA MWANSITI HAPA FINLAND. PIA NIMETUMA EMAIL KUHAKIKISHA JAMBO HILO. MAJIBU NILIYOPATA NI YA KIBABAISHAJI. NIMEOMBA ANUANI YA HIYO TAASISI, HOLA, SIMU HOLA, NAMNA YA KUFIKA KWENYE HIYO OFISI HOLA.
    UKWELI NI KWAMBA HAKUNA KITU KAMA HICHO. CHUNGENI SANA.

    ReplyDelete
  12. Jamani Kanyaboya hiyoo shauri zenu. Kwanini asiwe maelezo hapa hadi tumwandikie huyu mama wa "Kifini" anaitwa Gloria Boiko????? mmmhh jina tuu hapa chale zinakucheza. Muwe waangalifu. Hakuna kitu hapa

    ReplyDelete
  13. Nimemuandikia huyu mtu na hili ni jibu nililolipata:
    "I am kindly appreciate that you written to us and we still working on the project and we have a million applications,

    and also this project goes to three countries which is Finland,Denmark and Norway.

    Please send to us your information i meant all certificates,school,birth and tell us you want to come to studying or working.

    To those who succeeded or elected, we will send them forms and open Visa for company name.

    Good lucky.

    Regards

    Boiko Gloria Thomson.(Manager)"

    Kwa mawazo yangu naona huyu mtu ni fake na haiwezekani kamwe akakutafutia kazi wakati wananchi wenyewe hawana kazi.

    ReplyDelete
  14. anoy Said wacha kudanganya watu, huwezi kipata accomodation kwa euro 300 kwa mwezi, labda kama mnachangia chumba watu watatu au zaidi (geto).
    euro 12000 kwa mwaka yuko sahihi.

    ReplyDelete
  15. mimi naamini kanyaboya hili...aache kuwambie marafiki yake atoe tangazo...acheni utapeli jamani...

    ReplyDelete
  16. Program kama hii nilishawahi kuona inaendeshwa Denmark na wana link ambayo inakupa details zote ambazo unahitaji kufahamu kabla hujapeleka maombi yako ikiwa ni pamoja na vigezo. Kwa wanaotaka kupata details za Denmark wanaweza kwenda kwenye hii link:

    www.nyidanmark.dk

    Kama mdau Mwasiti ana nia njema ya kuwasaidia watanzania, awasaidie kwa kutoa website kama hiyo ya Denmark ili watu ama waamue kuomba wenyewe moja kwa moja ama waombe kwa kupitia kwa agent.

    Kwa kuwa tayari tumeambiwa Gloria Thompson Boiko ni agent, maana yake ni kwamba yeye ana-facilitate hizo applications kwa malipo ya fee fulani. Ma-agent wengine huwa ni matapeli, wanaweza kuweka hizo fee na kuongeza gharama nyingine za uongo.

    Pia kwa malengo ya kusaka kazi, lazima watataka wajue kama mwombaji ana uwezo wa kumudu gharama za maisha na hapo ndipo palipo na mtego kwa kuwa mtu itabidi a-reveal info za bank na hapo ndipo wenzetu wa Nigeria wanapoingia kazini na kufanya kweli.

    Tuwe makini sana, maana siku hizi hawa wenzetu wa Nigeria wanajua mpaka kiswahili. Juzi nimepokea msg kutoka kwa mtu ameandika kwa lugha mbili, kiswahili na kiingereza. Lakini ni hao hao matapeli.

    Siyo kwamba ninam-discredit Mwasiti (aliyetuma bandiko kwa Machuzi), bali ni swala la kufikiria nje ya box. Dunia ya sasa imebadilika sana lolote linaweza kutokea. Kuna mengine yanaweza kuonekana ni ya kiukweli ukweli, lakini kumbe ni utapeli.

    Ukisoma between the lines kuna missing info nyingi na pia kuna hints kibao ambazo zina raise red flag.

    Kwanini huyu mtumaji wa info aseme wazi kwamba agent ni mama wa kifinn? Ili atupe confidence kwamba ni kitu cha kweli?

    Pili, sijawahi kuona kuna agent wa kutafuta wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma. Ina maana yeye anatoa scholarship na kuomba admission kwenye universities ama colleges?

    Mara nyingi hizi opportunities za kwenda shule ukienda kwenye ofisi za ubalozi utapata yote hayo. Sijawahi kuona ma-agent wa deals za shule, bali vyuo husika huwa vinatuma watu wa admission/recruitment ya wanafunzi na hasa kama wanaona kuna wanafunzi wengi wanatoka nchi fulani basi wanaweza kwenda kuwa-sensitize kwa kutoa seminar ama kuwa info za muhimu ili waweze kuomba nafasi za masomo kwenye shule husika, lakini siyo hii deal ya huyo Boiko.

    Kuna mengi ya kujiuliza kabla hujaamua kuuvaa mkenge.

    ReplyDelete
  17. Mdau uliyeuliza namba za simu, physical address, na mengineyo wewe ndo umemaliza game lote.

    Kama kampuni ya huyo mama inaweza ku-handle applications zaidi ya milion 3, maana yake ni kwamba wako registered, wana ofisi, wana website na pia wana simu na fax. Sasa kama hawezi kutoa details zote hizo, hiyo ni kanyaboya. Pia kutumia address hizi za mtaani kama yahoo, hotmail, gmail, ymail, msn na nyinginezo inaongeza utata zaidi. Those e-mail addresses are not official kwa kuwa mtu yeyote anaweza kufungua account any time na kwa kutumia jina lolote na hakuna verification ya majina.

    ReplyDelete
  18. Yaani ina maana waTanzania wameungana na Wa Africa magharibi kututapeli? Maana huu ujumbe umekuja kwa Michuzi kwa lugha ya kiswahili!!! Hao wa Naigeria na Waghana wamejulia wapi kiswahili? Nivizuri kufuatilia na kujua ukweli, ila ukiona tu wanaanza kukuomba pesa,kimbia.

    ReplyDelete
  19. ushindwe na ulegee kwa ushuhuda wako wa uwongo kwenye blog ya jamii

    ReplyDelete
  20. Jamani msidanganyike!!! hakuna Mtanzania anayeitwa Mwasiti hapa Finland!!! wizi mtupu!!!.Yaani wazawa wenyewe wanapunguzwa makazini kila kukicha, ndio waje wachukue toka Africa?

    ReplyDelete
  21. Wadau mimi baada ya kumuomba anuani, namba za simu na website yao, na hivi ndivyo nilivyojibiwa.

    {Thank you for sending your CV.
    About give you our contacts sorry we are not provide our contacts espeacially website for now due to security safety,this is our first time waking on this project to African Countries.
    After been elected we will provide you some of our contacts,we will let you know as soon as possible
    Good lucky
    Regads
    Boiko Gloria Thomson(Manager)}

    Mimi naona kwa kutusaidia Ankal angetuwekea email ya Mwasiti ingekuwa rahisi zaidi. Kwani naona dada Mwasiti amekuwa kimya sana ili hali yeye ndiye angekuwa msaada mkubwa katika hili

    Nawasilisha.

    Mdau

    Kigilagila

    ReplyDelete
  22. HIVI MNAWAJUWA WAZUNGU NINI!!! SASA HIVI WANAPIGA KELELE JUU YA WAHAMIAJI ULAYA KOTE WANAKAMPENI KUBWA YA KUFUKUZA WAHAMIAJI, UKIENDA KUONGEZA VISA UKIPATA BASI UNA BAHATI YA MTENDE WATANZANIA KIBAO WANARUDI NYUMBANI TOKA HUKU ULAYA, WAMEWEKA MASHARITI MAGUMU KWELI KWELI, NI SIS WA-AFRIKA TUUNGANE NASI TUWACHACHAMALIE, HUKU MTU ANA PhD NI MLINZI KISA NI KUTOKA NJE YA EU WAKIJA KWETU TUNAWAPA KAZI WAKATI UMEFIKA SASA NA SISI KUWA NGANGALI KAMA KUSOMA WATU WETU WENGI WAMESOMA SASA WANAWEZA KUSHIKA HIZO NAFASI ZETU HUKO NYUMBANI, HAWA SI WATU NI VIATU, HALI YA UCHUMI WAO NI MBAYA HASA UK, GREECE, PORTUGAL WANAFUKUZA WAAFRIKA SASA KISHENZI HAKUNA MTU ATAKUITIA KAZI ULAYA SIKU HIZI NI UONGO TUPU HUO

    ReplyDelete
  23. Jamani angalieni huko mnaotaka kwenda nje...
    1) Wengi wa waswahili walioolewa na watu wa west wanamaisha magumu sana. Tukikutana nao wanajidai kutanua kama watu wa huko. Sasa wakiona hela hailingani na matanuzi yao wanajiunga na wanaume zao kufanya mchezo mchafu. Hayo maelekezo yatakua yameandikwa na mbongo kabisa wala sio mkenya. Kiswahili chake ni cha bara. na kama anajua kinachoendelea SHAME ON HER. Na ametumia jina la kiswahili ili watu wafikiri ni kweli Mwasiti....

    2) Hizo email watu walioandika zikajibiwa kama kweli ni mtu aliyeenda shule anaelewa kutumia hata word process. Hamna hata space baada ya comma na makosa mengine mengi mengi sana.

    3) Kama wanafanya hayo mambo kweli uandike email leo leo na ujibiwe leo leo? Ina maana wanawanyakazi wengi sana ua ni auto respond hiyo wanatumia?

    3) English ya mtu aliyemakini na kazi sio hiyo. English imeenda upande kweli Please send to us your information i meant all certificates,school,birth and tell us you want to come to studying or working., To those who succeeded or elected, we will send them forms and open Visa for company name., About give you our contacts sorry we are not provide our contacts espeacially website for now due to security safety,this is our first time waking on this project to African Countries.
    ,


    Kuna red flags kibao na stay away na mtanzania aliyeolewa na mnigeria, mghana au msenegal wa mitaani....wanapenda kuishi maisha ya juu lakini hela hawana

    ReplyDelete
  24. Hakuna mtanzania anaitwa mwasiti huku finland, Watanzania tuko wachache na karibu wote tunajuana. Hii ni kanya boya , ukiingia mkenge utaibiwa, chunga.

    ReplyDelete
  25. Nawashakuru sana watz wenzangu kwa ushirikiano mkubwa mliouonyesha kuhusu suala hili.

    Mimi mwenyewe nimejaribu kufanya mawasiano naye lakini anakuwa mjanja mjanja fulani hivi. Nimei-flag, bado naendelea kuwasiliana naye ili nijue mwisho wake.

    Tuendelee kusaidiana ndugu zangu.

    ReplyDelete
  26. tinga tinga limeingia kwenye mnuso..eti kazi bwerere..haaahhaa ze suomi hii 2010?

    Yaani huyo mtu habari kweli hayupo ze seriazi..Maana hata wanaofanya biashara ya kuhaba wanaweka NUMERO za hewani na TOVUTI zao.

    Tutafika tu

    ReplyDelete
  27. Msitoe vyeti vyenu.....mkitoa tu watu watavitumia, na hasa cheti cha kuzaliwa. Sababu Ulaya Jina lako na tarehe yako ya kuzaliwa ni dili inayoweza kutoa information zako zote. Michuzi tusaidie kuwasiliana kwanza na huyo Mwansiti kabla ya yote kisha tupe mlishonyuma (feedback)

    ReplyDelete
  28. Jamaa kanimaliza kweli na chorus yake ya mwisho:
    'Mwisho kabisa nakutakia afya njema Ankal na kila la kheri na Mungu akujalie neema,subira na upendo Waasslam
    Mdau Mwasiti'

    NB:Hii kweli ni sanaa kwenye jumba la sanaa

    ReplyDelete
  29. Michuzi hupo, toa tangazo haraka kuwa Matapeli, we unaona watu wa Finland wenyewe wanasema hakuna.
    huyo mbongo anataka kutapeli watu, kama msichana kapata bwana wa kinigeria so wanakula kihivyo.
    kama blog ni ya jamii nakuamuru kanuusha hilo tangazo faster.kabda sijaifungia kama zeutamu, ahhaaaa

    ReplyDelete
  30. WAJINGA NDIO WALIWAO...MCHONGO HOHOHO HAYA PELEKENI VYETI VYENU NA HELA WATU WASHIBE.....WAAFRICA WENGINE WAPUMBAVU KWLI NA WAMEGUNDUA WABONGO NI WAJINGA NA MAZOBA NA WAVIVU KUFIKIRI SO WANAWEKA MTEGO SASA....WEWE MCHONGO HATA HIYO KAMPUNI HAINA SITE KWELI OFFICIAL ORGANISATION INAKOSA WEBSITE NA SIO TU HILO INA EMAIL YA YAHOO HEHEHEHEHE.KWA UZOEFU WANGU NILIOKAA ULAYA SIJAONA HII.TULIENI BONGO JAMANI SIKU HIZI ULAYA NI MASHAKA TU SISI WENYEWE TUNATAKA KURUDI NYUMBANI KULIMA.ULAYA ENZI HIZO SIO LEO,LEO MTU AKIRUDI NA SURUALI MOJA MSISHANGAE.

    ReplyDelete
  31. kweli hii haijatulia!! hii ni kanyaboya kabisa!! kuna jamaa wa finland alitupa link nzuri tu zinazoeleweka mwanzoni mwa mwezi wapili. mie niliwasiliana nae wakati nikiwa nimeshatuma na jamaa walinijibu. ila bahati mbaya sikukamilisha docs na jamaa alinisisstiza kwamba kule hakuna njia za mkato lazima mtu uende ukiwa umejiandaa sana!! so mazee tusikurupuke bila kufanya utafiti wa kutosha..
    hii ya dada mwasiti naona kimeo
    wizi mtupu
    "anataka kudirect wanaume wote ktk choo cha wanawake "

    ReplyDelete
  32. Please be careful with kind of people, they are very dangerous, i kindly advice you may friends who are looking for the job, try to first look for the experience within the country either by doing internshing or volunteering. By so doing you will get more opportunities to move forward. Try www.unjobs.org You will get many interns posts, volunteers post and job vacancies. Those in need of scholarship please try to visit. www.globalgrant .com their branch is at POSTA- SAMORA STREET.WISH YOU ALL THE BEST & AND GOD BLESS YOU.
    Mwanuzi

    ReplyDelete
  33. me nilitaka hadi kufika mwisho wa mchezo so nimefanya mawasiliano naye hadi hatua ya mwisho na hiki ndo alichojibu hapa ndo nilikuwa napataka huyu nimwizi tu
    Congratulations you has been chosen and qualified to join other African to this program

    This program is initiative of NGOs who are driving this project to help Africans to get job and studying in developed countries, they believe that Africans can if they be given the opportunity.

    Opportunity has given now to you; you should be an example to Africans in order to help other Africans to the next year to get also this opportunity.

    But you should know that there is cost will be covered by yourself; these cost are, to open Visa for you, medical checkup, Insurance, service and ID cards. The total amount you should pay is 350$ and other cost covered and everything remain will be paid by NGOs.

    If you can pay this covered cost please let us know as soon as possible, so that we can tell you were you should pay and how and dead line of payments and if also you cannot pay please let us know also so in order to give this opportunity to other people who have been not selected or qualified and they need this chance which has given to you.

    After payment please send to us the copy of your passport in order for us to open Visa for you, to prepare admission letter, forms. And in admission letter, forms it will show there which country you will go, we will continue to give you instruction before arrived in the country which intended.

    Once again Congratulation, I wish you will take the chance.

    Regards

    Thomson.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...