Ras Nas toka Norway (shoto) alikuwepo kuwakilisha wanamuziki wa Kitanzania Ugahibuni. Mada aliyotoa ya kudai wanamuziki walio Diaspora kukumbukwa kwenye tuzo hizi ilikuna wengi na waandaaji walitoa ahadi ya kuliangalia swala hilo kwa uzito unaostahili
Meneja wa Kilimanjaro lager George Kavishe akifafanua jambo wakati wa semina elekezi ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards iliyofanyika leo ukumbi wa Paradise City hotel jijini Dar na kuhudhuriwa na mamia ya nyota wa muziki nchini. Hii ilikuwa ni semina ya kuwekana sawa ya jinsi mchakato wa kupata wanamuziki bora wa 2009 utavyoenda

wataalamu wa Deloitte Touche ambao watasimamia kura za kupata wanamuziki bora
Afisa wa Baraza la Sanaa (BASATA) Angelo Luhala

akijibu hoja na kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa

wanamuziki wa bendi mbali mbali walikuwepo. Hapo mbele toka shoto ni Jose Mara wa Ngwasuma akifuatiwa na Khalid Chokoraa na Kalala jr wote wa Twanga Pepeta

Toka shoto mbele ni Lwiza Mbutu wa Twanga Pepeta, Mheshimiwa Temba na Chege wa TMK. Nyuma kuna Hussein Machozi, mdau na Profesa J.

Toka kulia ni Mr. Ebbo, Mkoloni, mdau, Mwana FA, AY, Master J na mdau

Toka shoto ni King Kikii, Sabah Muchacho, Matei Super Minofu na Hassan Rehani Bitchuka

Taasis Maela wa Akudo Impact 'Wazee wa Masauti' (kulia) na wadau wengine






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mwana FA si alisema hataki kujihusisha na Tuzo hizo sasa imekuwaje yupo ndani ya nyumba?

    ReplyDelete
  2. Proma, DarMarch 10, 2010

    Mithupu yaelekea mambo ya "kisanola" na "masebene" yanakupiga chenga kidogo. Huyo unayemtambulisha kama Christian Bella ni Tarsis Masela, Kiongozi Msaidizi wa "wazee wa masauti". Edit please!

    ReplyDelete
  3. ANKAL UMECHEMSHA HUYO SIO CHRISTIAN BELLA NI TAASIS MASELA

    ReplyDelete
  4. FANYENI HIVYO BASI KUSAIDIA MASHULE NA MIRADI YA KUSAIDIA UMMA. TBL KAZI YAO NI KUJIINGIZIA ELA TU LAKINI KUTOA KUSAIDIA MASKINI HAWAWEZI. WAIGENI WENZENU VODA.

    ReplyDelete
  5. HAFSA KAPOTELEA WAPI????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...