Mshauri (Counsellor) katika Ubalozi wa India hapa nchini Bw. Ngulkham Gangte (kushoto) akifafanua jambo katika Ukumbi wa MAELEZO) jijini Dar leo juu ya kuanza tamasha la filamu la nchi nane za Asia ambazo ni India, China, Japan , Iran , Indonesia na Korea.Wengine wa kwanza kutoka kulia ni Mwambata wa masuala ya habari na utamaduni wa Ubalozi wa India Bw. Sanjeev Manchanda, wa pili kulia ni Mwambata wa habari na utamaduni wa Ubalozi wa Indonesia Bw.Sukamto na wa tatu kutoka kulia ni Mwambata wa masuala ya Utamaduni wa Ubalozi wa Iran Bw. Saeed Omidi. Tamasha hilo linatarajia kuanza kesho saa moja usiku katika Ukumbi wa New World Cinema na litakuwa bure. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Might be a useless comment: Maelezo yaonekana chafu..! Press conference zingi zafanyika hapo, ingependeza pangekuwa safi.

    ReplyDelete
  2. hivi kuna mwandishi aliwahoji hali ilivyo kwa watoto wetu huko kwao au wanakula bata tu na kutangaza filamu zao????
    au waandishi wetu walingangania tu..... 'hey mr ambasada do you know kanumba..'

    ReplyDelete
  3. Sasa ukuta wa maelezo unaonekana ni mchafu kiasi hicho kweli kinachosemwa hapo kineleta maana kweli? ni wakati wa waandishi habari kukamata brush na kupiga rangi wenyewe maana ukisubiri fungu la vizara labda kama waziri mkuu atakuja kuongea hapo. Na ndiyo inaposhangaza kwamba wakati viongozi wakuu wakitaka kutembelea mahali na usafi unafanyika najiuliza je wao tu ndiyo wanatakiwa kufanyiwa hivyo? wakati kodi wanasamehewa sisi walipa kodi hatufurahi matunda ya kodi. Hii imekaje wa ndugu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...