Kikosi cha Yanga kilipokuwa Brazil miaka ya 70.
marehemu Bona Max ni wa kwanza kushoto waliochuchumaa.
HABARI ZINASEMA WINGA MACHACHARI WA YANGA ENZI HIZO, BONA MAX, AMEFARIKI DUNIA IJUMAA USIKU HUKO AFRIKA KUSINI. CHANZO CHA KIFO CHAKE HAKIJATHIBITISHWA, ILA DADA WA MKE WAKE MAMA GERE AMETHIBITISHA KUTOKEA KWA KIFO HICHO NA KUELEZA ALIKUWA AKIUMWA.
MAMA MAGERE AMEIAMBIA GLOBU YA JAMII SASA HIVI KWA SIMU KWAMBA MIPANGO INAFANYWA KUULETA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI SIKU YA IJUMAA IJAYO NA KWAMBA MSIBA UKO TANDIKA SOWETO.
MAREHEMU BONA MAX ATAKUMBUKWA KWA UMAHIRI WAKE WA KUCHEZA WINGA YA KULIA KWA UHODARI NA KASI YA AJABU, PAMOJA NA MAJALO ZILIZOZAA MAGOLI MENGI YA YANGA ENZI HIZO.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI - AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. nimepokea habari za kaka Max kwa msituko mkubwa sana kaka yetu mpendwa Max tutakumbuka naima ulala mahali mapema amen,

    mdogo wako Manchester.

    ReplyDelete
  2. WATOTO WA VICTOR HAO.

    ReplyDelete
  3. RIP BONA MAX . NAAMINI HII LILIKUWA MIAKA YA 70, HASA 1974/75

    ReplyDelete
  4. RIP Bona Max.

    That is the Young Africans I used to love.

    The years should read 1970s and not 1980s.

    Anyway, again RIP Bona Max.

    ReplyDelete
  5. RIP my friend Bona Max. Mimi nilikuwa rafiki yake Bona na classmate wake 1968 -1971 at St Joseph's Forodhani Sec School. The funny thing is back then tukicheza ndiki(soccer pickup game) Bona alikuwa Simba halisi like me so we always played on the same side

    Azania Bitoz

    ReplyDelete
  6. Huyu Sio Baba yake Oscar BomaMax kweli? Mtoto wa Temeke?

    ReplyDelete
  7. Rip Bona max imekuwa pigo kubwa hapa cape Town wiki iliopita wamefariki watanzania 7 kwa ajali wengine na mmoja kachomwa kisu na Baba mwenye nyumba wake na mmoja kafa kwa stroke basi balaa tu lakini mungu atajalia tutawarudisha wote tz

    ReplyDelete
  8. Michuzi,
    Hiyo picha Yanga ilikuwa Brazil 1974 ilienda kwa kujiandaa na mashindano ya Klabu bingwa Tanzania wakati huo ilikuwa ni knock out si ligi kama ilivyo sasa na ilikutana na Simba kwenye fainali uwanja wa Nyamagana Mwanza na yanga walichukua hilo kombe kwa kuwafunga Simba goli 2-1 na katika mchezo huo nafikiri Marehemu Bona max alikuwa ndiye mchezaji aliyekuwa na umri mdogo zaidi ya wote waliocheza mchezo huo na aling'ara vizuri mechi hiyo kiasi ambacho Mohamedi kajole "machela" beki mkali alikuwa uchochoro hata kufikia kumvuta bukta hiyo ndio hasa mechi iliyomfanya ajulikane na akumbukwe hata leo kwenye fikra za wapenda soka hasa kwa wakati ule wa mwanzoni mwa miaka ya 70.
    Kama kumbukumbu yangu imepinda sehemu wadau mnaweza kuionyosha.

    Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - AMIN

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...