Mkubwa kuna kitu moja inanisumbua sana kichwa, ni kuhusu hizi website za Serikali mbona aibu?? Nyingi zipo down, nyingine design ovyo na kushangaza zaidi ni hii web ya Tanzania Investment Centre ipo down kwa muda sasa.
Hivi Serikali na wizara zake wanadhani watapata wapi investors wakati inaonesha technology ipo down ktk issue ndogo kama hii! bora ingekuwa mtu kama mimi binafsi lakini sio serikali. kwa mfano, nipo ktk research na nashindwa kuifanya kutokana na website ya
tic.co.tz
ipo down! Utawala upo wapi????

Please watoe hawa jamaa ktk blog ili wawajibishwe na uzembe huu. Please piga debe kuhusu hii issue kwa sana tu mpaka kieleweke. Aibu Sana!
Mdau wa Leeds

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. HAKUNA JAMBO LINALONIKERA SANA KAMA KUONA TOVUTI YA SERIKALI YA JAMUHURI YA TANZANIA HAINA WIMBO WA TAIFA ULIO SAHIHI. UKICHUKUA MANENO YA WIMBO YANAYOPATIKANA KWENYE TOVUTI KISHA UKAANZA KUIMBA UKIFUATISHA TYUNI YA WIMBO ULIOMO KWENYE TOVUTI HIYOHIYO UNAPOKALIBIA MWISHO TYUNI INAIISHA NAWE UNABAKIWA NA MANENO BILA TYUNI! AIBU TUNASHINDWA HATA KUWEKA SAWA WIMBO TULIOUIGA! anyway watanzania ni wazito wa kufikiri na kutaka kitu sahihi, hivyohivyo inatosha watamalizia wenyewe si mradi wameelewa lengo.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kabisa mdau hali ya tovuti mashirika mengi hapa bongo hazipo kwa ajili ya utumishi kwa umma bali kutimiza wajibu tu.Hakuna usimamizi wa karibu katika kuhuisha habari na matukio na inaonekana kuwa hakuna wanazuoni mahiri na makini katika vitengo vya teknohama.Huu ndiyo utendaji wetu ambao umejengwa katika utamaduni wa kuripoti saa za kuingia kazi na kutoka lakini hakuna ripoti ya kazi mhusika ametimiza kwa siku husika.Naomba wadau mjibu swali hili:"WEWE UMEPATA KAZI NA JE KAZI IMEMPATA MTU?

    ReplyDelete
  3. KWA UJUMLA SISI WATANZANIA WANAFIKI NA HATUNA UZALENDO KABISA NA NCHI YETU.MTU AKIPATA AJIRA ANAFIKIARIA MIRADI YAKE BINAFSI NA JINSI YA KUTUMIA RASLIMALI ZA OFISI YA UMMA KUNEEMESHA FAMILIA YAKE NA SIYO TAIFA LAKE.EEEEH MUNGU LINUSURU TAIFA LETU NA HIZI HISIA ZA UMIMI KWANZA ILI TUWAFIKIE WAJAPANI NA WACHINA.

    ReplyDelete
  4. Kaka uliyotoa comments nashukuru hata umeandika kwa kiswahili wasioijua lugha wasije wakaona ujinga wetu..Ankali ni aibu sana.back to my point, kitu kikishakuwa cha umma/serikali hakuna mtu anaweza ku take care sana. na hilo ni tatizo letu watanzania na ninamifano mingi sana.angalia magari,hospitali,ofisi za serikali zinavyoendeshwa hakuna anayeweka mkazo kwamba hiki kitu ni chetu na ni cha sisi watanzania.. kila mtu akisahapa mshara hakuna anayejali kuangalia website inamapungufu sana.kaka uliotoa comment hapo juu kweli ni aibu kubwa sana kwa sisi watanzania.Mbona Blog ya kaka Ankali iko safi, update na iko fasta!! je yeye amewezaje kufanya hayo yote..au yeye anatokea nje ya nchi may be anatumia teknologia nyingine?? no hatujawa makini na post tulizonazo serikali.wacha niachie tu hapo hata mimi inaniuza sana na kweli hata nasikia kutokwa na machozi..basi
    Mdau Ughaibuni

    ReplyDelete
  5. Mdau unachosema kwa kweli ni sahihi kabisa, mimi nimeijaribu hii www.airtanzania.com mara ya kwanza mwaka 2008 ikadisplay kuwa ipo under maintenance, mpaka leo hii miaka miwili ishapita bado ipo under maintenance sasa sijui ni maintenance ipi inafanyiwa, na kwa uhakika inawezekana ishapita miaka mingi zaidi ya hiyo maana sikuwahi kuifungua kabla. Kama mnakosa rasilimali watu mbona kuna magraduate wengi tu waliosoma IT wapo mtaani hawana kazi ?
    POOR TANZANIA, tunashindwa kuwa na website, its very sad.

    ReplyDelete
  6. yaani navyopata uchungu natamani hata nivunje hii screen ya comp.hakuna mtu ana machungu ya vitu vya serikali.. sasa serikali ni nani?? nani anatakiwa aviangalie vitu vyote hivi?? ni hao wadau walioko huko na wenye madaraka hayo.. ila kwa sababu wanalipwa mishahara na wanaishi maisha powa hakuna haja kwa wao kujiumiza kwa kuangalia kila kitu.. kweli na roho ituume.Nilishafanya kazi ofisi moja ya serikali inayotoa huduma kwa jamii.. wafanyakazi wengine ila sio wote walikuwa wanasema nafanya kazi kama ya baba yangu wao wanataka wakae wapige umbea tu kwani kuna shida si pesa inaingia.. kweli watanzania tuamke kwa kuangalia hilo jambo kwa ukaribu zaidi.
    ni mimi mdau Ughaibuni

    ReplyDelete
  7. kaka michuzi
    Pamoja na Taasisi zote kuwa hata na tovuti yaani mimi ninahuzunika sana nilipogundua Wizara Nyeti kama ile ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa haina Tovuti kabisa yaani iots as good as zero...yaani mimi I dont understand what is the priority pale...kuvaa suti na tai na kukimbizana na safario za ughaibuni tuuuuu kaka michuzi hili ni janga na siyo kitu simple kama wananchi wanavyofikiri...
    Yaani wizara inayotuunganisha na dunia hawana hata TOVUTI....achilia mabli hizo taasisi nyingine zenye tovuti ambazo ziko hoiu...something is wrong somewhere....

    ReplyDelete
  8. mishahara haitoshi...hivyo muda mwingi tunautumia kufanya mambo mengine ili siku zikutane....msiongee tu kama maigizo..ukweli maisha magumu sana ..hivyo hata akili haitulii ofisini...mtu akiwa na njaa,kamwe akili haitatulia...hali hii itaathiri uwezo wa kufanya maamuzi sahihi..then flow yote inaathirika...mimi nimeshafanya kazi miaka 20 serikalini...tunabadilika kwa mbinde sana...thats fact!!!

    ReplyDelete
  9. mdau kutoka Leeds ujatulia, unataka ku-invest nini,hadi infomation uzipate katika hizo site, unawezakwenda face to face kwawahusika na usipate jibu..we unacheza na Bongo, dunia inapiga hatua mbele sisi ni bora tungekuwa tumesimama bali tunarudi nyuma, na sikujuwa BONGO imekuwa nchi ya kiFALME naona kuna familia moja wanagawana madaraka tu kama hamna watu wengine..inatosha kwa leo!

    ReplyDelete
  10. wewe unayesema mishahara haitoshi unatumia muda mwingine kutafuta madili.. sasa kwa huo muda mdogo ukiwa kazini unakuwa unafanya nini?? story sio. hampo serious.. nchi hii itabadilika tu kukiwa na watu wenye uchungu na nchi hii. kama huwezi kazi bora uachie ngazi na ufuatilie madili yako..kweli iko kazi mi naona sasa kweli lazima kila mtu ashike kidedea na kuwawajibisha watu.. wanaota vitambi tu maofisini ila hakuna afanyae kazi.mbona wataalam waku wengi tu wanaoweza fanya hizo kazi.. wako ma graduate wengi tu.. au ndio nchi hii imeshakuwa ya Kifalme!!

    ReplyDelete
  11. Mimi nashangaa mnalalamika wakati tovuti ya taifa tunayo hii ISSAMICHUZI a.k.a ankal, kila siku tunapata habari za nchini. Sina haja na hizo zingine.

    ReplyDelete
  12. Haya ndiyo matokeo ya kuthamini vyeti na kudharau ueledi na vipaji na ndiyo chanzo kikuu cha wizi wa mitihani kwa miaka yote.Serikali inataka vyeti na siyo uwezo wa mtu wa kufanya kazi.Ajira zetu zimebakia kwa babu na wajukuu wa familia ile ile.Unaambiwa usimguse huyo umesahau kuwa babu yake ndiye alikufanyia usaili na ukapata ajira japo kura zako hazikutosha.
    Huwezi amini lakini amini kuwa Tazara hawana website mpaka sasa.Bila kutafuna maneno naomba tukubaliane kuwa utendaji wetu unaojali kada za kisiasa zaidi kuliko uchumi makini na endelevu ndiyo mauti ya nchi ya Tanzania.

    ReplyDelete
  13. Mbona website ipo hewani? ni www.tic.co.tz au ni www.airtanzania.com

    ReplyDelete
  14. Nashukuru sana, website sasa imerudi hewani na naweza kufanya Research zangu.

    Kweli Michuzi Unatisha! Naona Vigogo wote wanakuogopa sasa hivi.

    Thank You very much for your help.

    ReplyDelete
  15. Mdau hata mimi nakubaliana kabisa na wanakosoa tovuti za serikali. Mimi pia nakwama sana katika research huku Canada, mambo hayaeleweki. Taarifa zinazotolewa ni chache sana na hazina ufafanuzi wa kutosha. Kwa mfano ukifungua tovuti ya National Bureau of Statistics (NBS) utaifunga mara moja nakuambia. Kwanza kuna 'news flash' wameweka juu ya takwimu ambayo inafunika data na huwezi kuifunga wala kuisogeza. Pili kuna links kwa ajili ya taarifa za mikoa lakini kamwe hazifunguki. Yaani ni madudu madudu tu. Wengine wanatoa contacts zao ili uwasiliane nao ukihitaji ila wala hawajibu, na ni mijitu inayoshikilia nafasi muhimu tu, takataka kabisa. Huu ni mfano mmoja tu. Mara nyingine mtu unaamua kubadilisha research topic ili kuikwepa Tanzania, ni aibu na fedheha kubwa sana.

    Nawasilisha dukuduku langu mjomba.

    ReplyDelete
  16. Hawa jamaa wa TIC ni bangi sana! Si website haipatikana tena!

    Dah! Tanzania kwanini tuko nyuma kwa kila kitu? Au Umeme umekatika ndio maana servers zipo down? Utasikia tu watakavyo jitetea.

    Hakuna Viongozi Bongo wote wababaishaji tu, Kama unashindwa kuhakikisha jambo dogo kama hili, Je unaweza ukawa convince investors to come and invest in the country? I don't think so.

    Tanzania Wake Up!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...