Beki wa Ethiopia, Woinshet Tsegaye Desta akilia baada ya mchezo ambapo Twiga Stars ilitoka nao droo ya 1-1 na kusonga mbele katika michauno ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za Afrika kwa wanawake katika mchezo uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar jioni hii. Katika mechi ya awali huko Ethiopia Twiga Stars ilishinda 4-0
Mashabiki wakishangilia bao la kusawazisha la
Twiga Stars lililofungwa na Asha Rashid 'Mwalala'
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Wanawake 'Twiga Stars' Esther Chabruma (kulia) akikabiliana na mabeki wa Ethiopia, Semira Kemar Aman na Beziihan Endale Alemar wakati wa mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa wa Uhuru jijini Dar leo jioni ambapo Twiga stars imeweza kuvuka ngwe hiyo kwa kutoa droo ya 1-1 hivyo kuwa washindi kufuatia mabao 4-0 waliyofunga Ethiopia wiki mbili zilizopita.

Asha Rashidi 'Mwalala' (katikati) akiipangua ngome ya Ethiopi a, shoto ni Semira Kemar Aman na Beziihan Endale Alemar wakati akielekea kusawazisha bao na kuifanya Twiga Stars isonge mbele.

HABARI ZINASEMA TIMU YA TWIGA STARS IMEPATA AJALI WAKATI IKIELEKEA HOTELINI BAADA YA BASI LAKE KUGONGWA KWA NYUMA NA LORI SEHEMU ZA KIGOGO. HAKUNA ALIYEJERUHIWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. SIMBA YAIBANJUA LENGTHENS BAO TATU BILA, MICHUZI TUPE PICHA ZA WEKUNDU WA MSIMBAZI WANAVYOTESA HUKO ZIMBWABWE KWA MUGABE.

    ReplyDelete
  2. well done girls!

    ReplyDelete
  3. Safi sana Twiga Stars, Nawafagilia.

    ReplyDelete
  4. hapa hakuna habari za Wekundu wala Yebo, hapa ni za Kitaifa tu, ankal itabidi tufanye harambee ili wakina dada zetu wapate misosi ya maana ili wawe kama madada wa zimbabwe si mnawakumbuka walivyoshiba

    ReplyDelete
  5. Wapi sister sister toka Mugumu Nyerere F.C.
    Maana hii ilikuwa ni namba ya kutumainiwa!

    ReplyDelete
  6. Bro Michu, mbona unakuwa kama sio mzalendo kulikoni? SIMBA katafuna wa2 Zimbabwe, hamna habari YANGA akifungwa habari zinakuwepo kwanini? Au wa2 wa Globu ya jamii wote ni YANGA??? Mimi ninakuombeeni duwa muumfunge Man U. Labda habari za Mnyama Mkali 2naweza kuzipata
    SIMBA oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
    Kigogo, Mbuyuni Dar a.k.a. Kigogo boy

    ReplyDelete
  7. Dada uclie ndo mpira ulivyo, lazima ukubari matokeo . Nimeckia Mnyama katafuna wa2 Zimbambwe bila ya huruma eti ni kweli???

    ReplyDelete
  8. sister sister toka Mugumu Nyerere F.C. saivi ni mja mzito hawezi kuche, we ngoja akishajivungua utaona vitu vyake.

    ReplyDelete
  9. Hongeleni Twiga lau mlete matumaini yaliyopotea
    Nagal Washnton

    ReplyDelete
  10. inaonyesha ama mlibahatisha kule ethiopia au mlibweteka na ushindi wa mabao4. inakuwaje kwao mshinde goli nyingi afu nyumbani mlazimishe sare. mi siwafagilii hata kidogo nguvu za soda tu

    ReplyDelete
  11. Wanamama kwa kupenda kulialia kama mtoto kapewa pipi

    ReplyDelete
  12. ASHA RASIDI'MWALALA'HII AIJAKA VIZURI BADALA KUYAENZI MAJINA YA WAKALI WETU WA ZAMANI CHITETE,MWAIJIBE,GESANI,ABASI SUNGURA,KULAGWA NK TUWE WAZALENDO KAMA PONDAMALI ALIVYO LIKATAA JINA LA MENSAH,AU VIPI MKUU KUANZIA LEO KWA KIWANGO NA KIPAJI CHAKE NA UKALI ALIONYESHA TUNAMPA ASHA RASHIDI'DILUNGA'

    ReplyDelete
  13. Anafagilia Yanga si ina rangi za kina JK sasa wewe kama unabisha sema, na wewe usiye na uzalendo wa kuwashangilia akina dada wewe ni MKIMBIZI TU rudi kwenu kwenye njaa, Pambaafu, BIG -UP ANKAL kwa kufagilia madada zetu

    ReplyDelete
  14. Mdau asante kwa taarifa.
    Sister Sister toka Nyerere FC Tunakupa hongera na kukutakia mema ujifungue salama na urudi kwenye dimba.
    Tuko pamoja katika sala na tunakukumbuka sana wakati tunacheza wote katika hiyo timu ndogo ambayo historia yake haitasahauliwa huko Mugumu, Shirati, Musoma na pale Butiama!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...