Spika wa Bunge, Mhe. Samuel Sitta akichangia katika mjadala kuhusu maswala ya kisiasa na kiuchumi Duniani wakati wa Mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika mjini Bangkok, Thailand, wikiendi hii. Spika wa Bunge, Mhe. Samuel Sitta, akifuatilia kwa makini ufunguzi rasmi wa mkutano wa 122 wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ulioanza rasmi jana mjini Bangkok, Thailand kwa kufunguliwa na Mtoto wa Mfalme wa nchi hiyo, Princess Maha Chakri Sirindhorn . Walioketi kusho ni balozi wa Tanzania nchini Malaysia anayesimamia pia Thailand, Mhe. Cisco Mtiro, Mhe, Dkt Christine Ishengoma, Mhe. Idris Mtulia na Mhe. Suzan Lyimo.
Binti Mfalme wa Thailand, Malkia Maha Chakri Sirindhorn, akifungua rasmi mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika ukumbi wa Centara Bangkok Convention Centre. Mkutano wa huo umeanza rasmi wikiendi hii kwa kushirikisha wajumbe toka zaidi ya Mabunge ya nchi 150 Duniani.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 122 wa IPU katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa rasmi jana. Picha zote na mdau Owen Mwandumbya wa Bunge




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mtu kumi, duh!!! Tanzania si nchi masikini, tusidanganyane. Ni sisi wenyewe hatujui priorities zetu. We spend a lot of cash in unimportant things leaving the majority of Tanzanians in absolute poverty.

    ReplyDelete
  2. Wachungaji wamjia juu Sheikh Yahya
    Na Restuta James

    Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini wamemjia juu Mnajimu maarufu, Sheikh Yahaya Hussein, kutokana na utabiri wake alioeleza kuwa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautafanyika na kueleza kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangwa.

    Viongozi hao ambao walikuwa kwenye kikao jijini Dar es Salaam kwa wiki tatu sasa, wameeleza kusikitishwa kwao na utabiri wa Sheikh Yahya na kuwataka Watanzania kumpuuza na kuendelea na maandalizi ya uchaguzi kama kawaida.

    Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste, William Mwamalanga, aliliambia gazeti hili Dar es Salaam jana kuwa ni aibu kwa taifa na Watanzania kutabiriwa mambo yao na kueleza viongozi wa dini wataliombea taifa ili liondokane na dhana hiyo. Alisema Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa amani na utulivu na kwamba watu wanaoitabiria nchi mabaya Mungu hatowavumilia.

    “Uchaguzi Mkuu ni jambo kubwa sana ambalo limefanyiwa maandalizi makubwa ikiwemo kuwaandaa wananchi kwa ajili ya kuchagua viongozi wao, hauwezi kupingwa na mtu anayeangalia nyota na mwezi,” alisema.

    Mchungaji Mwamalanga aliwaonya wanasiasa na watu wote wanaotegemea nguvu za giza na utabiri wa Sheikh Yahya wataanguka kwenye nyadhifa zao na kuwataka wamrudie Mungu kwa kutubu ili waweze kufanikiwa katika shughuli zao.

    Alisema utafiti walioufanya hivi karibuni umebaini kuwa wabunge 43 na Mawaziri 11 wanategemea nguvu za giza na utabiri wa Sheikh Yahya.

    Hata hivyo, viongozi wa dini wamewaonya viongozi hao kuachana mara moja na imani hizo na kumrudia Mungu kwa kuwa katika uchaguzi mkuu ujao hawatashinda.

    Mchungaji huyo amemwonya Sheikh Yahya kuacha mara moja utabiri kwa kuwa nia yake ni kuvuruga amani ya nchi na kuwajengea hofu Watanzania.

    Mapema wiki hii, Sheikh Yahya aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine alitabiri kuwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautafanyika kwa madai kuwa nchi itakumbwa na machafuko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...