TANZANIA STUDENTS ASSOCIATION BANGALORE
(TASABA)
WANAFUNZI WA KITANZANIA NUSURA
(TASABA)
WANAFUNZI WA KITANZANIA NUSURA
KUUWAWA KWA MOTO BANGALORE -INDIA
Tarehe 11/03/2010 majira ya saa 11:30 wanafunzi wawili ,Hamis Mbelwa Fintan mwenye na Olais Alexendra Siarra waliokuwa wanakaa No.1093/1.11th Cross,Swarnanagar,Robertsonpet,KGF-563 122. Walinusurika kuuwawa kwa moto baada ya fujo iliyofanywa na wahindi wakidai kuwachukia waAfrika.
Tarehe 11/03/2010 majira ya saa 11:30 wanafunzi wawili ,Hamis Mbelwa Fintan mwenye na Olais Alexendra Siarra waliokuwa wanakaa No.1093/1.11th Cross,Swarnanagar,Robertsonpet,KGF-563 122. Walinusurika kuuwawa kwa moto baada ya fujo iliyofanywa na wahindi wakidai kuwachukia waAfrika.
Wahindi hao waliamua kuchukua mafuta ya petrol na kumwaga dirishani na mlangoni, walifanikiwa kuwasha moto kupitia malangoni na moto kuanza kuingia ndani wakati vijana hao wakiwa ndani. Kwa bahati nzuri walifanikiwa kuuzima moto uliokuwa unaingia ndani na ule wa nje wasamalia wema waliuzima, bahati nzuri petrol ilikuwa chache hivyo hakuna madhara makubwa yaliyotokea.
Nilipopata taarifa hii nilitoka na kufika kituo cha Police cha Hennur Cross, nilitoa taarifa hiyo wakatoka maafisa wa police na kufika sehemu ya tukio wakati huo mimi nikiwa nimebaki kituoni. Baada ya dakika 30 police walirudi bila watuhumiwa, nilipouliza walinijibu nirudi nyumbani wameshawatuliza na hawatarudia tena nilibishana sana na police juu ya hilo maana walipofika waliwakuta watuhumiwa na kuwaachia waende huru.
Nilipopata taarifa hii nilitoka na kufika kituo cha Police cha Hennur Cross, nilitoa taarifa hiyo wakatoka maafisa wa police na kufika sehemu ya tukio wakati huo mimi nikiwa nimebaki kituoni. Baada ya dakika 30 police walirudi bila watuhumiwa, nilipouliza walinijibu nirudi nyumbani wameshawatuliza na hawatarudia tena nilibishana sana na police juu ya hilo maana walipofika waliwakuta watuhumiwa na kuwaachia waende huru.
Nilizidi kupigania haki lakini walinijibu “This is India not Tanzania and we have to cop with them like it or not” niliwauliza kama huo ndio utamaduni wao wa kumwagia watu petrol na kuchoma moto kutaka kuwaua? Wakasema kama naona hawajanisaidia niende kutafuta msaada mahali pengine.
Nilisikitika sana kwa kauli za police hasa ukizingatia kuwa toka kifo cha mwenzetu Imran Mtui ni mwezi tu na siku 7 mpaka sasa na hatujapata taarifa ya kuridhisha kutoka kwa police halafu linatokea jaribio lingine la kuua kwa kutumia petrol.
Hali hii inatisha hasa nikiwa kama mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi kuona raia wenzangu wanatishiwa kutolewa maisha yao kwa moto na bila hatia huku police wakiona jambo hilo ni la kawaida kwao na kuwaachia watuhumiwa waende huru. Watu hawa wanaishi nchini kwetu kwa amani na kufaidi matunda ya uhuru na uchumi wa nchi yetu bila bugudha.
Baada ya kuona hakuna masaada kutoka police niliwashauri Hamis Mbelwa Fintan na Olais Alexendra Siarra wahame mahali pale kwani hapana usalama tena. Tunaomba sana msaada toka nyumabani na ofisi zetu za ubalozi zilizopo New-Delhi India kutafuta jinsi ya kufanya waTanzania waishio Bangalore –India na kwingine kote kuishi kwa amani, imezoeleka kuwa mara zote wanafunzi ni wakorofi lakini kwa tukio hili nakataa kabisa kama chanzo ni wahanga hawa bali ni chuki binafsi iliyoko dhidi ya wa Afrika ambayo inatufanya tuishi kwa uoga na wasiwasi mkubwa sana. Leo hii petrol ilikuwa chache siku nyingine itakuaje? Je wangefanikiwa kutoa roho za vijana hawa majibu kutoka vyombo vya dola vya India ingekuwa ni nini? Au wangesema wamejiua tena vijana hawa kwa moto? Haya ni maswali machache ya kujiuliza.
“Mungu ibariki Tanzania, Mungu tubariki wanafunzi wa kiTanzania tuishio Bangalore India”
Fidelis Msomekela
Mwenyekiti – TASABA
+919742176980
Baada ya kuona hakuna masaada kutoka police niliwashauri Hamis Mbelwa Fintan na Olais Alexendra Siarra wahame mahali pale kwani hapana usalama tena. Tunaomba sana msaada toka nyumabani na ofisi zetu za ubalozi zilizopo New-Delhi India kutafuta jinsi ya kufanya waTanzania waishio Bangalore –India na kwingine kote kuishi kwa amani, imezoeleka kuwa mara zote wanafunzi ni wakorofi lakini kwa tukio hili nakataa kabisa kama chanzo ni wahanga hawa bali ni chuki binafsi iliyoko dhidi ya wa Afrika ambayo inatufanya tuishi kwa uoga na wasiwasi mkubwa sana. Leo hii petrol ilikuwa chache siku nyingine itakuaje? Je wangefanikiwa kutoa roho za vijana hawa majibu kutoka vyombo vya dola vya India ingekuwa ni nini? Au wangesema wamejiua tena vijana hawa kwa moto? Haya ni maswali machache ya kujiuliza.
“Mungu ibariki Tanzania, Mungu tubariki wanafunzi wa kiTanzania tuishio Bangalore India”
Fidelis Msomekela
Mwenyekiti – TASABA
+919742176980


Poleni sana wadau.Inabidi kufanya maandamano Bongo hawa jamaa hawame kwenye nyumba zetu za NHC na nina hisi kijana mwenzetu NEHEMIAH KYANDO Mkurugenzi wa NHC atatusikia,hawa jamaa kama vp tuwafukuze tu hapa Tz na nyinyi mrudi Bongo na uhusioano na India uhishe.
ReplyDeletehivi wanafunzi wanaenda india kufanya nini,au ni kasumba ya kiafrica kusoma nje ndo ujione uko kwenye level nyengine,mbona tz saa hivi vyuo vingi tu,au jaribuni kuja ulaya kusoma,kama visa ngumu basi bora msome nyumbani,maana india njaa kali,wao wenywewe kila siku wanaingia huku ulaya kusoma.atlist kungekuwa na kazi tungewaelewa nnaenda kusoma na kufanya kazi.sasa huko njaa tupu,si mara mia mkasome arusha,vyuo vizuri na hali ya hewa safi kabisa.mkitaka kujirusha nairobi only 4hours.
ReplyDeletekweli dunia ni mihangaiko,watanzania wanaenda india kusoma,india wao wanaeda malasyia,na malaysia wao wanaenda europe na usa kusoma,wazungu nao hivyo hivyo,wamarekani wengi wanakimbilia europe kusoma,na europe wanaenda usa.kweli maisha kuhangaika,ata uwe na kila kitu hutaridhika,unaweza kukuta hao wanafunzi wa tz india,wangeweza kusoma bongo na kupanga nyumba pembeni ya chuo na gari pia.
ReplyDeleteKwa vile hawa wahindi wanatangaza vita na ndugu zetu walio India na serekali yao haichukuui hatua,labda ifike hatua na sisi tuanze kuwapa kichapa wahindi walioko Tanzania, labda ndio watajua kuwa tumechoshwa na yanayofanyika India.
ReplyDelete2 . Lakini la pili, tutafuteni sehemu mbadala ya kusoma badala ya India, kama vile Malasia, Singapore na nchi nyingine zenye unafuu wa maisha.
3. Serekali yetu,itoe tamko kulaani na kuomba tamko la serekali ya India juu ya uoza unaoendelea huko.
4. Mwisho tunasikitika sana kwa yale yanayotokea INDIA, na tunaomba dawa yoyote itakayokomesha haya itolewe sasa na wala sio wakati mwingine.
Mdau,
Pigaboksi, Norway
Mwanzoni nilikuwa nikisoma hizi habari za wanafunzi wetu ambao wapo India nikadhani ni forojo.
ReplyDeleteLakini inaonekana ni kweli wanapata shida.
Kwani hali ikoje kwa Waafrika wengine? Naamini kuna Wanigeria, Wakenya, Waganda nk. Au Watanzania mnaonewa kwa vile kutambuliwa kwa sura kuwa hawa ni Watanzania, si Wakenya, si Wanigeria nk? Hebu tupeni ufafanuzi hapo.
ReplyDeleteUkweli ni kwamba ubaguzi uko sehemu yoyote. Tofauti ni kwamba ukubwa wa tatizo ni tofauti kulingana na sehemu. Mwaka jana Warusi walikuwa wanafukuza (yaani kukimbiza kama mbwa vile ukionekana) wageni mitaani. Si kufukuza tu - nia ni kuua mgeni anapokamatwa. Na si Waafrika tu bali Waasia, Wazungu wengine wasiokuwa Warusi. Tofauti ni kwamba Mwafrika hawezi kujificha ktk nchi ya Wazungu.
Serikali yetu inabidi iyafanyie kazi madai haya na kuchukuwa hatua sitahili ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri kwa raia wake wakiwemo prospective students. Kazi ya serikali yoyote duniani ni kulinda raia wake. Wahindi walibaguliwa Australia, serikali ya India ilitoa tamko vilevile. Hiyo ndiyo kazi ya serikali makini.
wadau msipige sana vijembe,mnavyoiona china na maendeleo yake yote,wachina wapo India kibao wanasoma.
ReplyDeleteNdo hivyo dunia kuhangaika.
njooni malaysia muone hao wahindi wanavyokula displini, tatizo serikali ya bongo hawaangalii upande wa pili wa shilingi, hakuna ushirikiano wa kweli kati ya muhindi/mchina na taifa lingine. Nyumbani wanakutesa kwao wanakutesa sheria inawaogopa, jamaa wanakula mbele na nyuma na hayo ndiyo matunda baada ya uhuru
ReplyDeleteWatanzania wenzetu India wanaomba msaada.
ReplyDeleteMbona Serikali iko kimya, hata taarifa tu kuwa watafuatilia kwa makini vilio hivi vya kuomba msaada kutoka kwa Watanzania wenzetu.
INAKUWA KANA KWAMBA HATUA UBALOZI INDIA!!!
Network Engineer (NE),
Reading, UK.
poleni sana ndugu zetu mlioko India, inasikitisha sana maana ma cousin Imran tulimzika bila kichwa, jana nimesoma kuna vijana 2 wamepigwa sana na police na wananchi baada ya kupata ajali, tena waligongwa wao, leo nasoma hay tena, twende mbele turudi nyuma, hivi ina maana sisi watanzania hatuna waziri anaehusika na haya mambo ya watanzania na wananchi wake walioko nje ya nchi au? haya waziri atasema yuko mbali, huyo balozi wa tanzania india anafanya nini au yeye watoto wake hawako huko mtaani??????? watanzania hatuna tabia ya kupigana wala chuki kwa wageni na ndo maana wanakaa na kufanya wanayotaka nchini kwetu na hakuna mwenye muda nao ila kama wataendelea hivi hata sisi uzalendo utatuchosha sasa, inasikitisha sana hawa watu, me wananikera basi tu sina nguvu yoyote ya kupambana nao. watu wenyewe masikini wanakuja kuponea ncini kwetu, kodi hawalipi, wanatufanya sisi tunaishi uswahilini wenyewe wametawala mji wote, daaaaaaaaaamn, mpaka lini?????
ReplyDeleteMichuzi na wadau wengine popote pale mlipo, mnaonaje tukianza kuwapa kitu BANIANI wote bongo manake sasa imezidi!Ndugu yetu wametuulia na bado tena wanataka kutuondolea wengine na nina uhakika wengi sana wamepigwa mitaani hukohuko uindini.Chakushangaza hawajui kama wenzao wanaishi kwetu? Mi nafikiri tuanze kunyoosha mmoja badala ya mwengine.Nyie mnasemaje wadau.
ReplyDeletehayo ni machache tu tunayoripoti katika blogi hii ya jamii... ila ukweli maisha yetu haswa sisi wa KARNATAKA State.. yaani Bangalore na Mysore tunadhalilikaga saana na hawa wahindi...
ReplyDeleteila mimi naamini ingekuwa ubalozi wetu na hata serikali yetu imenyanyuaga mdomo na kulaani haya yanayowapaata wananchi wake basi naaamini yangepungua na sisi tukaishi kwa amani..
Ila ubalozi upo kwa ajili ya kuendeleza biashara na India ila swali letu BIASHARA NI MUHIMU KULIKO MAISHA YA WATANZANIA?
Laiti ningalikuwa Tanzania,ningeliuwa muhindi mmoja waone hasira nilizonazo.
ReplyDeleteMichuzi na wewe acha kujipendekeza kwa hao wahindi wenu,wakina richa
JK nae ni loser tuuuu,haiwezekani vijana wanateswa kiivo yeye kapiga kimya.
Mwenyekiti wa wanafunzi na nukuu mistari yako 'Watu hawa (wenye asili ya kiasia) wanaishi bila kubughudhiwa(Tanzania)'?!
ReplyDeleteHivyo hata wewe Mwenyekiti ni mbaguzi kama hao Wahindi wa India.
Kwa nini usizungumzia lililotokea na sio kuwaburuza Watanzania wenye asili ya kiasia ktk hilo sakata la wanafunzi wa Kitanzania nchini India.
Ankal nakusaidia kuwakemea vikali watu wote wenye hisia za kibaguzi na kuzileta ktk blogu ya jamii.
Hoja kama hizi zisizolenga ku-focus ktk issue halisi ya wahuni wa mitaani India kuwatishia maisha wanafunzi wa kitanzania, zikataka kuleta machafuko Tanzania inabidi zikemewe kwa nguvu zote.
Juzijuzi tu kuna m-Canada kafanya vioja Tanzania, lakini issue hiyo ikamuandama mkosaji na sio Wa-Canada wote. Pia serikali ya Canada ikataarifiwa kuhusu jambo hilo la raia m-diplomasia kutemea watu mate.
Hivyo ndugu zetu, dhahama hiyo inawaandama Watanzania tu, je wanafunzi wengine wa Uganda, Kenya n.k hawakumbwi na tatizo hilo. Na kama ndio basi inabidi kama jumuia ya wanafunzi toka Afrika(Wa-asili zote) mlifikishe jambo hilo ktk mamlaka za juu za India, maana Umoja ni Nguvu, Utengano ni Udhaifu.
Mdau
Jijini London.
Halafu kila siku JK anaapisha Mabalozi hivi hawa kazi zao ni nini vile? Mambo kama haya yantokea na hao mabalozi wanatumbua tu pesa ya walipa kodi wa Bongo. Bora kusiwe na mabalozi kieleweke.
ReplyDeleteNa wewe mwenyekiti kutuomba msaada nyumbani hebu fafanua unataka tufanyeje hasa.
SERIKALI YETU INAYASIKIA HAYA NA IKO KIMYA TU. NA NYINYI WAANDISHI WA HABARI FANYENI ASSIGNMENT NENDENI HAPO BONGO NYUMBANI UBALOZI WA INDIA NA KU-RAISE HII ISSUE NA WAKATI HUO HUO NENDENI WIZARA YA MAMBO YA NJE HAPO NYUMBANI KUPATA TAMKO LA SERIKALI JUU YA HII, PIA MUENDE UBALOZI WETU INDIA KUPATA HABARI HII AS WELL WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA INDIA NA ELIMU YA JUU YA INDIA NA HAPO NYUMBANI HIZO NDO HABARI ZA KUFUATILIA NA KUFANYA DOCUMENTARY SAFI AWARD WINNING SI KUTAFUTA HABARI RAHISI NA CHEPESI TU, I MEAN RAHISI IN TERMS OF MONEY AND HOW TO GET THEM, MEDIA INDUSTRY IS MORE THAN MONEY MAKING MACHINE. NI HUDUMA YA JAMAA INAYOPIGANIA HAKI ZA JAMII PIA MAHALA POPOTE DUNIANI
ReplyDeleteKwani mko huko kwa scholarship au mnalipa wenyewe. Aina maana kung'ang'ana na sehemu isiyo na usalama mind kwamba serikali yetu aina sauti kwa mgeni yeyote aliye nje wala ndani ya nchi.
ReplyDeletepoleni sana kwa kweli wanafunzi muishio India, wajua kiujumla hawa watu weupe wooote duniani huwezi kuwajua ubaya wao mbaka ukakae ktk nchi zao ndio hasa utajua kasumba zao, kwa kweli ni watu wabaya saana, na hasa kwa waafrica, sijui sie waafrica tunabahati mbaya gani kwa kweli Mungu atusaidie kwa hilo,lakini ni kweli watu weupe hawatukubali kabisa japo sie twawafagilia kila siku hata wakiwa ndani ya nchi yetuz,na hii sio waliopo india tu basi no popote pale hata waliopo ktk nchi za ulaya pia cha moto wanakiona japo kiamaisha waishi vizuri tofauti na home,cha msingi twakuombeni kheri Mola akuhifadhini mmalize masomo yenu kwa salamu na mrejee mahomu kweni mkiwa wazima, hiyo mijitu myeupe ndivo ilivo muivumlie tu na kuweni chonjo nao, isije ikakuuwenu ndugu zetusie tunakumaindini unajua pia bongo yawamaindi vilevile hayo ni just maisha tu na kusoma,mungu akujalieni mumalize masomo yenu salama na kurudi home wazima.
ReplyDeletepoleni sana kwa kweli wanafunzi muishio India, wajua kiujumla hawa watu weupe wooote duniani huwezi kuwajua ubaya wao mbaka ukakae ktk nchi zao ndio hasa utajua kasumba zao, kwa kweli ni watu wabaya saana, na hasa kwa waafrica, sijui sie waafrica tunabahati mbaya gani kwa kweli Mungu atusaidie kwa hilo,lakini ni kweli watu weupe hawatukubali kabisa japo sie twawafagilia kila siku hata wakiwa ndani ya nchi yetuz,na hii sio waliopo india tu basi no popote pale hata waliopo ktk nchi za ulaya pia cha moto wanakiona japo kiamaisha waishi vizuri tofauti na home,cha msingi twakuombeni kheri Mola akuhifadhini mmalize masomo yenu kwa salamu na mrejee mahomu kweni mkiwa wazima, hiyo mijitu myeupe ndivo ilivo muivumlie tu na kuweni chonjo nao, isije ikakuuwenu ndugu zetusie tunakumaindini unajua pia bongo yawamaindi vilevile hayo ni just maisha tu na kusoma,mungu akujalieni mumalize masomo yenu salama na kurudi home wazima.
ReplyDeleteswala hilo limetusikitisha sana,
wenu (mgodoka)
Nakubaliana na mdau namba mbili, hebu acheni kwenda huko India tafuteni maeneo mengine.
ReplyDeleteFedha munawapelekea za mafunzo, nyumba zao munakodi, vyakula na nguo zao munanunua na bado wanawapiga. ONDOKENI ONDOKENI ONDOKENI.
Ila sikubaliani na kuwanyang'anya nyumba hawa walioko hapa Dar ambao wengine hawajawahi hata kufika huko India.
Hata askari wa bongo wako hivyohivyo.
ReplyDeleteHivi hamjui kuwa wahindi wengi huenda kusoma ulaya kwa sababu vyuo vyao viko hoi?
Fidelis elezea kiu-kubwa na ki-uwazi nini chanzo cha hiki kisa cha kumwagia petroli wanafunzi hao wa kitanzania ,na sio kusema tu walimwagia petroli.
ReplyDeleteTuambie kosa au tuhuma kama vile, walikopa fedha hawajarudisha? walikopa mapenzi uswahilini hawakulipa haki yao, walitongoza watoto wa kike wa kihindi? au walilala na wake zao au mabasha zao au walivunja ndoa za watu , na au waliifanya nini hasa? Then tujue kisa cha wahindi hao kutaka kuwachoma.
Pili, Mimi nataka niseme tu , kwamba hii barua umeandika kwa jazba sana na kwa upande mmoja.Yaani kuanzia jitihada zako za kwenda kuwatoa na sio sababu uliosikia au polisi waliokuambia kwamba ndio iliyochochea huu mushkeli, zogozogo au tukio.
Tatu naomba kukuelewesha kwamba Kila nchi hasa hizi zinazoendelea raia wao hupewa sana haki na hilo halina mjadala, hata hapa kwetu nchi isiyoendelea ya Tanzania.
Nne,kusema eti wahindi TZ wanapewa haki na kuishi kwa amani ni kuonyesha jinsi ambavyo huna data na jinsi ulivyo na jazba, mbaguzi. Wahindi walio TZ asilimia tisini (90%)ni wazawa na ni raia kamili wa TZ. Sio sawa kabisa kuwalinganisha na wanafunzi wakiTZ wanaosoma India. Hawa ni wazawa halisi sawa na mimi au wewe ila wao asilia yao ni India, na wakienda pia India kusoma wao huitwa WATZ na sio wahindi. Soma historia uone kwamba waTZ wenye asili ya India wamekuwepo maeneo hayo ya NHC uhuru, Kariakoo na sehemu za kati za miji mingine mikuu ya TZ hata kabla ya UHURU na wengi wao, Mababu zao walishiriki kikamilifu katika kampeni za kuleta uhuru TZ, zaidi hata ya babu yangu mimi au babu yako wewe Mzee Msomekela, aliyekuwa huko Mbeya akilima mpunga.Elewa historia kwamba Wahindi wengi waliondoka TZ wakati wa vuguvugu la UHURU na wachache waliobaki, walisaidia na kushiriki kwa umaskini wao kutetea haki za weusi na wao wahindi ili kudai uhuru.sheria za mwaka 1961 za Tanganyika Huru ziliwapa uraia sawa na babu yako, kwani kabla ya hapo mababu zetu walikuwa raia wa koloni la Uingereza.
Acha jazba na mambo ya rangi, hapa .
Mwisho, Fidelis Fuata sheria , na elewa pia sheria za India na utoe mapendekezo kama ulivyofanya ya kuomba wanafunzi kujitahidi kukaa sehemu moja. Pia waombe waache tabia zilizofanya wananchi wakaamua kuwachomea nyumba.
Elewa hapa hapa tu Tanzania watu wanachomwa moto kila kukicha, kama wezi, walozi, wagoni na bado sijaona mtu akienda polisi kusema mbona fulani hajafungwa au hajashikwa kwa kumchoma mwizi yule moto magomeni, au kabila lile linachomwa sana na sio haki.
Tupe source na sio blame next time au ubaguzi wa rangi kwa WATZ ambao in one way or onother hawahusiki na what happened in India.
Wazungu walitutawala, wakatufanya watumwa, wanatutawala hadi leo na still hatujasema wanaishi kwa amani Africa. Nakuomba uache ubaguzi na soma upate elimu na kuleta hiyo Technology hapa nyumbani.
hii minyang'au hii dawa yao ni idd amini tuu aliifagia yote kule uganda alifanya jambo bora kabisa ni mibaguzi kweli hata hapo bongo we nenda pale coco beach utakuta imejipanga mafungu yenyewee utadhani beach ya kwao anzeni kuwapa kichapo ili ubalozi wao bongo upige kelele waone mkuki kwa nguruwe ulivyo mtamu
ReplyDeleteTANZANIA TUNATAKA KUMSIKIA WAZIRI WA MAMBO YA NJE ANAONGELEA NINI KUHUSU HII KITU? NA BALOZI WA KUTOKA INDIA HAPA NCHINI TANZANIA ANALIONAJE HILI SWALA?
ReplyDeleteSABABU WOTE TUNAJUWA WATU WA INDI WAKIFANYIWA UNYAMA KAMA HUU NCHI ZA WATU WANAANDAMANA SANA WATANZANIA WAPANGE SIKU KUANDAMANA UBALOZI WA INDIA NA HII TABIA YAO, IONGELEWE HUKU UBELIGIJI.
JE WADAU MNAONAJE TUKIWACHA KUHUSU WATU KUSOMA HAPAHAPA MBONA SIE TUNAWATIZAMA KWA UZURI?.
Hii habari ikifikishwa kwenye vyombo vya habari vya india hii tabia itapungua sana...kwanza kwa sababu wahindi hawapendi kuchafuliwa.........pili ikifiwa na watu wakubwa wenye utu watasaidia kwa asilimia kubwa sana.hivyi vipolice hata kizungu tu havijui......Kitu chengine ndugu zangu watanzania tuna mambo mengi sana,unaweza kuta hili tukio lina uingiliano na mambo mengine,(madem,ugomvi,matusi,zarau)ikiwa ni tukio lakulipiza kisasi...but hayo ni mawazo tu jamani dont talk this personal.......................
ReplyDelete...................ni landloard sainkpury pale.....young z
1.POLENI SANA WADUA.UKWELI WA MAMBO INDIA NI NJAA KALI..WALA HAKUNA MPANGO.NI MARA KUMI UPATE ELIMU YAKO YOTE BONGO.
ReplyDelete2.KUANZIA SASA MIHINDI YOTE ILIYOKUWA BONGO TUWAPE VIBANO WARUDI KWAO.
3.WATANZANIA NA WAAFRICA WA NCHI ZINGINE RUDUNI MAKWENU,KAMA ELIMU ATA AFRICA INATOA ELIMU NZURI.SIONI SABABU YA KUENDELEA KUSOMA INDIA!!!
4.NALAANI VITENDO VYOTE VYA KISHENZI WANAVYOFANYIWA WAFRICA WEZANGU HUKO INDIA.
mdau...taifa kubwa.
Ankal hii kitu naomba uiwakilishe kwa Waziri wa Mambo ya nje bwana Bernad Membe, balozi wa India nchini Tanzania na ikiwezekana Ikulu na wote itakua vyema walitolee tamko hili suala ili tujue ukweli wa hii habari na ukubwa wa hili tatizo kabla ya hii habari kuleta madhara kwa pande zote mbili. Ikiachwa hivi hivi basi jua ipo siku watanzania watachomwa moto kweli au watz wakawalipiza kisasi kwa wahindi wasio na hatia waliohapa Tanzania.Ni jambo la msingi kama ukweli halisi ukajulikana kuhusu hii habari ikiwezekana balozi wa India aombe radhi na kuhatuhakikishia usalama wa ndugu zetu huko India.
ReplyDeleteNB
Wachangiaji wa humu wanasahau kwamba hakuna Indian mwenye asili ya Tanzania bali kuna Watanzania wenye asili ya India so ni rahisi kwa sisi kuonekana wanaxenophibia tuki retaliate so please Michuzi validate this story for us
RUDINI NYUMBANI JAMANI UHAI KWANZA MAMBO MENGINE BAADAE
ReplyDeletePoleni sana ndugu zetu wa India, nakuelewa unavyojisikia ndugu mwenyekiti ndio maana umeandika kwa hasira sana taarifa yako.
ReplyDeleteUshauri wangu kwenu
1.Mjaribu kuwasiliana na ubalozi na kutafuta ufumbuzi wa matatizo haya ingawa nafahamu sana balozi zetu nchi za nje zinavyojiweka mbali na wananchi wake na hilo si kwenu tu lakini naamini wakati huu wa matatizo wanaweza kuwasikia kidogo
2.Ushauri kuwa mrudi nyumbani sifikiri hivyo cha msingi mshikamane na kupigania haki zenu na haya matatizo yataisha huwa ni ya msimu tu.
kuna mdau hapo juu aligusia pia Urusi lakini akumbuke kuwa Urusi wakina Katya na Masha ni wakarimu sana hivyo wadau wa kule walikuwa wakikimbizwa mtaani nakuitwa manyani basi jioni wakiwasimulia akina Katya na Olya matatizo yote yanatatuliwa na wanafarijika kifikra sijui hari ipo vipi India.
hawa wahindi ni wapuuz sana,mm nipo urus miak kadhaa lkn hata siku mmoja cwez kumpenda mtu mweupe au muhindi,hv ukiniita mmbaguzi c kosa kwangu,HV NINA SABABU GANI YA KUMPENDA MTU AMBAYE HANIENDI NA KWANI NALALA KWENYE PUA ZAKE?,WAENDE ZAO HUKO,C TZ TUKIAMUA WATARUDI KWA KWA MIGUU WE NGOJA TU!
ReplyDeleteKama mnaonewa tuu kwa sababu ya rangi ya ngozi yenu basi nina laaani sana hawa ponjoro wa huko. Balozi lazima aingilie na serikali lazima iingilie vilevile kuzima huo ushenzi.
ReplyDeleteLakini washikaji kama mna mambo yenu ya kufuatilia wasichana na mademu wa kihindi badala ya shule iliyowapeleka hilo mtajua wenyewe, kweli watawamaliza hata kama serikali ya wahindi na bongo zikifanya nini.
Si uongo wabongo tunapenda sana mademu, tuwe waaungwana tufuate mila za wenyeji, tuache uharibifu. Nina hamu kubwa kujua nini chanzo cha hiki kisa, sio tuu eti ponjoro gafla wanataka choma watu. Lazima kuna chanzo kilicho wachochea kutaka kufanya hilo.
Sisi wote watu wazima, tunaomba vijana fanyeni kilichowapeleka, na waachieni wahindi mambo yao wenyewe.
Mdau USA
Ondokeni huko ...najua wengi wenu mko huko kwa scholaship za serikali lakini kama nchi haikooperate si muondoke wote na mara watajua upungufu wa hela inayokwenda huko kwao? Nahisi india yote kuna wabongo zaidi ya 10,000 sasa mkiondoka wote au serikali ikisema haitasomesha tena mtu huko si watapata jibu hao?
ReplyDeleteONDOKENI MUWAANCHIE NCHI YAO. MTAULIWA BURE
HAO WADAU WALIOSEMA OOH UBAGUZI, NAFIKIRI NI WAHINDI JAMANI!! MAANA MTANZANIA MWENZETU AMEUWAWA!!! MNATEGEMEA TUTAKUJA KIULAINI JAMA! OOH WALISAIDIA KUDAI UHURU! JAMANI HIVI HAMJUI HISTORIA YAO HAWA! MBONA HATUISHI NAO VINGUNGUTI BAADA YA HUO UHURU! OOH BARUA IMEANDIKWA KIHASIRA!!!! OFCOURSE NDIO U TANZANIA HUO.. AMANI LAKINI CHOKOZA UONE! MPO WABONGO??? TUINGIENI JAMATINI PALE, TENA MIDA YA JIONI JIONI
ReplyDeleteWADAU MI NAFIKILI WATU WOTE TUNAZIJUA BALOZI ZETU ZILIVYO POPOTE PALE DUNIANI JAPOKUA KUNA BAADHI ZA UBALOZI NI KWELI ZINA JITAHIDI KUTOA USHILIKIANO PAKE TATIZO LINAPO TOKEA ILA NYINGI HUWA ZINA KAAGA KIMYA NA UNAPO KWENDA KUTOA TAHARIFA YA TATIZO FURANI UMEPATA BASI HUWAGA KWANZA UTUPIWA RAWAMA WEWE KUWA HA UYU NDIO MKOLOFI NA BIRA KULIFATILIA KWA UNDANI NI NINI KIMETOKEA AU TUMSAIDIE VIPI RAI WETU HATA KAMA ULIKAMA NA MADAWA YA KULEVYA KINACHOITAJIAKA SI KUKAA KIMYA ILA KINACHOTAKIWA NI KUKUAKIKISHIA WEWE RAIA WAKE UANATENDEWA HAKI SI KUKAA KIMYA . ILA NILIKUA NA MAANA PENGINE HATA UBALOZI WETU HAWAJUI AU KWASABABU ATUJASIKIA KITU CHOCHOTE TOKA UBALOZI WETU UKO INDIA NAINAWEZEKANA PIA HATA SEREKARI YETU PIA HAWAFAHAMU KITU CHOCHOTE ILA TUNAOMBA BALOZI ZETU MSITUSALITI NAMNA HII NYINYI MPO UKU KWA SABABU YA TAIFA LA WATANZANIA SI KWASABABU YA NYIEKUKA UKU NA KUFANAYA MAMBO YENU . SISI TUNAJUA TAIFA LETU NI MASIKINI NA BALOZI ZETU AZINA PESA ILA TATIZO ATUOMBI PESA UBALOZINI NI TUNAOMBA MSAADA HILI TUWEZE KUPATIWA HAKI ZETU PALE PINDI TUNAPOITAJI MTUSAIDIE MBONA WENZETU AFRICA MANGARIBI WANA PEWA USHILIKIANO MZULI KULIKO SISI NA WAO WENZETU NI WANA MATATIZO KWELI KWELI TENA YA HAJABU HAJUBU. ILA BALOZI ZAO ZINAPO SIKIA KAMA RAIA WAKE KAMATWA AU KUNA KITU KIMEMTOKEA BASI UJITOKEZA NA KUMSADIA MI NAAMINI KAMA SERIKARI YETU INAJUA ALAFU INA KAA KIMYA BASI ILO NI KOSA KUBWA KWANI UNAVYO ONA UMU NDANI WADAU WANAVYO ANDIKA WALIVYO NA DUKUDUKU BASI MJUE IPO SIKU MWANAFUNZI MMOJA AKAJA KUULIWA UKO INDIA NDUGU WA UYO MTANZANI NAO WAKAAMUA KUTOA HASIRA ZAO KWA KUMKAMATA MUHINDI[KI AU KIBIBI CHA KIDOSI KINACHOTEMBEA KITOVU INJE NA KUKISHUGHULIKIA YOYOTE KULE TONW NA KUTOA HASIRA ZAO MBAKA SEREKARI HIYANZE KUFATILIA ITAKUA IMECHELEWA KWA SABABU UYU MDOSI WA BONGO PENGINE HATA UKO INDIA AKUJUWI NA MWENYEWE KAZALIWA PENGINE SHINYANGA KWAIYO NILITAKA KUSEMA WE BALOZI WA TZ INDIA KAMA UNAJUA ALAFU UNAUCHUNA SHAULI YAKO WE UCHUNE TU UJUWE AYA MATATIZO YANA WEZA KUKUGHAKIMU KAMA UAMINI WE ANGALIA SINMEMA INAWEZA IKACHEZWA . MWISHO POLENI SANA WA TZ WA INDIA SISI WOTE TUNA MATATIZO NA MAUBALOZI YETU
ReplyDelete