Mlemavu wa Ngozi ( Albino), Said Abdallah ( 41) ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Melela , akiwaamelazwa wodi namba moja ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ,kuazia juzi baada ya kukatwa kiganja cha Mkono wa kushoto wakati wa ugomvi baina ya wakulima na wafugaji wa Jamii ya Kimasai pia wa Kijiji hicho cha Wilaya ya Mvomero Mkoani hapa.
Picha na Habari
Na John Nditi, Morogoro

MAMIA ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wamekuwa wakifurika katika wodi ya wagonjwa ya namba moja katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kumwangalia Mlemavu wa ngozi ‘ Albino’ Said Abdallah ( 41) aliyekatwa kiungo chake cha kiganja cha mkoni wa kushono na vijana wawili wa Jamii ya kimasai na kutoweka nacho kuzikojulikana.

Abdallah ,ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Melela Mlandizi, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro alikutwa na zahama hiyo Aprili 10, mwaka huu majira aya saa nane mchana wakati akikata kuni kwa ajili ya kwenda kuuza ili kupata fedha za matumizi yake ya kila siku.

Akizungunza na HabariLeo ,jana akiwa kitandani kwenye wodi namba moja, alisema alivamiwa siku hiyo na vijana wawili kimasai mara baada ya kuombwa awapatie tumbaku ya kuvuta na wakati akiinama kuwachukulilia walishitukia akipigwa fimbo nyingi kichwani, uso na hivyo kuzimia kwa kupoteza fahamu.

Kwa mujibu wa Mlemavu huyo kuwa baada ya kuziduka alijikuta damu nyingi ikiwa imetapakaa sehemu aliyolala huku mkoni wake wa kushoto ukiwa umekatwa kwenye kiganja na kuchanwa sehemu ya jicho la kulia.

Alisema alipiga mayowe kwa ajili ya kuomba msaaada ambapo walijitokeza baadhi ya majirani kumsaidia na vijana hao kukimbia lakini walipofika kuwamgalia walimwona amekatwa kiungo chake cha mkono na walipokitafuta walishindwa kukiona.

“ waliponipinga na fimbo nyingi nilipoteza fahamu na kuzimia…lakini baada ya kuzinduka nikajikuta mkono wangu umekatwa na damu zimetapakaa …majirani walinisaidia kutafua sehemu iliyokatwa lakini hawakuiona kamwe …kikawa kimetoweka na hao vijana wa kimasai’ alisema Mlemavu huyo wa Ngozi

Hata akielezea sakata hilo, alisema siku ya tukio hilo alikuwa na mzigo huo wa kuni akipekela Kijiji cha Kipera pia ni katika Wilaya ya Mvomero, kwa lengo la kuziunza na kuoata fedha , lakini akiwa jiani walijitokeza hao vijana wa kimasai na kumwomba tumbaku ya kuvuta.

“ mimi nilikuwa nikivuta tumbaku ….waliponiona waliniomba niwapatia tumbaku ….nikaima chini ili niwachuliwe kwenye mzigo wangu , lakini kitendo cha kuinama tu wakanivurumishia kipigo cha fimbo kichwani na usoni nikazimia…nilipozinduka nikaona damu nyingi na kuangaalia sina kiganja kimekatwa” alisema Abdallah

Hata hivyo alisema kufiatia tukio hilo majirani walipekeleka taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Mzumbe na wengine kumsaidia kufikisha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.

Aidha alisema wamasai hao walikuwa na visa kwa kitendo cha kuwazuia wasiingize mifugo yao kwenye eneo la kisima cha maji ya kunywa na katika mashamba yaliyopandwa mahindi mwaka huu na wananchi wa Kijiji hicho.

“ wakati fulani tulizikamata ng’ombe za wamasai hao na kutoa taarifa kwa Mtendaji na Kituo Kidogo cha Polisi cha Mzumbe …lakini baada ya hapo majirani waliniambia kuwa vijana wa kimasai wananitafua kwa kuwa mimi ” alidai kusema Abdallah

Naye Nuru Abdallah Mkazi wa Modeco Kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro ambaye ni kaka yake , akiwa wodoni hapo alisema walipata taarifa ya kaka yao kukatwa kiungo cha mkono wake na ndugu zao wanaoishi naye Kijijiji Melela.

“ hiki kitendo ni cha kushangaza …sisi nduguzake tusingekuwa na wasi wasi iwapo kuingo kilichokatwa kineonekana …lakini hakipo , wasi wasi wetu huweda kuna jambo limefichwa ndani yake kuhusu uwezkano wa kuzuka biashara ya viongo wa binadamu hasa Albino “ alisema Nuru

Mwenyekiti wa Chama cha Malbino Mkoa wa Morogoro, David Mganga , ambaye alimtembelea Hospitalini hapo jana jioni kwa ajili kumjilia hali na kupata maelezo ya kina kuhusiana na tukio hilo ambapo alisema kuwa hilo ni tukio la kwanza kutokea Mkoani Morogoro.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alitia shaka juu ya kutoonekana kwa kiungo hicho kama ulikuwepo ugomvi kati ya wafugaji na wakulima kuhusiana na malisho ya mifugo kwenye mashamba ya wakulima.

“ Sisi kama Chama tunatilia shaka juu ya kadhia hii kwa vile ingekuwa ni ugomvi wa kawaida na wamemkata mkono basi ungeonekana sehemu hiyo …tuna hisi wimbi la kutafua viungo vya Albino vimeingia Morogoro” alisema Mwenyekiti huyo

Hivyo ameviomba Vyombo vya Dola vya Mkoa wa Morogoro na Viongozi wote wa Serikali kujipanga vuzuri kuweza kuchukua hatua ya kudhibiti hali ambayo inaweza kujitokeza kuwa baadhi ya watu wananunua viungo vya Albino.

Mbali na kuviomba Vyombo Vya Dola, pia amewataka Walemavu wa Ngozi wanapotishiwa na mtu yeyote yule ni budi kutoa taarifa katika Vituo vya Polisi na Mamlaka nyingine za Kiserikali na kama Chama kichaendelea kufanya uchunguzi wake ili kuona kama vitendo vya kikatili juu ya Ablino vimeingia Mkoani hapa.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Grory Kata ya Mji Mpya, Manispaa ya Morogoro, Fortunatus Majengo, ambaye ndiye aliyemshuhudia siku ya kwanza akiletwa Hospilini hapo na baadaye kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Chama hicho cha Maalbino alisema kuwa kitendo hicho ni sawa na fumbo kubwa.

Hivyo ameishauri Serikali ya Mkoa kuanza kufuatilia tukio hilo la aina yake ambalo halijawahi kutokea katika mikoa ya Kanda ya Mashariki ukiwemo wa Morogoro kwa mlemavu wa ngozi kukatwa mkono na kiungo chake kutoweka licha ya kinachodaiwa ni mazingira ya ugomvi baina ya pande mbili hizo.

“ hili ni fumbo kubwa …kama ni ugomvi basi mkono huo ugeonekana sehemu ya tukio , lakini umweshindwa kuonekana …kitendo hiki ndicho kinatoa fumbo hili” alisema Mchungaji huyu ambaye alifika Wodini kwa ajili ya kumwombea Abdallah apone haraka

Nao baadhi ya wananchi walifika wodini hapo , wakizunguzia tukio hilo la kwanza na la aina yake , kwa nyakati tofauti walisema kuwa kitengo hicho ni cha kikatili na hivyo kulikata Jeshi la Polisi linawasaka wahusika hao na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

“ tumeshikwa na butwaa …mambo haya tulikuwa tukiyasikia mikoa mingine hasa ya ziwa …lakini sasa yameingia kwenu , ni budi tukilaani kitendo hiki cha kikatili cha kukata kuingo cha binadamu na hasa huyu Albino kwa imani za ushirikina …ni lazima watafutwe “ alisema baadhi ya wananchi hao.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kukatwa mkono mlemavu wa Ngozi ‘ Albino’ na kusema kuwa lilitokea wakati wa ugomvi wa kawaida kati ya vijana wa Jamii ya wafugaji wa kimsai na wakulima wa eneo hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo kuwa wafugaji wa kimasai wanadaiwa waliingiza ng’ombe kwenye mashamba ya wakulima na hivyo kukatokea mtafaruku baina ya pande hizo mbili kushambuliana ambapo Albino huyo alikuwa mingoni mwa walikuwa wakipambana wafigaji wa jamii hiyo.

“ ni kweli hili tukio la Albino kukatwa kiganja cha mkono limetokea Aprili 10, mwaka huu eneo la Kijiji cha Melela …zilitokea rasha kati ya wakulima na wafufaji wa kimasai ambao wandaiwa waliingiza ng’ombe hao kwenye mashamba ya wakulima na katika sakata la ugomvi huo Albino huyo alikatwa mkono huo” alisema Kamanda huyo

Hata hivyo alisema bado sehemu ya kiungo cha Albino huyo kilikuwa bado hakijapatokana na kwamba Polisi imeanisha uchukuzi wa kina kuhusu tukio hilo ambapo mmoja wa washukuwa wa jamii ya wafuigaji wa kimasai ametiwa mbaroni kuisaidia Polisi kuhusiana na tuko hilo.
Baadhi ya majirani wakimfariji Said Abdallah ( 41) Mlemavu wa Ngozi ( Albino) liyelazwa kuanzia juzi wodi namba moja ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro , baada ya kukatwa kiganja cha Mkono wa kushoto wakati wa ugomvi baina ya wakulima na wafugaji wa Jamii ya Kimasai wa Kijiji cha Melela , Wilaya ya Mvomero Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Grory , Kata ya Mji Mpya, Manispaa ya Morogoro, Fortunatus Majengo, akimwekea mikono kichwani na kumwombea, Mlemavu wa Ngozi ( Albino) , Said Abdallah , liyelazwa kuanzia juzi wodi namba moja ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro , baada ya kukatwa kiganja cha Mkono wa kushoto wakati wa ugomvi baina ya wakulima na wafugaji wa Jamii ya Kimasai wa Kijiji cha Melela Wilaya ya Mvomero.Mwenyekiti wa Chama cha Malbino Mkoa wa Morogoro, David Mganga , ( kushoto) akiwa wodini akisikiliza maelezo ya Mlemavu wa Ngozi ( Albino) Said Abdallah ( 41) Mkazi wa Kijiji cha Melela , liyelazwa kuanzia juzi katika wodi namba moja ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro , baada ya kukatwa kiganja cha Mkono wa kushoto wakati wa ugomvi baina ya wakulima na wafugaji wa Jamii ya Kimasai pia wa Kijiji hicho kilichopo Wilaya ya Mvomero.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mi nasema ivi....wanaglobu woooote toka pande zote za dunia tuchague siku na muda maalumu, waisilamu kwa wakristo, tuwaombee dua ndugu zetu maalbino Mwenyezi mungu awape kinga na amani. Na mwenyezi mungu awalaani watakaowafanyia unyama ndugu zetu maalbino kusanzia siku na wakati huo.

    Nakasirishwa mpaka nakosa la kusema, ubinadamu watu wengine hawana kabisa....what a shame!.

    ReplyDelete
  2. UNYAMA UNYAMA UNYAMA KWELI TUTAFIKA?

    INASIKITISHA,INAUMA,INAKERA SANA

    MUNGU ATAKUSAIDIA BWANA SAIDI NA KWA UWEZO WAKE MUUMBA ATAWAANGAMIZA MAADUI WAKO

    NINGEOMBA ANKAL UTUWEKEE CONTACT ZA HUYO BWANA SAIDI KAMA YUPO NA SIMU

    NAOMBA NITAFUTIE NAMBA YA SIMU ILI NIWEZE KUWASILIANA NA BWANA SAIDI ILI NIWEZE KUMPA POLE

    LENGO LANGU NI KUMPA POLE NA KUJARIBU KUMUULIZA NJIA GANI NAWEZA KUMTUMIA MSAADA KWANI NAJISKIA KUMCHANGIA CHOCHOTE KUTOKANA NA MASAHIBU YALIYOMPATA

    mwana jamii wa mahakama kuu ya dunia.

    ReplyDelete
  3. Hii ni dhambi sana....Mungu atawalaani hawa wanaofanya hivi...

    ReplyDelete
  4. NI KITU CHA AIBU, HUZUNI NA KUSIKITISHA SANA NA SERIKALI YETU LAZIMA ITOWE TAMKO NA HASA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MWAKA HUO VYAMA VYA SIASA LAZIMA VITOWE TAMKO.SERA JUU YA JAMBO HILI NA MALBINO JIKUSANYANI MUANDAMANE KUDAI HAKI YENU YA KUISHI SAWA KAMA BINADAMU WENGINE NA KUPEWA ULINZI WA KIPLOSI NA KIJAMII KAMA MNAVYOSTAHILI. HILI NI JAMBO LA AIBU SI KWA WATANZANIA TU BALI HATA KWA SERIKALI LINATUTIA AIBU DUNIA KOTE, MTU YEYOTE MWENYE ACCESS NA INTERNET GOOGLE TU HABARI ZA ALBINO TANZANIA UTAONA WANAVYOTUPAKA WATU DUNIANI HUKU, HATA KWENYE YOU-TUBE SEARCH TU UTAONA AIBU TUNAVYOPATA WATANZANIA, RAIS HASA KIKWETE LISEMEE HILI NI AIBU KUBWA. TASISI ZOTE ZA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI ZINATUPAKA KICHIZI JUU YA HILI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...