Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake ya Tuzo Milionea leo usiku (13/04/2010) itampata mshindi mwingine mmoja mwenye bahati atakayejinyakulia Tsh 100 Milioni pesa taslimu.
Bw. Renatus Mkinga ndiye aliyejinyakulia kitita cha Tsh 100 Milioni mwaka jana kwenye awamu ya kwanza ya promosheni ya Tuzo Milionea.

Awamu ya pili ya promosheni ya Tuzo Milionea yenye lengo la kuwashukuru wateja waaminifu wa Vodacom, ilizinduliwa mwezi Januari mwaka huu na leo hii usiku ndiyo itafikia tamati.

Mbali na zawadi kubwa ya Tsh 100 Milioni, pia kulikuwa na zawadi za kila siku ambapo mteja mmoja mwenye bahati aliweza kujinyakulia Tsh 100,000 za muda wa maongezi ILA SIKU. Jumla ya wateja 84 wenye bahati walijishindia Tsh 100,000 za muda wa maongezi na wote wamekwisha tumiwa zawadi zao hizo kwenye zao.

Macho na masikio ya watanzania na zaidi wateja wote wa Vodacom waliojiunga na promosheni hii ya Tuzo Milionea kwa kutuma SMS yenye neno TUZO MILIONEA kwenda 15588 au TUZO MILIONEA kwenda 123 watakuwa wakishuhudia LIVE kwenye luninga zao kupitia kituo cha ITV kuanzia saa tatu na nusu usiku.

Hakikisha simu yako ya Vodacom unaiwasha na ipo karibu na wewe kwa kuwa unaweza kuwa mshindi wa kitita hiki.

Vodacom Tanzania inapenda kuwashukuru wateja wake wote waliojiunga na promosheni hii ya Tuzo Milionea na inawapongeza washindi wote 84 waliojinyakulia Tsh 100,000 za muda maongezi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...