Amani akiwatumbuiza wapenzi wa jijini London.

Mwimbaji maarufu tok nchini Kenya, Amani alikonga nyoyo za wapenzi wa muziki jijini alipofanya shoo yake ya kwanza jijini London siku ya Ijumaa ya tarehe 2 katika ukumbi wa Ambassador. Amani ameahidi kufanya makubwa zaidi kwenye maonesho yake manne nchini Uingereza, ambapo atatumbuiza Reading, Bristol na London tena.
Mwanadada huyo alianza shughuli zake za muziki miaka saba iliyopita. Beyonce na Mariah carey ndiyo waliomtia changamoto ya kuanzaa kuimba Kenyan Pop. Nyimbo zake nyingi zinahusu mapenzi na anaimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili/English.
Ameshatoa album moja inayoitwa "Tamani" yenye nyimbo 10. Album hiyo ina nyimbo inayopendwa sana na mashabiki wa muziki "Missing You My Baby". Amani ameshapata tunzo nyingi ikiwemo tunzo ya best female MTV African Awards. Mpiga picha maarufu nchini Uingereza Bw. Shabani Kawawa akiwa na Amani muda mfupi kabla ya kutumbuiza katika ukumbi wa Ambassador jijini London.
kushoto DJ Richie katikati Amani wakiwa na mwandishi wa BLOG ya TZ-ONE Ally Muhdin
Amani akiwa na wadau waliojitoleza kwenye kuangalia onyesho lake jijini London.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Pardom me, but who is she? may be this time michuzi will allow my question to appear here. thank you.

    ReplyDelete
  2. Yeah ila angevaa kitu kama min-skirt angependeza zaidi kwani huyu dada ana mguu balaa...mguu wa kufa mtu.

    ReplyDelete
  3. To Anonymous (Sun Apr 04, 01: 43:00pm):

    SHE IS A SINGER!!.....DUUH!

    ReplyDelete
  4. acha uvivu,shughulisha bongo lako,soma maelezo yote utajua ni nani,kumbuka vilevile huwezi kumjua kila mtu.

    ReplyDelete
  5. Jamani AY .... ilikuwaje?
    mZOZAJI

    ReplyDelete
  6. nakubaliana na mtoa maoni wa 2, kwani dada yetu kapendeza sana ila hiyo suruali tu angeitupa na kuvaa sketi afu na michuzi angetuwekea kaji clip kake hapo tuone mauno anavyoyatoa tuone hicho kipaji chake.

    ReplyDelete
  7. amependeza ile mbaya!

    ReplyDelete
  8. TeQuann na mdau wa Sun Apr 04, 10:21:00 PM labda kiingilish kinakushindeni lakini suali linabaki pale pale who is she?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...