
Ni vijana ambao mpaka hivi sasa wanaweza kusema ‘wana mafanikio” fulani kutokana na kazi zao za muziki.Walianzia East Coast na mara kundi hilo lililokuwa na makazi yake pale Upanga-Dar-es-salaam,liliposambaratika wao wameendelea kuwa pamoja kama marafiki na pia wasanii wanaoshirikiana.
Tunawaongelea Mwana FA na A.Y ambaye siku chache zilizopita alipata tuzo ya Teenz kutoka nchini Kenya kama Favourite Artist wa East Africa. Safari hii wimbo unaitwa Usije Mjini. Kwanini nisije mjini wakati mjini nasikia ndio mambo yote? Kila mtu anataka kuja mjini.Mjini hata kwa kuuza maji tu unaweza kujipatia kipato.Mjini kuna starehe zote…inaaminika. Sasa kwanini A.Y na Mwana FA wanasema Usije Mjini? Sikiliza kwa makini tungo hizi;
Nenda kwa Globu kaka ya Jamii Bongo Celebrity
Daa!
ReplyDeleteWimbo umetulia ile mbaya. Big up Mwana FA and AY kazi nzuri.
Usije mjini kuna manyoya na wamasai wamewanyang'anya deal wamakonde huku mjini hawawindi Simba wanasuka dada zetu tu!Ni baadhi ya maneno ya wimbo huo, nimecheka sana.
Mdau