Hayati Dominic Mwita
Chumba cha habari cha Daily News na HabariLeo kimeghubikwa na majonzi kufuatia habari ya kifo cha Dominic Mwita (32), aliyewahi kuwa mwandishi wa habari kwenye makampuni hayo kabla ya kuhamia kitengo cha habari cha UNICEF jijini Dar.
Kifo chake kimesababishwa na ajali ya barabarani siku ya Ijumaa usiku wakati marehemu aliyekuwa anatoka harusini na gari yake aina ya RAV4 aliingia kwa nyuma semi-trela lenye namba T632 AGH lililokuwa limesimamishwa katikati ya barabara kiasi cha mita 100 hivi toka daraja la Mbezi Beach jijini Dar.
Kamanda wa polisi wa Kinondoni Elias Kalinga amethibitisha kutokea ajali hiyo na kusema uchunguzi unaendelea. Aliongezea kusema tela hilo lilisimamishwa katikati ya barabara bila wenyewe kuweka tahadhari ya traiengo ama ala ingine kwa watumia barabara wengine.
Msiba uko nyumbani kwa shemeji wa marehemu, Bw. Fred Mwita, huko Mbezi Makonde ambako mipango yote ya mazishi inafanyika.

Marehemu Dominic, ambaye amewahi kufanya kazi Posta na Nyanza bottling huko Mwanza, amefanya kazi Daily News kati ya mwaka 2003 na 2005 kabla ya kuhamia UNICEF.

Mola aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu

AMEN


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. This is so sad to hear he was such a gentlemana dn a very good fella, R.I.P Dominic.

    ReplyDelete
  2. Mungu amwangazie Mwanga wa Milele na apumzike kwa amani. Amen.

    ReplyDelete
  3. oh my god!mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema amina.poleni wafiwa.japo simjui lakini tukio linasikitisha sana tunapoteza watu,vijana wajenga taifa,innocent people kwa uzembe.polisi waangalie sheria za barabarani zifuate sio kupokea hongo tu na kuacha hali ileile inaendelea.

    ReplyDelete
  4. Baba UbayaApril 25, 2010

    dear ooh dear!!!when will these drivers learn????madereva wengi hapa nchini kwetu hawajali usalama wa maisha ya wengine,sometimes hata yao wenyewe.ni lini uzembe kama huu utapungua?na kuna uwezekano hata taa za dharura za hilo gari kubwa hazikuwashwa.how abt walau viji-alama vya majani?
    jamani kuwe na adhabu kali kwa MADEREVA WAZEMBE.
    R.I.P Dominic.

    ReplyDelete
  5. nafikiri serikali ingeanzisha sheria kali za hawa watu wanaosababisha ajali ikiwemo za kuwafutia leseni makampuni ya usafirishaji yanayotuua kila siku na kuwalipa fidia kali wafiwa na majeruhi nafikiri makampuni ya usafirishaji yangekuwa yanaajiri madereva wanaostahili na wangeendesha kwa akili pia
    poleni sana ndugu wa Dominic kijana mdogo sana maskini Mungu ailaze roho ya marehemu peponi.Amen

    ReplyDelete
  6. Marehemu alikuwa handsome sana, kwa kweli ametutoka kabla ya wakati.

    ReplyDelete
  7. Kama KWELI aliyetoa ndie aliyetwaa, Jina la Bwana na lihimidiwe. Maana nguvu ya kiza nayo ipo. Cha muhimu apumzike kwa amani.

    ReplyDelete
  8. Poleni wafiwa. Ajali za barabarani zinatuulia watoto wetu. Usalama barabani tafadhalini ufumbuzi upatikane wa kuzuia hizi ajali zimezidi sana. Traffic control mko wapi?

    ReplyDelete
  9. namkumbuka huyu marehemu enzi zile kule SAUT malimbe 2003

    ReplyDelete
  10. R.I.P Dominic

    poleni wahusika wote wa msiba,
    tumepoteza mmojawapo wa wachapa kazi muhimu saana katika ujenzi wa Taifa.Mungu ampumzishe mahali pema peponi.

    Mickey Jones
    Denmark

    ReplyDelete
  11. Naomba kutwaa fursa hii kuwapa mkono wa pole familia na ndugu wa wa ndugu yangu marehemu Dominick. Lakini pia niwape pole wahitimu wenzangu wa SAUT 2003 na wote wanaomfahamu marehemu hasa Fr. Ted Walters, Mzee Nkwabi Ng'wanakilala na Fr. Charles Kitima. Ni huzuni kuu iliyoko moyoni mwangu kwa kuondokewa na rafiki yangu wa karibu sana ambaye nilimthamini na kumuona kama kaka wa kuzaliwa naye tumbo moja. Tulisoma darasa moja na kukaa chumba kimoja pale Malimbe - SAUT.

    Dominick alikuwa Katibu Mkuu wa serikali wanachuo 2001/2002. Alikuwa na uwezo na kipaji cha aina yake cha kujenga hoja na kuyachambua mambo. Dominick alikuwa mchapakazi mzuri, mwenye kujituma na mzalendo hasa. Hakika tumepoteza hazina muhimu ya mwanamapinduzi katika taifa letu.

    Kifo chake kimetokea wakati akiwa ni kijana mdogo. Maisha kwake yalikuwa bado ni mapya yaliyojaa matumaini mengi. Nilipokutana naye Januari-Machi mwaka huu afya yake ilijaa utomvu wa uzima na moyo wenye furaha. Niliongea naye kwa simu Alhamis 22/04/2010 akiwa ni mwenye hamu ya kutimiza malengo aliyokusudia katika maisha. Tulikuwa na mipango mizuri sana ya kimaendeleo.

    Nashindwa kuendelea kuandika machozi yananitoka kwa huzuni na simanzi. Dominick umetangulia mbele ya haki nasi tu nyuma yako kwani ipo siku nasi saa yetu itatimu. Siku moja tutakutana kwa kudra zake Jalali kwani kila nafsi itaonja mauti.

    Namuomba Mola Karima aipe subira familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

    Buriani Kamaradi. Buriani Mwenza Katika Harakati. Buriani Dominick. Daima nitakukumbuka kwa sala na maombi.

    Raha ya Milele Mpatie e Bwana, Na Mwanga wa Amani Mwangazie.

    Mola Aiweke Roho Yako Mahali Pema Peponi.

    Amina.

    Na Amani Millanga

    ReplyDelete
  12. Sheria ya usalama barabarani ni zero Tanzania. Yaani ikiishaingia saa moja usiku Traffic police wakiona hakuna cha kukusanya kwa leo wakapige mahesabu basi hapo sasa ni "Law of the junggle" inachukua mkondo wake. Kuna lugha ya "Kaliona" yaani ukijiingiza kivyakovyako.

    Umefika wakati sasa hivi kuanza na mfumo bora wa utoaji leseni za udereva. Police wasiruhusiwe ku-recommend leseni bali wao wawe enforcers tu. Kuundwe idara maalumu ya Vehicle and driving Licence iwe chini ya TRA ambayo itakuwa na watu maalum na watumie mfumo wa digital kutoa licence ambayo mtu haipati mpaka apitie mafunzo na kufaulu Computer based test and practical test. Na wakati wote wa test anarekodiwa na CCTV kama ushahidi. Kila muidhinisha leseni inawekwa ID yake kwenye leseni na kila mwaka tathmini inafanyika je ni muidhinishaji gani watu wake wamekuwa careless kwa more than 30% then anashushwa daraja.

    Hii itawafanya watu kuweka mbele usalama kwani life haina spare ukifa umekufa.

    Pili kuendesha huku umelewa nayo iwekewe sheria kali sana, kwa mtu yeyote akikutwa anaendesha huku amelewa kupita kiwango digital reading zake zinarekodiwa na kukatwa points mpaka mwisho kufungiwa kabisa kuendesha.

    Marehemu alikuwa anoteka Harusini, there is a lot of factors here juu ya kifo chake

    Mwisho tutakuwa tunawatakia watu walale mahali pema kwa uzembe wa kufuata sheria mpaka lini?. Ule msemo wa ajali haina kinga ni kuhalalisha uzembe kinga ipo, kwa kuwa
    1. Madereva waliqualify
    2. Sheria kufuatwa na kusimamiwa ipasavyo
    3. Matengezo na kuelemisha watu kuacha kupenda ubwete kwa kununua spare fake etc.

    R.I.P Marehemu Dominic

    ReplyDelete
  13. kifo cha huyu kaka kimenishitua sana, kweli maisha ni mafupi hasa kwa nchi zetu zilizojaa uzembe,

    poleni sana wafiwa, nimesikitika kama vile namjua baada ya kusoma message ya rafiki wa karibu wa marehemu, pole kaka kweli kifo hakina huruma, DR. Lemmey aliimba, kifo kifo kifo, kifo hakina huruma


    RIP MWITA

    ReplyDelete
  14. Nirudi tena baada ya kusikiliza You tube wimbo wa kifo wa Dr. Remmy nimetafakari sana kuhusu kifo, naomba msikilize wimbo huo
    http://www.youtube.com/watch?v=58OK5S6COQM

    Kweli kifo hauna huruma, jamani serikali hizi ajali za uzembe barabarani, tusaidie viongozi

    RIP Mwita

    ReplyDelete
  15. Earth's loss is heaven's gain...

    Ingawaje jimfahamu lakini inasikitiha sana kuona maisha yanakatishwa hivi na ajali ambazo zinaweza kuzuilika.

    RIP...

    ReplyDelete
  16. Tuliomfahamu Dominic, kwa kweli tumepoteza rafiki na ndugu. Ni kijana aliyekua mchapa kazi na muadilifu hasa, alizingatia kanuni za maisha, tunamwomba Mungu amkarimu kwa kumpa raha katika makao yake.
    Swali kwa mamlaka husika na usalama barabarani,"Hivyo mnaposikia watu wanapoteza maisha kwa uzembe wa madreva mnaona kama hamuhusuiki ila familia zinazipoteza ndugu?" Sasa tumeshachoka na hali hizi, badilisheni mfumo, someni na sikilizeni mawazo ya wadau mbali mbali wajibikeni, madreva walevi, wazembe, wasio naleseni kwanini mnawavumulia? na wenye magari, dreva wako naposababisha ajali kama hii, hivyo unajisikiaje? kuna wakati naogopa madreva wa aina hii jamii itachukua sheria mkononi kama vibaka wanavyoangamizwa. Tuwajibike.
    Poleni familia ya Mwita, poleni vijana marafiki zake.
    RIP Dominic

    ReplyDelete
  17. inasikitisha kuona kijana mdogo anakufa kwa uzembe hivi. tanzania law enforcement ni zero kabisa, na hatuta endelea kabisa bila law enforcement.
    madereva wanaosababisha ajali kwa uzembe wa hali ya juu wangekua wanafungwa maisha.

    ReplyDelete
  18. Poleni wafiwa.

    Ina maana sasa Tanzania madereva tuchukue 'defensive driving mentality', kwa maana kuwa ikifika usiku wa giza totoro tuendeshe magari yetu mwendo wa kilomita/maili 10(kumi) kwa saa.

    Maana natujui kama mbele yetu kuna dereva mzembe kaliacha gari barabarani bila tahadhari zozote. Pia sheria barabarani hazifuatwi kabisa na madereva, pia polisi wa trafiki hawawezi kuwepo kila mahali na saa zote 24 kwa siku kushindikiza madereva wazembe kufuata sheria.

    Mdau
    Bongo.

    ReplyDelete
  19. Wapendwa WATANZANIA WENZANGU,,,ni siku chahceh tu zimepita toka ajali ya kifaru iliyopepeleka watu takribani 15 kubaki na vilema vy amaisha na mmoja kupoteza maisha kutokana na ajali ambayo chanzo chake hasa kikubwa ni uzembe wa LORI kuligonga basi la ROMBO EXPRESS,LORY liligongana na BUFALO huko KISANGARA,LORI liligongana na SABCO huko MBEYA,LORI LILIGONGA TASHRIF HUKO HALE TANGA,LORY LILIGONGA MOHAMED TRANS HUKO KOROGWE,,hivi haya malori kwa nini yanakatika maisha ya wenzetu mapema namna hii? Noo way serikali iliangalie swala la MALORI imekuwa too much sasa,,,Dominic pumzika kwa Amani Brother,,,na sisi tuliobaki tunaodrive chonde chonde wakati wa usiku kama hakun agari mbele yako ni afadhali UKAWASHA TAA FULL,,huwa zinasaidia maana vicheche( magari yanayopaki bila tahadhari) ni mengi,,watu wengi wana magari ila hawajua hata maji yanaongezea wapi(am sory for ths) angalizo barabara za MANDELA,MOROGORO,NYERERE BAGAMOYO wakati wa usiku,,mimi mwenyewe nimenusurika hivi majuzi kwa kweli,kama ni kutangaulia mimi ningetangulia ijumaa kablda ya Dominic,,ila namshukuru Mungu kwa kweli

    Famil;ia ya Domicic,ma school mate,wafanyakazi wenzake nawapeni pole sana,,na Mungu ampe pumziko la milele ndugu yetu na kijana mwenzetu

    Amein

    ReplyDelete
  20. pole sana ndugu wanajamii

    nimesikitika sana niliposoma message za hapo juu, he was young 32, sasa ndiyo alikuwa anaingia kwenye ujana utu uzima,na kazi nzuri-UNICEF, kweli kifo hakina huruma.

    Tanzania, watu wengi wanakufa kwa uzembe wa viongozi, huduma mbovu hospitali, ajali za barabarani, rushwa kila kona, kwa sisi tunaoishi nchi kama Finland, tunaona tofauti kubwa sanaaaaaa, sio kuhusu maendeleo bali kuhusu risks za maisha ni kama hakuna kabisaa kwa sababu kila mtu anatenda wajibu wake. Hapa Finland nikiamuka najua nitakula, nitalala na kesho nitaamuka, Bongo huwezi hukikosa kibaka, ni huduma feki hospitali, hukikosa hiyo ajali ya daladala na rushwa kila kona, ni aibu na hatari jamani, tubadilike, ndiyo maana nasema kheli nibebe box lakini nina uhakika kuishi,

    RIP MWITA

    ReplyDelete
  21. Nadhani imefikia wakati nguvu za jamii zitumike katika kukabiliana na madreva wa aina hii, mfano jamii ikiona dreva mmoja kapaki gari kizembe barabarani ama anendesha kwa mwendo hatarishi, hakuna sababu ya kungojea trafiki ama nini, ni kumshughlikia na kama kapaki tu lori lake kizembe hayumo, ni kushughulikia hilo gari hata kulichoma moto, tumeshapoteza ndugu zetu wengi na wengi tuekuwa vilema kutokana na hawa madreva, ajabu wenzetu Ulaya madreva awanajali sana maisha yao na ya wenzao, huwesi sikia uzembe wa aina hii wa mtu kupaki gari katikati ya barabara, mfano huyu dreva, ukiuliza alikuwa anafanya nini ma alikuwa wapi, jibu utakalopewa litazidisha uchungu, na pengine mpaka sasa hajajitokeza hata kutoa pole, mara zote tufikirie wenzetu, hebu madreva fikirieni tabu mnazosababisha kwa hao mnaowasababishia vifo. Bado naona nguvu ya jamii sasa itumike, wahusika wameshashindwa kazi kwa kulea uzembe,siombei mabaya, lakini mjue nyie madreva wasababisha vifo dawa yenu ipo sasa mikononi mwetu, tumeshachoka kutusababishia vifo na ulemavu. SASA BASI!
    Pole familia ya Dominic, RIP Dominic

    ReplyDelete
  22. Anon wa Mon Apr 26, 11:36:00 AM

    Ushauri wako ni mzuri sana, overspeeding is dangerous, ila kwa mwendo wa 10km/h usiku ni kama vile umefukuzwa na simba halafu ukapanda mti ukamkuta nyoka juu ya mti. Yaani kwa mwendo huo usiku utashitukia mpo kumi ndani ya gari moja na walioingia wote ni vibaka.

    Cha muhimu hapa ni Jeshi la polisi kufanya kazi yake, Doria kwa sana (Japo nao wanauza mafuta na kupaki eneo moja wakisubiri asubuhi). Mtazamo wangu ni kuwa Jeshi la polisi livunjwe, JWTZ lichukue nafasi hiyo kwani kwa sasa hatuna vita.

    Yaani iwe ikifika usiku tu Tunaingia kwenue Marshal Laws, Wakati jeshi la polisi likisukwa upya kwa vifaa vya kisasa na utaalam.

    Jeshi la polisi linahitaji kuajiri watu wenye akili sana siyo standard seven and form four failures. Tukifanya hivyo kwa miaka miwili wananchi watajenga mazoea ya kufuata sheria na hivyo kupunguza maafa.

    ReplyDelete
  23. Anon wa Mon Apr 26, 01:01:00 PM

    Ushauri wako hapana, haufai haufai haufai. Tanzania ni nchi ya utawala wa sheria utakapowaachia wananchi kujichulia sheria mkononi sasa itakuwa ni bora tukaishi mbuga ya Nyahua, serengeti, manyara bila kuwa na bunduki tent wala panga yaani kugombana na wanyama wengine uwashinde ili uendelee kuishi.


    Tatizo ni usimamiaji wa sheria na uwajibikaji. Tuanza na kuwawajibisha viongozi wanaoteua watendaji wavivu kwenye sanduku la kura October, hawa wakiona masilahi yao yapo hatarini kwa kukataliwa na wapiga kura basi watakuwa makini sana kuhakikisha kuwa wanawawajibisha hao watendaji wazembe kabla ya wao kuwajibishwa na wananchi.

    ReplyDelete
  24. Kama tatizo ni usimamiaji wa sheria na uwajibikaji, hapo ndipo naungana na mdau wa hapo juu aliyependekeza nguvu ya wanannchi kusimamia haya na kutekeleza, sasa kama hao wenye mamlaka hawafanyi kazi ni nani wafanye kama siyo wananchi, ni uamuzi mbadala pale wenye mammlaka wanaposhindwa kazi na walowaweka wanaposhindwa kuwaadibisha na kuwawajibisha. Haipandi kichwani kila siku tusikie ndugu zetu wanakufa ama wanapata ulemavu kutokana na uzembe wa mtu, ingekuwa ni natural calamities tungeelewa lakini si haya ambayo tunaweza fanya na kuyathibiti, naungana na mdau, pale inapooekana wenye mamlaka wameshindwa basi nguvu ya wananchi ichukue nafasi, hapa ndipo tutafikiri upya na kufanya maamuzi.
    Poleni wafiwa, poleni marafiki wa Dominic.

    ReplyDelete
  25. He was more than a friend I should say a brother. We were always hanging out together to an extent of many people thinking we were also together the day he had that fatal accident. We had alot of investment plans too for the great future of our families...

    He will always have a special place in our hearts because I believe if you got to know him then he must have touched your heart in one way or the other, he was gifted I guess....

    One precious memory you left us is our baby girl Dominica and her mother Angela. I promise to take care and support both of them as they were mine. By the way Dominica & my Brandy are blending up very close as they both grow up. Just like their fathers....

    Look up to us from heaven above and keep praying for us to always walk on the road of lightousness and finally meet again in the never ending heaven.

    You will always be missed, ofcourse tears go down whenever I remember you...MISS YOU BROTHER!!.

    Frankie Fransis

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...