KWA muda sasa yamekuwapo malalamiko kupitia vyombo vya habari na hata mazungumzo mitaani, kuhusu usalama wa magari yanayoegesha katika eneo maarufu la biashara la Mlimani City lililoko barabara ya Sam Nujoma, Mlalakuwa, Dar es Salaam.

Malalamiko hayo yamekuwa yakihusu wizi wa magari na mali ndani ya magari ya wateja wanaofika hapo kujipatia mahitaji yao katika maduka makubwa ya Game na Shoprite, lakini na wale wanaofika hapo kwa shughuli za kibenki, starehe na masuala mengine ya kibiashara na kijamii.

Ni wazi kuwa palipo na watu wengi kunaweza kusiharibike jambo, lakini wakati mwingine jambo huharibika na kusababisha hasara kubwa kwa jamii, ambapo hasa hili la wizi ndilo huwa baya zaidi, kwani mteja huwa na imani na usalama wa mali yake, lakini mwishowe matokeo yake kuwa kinyume.
Habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. asiwasi wangu hupo kwa walinzi wenyewe hapo Mlimani city. Nilikuwepo hapo siku moja na kumona mmoja wao hakipita katika magari na kuchungulia ndani ya kila gari alilopita. Sasa nilishindwa kuelewa kama huo ndio ulinzi anaoufanya au ni namana ya kujua kilichopo ndani halafu aweze kuwapa information we...kwa mtazamo wangu walinzi wana nafasi nzuri ya kuchunglia kwenye magari kuliko vibaka na kuna uwezekano mkubwa sana kwa wao kushirikiana na vibaka has ukizingatia mshahara wanaopewa na utaratibu mbovu wa kuajiri katika haya makampuni

    ReplyDelete
  2. DAWA NI KUSUSUA KWENDA KUNUNUWA VITU HAPO HADI HAPO WATAKAPOCHUKUWA HATUWA YA KUDHIBITI HUO WIZI, IT IS AS SIMPLE AS THAT. I AM SURE THOSE STUFF WE GET FROM THERE WE CAN GET THEM FROM ELSEWHERE IN TOWN, INNIT? KINACHOONEKANA HAPO WEZI WANASHIRIKIANA NA WAHUSIKA HAPO.

    ReplyDelete
  3. Ndiyo siku hizi kila sehemu ya mikusanyiko na wezi pia wapo tele. Nikikusimulia yaliyotupata Rozi gaden hutaamini maana ule si wizi ila unyang'anyi. Nalaumu tamaa yangu ya supu, ya laiti ....

    ReplyDelete
  4. hao walinzi ndio wezi wakubwa, na ukienda ripoti kwenye management wanakuambia parking at owners risk,which is not right at all..

    ReplyDelete
  5. KAKA YANGU ALIIBIWA GARI MPYA MWAKA JUZI 2009 HAPO MLIMANI NA WALIOHUSIKA NI WALINZI WA HAPO SABABU KAKA YANGU HAKUWA MTU WA KUPENDA MAKUU NA YEYE ALIKUWA NI MGENI(ANAFANYA KAZI KAMPUNI YA MAFUTA HUKO MANAMA.BAHRAIN)ALIPUZIA UJINGA WA MAASKARI WALIOONEKANA WANATAKA KUENDELEA KUMTAFUNIA PESA JAPO GARI YAKE ILIKUWA MPYA 2001 TOYOTA CRESTA GX100 ALIWACHANA NAYO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...