Wanafunzi wote watanzania wanaosoma katika chuo kikuu cha Lumumba Moscow-Russia ,mnataarifiwa kwamba fomu za kugombea uongozi wa T.S.U kwa wale wanaotaka zimeanza kutolewa.Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 13/5/2010.Nafasi za uongozi zitakazo gombewa ni:-

1.Mwenyekiti wa T.S.U.
2. Mwenyekiti msaidizi wa T.S.U.
3.Katibu Mkuu wa T.S.U.
4.Katibu Mkuu msaidizi wa T.S.U
5.Katibu wa Elimu.
6.Katibu wa Elimu Msaidizi.
7.Katibu wa Fedha.
8.Katibu wa Fedha Msaidizi.
9.Katibu wa utamaduni, michezo na masuala ya Jamii.
10.Katibu Msaidizi wa utamaduni, michezo na masuala ya Jamii.

Form zinapatikana kwa Swilla Livingstone, Block 10 room 715.Pia zinapatikana kwa Mkange Habibu Shaha(Block 2 room 356 ).Uchaguzi utafanyika tarehe 15/5/2010 siku ya jumamosi.Ni matumaini yangu kwamba mtajitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili tupate viongozi makini,wachapakazi na waadilifu.
Swilla Livingstone M.
(M/kiti tume ya uchaguzi T.S.U)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nimesubili fulanazzzzz hadi nimechemka yaani toka nilivyompa Anuani yangu Ankal hadi leo haijafika, na amini hata ingekuwa inatoka mbiguni ningekuwa nishaipata. sasa Ankal sema kweli kama ilikuwa April fool tujue.
    James.
    Mkungugu.

    ReplyDelete
  2. Tumeona nafasi zingine zote zimetajwa, je ya M/kiti wa Tume ya Uchaguzi TSU, mbona haijatajwa? Au yeye anachaguliwa kwa taratibu tofauti!! zipi?

    ReplyDelete
  3. mmeshindwa kutafutana wenyewe chuoni mpk mje mtangaze huku,inaelekea ndio maana matatizo yanawaandama hamna ushirikiano kbs.ajabu na aibu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...