Waziri Mkuu wa UK, bwana Gordon Brown ameshatangaza rasmi kuwa wananchi na wakazi waruhusiwa wa UK watakwenda kupiga kura Alhamisi ya tarehe 06 Mei 2010 kumchagua Waziri Mkuu wa UK.

Kwa mara ya kwanza katika historia, uchaguzi mkuu wa UK wa mwaka huu 2010 utafanyiwa maandalizi ya mdahalo (Debate) ambayo itarushwa moja kwa moja kwenye TV za taifa kuwapatia wananchi kusikia sera za viongozi wagombea ili wananchi wapate uamuzi wa kumchagua Waziri wa UK wa kuongoza nchi yao hasa katika hali hii ngumu ya kiuchumi.

Gordon Brown atakuwa ni Waziri Mkuu wa kwanza kukubali kufanya mdahalo (Debate) kwenye TV katika historia ya UK ambayo haijapata kutokea kwa viongozi wote waliopita kufanyiwa midahalo ya namna hii kabla ya uchaguzi wao.

Alhamisi ya tarehe 15/04/2010 TV ya taifa, kanati ya (ITV) itarushwa hewani mdahalo huo moja kwa moja kwa wananchi wapate kuona saa 8.30pm (usiku), na Ahamisi ya tarehe 22/04/2010 kanati ya SKY News (Channel 501 au 517 kwa kuangalia kwenye HD) saa 8pm (usiku), na kumaliziwa na Alhamisi ya tarehe 29/04/2010 kanati ya BBC saa 8.30pm (usiku).

Miezi ya nyuma wananchi mbalimbali wa UK walikuwa wakivutana katika suala la upigaji kura nchini UK. Baadhi ya wananchi wanasema hawatoenda kupiga kura kwasababu mbalimbali za kidini, baadhi ya wananchi wanasema hawatoenda kupiga kura kwasababu mbalimbali za sera za kisiasa, na wengine wanasema LAZIMA waende kupiga kura kwasababu kura ndiyo mtu sauti yake ya kusikilizwa na serikali na ndiyo inayomchagua kiongozi unayemtaka kutokana na sera zake.


ZENJYDAR imejaribu kukusanya habari kutoka vyombo tofauti vinavyoaminika hapa nchini UK (reliable sources) ili kukupa wewe uamuzi wa mwisho kuamua kama ni Mwananchi wa UK, na unaishi UK, kura yako itakuletea manufaa gani ukiwa kama ni Mwananchi wa nchi hii.

Maulamaa wa Kidini ya Kiislam UK wamepitisha kwa Muislam kupiga kura nchini UK ni sawa kwa kupigia kura chama ambacho sera zake zinalingana na mshikamano wako, na vilevile ni sahala kwa maisha yako nchini UK; kwa maelezo zaidi bonyeza hapa.

Redio stesheni maarufu ya LBC (London Biggest Conversation) 97.3 FM ya London ambayo husikilizwa na mamilioni ya wananchi wa UK ambao wapo UK na nje ya UK kwa njia ya redioni na njia ya mtandaoni, imekuwa ikihimiza sana wananchi wa UK kupiga kura kwa kuchagua kiogozi wanayemuona sera zake zinalingana na mshikamano wako, na vilevile ni sahala kwa maisha yako nchini UK, na, wameanzisha kampeni ya kwenye mtandao wanayoita "Which party agrees with you?", kwa maelezo zaidi bonyeza hapa.

Kwa kuwa hii ni mara ya kwanza UK kufanya mdahalo (Debate) ya uchaguzi kwenye TV, tunaangalia upande wa pili wa Antlantic, United States of America, vipi walikuwa wakifanya miaka yote hiyo ya nyuma iliyopita tangu miaka ya 80. Jim Lehrer ambaye alikuwa ni mmoja wa matayarisho ya midahalo ya marais wa Marekani, anatoa 'tips' au ushauri wa kupata ushindi wa midahalo ya TV, kwa maelezo zaidi bonyeza hapa.

Haya! sasa mpira uko kwako na muda unaondoka, kama bado hujajiandikisha, tafakari, kaulize upate jibu la kukutoa shaka na mpaka upate jibu la kukuridhisha, na iwapo utataka habari zaidi za upigaji kura nchini UK bonyeza hapa.

--
Zenjydar Community Association
www.zenjydar.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Na sisi Raisi wetu nae akubali lu debate na wagombea wengine november. Before uchaguzi ??

    ReplyDelete
  2. yahusu!!mweee

    ReplyDelete
  3. NENDENI MKAWAPIGIE LABOUR WALIOWALETENI NA KUWAPA MAKARATASI MUONYESHE SHUKURANI KIDOGO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...