Hi Brother Michuzi,
Katika kuangalia internet, nilikumbana na hizi habari zisizo za ukweli kutoka kwenye hii kampuni inayojifanya imeshajenga daraja la kigamboni which is not true. Hebu bofya hapo chini:
http://www.ace-consultants.com/transportation-bridges-kigamboni.htm
Mdau Robert

--------------------------------
Ili kuhakikisha kwa dhana ya 'lisemwalo lipo, kama halipo laja" ripota wa Globu ya Jamii aliyetumwa kutembelea sehemu za Kurasini ambako daraja la Kigamboni Bridge linatarajiwa kujengwa amekuta patupu asubuhi hii, hali kadhalika maeneo yote ya mwambao wa pwani hiyo hadi Feri hakuna kitu kama hicho na hivyo kudhibitisha kwamba habari hii si ya kweli. Vile vile katika kufuatilia kwa wanaohusika nao pia wameshangaa na wamesema mambo bado. Wadau mnasemaje?
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. hi Ankal, mie nimeipitia site yao, walichoandika ni project covers the feasibility study of Kigamboni bridge, na wao ni consultant hivyo hawawezi kujenga daraja, nafikiri mdau aliyepost hii akuisoma hii article vizuri, inaonesha wazi hawa ni consultant ambao huchora na kufanya upembuzi yakinifu wa miradi,
    na uchambuzi wa mradi kama huu wa kigamboni unaweza kufanywa na consultants zaidi ya mmoja.
    Hivyo sioni udanganyifu wowote kwao

    ReplyDelete
  2. Picha walizoweka ni za daraja la Mto Rufiji na daraja la Mto rufiji (sasa linajulikana kama daraja la Mkapa) halikujegwa kwa mtindo wa build, operate and transfer (BOT).
    Cha kujiuza ni je walishiriki kwa namna yoyote kwenye ujenzi wa daraja la Rufiji?

    ReplyDelete
  3. Hii habari inawezekana ilitolewa tarehe 1 April 2010

    ReplyDelete

  4. Hamna neno.

    Siyo kwamba kila kitu kinachosemwa lazima kiwe cha ukweli. Caveat Emptor.

    ReplyDelete
  5. Ankal hiyo ni kama proposal yao. Twaweza ikubali au kuikataa na tukachagua nyingine. Ila mimi sijaipenda hiyo. Chunguza picha ya pili. Je ni kweli kuna majani ktk ya bahari yenye mawimbi?.

    ReplyDelete
  6. ni kweli,ndio maana Mkuchika amesema tutumie lugha ya kimatumbi,maana ingekuwa ni ya kimatumbi ingekuwa rahisi kueleweka.ila pia hakufanya kosa kurusha watu wachangie mawazo.mfano
    urefu wa kimo cha daraja unanitia shaka,je ni kweli hapo chini meli zinaweza kukatiza?

    ReplyDelete
  7. Ankal, labda ni lile la mto Ruvuma kule sehemu ya Mtambaswala. Kwa maana hata mazingira yake katika hiyo picha hayaonyeshi kuwa ni ya bahari, bali ya mto. Hata hayo magugu yanayoonekana si ya bahari, kwa kawaida huota kwenye maji baridi.

    Nahisi hivyo.

    ReplyDelete
  8. hawa jamaa ni wahuni ndo kama RITES ya india, wanasema "the bridge was constructed....". Hii inaonyesha ni jinsi gani Richmond ilivyotumia njia kama hii kuwahadaa akina Lowasa na wenzake.

    ReplyDelete
  9. "The project covers the FEASIBILITY STUDY for construction of the Kigamboni Bridge in Dar Es Salaam, Tanzania."

    ReplyDelete
  10. english ni noma kaka

    ReplyDelete
  11. hi ankal,napenda kutofautiana na mchangia hoja wa kwanza,nafikiri alisoma mstari wa kwanza tu, ukiendelea mbele utaona kuna sehemu wanasema ...was constructed at Kurasini area just near the Tanzania Harbours Authority then anaendelea kusema the bridge was executed under the Build Operate and Transfer (BOT)scheme. Mimi nimeelewa kuwa wanasema kazi ilisha fanyika na ndiyo maana wameiweka katika profile yao.
    Ni kawaida kwa makampuni kujikuza sana nafikiri uchunguzi ukifanyika katika hizo projects nyingine walizoziweka kwenye profile yao, utakuta kuna udanganyifu mkubwa. Tuwe makini jamani makampuni mengine ni ya kitapeli.. all the best

    ReplyDelete
  12. "hi Ankal, mie nimeipitia site yao, walichoandika ni project covers the feasibility study of Kigamboni bridge, na wao ni consultant hivyo hawawezi kujenga daraja, nafikiri mdau aliyepost hii akuisoma hii article vizuri, inaonesha wazi hawa ni consultant ambao huchora na kufanya upembuzi yakinifu wa miradi,
    na uchambuzi wa mradi kama huu wa kigamboni unaweza kufanywa na consultants zaidi ya mmoja.
    Hivyo sioni udanganyifu wowote kwao"

    Ukiangalia the contents of the picture inasema "the bridge was constructed in Kurasini area", so maybe it is a feasibility study as you said, but they need to use a more comprehensive language, as that one is confusing.

    ReplyDelete
  13. Kigamboni Bridge

    The project covers the feasibility study for construction of the Kigamboni Bridge in Dar Es Salaam, Tanzania. The bridge, which measures about 560 m long, 14 m wide and is a 3.75 m two-lane carriageway with provision for cyclists and pedestrians, was constructed in the Kurasini area just near the Tanzania Harbours Authority.

    The bridge was executed under the build, operate and transfer (BOT) scheme.

    Nimeamua kuweka maneno yao yote ili kuonyesha kwamba aliyemtumia ankal hajakosea, angalieni hiyo tense waliyotumia, (nimebold) ndio mtapojua hawa jamaa wanamaanisha hiyo project ilishajenga!
    Pia kutumia picha ambayo sio ni kosa, maana watu watajua project yenyewe ndio hilo daraja, maana chini ya hizo picha wameandika Kigamboni Bridge!

    ReplyDelete
  14. Hili ni daraja la Ruvuma bridge kule Mtambaswala-Masasi ambalo limejengwa na mkandalasi China Geo na lilisimamiwa na Norconsult. Hapa likiwa linamaliziwa spans za mwisho upande wa Msumbiji.

    ReplyDelete
  15. DARAJA TULIJENGA ILA BALALI ALIPOKIMBIA NA FEDHA IKABIDI TULIVUNJE...LOL,ANYWAY LABDA NICHANGIE KIDOGO HAPA KUTOKANA NA MTAZAMAMO WANGU,ALIYESEMA HII NI FEASIBILITY STUDY HAKUKOSEA NA ALIYESEMA DARAJA LIMEJENGWA NAE HAKUKOSEA MMMMH KWANINI?KUTOKANA NA SITE YA HAO JAMAA SIJUI WAKANDARASI WAMESEMA WAMEFANYA FEASIBILITY STUDY THAT'S FINE ILA WAKAENDELEA MBELE KUSEMA WAME EXECUTE HIYO PROJECT...LABDA NIONGELEE KNOWLEDGE NILIYONAYO KIDOGO KUHUSU PROJECT...PROJECT YEYOTE HUWA NA PROCESS GROUP WENGINE HUITA PROJECT LIFE CYCLE,HUWA KUNA INITIATION,PLANNING,EXECUTION,MONITORING AND CONTROL NA MWISHO CLOSURE,HIYO FEASIBILITY STUDY IPO NDANI YA INITIATION AMBAYO NDIO FIRST PHASE KATIKA PROJECT AMBAYO INAANGALIA FAIDA NA HASARA ZA KUFANYA PROJECT NA VILE VILE KUANGALIA UKUBWA WA PROJECT NA VILE VILE COST ZAKE,SASA HAWA WAKANDARASI SIJUI NANI... WAMESEMA WAMEFANYA HIYO FEASIBILITY STUDY WAKAENDA HADI KWENYE PHASE YA EXCUTION,EXCUTION HI PHASE AMBAYO HUFANYWA BAADA YA PLANNING,WAKISHA FANYA FEASIBILITY STUDY,THEN WANA PLAN HALAFU HIYO PLAN UNAIWEKA INTO REAL THING YAANI (EXCUTION).NA KUTOKANA NA MAELEZO YAO HAPO CHINI WANASEMA WAME EXECUTE NA WAKAWEKA PICHA YA DARAJA THEN WAKAANDIKA KABISA KIGAMBONI,HUPO KIDOGO WAMECHANGANYA WATU....ANYWAY UNAJUA HII NI DUNIA YA BIASHARA SO WATU WANATAFUTA UJANJA UJANJA ILI KUPATA TENDA NA KWASABABU SISI WAAFRIKA AKIJA MKANDARASI HUWA HATUANGALII SANA HISTORIA YA HUYO MTU TUNAKURUPUKA TUNAMWAGA MAHELA WATU WANAKULA KAMA ILIVYOKUWA RICH..MOND.KAZI KWENU WADAU LETS READ BETWEEN THE LINES...NAFIKIRI NIMEELEWEKA KAMA KUNA MWENYE MTAZAMO MWINGINE ASEME TUJIFUNZE ILA HILO TANGAZO NI WIZI MTUPU

    ReplyDelete
  16. Lugha gongana hapa, 'was constructed in the Kurasini area just near the Tanzania Harbours Authority'. manake daraja liko tayari sio proposal kama wanavyodai wadau wengi hapa. washikajii wanapalilia CV na Mkapa Bridge

    ReplyDelete
  17. Acheni bla bla!
    Hakuna daraja kwenda Kigamboni na hakuna Study iliyofanywa na hao jamaa kuhusu Kigamboni!
    Matapeli! Hakuna cha bla bla!

    ReplyDelete
  18. NASIKIA KWENYE VITABU VYA SERIKALI INAONYESHA KUWA DARAJA LIMEKWISHAJENGWA NA PESA ZIMEKWISHALIPWA, KWA HIYO KAMA MNASUBURI DARAJA LIJENGWE...TOO BAD FOR YOU GUYS. KWELI BONGO TAMBARARE, MTU KESHAKULA MAPESA HAPO..........

    ReplyDelete
  19. ANKAL NA WADAU HII NI CHANGAMOTO KWA SERIKALI KUTIMIZA AHADI YAKE KUJENGA DARAJA LA KIGAMBONI.
    ALIYETENGENEZA HABARI HII ANA UJUMBE WENYE KITENDAWILI KWA JAMII YA WATANZANIA.HAPA NAONA WATU WANAACHA MADA MEZANI NA KUKIMBILIA KWENYE DARASA LA LUGHA.KITENDAWILI TEGA NIPE JIBU UKISHINDWA NIPE MJI:DARAJA LA KIGAMBONI LIMESHAJENGWA,LINAEENDELEA KUJENGWA AU LITAJENGWA KABLA YA ------------------------------?

    ReplyDelete
  20. mimi naota watakuwa wamekosea maana hilo daraja linafanana na lile la mto rufiji ambalo linaitwa mkapa bridge

    ReplyDelete
  21. Ni kweli wanasema wameshajenga. Soma yote, si msitari wa kwanza tu. Wadau kaeni chonjo. Sasa hivi mtasikia kuna mabilioni yameliwa na kampuni hiyo ya ACE ndiyo iliyofanya kazi hiyo au itafanya kazi hiyo. Wizi mtupu. Uwazi zaidi unatakiwa.

    ReplyDelete
  22. Wabongo kweli nuksi!! Mwekezaji kasema kahusika katika suala zima ujenzi wa daraja, na picha kawawekea na ujiko kajipa; nyie hamtaki!

    Vielelezo vyote vinaonesha daraja limeshajengwa na magari yanavuka kwa mamia kila siku kwenda Kigamboni; anayetaka kupanda pantoni aendelee kwa starehe zake!

    Ili muweze kuona daraja hilo la kisasa mnatakiwa kuchangia Bilioni 40 kwenda Chama cha Mapinduzi; wakisharudishwa tena madarakani ndio watawaonesha daraja lenyewe.

    Kwani hii ni mara ya kwanza kuangalia makaratasi na kuona vitu vimenunuliwa na pesa zimelipwa na kuonesha vimepokelewa lakini havipo? Kama hamuamini someni ripoti ya Mkaguzi Mkuu iliyotolewa juzi (unaweza kupata kwenye http://www.mwanakijiji.com) utaona kuwa hii ni njia ya kawaida kabisa ya utendaji ambayo mara kwa mara imeonekana kukubalika.

    Mazingaombwe siyo lazima umkate mtu vipande; bali hata kuwafanya watu waamini kuwa kilichokuwepo hakipo na kilichopo sicho!

    SAIDIA CCM WASHINDE!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...