Ndugu Salim Mfungahema
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Yah: KUSIMAMISHWA UONGOZI KWA
KATIBU MWENEZI SERA NA ITIKADI: TAWI LA CCM MOSCOW-URUSI

Kamati siasa ya Tawi la CCM-Moscow kama kamati ya Maadili ya Tawi, imefanya mkutano wake wa dharura tarehe 1 April 2010 chini ya Mwenyekiti wa CCM Tawi , Mhe, Dr. Alfred Kamuzora Mjini Moscow-Urusi. Wajumbe 9 kati ya 12, walihudhuria mkutano huo, Sawa na 75%, na kuruhusu Mkutano kuendelea na agenda .

Katika mkutano huo, Kamati ya Siasa ya tawi imejadili kwa kirefu Mwenendo wa katibu mwenezi sera na itikadi wa tawi Ndg. Salim Mfungahema. Kamati ya Siasa ya Tawi ilipokea na kujadili taarifa za tuhuma zilizomkabili Ndg. Mfungahema akiwa kama kiongozi mwandamizi wa tawi kama ifuatavyo:

Kusambaza waraka wa uchochezi kwa wanachama kinyume cha Katiba ya Chama Cha Mapindizi na kuleta mgawanyiko ndani ya Tawi, pasipo kuwasilisha Waraka huo katika vikao husika vya Tawi ili Kujadiliwa kwa mujibu wa katiba ya Chama Cha Mapinduzi ibara ya 14(4), (5).
Kuwa na dharau, kutokuwa na Heshima na uadilifu kwa viongozi wenzake wa Tawi, kuwakashifu viongozi wenzake kwa hiyo kuvunja katiba ya CCM ibara ya 14 (7),.
Kueneza sera za Uongo, na Kubuni Mambo yasio ya kweli na kushindwa kutoa vilelezo yakinifu kutokana na mambo anayozungumza/kuyasikia. Kamati Imegundua ni Mwongo na mchonganishi na mwenye nia kuvuruga Ustaarabu wa Wanachama kwa Viongozi wao.
Kueneza taarifa za Uchochezi na chuki kwa wanachama na Viongozi wa Tawi.
Kuidanganya Kamati ya Siasa na Halmashauri kuu kwa hiyo kuvunja katiba ya CCM ibara ya 14 (4), Kujichukulia Madaraka binafsi bila Kufuata Katiba na Ushirika, kubadili tafsiri za Maamuzi pasipo viongozi wengine kufahamu.
Kwa kufanya hivyo na mambo mengine, Kamati ya siasa imeridhia kuwa Bwana Mfungahema amekiuka miiko ya uongozi kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya CCM, ibara ya 18 (1) (2) na ahadi za mwanachama ibara 8. Pia katika Mwongozo wa Tawi la CCM Moscow Vipengere vifuatavyo:,Masharti ya mjumbe wa kamati ya siasa ibara ya 1:1.5(a). Utendaji: ibara ya 8:1(d) na (e) na ibara ya 8:2 na 8:3 ya Mwongozo wa Tawi 2008.

Kwa hiyo basi, Pamoja na kushauriwa katika vikao mbali mbali vya Chama ngazi ya Tawi kwa kuzingatia miiko ya uongozi bila kubadilika, na kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ibara ya 39(9) kikao cha kamati ya Siasa kama kamati ya Maadili ya Tawi kimeona kuwa Bwana Mfungahema ameshindwa kutimiza matarajio ya wanachama zaidi ya kuzalisha migogoro ndani ya Tawi. Kwa kuzingatia hilo, Kamati ya Maadili katika kikao chake kilichokutana 1/4/2010, imemsimamisha Uongozi Ndg. Salimu Mfungahema hadi itakapotangazwa vinginevyo kutokana na vitendo vyake vya kukosa uaminifu, maadili ya uongozi na matumizi mabaya ya madaraka aliyokuwa nayo. Uamuzi wa kutoa adhabu hiyo kwa kiongozi huyo, umetolewa baada vikao viwili tofauti kwa mujibu wa Kanuni za Maadili toleo la 2002 na Katiba ya CCM.

Awali, Bwana Mfungahema, alipewa muda wa zaidi ya mwenzi mmoja kujibu mambo mbalimbali yaliyokuwa yanamkabili au/na ili abadili mwenendo wake, lakini hakutekeleza

Pamoja na adhabu hiyo ,Kamati ya siasa imemweka chini ya uangalizi, na kwa kipindi chote anatakiwa asijihusishe na mambo yanayomhusu Katibu Mwenezi wa Tawi. Mambo yote yanayohusiana na Katibu Mwenezi wa Tawi yatafanya na Katibu wa Tawi hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo. Ikigundulika anaendelea na siasa za chuki na kuwagawa wanachama , basi hatua nyingine kali zitachukuliwa dhidi yake.

Hata hivyo,Bwana Mfungahema bado ana haki yake ya kikatiba kukata rufaa dhidi ya hatua hiii ndani ya siku 15 tangu uamuzi huo ulipopitishwa rasmi, kama anadhani hajetendewa haki. Maelezo ya Rufaa yakiambatana na vielelezo yakinifu na ushahidi yanatakiwa yawasiliwe kwa katibu wa Tawi, na Baadae kujadiliwa na kamati husika kwa Mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapindizi ibara ya 19(2) Kushindwa kukata rufaa au Kamati kutoridhia vielelezo kutapelekea kuthibitishwa kwa adhabu dhidi yake.

Kutokana na sababu hizo, Kamati ya siasa imetumia madaraka yake iliyopewa kumsimamisha uongozi bila kumuonea kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ibara ya ,39 (9) na mwongozo wa Tawi, na kanuni ya Maadili ya CCM..

Mwisho: kwa niaba ya Kamati ya siasa ya Tawi, Nawataka wanachama wote wa Tawi kudumisha umoja wetu kama kawaida na kufuatilia kwa karibu utendaji na taarifa za tawi ambazo zipo katika website ya Tawi www.ccmmoscow.blogspot.com ili kuondokana na Upotashaji wa Taarifa:. hasa kufahamu Taratibu za uchaguzi wa Viongozi wa Tawi letu hapa Urusi kwa kuanzia ngazi za mashina, Jumuiya ndani ya Tawi,na baadae Uchaguzi wa viongozi wa juu wa Tawi na wajumbe Kamati ya siasa , Mchakato huo wa Uchaguzi, ulijadiliwa na Kupitishwa na kikao cha Halmashauri kuu Tawi cha tarehe 27/3/2010. ambapo Utekelezaji wake Unaanza mapema zaidi 1 july 2010 kulingana na ratiba ya Mwongozo wa Uchaguzi Tawi la CCM MOSCOW:

Kidumu Cham cha Mapinduzi.

Aksanteni!

Imeandaliwa na: Bi Neema Charles Kangese - Katibu wa Tawi

- Imehakikiwa na: Dr. Alifred Kamuzora Mwenyekiti wa Tawi– CCM-URUS.

Taarifa zaidi zinapatikana katika Tovuti ya Tawi : www.ccmmoscow.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. MATAWI YA CCM NJE YA NCHI HAYATAKI MZAHA, HUKU BONGO ITABIDI TUIGE MIFANO HII, MKIJA BONGO SI MTAFURUMUSHA WATU NYINYI, BALAA HII

    ReplyDelete
  2. Bi Neema (Katibu wa Tawi) na Ndugu Kamuzora (Mwenyekiti wa Tawi),

    Mmewasiliana na Dinah Marios? Kama bado fanyeni hivyo haraka ili awateleeni matarumbeta, kibao kata na biriani ya kumsuta na kumng'oa madarakani Ndugu Mfungahema (Katibu Mwenezi)!

    ReplyDelete
  3. UNCLE HATUTAKI MATAWI YA VYAMA VYA SIASA NJE YA NCHI. HIVI WATU WAMECHANGANYIKIWA AU NI NINI?

    NI MIMI MKEREKETWA WA MASKANI YA CCM STONE TOWN

    ReplyDelete
  4. mimi kama mwanachama ningeomba wanachama wote wa ccm-russia tuungane ili tuweze kujua sababu za kujiudhuru katibu mkuu mh.livingston swila,pia na kusimamishwa kwa mh katibu mwenezi bw salim mfungahema,ni kweli tunajua watanzaia wote wa moscow hatumkubali mfungahema ila kwa sasa ina bididi tusiangalie mabaya ya huyu mheshimiwa bali tuangalie kwanini viongozi hawa waliposhauri uchaguzi mkuu ndipo waonekane hawana nidhamu?wanachama wenzangu inabidi tuungane kudai uchaguzi mkuu kwan ni haki yetu ya msingi,hawa wakina kamzola,bakunda na asenga ni wakina nani katika chama,kazi ya kuanzisha chama imekwisha hivyo waitishe uchaguzi mkuu!WANACHAMA WENZANGU NAOMBA TUSIKUBALI UTAWALA WA HAWA WATU WENYE UCHU NA URAFI WA MADARAKA,TUJIULIZE KWANN HAWATAKI KUITISHA UCHAGUZI?KUNANINI WANACHOFAIDIKA NACHO ZAIDI?AMKA SASA MWANA CCM-MOSCOW TAMBUA UMUHIMU WA ELIMU YAKO NA SIO KUENDESHWA KAMA GARI BOVU!!!

    ReplyDelete
  5. Hang on hivi nanyi si mtakuwa mumevunja sheria zenu ibara ya 14 (7),. kwa kumkashifu hapa kwa kumuita muongo na mengineyo? jee kulikuwa na haja ya kuyatangaza hayo hadharani? si mgelisema tu kuwa amekwenda kinyume na sheria zenu?

    kiungwana hapo nanyi mumekosea.

    ReplyDelete
  6. Michuzi naomba kukupa point ambayo hivi majuzi ilijadiliwa katika moja ya kongamano za bloggers, point hiyo inahusu legal wrights matumizi ya picha za watu katika blogs.

    Kwa ufupi tu ni kuwa unless picha hii iliyoiweka hapa, ya mtuhumiwa ameidhinisha uitumie katika blog yako unaweza kujikuta uko pabaya.

    Baya zaidi ni kuwa kuna third party waliokupatia hii picha, kwa hivyo unless kama mtuhumiwa ametia saini kuidhinisha matumizi ya picha yake kwa matumizi ya ccm urusi, ccm urusi watakuwa wamefanya makosa kutumia picha yake na kukupatia wewe picha hiyo uiweke kwenye blog yako.

    kuna tafauti kubwa na sheria tafauti katika ya bloggers kama wewe na mimi na vyombo vya habari katika matumizi ya picha za watu. sheria inayowalinda wanahabari katika matumizi ya picha za watu hailindi wana-bloggers hata kama mwenye blogger ni mwandishi wa habari. sheria inamlinda mwana-blogger pale tu ikiwa anatumia blogg inayomilikiwa na muajiri wake.

    kwa maana hiyo, kila mmoja anajuwa kuwa hii ni blog yako na sio ya daily news, kwa hivyo kila kinachotokea hapa ni jukumu lako.

    Ushauri wangu kwako ni kuitowa hiyo picha hadi pale utakapohakikishiwa na ccm urusi kuwa wanahaki ya kutumia picha hiyo na wamekupa idhini ya kuitumia, otherwise unaweza kukuta mtuhumiwa anakufikisha kwenye vyombo vya sheria.

    Angalia mfano wa facebook, kabla ya kuweka picha kuna mahali una tick kuonyesha kuwa unaruhusa ya kubandika picha ulizochaguwa katika ukurasa wako.

    michuzi nawe unatakiwa uwe unapewa uhakika huo kabla ya kubandika picha za watu hususan inapokuwa ni za aina ya kushutumiana kama ilivyo hii.

    ahsante sana
    Ahmed seif
    Web developer
    uk

    ReplyDelete
  7. kazi bado ipo

    ReplyDelete
  8. KAZI KWELI KWELI,WENZENU WANKUJA HUKU KU INVEST KWENYE VIWANDA,NYIE MNAENDA ULAYA KU INVEST POLITICS.

    KWISHNEI

    ReplyDelete
  9. Hawa viongozi wanatakiwa Tanzania sio Moscow maana viongozi wa CCm TZ wangeshika adabu.

    Kazi nzuri uongozi wa Moscow. Tunaomba wengine waige mfano sio kuwa mnabebana tu wakati viongozi wengine hawafai1

    ReplyDelete
  10. mjumbe wa kamati ya siasa ya TawiApril 05, 2010

    Huyu mtu ni msumbufu sana. afadhali tuu aondolewe alikuwa anataka uenyekiti huyo ndo maana maneno mengiiiii hadi kutoa waraka kama ule wa .......

    ReplyDelete
  11. Pamoja na yote hebu tuangalie hasa umuhimu wa matawi ya CCM kwa Tanzania.

    1. Chama cha siasa ni kukundi cha watu waliougana wakiwa na dhamira moja kuu nayo kushika uongozi wa nchi - Je matawi ya CCM nje ya Tanzania yana dhamira gani?. Moja ni kutaka kujipenyeza katika nyadhifa pindi wakifulia nje ya nchi. Mbili kutaka kupata favour wanaporejea nchini. Tatu ni kukusanyika kwa ajili ya nyama choma na bia na kujirusha kitu ambacho hakina tija yoyote.

    2. Matawi haya hayana umuhimu wowote kwa Tanzania zaidi kuwagawa kwani wale wasiokuwa na interest kwenye si-hasa wanaona ni waste of time, nafikiri huyu waliyemfukuza atakuwa mmoja wao, kaona anapoteza muda bure. Waliomuweza wanataka kuwaonesha vionbgozi waliopo bongo kuwa huyu hata akirudi msimpe ulaji wowote.

    3. Kwa walio bongo, umuhimu wa tawi unakuja pale linapokuwa na potential ya kuongeza kura za wagombea uongozi, sasa ninyi wa nje mnapoteza muda wenu, bebeni box mkasaidie ndugu na jamaa zenu bongo msipoteze muda for nothing nobody cares about you ata home.

    ReplyDelete
  12. Mfungahema karibu sana CCJ. Enzi za chama kimoja ni kweli lingekuwa ni pigo kubwa, zama hizi ukiona ya CCM yamekuchosha usipatwe na ugonjwa wa moyo bure - CCJ ipo, CHADEMA kipo, TLP (punde mwenyekiti ataanza kutangaza nafasi ya mtu wa kumrithi), CUF ipo, nk. Wazee wa CCM na warithi wao bado wana ndoto za ukiritimba wa CCM, lakini alama za nyakati (ambazo kwa bahati mbaya hawataki kuzisoma) zinaonesha mwanzo wa mwisho wa ukiritimba.

    ReplyDelete
  13. watanzania ni Vichwa maji kwenda kuanzisha mashina nje ya Nchi. Usingizi bado ni mzito sana.

    ReplyDelete
  14. watanzania na majungu wakiwa nje kumbe bado yapo? ndio maana baadhi yetu hatutaki kuwa wanachama wa vyama vya siasa vya nyumbani na hata uwanachama wa umoja wa watanzania, kwa sababu daima kunakuwepo na chuki na fitina miongoni mwa wanachama.

    mdau
    UK

    ReplyDelete
  15. Hivi ninyi mna fikiria nini kichwani mwenu? Mliondoka Tanzania kwenda nje kuendesha siasa za CCM mkitegemea zita work? Au mlikwenda nje kusoma? Kama mnaipenda sana CCM, kwa nini msirudi Tanzania mkagombee ubunge? Acheni kuchekesha, CCM ni political organization. Kichwani kwenu mnafikiri kuwa na CCM ugenini ni jambo la maana? Itakuwaje Conservative Party ya UK au Republican Party ya hapa tuliko US iwe na branch Dar? Come on now, let's be serious. Stop this CCM overseas branches BS. It doesn't make any sense at all.

    ReplyDelete
  16. Ulaji tu hamna kingine. Yaani matawi yote ya nje ya nchi nikufanya fundraising na bla bla. Yamechachamaa sasa sababu ya uchaguzi mkuu october baada ya hapo yanapumzika.People wake up msiuze uhuru wenu.

    ReplyDelete
  17. Gwaba KuliaApril 05, 2010

    Huu ndio upuuzi wa mwisho.

    Naunga mkono suala la matawi ya chama chetu yaletwe katika Mkutano Mkuu wa CCM Taifa tujadili.

    Tunawaomba alika Maina warudi waje wagombee uwenyekiti wa matawi mfano hapo Kabwana - shirati aone.


    CCM-London sisi tunajua ni Research:  Centre for Cold Matter wala hakuna Chama cha mapinduzi huku.

    ReplyDelete
  18. watu mnapata madivoika na bado mnaangaika na vitu visivyokua na msingi.majungu unafiki na umbea ndo huu.watu wanaotaka kushikilia madaraka washatolewa kwenye uongozi wa jumuiya mara kibao,wataweza kuiongoza CCM?kuharibiana kusikokua na msingi

    ReplyDelete
  19. Baada ya kunyimwa mikopo mmeona mjiunge na Chama cha Mafisadi ilimfanikiwe! Kumbukeni kuwa waliokuwa wanawatetea si wote ni wana sisiemu. Nyambaf mko tayari kuuza utu wenu kwa vitu ambavyo ni haki yenu. You suck!!!?
    BTW Hivi ninyi mmeenda kusomea uhandisi, udaktari au Siasa?

    ReplyDelete
  20. Mimi ni mmoja wa wanachama tawi la moscow,napenda kumpa pole sana bwana Mfungahema kwani watu anaofanya nao kazi ni wanaucha na madaraka,yaani bwana Chriss Bakunda na Boniface Assenga,lakini nampa pongezi kwakushauri uchaguzi ufanyike kwani ilo ndilo lilomsababishia matatizo yote hayo,pongezi kwake kwani ni mfanya kazi mzuri,ila kama hili tawi la Moscow litaendelea kuendeshwa na watu watatu hatutafika popote,kama mnataka kweli democrasia itendeke basi acheni uchaguzi ufanyike na si kuwasimamisha watu bila ya sababu zisizoeleweka,kwani hayo yote mliyoandika hapo ni ya uongo na nyie ndio waharibifu wa hiki chama,kwani mlishataka kuharibu chama cha UMOJA WA WANAFUNZI MOSCOW,sasa mnahamia CCM,hvi mnataka nini nyie watu wawili??????? Alafu just for your benefits mnamfanya mwenzenu aonekane mbaya mbele ya wajumbe wengine wa tawi,je nyinyi kweli ni viongozi wazuri?????????????????

    ReplyDelete
  21. HAHAHAHAHAHAHAHAHHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAH!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! UKISIKIA WATU WAROHO WA MADARAKA NDO HAWA,HII BARUA HAIJAANDIKWA NA KATIBU WA CHAMA BI.NEEMA CHARLES BALI IMEANDALIWA NA WATU WATATU KATIKA CHAMA KWA LENGO LA KUMCHAFUA BWANA MFUNGAHEMA,BWANA MFUNGAHEMA HUKU NDO KUKUA KISIASA,ILA ENDELEZA KUWAELEZA WAJUMBE KUHUSU KUFANYA UCHAGUZI KWANI KUNA JAMBO PALE HAO JAMAA KWANINI HAWATAKI KUTOKA???? BONIFACE,BAKUNDA NA KAMUZORA ACHENI MCHEZO MCHAFU

    ReplyDelete
  22. Nguru KanyaApril 06, 2010

    Uncle mambo,

    Yaani hawa ni smart kuliko Baba wa Taifa katika masuala ya siasa na hususani CCM?

    Mbona wakati wake hakuwahi hata kufukiria kufungua tawi huko Urusi wala China wala Uingereza ingawa aliwapenda watu wa huko na alishirikiana nao vyema?


    Tafadhali sana msituharibie Chama. Tusipokuwa macho hili nalo sasa ni tabaka linakuja.

    Kufumba na kufumbua tutakuwa na tabaka la CCM (wa nyumbani) na CCM (diaspora).

    Mzee wetu Makamba, tafadhali usiliangalie hili jambo kama mzaa ebu chukua hatua maana sisi bado tunakuaminia. Mkichelewa siku moja mtaikumbuka hii blogu ya Michuzi na ubini wangu!

    Imeanza kidogo kidogo, sasa subirini muziki wake baadaye?

    a. Utasikia, tunataka tupate Makatibu wa Wilaya & Mikoa (diaspora) na waajiriwe na walipwe mshahara toka Chamani.

    b. Utasikia, sasa nasi inabidi tuwe na wawakilishi wa Mkutano Mkuu Taifa na pia Halmashauri Kuu kama wengine. Na hao watu watadai kusafirishwa wakati wa vikao na kutunzwa sawa na wengine maana huwezi kusema kuwa Katiba inaeleza kuwepo kwa Tawi la CCM lenye haki kiduchu kuliko matawi mwengine!

    c. Utasikia, hivi mbona sisi tumebaguliwa hatuna mzungumzaji wetu katika Kamati Kuu (T)?

    d. utasikia, mbona nasi tuna mchango mkubwa tu kama wengine kwa nini tusiwe na Wabunge wawakilishi kutokea CCM disapora?

    e. Utasikia na sisi tunapendekeza mgombea uraisi wetu kutoka diaspora kwa tiketi ya CCM!!!!!!

    ReplyDelete
  23. WEWE Tarehe Tue Apr 06, 04:39:00 AM, Mtoa Maoni: Nguru Kanya

    INAONEKANA NA WEWE NI MMOJAWAPO WA HAO CCM DIASPORA
    "UTASIKIA" a - e, KWELI KWENYE MSAFARA WA MAMBA HATA KENGE WAPO

    ReplyDelete
  24. Nguru Kanya "UNCLE MAMBO" SOUNDS FAMILIAR!!

    ReplyDelete
  25. Naomba tuambiwe sababu halisi kusimamishwa kwa bwana Mfungahema,kama ni utovu wa nidhanm ni kwa vipi?na amefanyaje?na alivyoukuwa anadangaya kasema nini?hayo ndo vitu vya kuwekwa wazi hadharani.Mbona alisema uchaguzi ufanywe wajumbe wote walisaini wakakubali hadi mwenyekiti mwenyewe?leo inakuwaje mmeona anahoja nzuri ya demokrasia kuhusu uchaguzi mnamsimamisha.Siungi mkono nashangaa barua yakutangaza kusimamishwa imewekwa kwenye mtandao na mkasema Bibi Neema aliandaa pale chini kama siyo kusingiziana mbona hamna sahihi ya Neema?Na Kamzora kuchanganyika haja weka sahihi.Hivi mkishitakiwa kwa kashfa hamwoni itakula kwa mmiliki wa blog ya CCM bwana Thomas Assenga?hamjui hata mnachokifanya tunasubiri uchaguzi ndani ya mwezi moja bila hivo hiyo TAWI IFUTWE MANA HATA HAIJAZINDULIWA RASMI MMESHAANZA UCHU WA MADARAKA.

    ReplyDelete
  26. Alikuwa kinara wa kupambana na ufisadi huyo kwiii kwiii kwiii

    ReplyDelete
  27. hahahhaha!eti DIASPORA!LOL,2fauti nini?home au diaspora mlemle ccm!kazi kwenu moscow na habari ndiyo hiyo Bw mfungatents......

    ReplyDelete
  28. Nguru KanyaApril 06, 2010

    Poa kabisa,familiar or not familiar,
    Hatutaki hii kitu ya kuchafua chama chetu kwa majina ya matawi ya ughaibuni.

    ReplyDelete
  29. CCM OYeeee ! Naipenda CCM kila uendapo utaikutaa...utaikutaa aaa aaa utaikuta ...pale Russia utaikutaaa aaa utaikuta...pale London utaikuta aaa utaikuta .....pale India utaikutaaa aaa utaikuta ...Na Tanzania imetawalaaaa aaaa imetawala ...

    CCM Juuuuuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...